wanasema kwamba mke wa mtu ni sumu, nimeshuhudia.............Jumapili ilyopita nilipotoka kanisani nikakuta kuna kikao katika nyumba niliyopanga, jamaa mmoja ambaye ni jirani alikuwa na mwenzake na baba mwenye nyumba. Niliitwa na kuombwa nijoin kwenye kikao kile ambacho sikuelewa nini agenda. Nilipofika ndio nikaelezwa kwa kifupi na baba mwenye nyumba nini kimemleta yule kijana. Kisa kilikuwa hivi....Jamaa kamtafuna mke wa mtu siku moja kabla ambayo ni Jumamosi, usiku mzima alikuwa anapata haja ndogo kwa taabu sana na anasikia maumivu hasa. Alipoona hali imekuwa mbaya akaomba msaada kwa rafiki yake ambaye ni jirani yangu na wanatoka sehemu moja na baba mwenye nyumba yangu. Baada ya huyu jirani kusimuliwa mkasa mzima akaona ni vema kumshirikisha baba mwenye nyumba. Nilipofika ndio walikuwa wanaumiza kichwa wafanye nini, waende kuomba msamaha kwa mwenye mali au waende kwa mganga. Mwizi anang'ang'ania aende kwa mganga akiungwa mkono na rafiki yake na baba mwenye nyumba anamtaka jamaa akaombe msamaha. Niliitwa kutoa maoni yangu nami nikaungana na baba mwenye nyumba, jamaa wakakubali kwenda kuomba msamaha wakiongozana na yule mzee. Mimi nilipewa onyo nisimueleze mtu kuhusiana na mkasa ule mpaka utakapoisha lakini hivi sasa kila mtu anajua hapa mtaani. Juzi ndio wamekamilisha kila kitu na jamaa hivi sasa hajaonekana tangu siku hiyo........................JAMANI MKE WA MTU NI SUMU KUWENI MAKINI!!