Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Willy Qulwi Qambalo wa Karatu wajiunga CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa

Wakati wote kuna maisha baada ya siasa na hasa hizi siasa za vyama.

Kwa vijana waliooa hivi karibuni na degree zao ndio hizi za sindimba na lugha ni vema wakawa makini na mustakabali wao wa kisiasa watazitesa familia zao bure.

Upinzani ni kama ngazi ya kufikia siasa za viwango ili uweze kusajiliwa CCM, lakini upinzani haukupi uhakika wa kile unachokitafuta kwa sababu hakipo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nassari mzungu wake hapendi shida. Ameenda upande wa pili apate cheo huku akipata muda wa kula bata na mzungu wake bila kuadhibiwa.
 
Kuna majimbo hata wasipoungana na ACT ,Chadema lazima ishinde Arusha,Hai,Mbeya Mjini,Tarime etc

Yes MEMBE ni Mtaji kwasasa!! Naunga mkono hoja.

Arusha sahau hilo, uje kuniprove wrong uchaguzi ukiisha! sasa kama mna ham msipate hata hio kura moja tenda muwekeni membe cdm, rudieni ule ule utopololo wenu wa lowasa, ccm hawarudii tena kosa baada ya magu kumaliza mda wake
 
Halafu bado unakuta Kuna watu Chadema wanakapigia debe Kale kajizi Shillah eti kawe Kabunge, kweli siasa ni utapeli mtupu hakuna cha Chadema wala CCM ujinga mtupu. Naachana na huu ujinga rasmi kila mtu apambane na hali yake tu
 
Kijana mdogo unakuwa malaya wa kisiasa. Asahau heshima aliyokuwa nayo hapo kabla.
Wacha aende ccm kuliko na manyangumi na mapapa
 
Anaonekana amechoka sana, kwani mlivyomtongoza hamkumpa pesa ya kujikimu?

Nimemsikia anasema hatagombea Ubunge, lakini anataka kumsaidia Magufuli, sijui anataka kwenda kupiga deki ikulu?!
 
Kwa kweli nimesikitika sana vijana ambao wangepigania mageuzi ya kimfumo wanakimbia kwa kulidhika na maendeleo ya majengo na mabarabara wanasahau wajibu wao wa kupigania haki na usawa kwa jamii pana
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Nassari na mbunge wa sasa wa Karatu,
Willy Qulwi Qambalo wameondoka rasmi ndani ya chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wamepokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa pamoja na viongozi wengine wa Chama mkoa wa Arusha.

Nasari amekishukuru CHADEMA kwa kumlea tangia akiwa mdogo na sasa ameamua kutumikia nchi yake na sina nia ya kugombea nafasi yoyote, kilichopo mbele yake ni kumsaidia Rais John Magufuli.


View attachment 1500768
Joshua Nassari akiwa anaingia kwenye Ofisi za CCM

View attachment 1500769
 
Wabongo njaa ndio tatizo sugu, Hela ndio mungu wao hawana utu wala chochote, Tz itahitaji miaka elfu 1000 zaidi kustaarabika watu kuwa wakweli katika mioyo yao, huyu Nassari, Kafulila, sjuli Lijuakali nk. na hata wengine waliobaki huko Chadema akili zao ni mbili mbili njaa za pesa zinawatafuna
 
Sasa hivi mpinzani akija CCM sidhani kama atapata uteuzi, muda ule ulipita..
 
Wakati wote kuna maisha baada ya siasa na hasa hizi siasa za vyama.

Kwa vijana waliooa hivi karibuni na degree zao ndio hizi za sindimba na lugha ni vema wakawa makini na mustakabali wao wa kisiasa watazitesa familia zao bure.

Upinzani ni kama ngazi ya kufikia siasa za viwango ili uweze kusajiliwa CCM, lakini upinzani haukupi uhakika wa kile unachokitafuta kwa sababu hakipo.

Maendeleo hayana vyama!

Huyu alinukuliwa zama zilekuhusu "Jamhuri ya Kaskazini". Mawazo ainaile hayafai kamwe. Hafai
 
Back
Top Bottom