Alikojoa Dagaa!!

kaeso

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
551
96
wanasema kwamba mke wa mtu ni sumu, nimeshuhudia.............Jumapili ilyopita nilipotoka kanisani nikakuta kuna kikao katika nyumba niliyopanga, jamaa mmoja ambaye ni jirani alikuwa na mwenzake na baba mwenye nyumba. Niliitwa na kuombwa nijoin kwenye kikao kile ambacho sikuelewa nini agenda. Nilipofika ndio nikaelezwa kwa kifupi na baba mwenye nyumba nini kimemleta yule kijana. Kisa kilikuwa hivi....Jamaa kamtafuna mke wa mtu siku moja kabla ambayo ni Jumamosi, usiku mzima alikuwa anapata haja ndogo kwa taabu sana na anasikia maumivu hasa. Alipoona hali imekuwa mbaya akaomba msaada kwa rafiki yake ambaye ni jirani yangu na wanatoka sehemu moja na baba mwenye nyumba yangu. Baada ya huyu jirani kusimuliwa mkasa mzima akaona ni vema kumshirikisha baba mwenye nyumba. Nilipofika ndio walikuwa wanaumiza kichwa wafanye nini, waende kuomba msamaha kwa mwenye mali au waende kwa mganga. Mwizi anang'ang'ania aende kwa mganga akiungwa mkono na rafiki yake na baba mwenye nyumba anamtaka jamaa akaombe msamaha. Niliitwa kutoa maoni yangu nami nikaungana na baba mwenye nyumba, jamaa wakakubali kwenda kuomba msamaha wakiongozana na yule mzee. Mimi nilipewa onyo nisimueleze mtu kuhusiana na mkasa ule mpaka utakapoisha lakini hivi sasa kila mtu anajua hapa mtaani. Juzi ndio wamekamilisha kila kitu na jamaa hivi sasa hajaonekana tangu siku hiyo........................JAMANI MKE WA MTU NI SUMU KUWENI MAKINI!!
 
kichwa cha habari na habari yenyewe ni tofauti.mimi nilidhani ni dagaa wa ukweli.jee huyo jamaa ana uhakika gani kama amefanyiwa?isije ikawa kaambukizwa ugonjwa wa zinaa.
 
sawa mkuu. mi ushali wangu naona nibola kwanza jamaa aende hospital akapime kwanza magonjwa ya zinaa km kasendwe, kisonono, n.k. alafu mengine yafate, niayo tu.
 
Dagaa wako wapi mkuu au ulimaanisha maumivu? Japo ni ukweli mke wa mtu sumu,pia si ujanja kuiba unyumba.
 
Sikubaliani na ushauri wa nyote kwenye kikao, inatakiwa akamwone Doctor, huyo atakuwa ameambikizwa namna fulani ya STDs. Kwenda kuomba msamaha ni kujiexpose zaidi na kuleta uhasama, chengine acheni uzinzi!
 
  • Thanks
Reactions: Sal
mnh mie naogopa khasaaa, na sasa naona tafarani mkasa huu namie wataka kuntokea,
kuna mjimama flani anakaa jirani na nyumbba niliopangisha karibu na chuo , chuo kiomoja hapa kisiwani Unguja, huyo mmama anauza kiduka, wakati naenda kununua vitu vya kupika akajidai kanipenda na kuna mtoto wa dadake anataka nimuowe(mie sjaoa bado) mwanzo nikakubali nikajua ananizengua tuu, mwisho nikamchomolea kwa vile huyo mtoto wenyewe yuko mbali, anakua mgumu kuelewa na saivi nishamstukia kua hana ukwaju wala ubuyu ila ananitaka yeye, mana anasema "wanaokuja hapa dukani wote nawaona hawajatulia kama weye, naitapenda kama utamuoa mwanangu, " saivi simwelewi, na zaidi mumewe tatizo mana watu wa huku wanapigana ndumba si mchezo, namuogopa huyo mumewe.
naogopa miee , nisije kojoleshwa dagaa namie
Eeh mungu nisaidie uniepushe na hili janga.
 
Mbona kuna jamaa alikojoa samaki mbichi, tena alimtoa kinyumenyume (yaani kuanzia mkia kwenda kwenye kichwa cha samaki, sijui alivumilia vipi ile miba ya samaki)
 
mnh mie naogopa khasaaa, na sasa naona tafarani mkasa huu namie wataka kuntokea,
kuna mjimama flani anakaa jirani na nyumbba niliopangisha karibu na chuo , chuo kiomoja hapa kisiwani Unguja, huyo mmama anauza kiduka, wakati naenda kununua vitu vya kupika akajidai kanipenda na kuna mtoto wa dadake anataka nimuowe(mie sjaoa bado) mwanzo nikakubali nikajua ananizengua tuu, mwisho nikamchomolea kwa vile huyo mtoto wenyewe yuko mbali, anakua mgumu kuelewa na saivi nishamstukia kua hana ukwaju wala ubuyu ila ananitaka yeye, mana anasema "wanaokuja hapa dukani wote nawaona hawajatulia kama weye, naitapenda kama utamuoa mwanangu, " saivi simwelewi, na zaidi mumewe tatizo mana watu wa huku wanapigana ndumba si mchezo, namuogopa huyo mumewe.
naogopa miee , nisije kojoleshwa dagaa namie
Eeh mungu nisaidie uniepushe na hili janga.

kuwa makini aisee..
 
kichwa cha habari na habari yenyewe ni tofauti.mimi nilidhani ni dagaa wa ukweli.jee huyo jamaa ana uhakika gani kama amefanyiwa?isije ikawa kaambukizwa ugonjwa wa zinaa.
Si ugonjwa wa zinaa ni dagaa, baada ya kuomba msamaha amerudi katika hali ya kawaida.
 
Back
Top Bottom