Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Salaam ndugu yangu,
Ilikuwa mwaka 2019 siku chache kabla ya Uchaguzi, Mzee mmoja aliyekuwa akigombea nafasi ya Uenyekiti alikuwa na ukaribu Mkubwa na mjomba wangu.
Mgombea huyo ilikuwa hakosi kuwaita Jamaa na marafiki (akiwemo Mjomba kwenye vikao vya pombe na bata nyinginezo).
Ghafla Mzee akaanza kujitokeza kusaidia mipira timu za Vijana pale mtaani kwetu kitunda kwa kununua mipira, vuvuzela, kununua maji jambo ambalo kila mtu alishangazwa.
Ilipofika usiku mmoja kabla ya Uchaguzi Mimi na ndugu zangu tukiwepo sebleni. Mjomba alirudi muda wa saa mbili usiku akakaa na Sisi. Baada kama ya dakika kumi akamtuma mdogo wangu awaite dada zangu na Shangazi wake sebleni mara Moja, dogo akafanya hivyo.
Tulipotimia wote sebleni nakumbuka mjomba akasema "Wanangu nimewaita hapa najua si kawaida, poleni sana kwa kuwasumbua. Nina ombi dogo tu ambalo nataka Kila mmoja kwa nafasi yake naomba anitekelezee."
Akauliza, si mnajua kuwa kesho tunachagua Wenyeviti wa Mtaa wetu wapya? Tukajibu "Tunajua Anko"
Akaendelea " Ewaaaah sasa Kuna yule Mzee (Jina namhifadhi) amekuwa mwema sana kwetu, hapiti sehemu akaniacha, amekuwa anatusaidia sana hivi karibuni Hata nyie naamini mmeona.
Tukajibu "Kweli kabisa Anko"
Akaendelea "Kesho ndiyo siku ya kumlipa fadhila ya asante kwa kumpigia kura. Hivyo, kwakuwa wote humu ndani (Watu nane) umri wenu unaruhusu naomba mkampigie kura Mzee yule.
Sauti chache zikasikika zikiitikia Sawa Anko hakuna shida.
Lakini kaka Mkubwa (mtoto wa Anko) aliyemaliza Chuo akajibu
"Baba hatumpigii kura kiongozi kwa kumlipa fadhila, tutaangalia sera na uwezo wake kutekeleza"
Kimoyo moyo nikasema Bro ana pointi hapa, atafika mbali.
Vipi wewe ulimpigia kiongozi wako wa Mtaa kura kwa kuzingatia nini hasa?