Ajali ya Meli: SUMATRA, lawama kwa viongozi na suala la muungano

hawampendi Pinda kwa sababu wanzozijua wao

Tuvunje muungano tu, siupendi
 
mkuu tumeshachoma ubani kwa kuwaombea wale wote waliofikwa na mauti, waliosalimika Mungu awaponye haraka. Mambo mengine tunamwachia Mungu.
 
Pinda? huyo anatafuta umaarufu kama wale waliotangulia, wana siasa ni watu hovyo sijapa kuona wao huo msiba kila mtu anautumia kwa ajili ya kujijenga kisiasa na misifa ya kipuuzi
 
Wakuu, nime-quote habari kwenye website ya gazeti la mwananchi kama inavyoonekana hapa chini:

"Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk alisema anakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili kumwajibisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa tukio hilo"


HOJA YANGU:

Waziri wa Miundombinu wa SMZ kwanini anaachwa, ila Pinda ambaye wazanzibari hawamtambui wanataka awajibishwe? Wao si waliikataa SUMATRA?
Kwani usafiri wa maji na barabara ni masuala ya muungano? kwa nini asimuwajibishe rais wa serikali ya mapinduzi zanzibar na wasaidizi wake akina maalim seif na wengine? waziri kiongozi anaachwa kisa? Mh mbunge hajui mipaka yake na masuala yahusuyo muungano. suala hilo alipeleke kwenye baraza la wawakilishi asitafute sifa.
 
Mkuu habari hiyo haiwezi kuwa fupi kama hivyo. Ongeza tujue ni kwa nini aseme anataka kumwajibisha Pinda?
Mh mbunge anadai serikali haina takwimu sahihi na jamaa wa KCB wanataka kuwasomesha yatima /wahanga waa msiba huo. sasa kachukua jukumu la kupata data kamili. Jamaa anaratibu michango na misaada inayotolewa na wasamaria. Ana lake jambo huyo.
 
Wakuu, nime-quote habari kwenye website ya gazeti la mwananchi kama inavyoonekana hapa chini:"Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk alisema anakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili kumwajibisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa tukio hilo"HOJA YANGU:Waziri wa Miundombinu wa SMZ kwanini anaachwa, ila Pinda ambaye wazanzibari hawamtambui wanataka awajibishwe? Wao si waliikataa SUMATRA?
Nyambwete;Nimeelewa vizuri hoja yako!!Najua bado wewe ni mgeni jamvini ...Wakati mwingine unachoweza kufanya weka link inayoweza kufanya anayetaka kupata habari zaidi aweze kuifikia!Unaweza kufanya hivyo ..kwa gazeti la mwananchi?
 
Mchungaji, hapo kwenye red: siku hizi mmeacha maji ya uzima wa milele?

FJM!! Kabla ya maji ya uzima lazima usafishe koo

Hili suala la ajali ya Meli tuachane na siasa tuepushe kutokea tena. Meli haizami kama shillingi pale Feri, ninaimani ilichukua masaa mengi kwa kuwa taifa letu nila wajinga basi hatukuweza hata kwenda saidia uokozi

Shame to all responsible elite in the govt
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wakuu, nime-quote habari kwenye website ya gazeti la mwananchi kama inavyoonekana hapa chini:

"Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk alisema anakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili kumwajibisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa tukio hilo"


HOJA YANGU:

Waziri wa Miundombinu wa SMZ kwanini anaachwa, ila Pinda ambaye wazanzibari hawamtambui wanataka awajibishwe? Wao si waliikataa SUMATRA?

wako wengi waliokuja na kauli za hajabu kama ya iyo ya Mbunge wa Ole. Mweshimiwa mwingine (mwenyekiti wa taifa-Chadema) yeye alidai usafiri wa majini usiku usitishwe. Wakati duniani kote sasa watu wanafanya kazi 24 hours. Mweshimiwa mwingine (Edward Lowasa) yeye alidai shirika la BIMA la Taifa ligalamie fidia kwa wahanga wa meli. Hajui kwamba Bima ailipi fidia kwa ajali inayotokea kwa uzembe. Kadri siku zinavyokwenda tunasikia mengi. Ila mpaka sasa kauli za kutoka kwa wanasiasa wetu, zinaonyesha kichwani hawanazo.
 
FJM!! Kabla ya maji ya uzima lazima usafishe koo kabla ya maji ya uzima.

Hili suala la ajali ya Meli tuachane na siasa tuepushe kutokea tena. Meli haizami kama shillingi pale Feri, ninaimani ilichukua masaa mengi kwa kuwa taifa letu nila wajinga basi hatukuweza hata kwenda saidia uokozi

Shame to all responsible elite in the govt
Nimependa point yako -- More than 6 hours watu wamehangaika bila msaada wowote, wengi wao mauti imewapata wakijaribu kujiokoa bila mafanikio.
Dalili ya taifa kufa ni mambo kama haya - leo hii ukiniambia nikutajie system hata mbili tu zinazofanya kazi kwa viwango nchini kwetu utakuwa umenipa swali gumu mno maana HATUNA hata moja.

Sasa saba usiku meli imezama, waokoaji wamefika saa moja asubuhi -- then kesho na mabango barabarani eti mnasherekea miaka 50 ya uhuru -- Mie hamnipati.
 
R U GUYS serious... Inavyosemekana SUMATRA haitambuliki Z'Bar kwanini PINDA awajibishwe?
 
Kwa nini Pinda? Wamwajibishe huyo Rais wa Zanzibar Dr. Shein na serikali yake wanaodai eti hawajui nani mmiliki wa Spice Islander!
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe. Sasa Pinda ana mahusiano gani na Mamlaka ya Zanzibar? Hapa ndipo unaona uozo kwenye katiba yetu. Ni hawa hawa wenzetu wa Zanzibar hawamtambui Pinda. Sasa iweje awajibishwe kwa issues za Zanzibar? Si wanadai Zenji ni nchi huru na kiongozi wake, kwa nini wasiwawajibishe wahusika wa huko Zenji??
 
Jamani someni MWANANCHI paragraph ya 17 kwenye habari ya meli ilipakia watu 3000.Someni habari mpaka mwisho mjue sabab.
 
Jamani someni MWANANCHI paragraph ya 17 kwenye habari ya meli ilipakia watu 3000.Someni habari mpaka mwisho mjue sabab.
Wenzetu wa visiwani hawaachi kunishangaza kwa hili sakata. Ni lama vile akili zap wameweka rehani kwa maruhani.Pinda na kuzama hiyo meli wapi na wapi. Katila hili heri kumuwajibosha Papa wa Roma.Ile dhana ya Zanzibar ni Nchi imeishia wapi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom