Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Sikonge Said Nkumba na mamia ya wanachama wa CHADEMA, warejea CCM

Robethn

JF-Expert Member
Aug 18, 2015
2,103
352
ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO LA SIKONGE (CCM) SAID NKUMBA NA WANACHAMA WA CHADEMA WAREJESHA KADI ZA CHADEMA KWA MAGUFULI
28.jpg

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Sikonge kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
29.jpg
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Sikonge Bw. Goerge Joseph Kakunda.
30.jpg
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Sikonge, Ndugu Said Nkumba akionyesha kadi yake ya uanachama wa Chadema ambayo aliikabidhi kwa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli na kuahidi kushirikiana na wana CCM katika kuhakikisha ushindi ni wa kishindo.
1.jpg
Said Nkumba (kulia ) akimnadi mgombea wa ubunge wa jimbo la Sikonge Bw George Joseph Kakunda.
19.jpg
Wakazi wa Sikonge wakishangilia baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Said Nkumba kurejea CCM.
23.jpg
Wazee wa Sikonge wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli.
31.jpg
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ulyankulu kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
32.jpg
Umati wa wakazi wa Ulyankulu wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli ambapo aliwaahidi kushughulikia tatizo la wakulima wa tumbaku.
33.jpg
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa jimbo la Ulyankulu Bw. John Peter Kadutu kitabu cha ilani ya uchaguzi ya CCM cha mwaka 2015-2020.
34.jpg
Mgombea ubunge wa jimbo la Ulyankulu Bw. John Peter Kadutu akionyesha juu kitabu cha ilani ya uchaguzi ya CCM cha mwaka 2015-2020 mara baada ya kukabidhiwa na mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
35.jpg
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Ulyankulu mara baada ya kumaliza kuwahutubia.
5.jpg
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Alhaji Abdallah Bulembo akiwahutubia wakazi wa Kaliua kwenye mkutano wa kampeni za CCM na kuwaambia wananchi hao kuipigia kura CCM kwani wapinzani wamepoteza ajenda.
7.jpg
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Kaliua Profesa Juma Kapuya.
8.jpg
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kaliua Profes Juma Kapuya akihutubia wakazi wa kaliua kwenye mkutano wa kampeni za CCM.

10.jpg
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kaliua kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
11.jpg
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Kaliua ambapo aliwaahidi kujenga na kuboresha bara bara, elimu, afya pamoja na kutatua tatizo la maji na bei za Tumbaku.
12.jpg
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipokelewa na Mzee samuel Sitta mara baada ya kuwasili Urambo kwenye mkutano wa kampeni.
13.jpg
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiongozana na Mgombea Ubunge Jimbo la Urambo Mama Magareth Sitta pamoja na mumewe Mzee Samuel Sitta.
14.jpg
Shabiki na mpenzi wa CCM akishangilia ujio wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli.

16.jpg
Mwakilishi wa Walemavu Ndugu Amon Anastaz Mpanju akihutubia wakazi wa Urambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli
17.jpg
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Urambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa ataijenga Tanzania mpya yenye maendeleo.
 
Watu wawili hao tu,,,ccm kwa kukuza hbr na kutia chumvi ni jadi yenu...anaondoka mmoja ukawa 1000 wanatoka ccm
 
Bado bulaya ,anajuta maana HALIMA kamwingiza mkenge aingie Cdm sasa naona anaanza kupotea taratibu
 
tumesha vunja kofuli na kumwaga pombe ccm mmechanganyikiwa amna abari mpya!
 
Wako wapi hao wanachadema? Pia ni vema ujue kwamba Said Nkumba ametokea ACT na si CHADEMA kama unavyotaka jamii iamini. Said Nkumba baada ya kushindwa kupata nafasi ya kugombea ndani ya Chadema alishatimkia ACT na kwasasa hatoki CHADEMA, hivyo msitafute kiki kupitia CHADEMA. Rejea alipoongea jana kwenye mkutano kama uliona taarifa ya habari ya Azam Tv.
 
maccm mnachekesha sana. Na vipropaganda vyenu uchwara. Huyu nkumba alisharejeshwa siku nyingi ccm kwa kukataliwa na wanachadema.

Hata sheree za ufunguzi wa kampeni za ccm pale jangwani alikuwepo. Sasa mnaigiza nini!

Safari hi ni mwisho wa maigizo yenu kipigo mtakachokipata mtajuta kumfahamu lowassa.
 
Ndugu zangu wapendwa wa TANZANIA,kwa hekima na taadhima,naomba tuangalie ahadi alizoahidi Dr.Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2010 - 2015,..Je alitekeleza? Na pia tuangalie ahadi anazotoa John Pombe Magufuli wa CCM ile ile katika kuusaka URAIS wa TANZANIA!! Ahadi za JK kwenye kampeni za kusaka Urais 2010 ni.....
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora (HAJATEKELEZA)
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini (HAJATEKELEZA)
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria- Igunga (HAJATEKELEZA)
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga (HAJATEKELEZA)
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma (HAJATEKELEZA)
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini (HAJATEKELEZA)
7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma (HAJATEKELEZA)
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera (HAJATEKELEZA)
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi- Kagera (HAJATEKELEZA)
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba- Bukoba Mjini (HAJATEKELEZA)
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini (HAJATEKELEZA)
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera (HAJATEKELEZA)
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera (HAJATEKELEZA)
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu- Kagera (HAINA MENO)
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya (MAUAJI YANAENDELEA)
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba- Kagera (HAJATEKELEZA NA ZILIZOPO MBOVU HAZIFAI)
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali (HAJATEKELEZA)
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika- Mwanza (HAJATEKELEZA)
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza (HAJATEKELEZA)
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote- Pemba (KERO HAZIJATATULIWA)
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro (HAJATEKELEZA)
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa- Mbeya mjini (HAJATEKELEZA)
24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa (HAJATEKELEZA)
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea (HAJATEKELEZA NA WALIMU WAMEPUUZWA WANAULIZA -SHEMEJI UNATUACHAJE?)
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya (HAJATEKELEZA)
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga (HAJATEKELEZA)
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa (HAJATEKELEZA)
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro (HAJATEKELEZA)
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini (HAJATEKELEZA)
31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora (HAJATEKELEZA)
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu (AMETEKELEZA)
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini (HAJATEKELEZA)
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)- Hydom Manyara (HAJATEKELEZA)
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa-Musoma (HAJATEKELEZA CCM NDIO CHANZO CHA CHOKOCHOKO)
36. Kulinda haki za walemavu- Makete (HAJATEKELEZA,WANATUMIKA KWENYE KAMPENI TU)
37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini (HAJATEKELEZA)
38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha (HAJATEKELEZA)
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini (HAJATEKELEZA)
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni- Kigoma– Kaliua,Tabora (HAJATEKELEZA)
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi- Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma (HAJATEKELEZA)
43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido (HAJATEKELEZA)
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga (HAJATEKELEZA)
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini (HAJATEKELEZA NCHI IPO GIZANI)
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo- Busekera, Wilaya ya Musoma, . (HAJATEKELEZA)
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido (HAJATEKELEZA)
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti – Ngorongoro (HAJATEKELEZA)
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara (HAJATEKELEZA)
50. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini (HAJATEKELEZA)
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa (HAJATEKELEZA NA HALI NI MBAYA SANA)
52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania- Iringa (HAJATEKELEZA)
54. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda (HAJATEKELEZA - CHOKOCHOKO ZA CCM ZINAHATARISHA AMANI)
55. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara (HAJATEKELEZA)
56. kuwapa wanawake nafasi zaidi- Kilolo ,Iringa (ANGALAU)
57. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar (HAJATEKELEZA)
58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa- Kabandamaiti mjini Zanzibar (HAJATEKELEZA)
59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti (HAJATEKELEZA)
60. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma (HAJATEKELEZA)
61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma (HAJATEKELEZA)
62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma (HAJATEKELEZA)
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma (MISAADA YA VYANDARUA NA VYOO KWA MSAADA WA WATU WA MAREKANI)
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam (HAJATEKELEZA)
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara (HAJATEKELEZA)
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha (HAJATEKELEZA)
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa- Kibaha. (HAJATEKELEZA)
66.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha (HAJATEKELEZA) N.K
CCM HAIAMINIKI TENA,WAKATI UMEFIKA CCM INAPASWA ITOLEWE KWA NJIA YA KURA MADARAKANI?..KWA NINI WASITEKELEZE AHADI HIZI KABLA YA KUAHIDI ZINGINE?....CHAGUA LOWASSA..CHAGUA UKAWA (CHADEMA/CUF/NLD/NCCR MAGEUZI)
 
Back
Top Bottom