Aina(4) za wanaume waliochanganyikiwa zaidi duniani

Fakyuol

Senior Member
Nov 26, 2023
142
311
πŸ–“πŸ–“πŸ–“πŸ–“πŸ–“πŸ–“πŸ–“ πŸ–“ πŸ–“ πŸ–“

~Sote tunaamini kwamba, "Wanaume wote ni sawa, ila tabia zao ndizo zinazo watofautisha....

Ndiooo!! Tabia zao ndizo zinazo pelekea uwepo wa makundi tofauti tofauti ya WANAUME

Likiwemo kundi hili la WANAUME waliochanganyikiwa zaidi DUNIANI πŸ““πŸ““πŸ““πŸ““πŸ““πŸ““

πŸ“£1. Mwanaume ambaye hataki kulea mtoto wa mwanaume mwingine ila bado anaamua kuoa mwanamke mwenye mtoto na kumwambia aache mtoto nyumbani kwa wazazi wake, badala ya kuoa mwanamke ambaye hana mtoto kabisa hata wa kusingiziwa.

πŸ“£2. Mwanaume anayeoa mwanamke msomi mwenye diploma ama degree yake.. kisha anamwambia aache kazi na awe na jukumu moja tu la kulea watoto nyumbani......Bro kama ulitaka kuoa mke.. aje kuwa mama wa nyumbani.. kwanini usingemchukua aliyeishia darasa la 4B badala ya kwenda kuua ndoto za mtoto wa watu aliye soma na kupambana kwa shida mpaka kufikia mbali huko alikofika?

πŸ“£3. Mwanaume mlevi anayeoa mdada wa watu mpole mcha mungu na kisha kuyageuza maisha yake kuwa jehanamu!!....bro unajijua kabisa kwamba wewe ni chapombe.. kwann usimtafute cha mpombe mwenzanko mkaoana ili muwe mnakunywa wote mpaka mnatambaa?

Badala yake ..unakaa kumjengea mdada wa watu maisha ya stress!

πŸ“£4. Mwanaume ambaye anampa ujauzito mdada wa watu..afu baadaye anakana kabisa kuwa haujui na wala hausiki na huo ujauzito... baadaye mdada wa watu..anapambana mwenyewe...anapitia magumu akiwa peke yake...na MUNGU saidia anajifungua salama..mtoto amekuwa kuwa kidogo...unajitokeza unadai mtoto ni wako na unatamani kumlea huyo mtoto!!

Bro..kama mtoto ulimkana mwenyewe akiwa tumboni kwamba si wako... Sasa inakuwaje ghafla tu hivyo amekuwa wakwako?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€—πŸ€—πŸ€— ongezea na wewe tabia NYINGINE ya wanaume wanaopatikana kwenye kundi hili la vichaa
 
Back
Top Bottom