Majoja
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 612
- 186
Wakuu naomba kuwasilisha.
Hili la ajali ya boti ya mizigo na abiria MV Spice Islands inaelekea ilikuwa inasubiri tu kutokea.
Kama kumbukumbu zangu haziniangushi, aidha mwishoni mwa mwaka jana au mwanzoni mwa mwaku huu maofisa wa SUMATRA walifukuzwa , tena kwa kejeli kubwa.
Sababu ya kufukuzwa kwao ni kwamba suala la kusimamia safari za meli sio la Muungano, hivyo basi hawakuwa wanahitajika kule Zanzibar.
Ilikuwa aibu kubwa kwa taasisi yenyewe na serikali ya muungano.
Leo nashangaa kwamba Kamati ya Bunge , chini ya Edward Lowassa inaenda kuchunguza tukio hili. Ni kwa ridhaa ya nani?
Sisi na mimi nawahurumia sana wananchi wasio na hatia waliopoteza maisha yao kwa sababu za kijinga kabisa.
Ni lazima waTanganyika tuwaoe misaada yote inayohitajika kupoza makali ya ajali hii, lakini sikubaliani kuingilia dola linaloelekea kujitenga kwa sababu yoyote ile.
Tunajua fika uwezo wa wenzetu wa Zanzibar pamoja na uswahili uliokithiri. Kabla maafa zaidi hayajatokea katika sekta nyingine inabidi wajifikirie upya katika mtazamo mzima wa Muungano.