Kwanini wazee wetu walipenda tuoe wanawake bikira?

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Ya kale Ni dhahabu ndiyo kitu ninachoweza kusema, Kwenye ndimi za waliotutangulia Basi Kuna hekima ndani yake.

Miaka iliyopita wazazi wetu walikuwa wao ndiyo wanapendekeza mtoto wao wa kiume Ni msichana gani amuoe, na walikuwa hawapendekezi tu Ila ukiona amependekezwa msichana Basi ujue amechunguzwa muda mrefu Sana na wamejiridhisha kuhusu mienendo na tabia zake.

Na walikuwa wanafanya hivyo kwa sababu muda mwingi mtoto wa kiume unakuta yuko shule muda mrefu hivyo kwake inakuwa ngumu kujua yupi aliye na tabia na mienendo mizuri.

Tuachane na hayo maana hapa nataka nije kuelezea kwa kina Sana sijui Kama wazee wetu walilijua Hili au kulikuwa Kuna kingine tofauti na hiki walikuwa wanakiangalia.

Manii ya kiume Ni ya thamani Sana zaidi ya kimiminika Cha kawaida, Haya ndiyo yamebeba taarifa zote za kijenetiki.

Hii inamaanisha kwamba pale mwanaume anapoacha mbegu zake kwa mwanamke anakuwa ameacha DNA zake ambazo zitahifadhiwa kwa mwanamke, Na Kama ikitokea mwanamke akapata ujauzito Basi hizi DNA zinaanza kuwa shared Sasa, Na ikitokea ujauzito ukatoka au ukatolewa Basi hizi taarifa zinaendelea kuhifadhiwa kwa mwanamke.

Wanasayansi hii kitu wanaiita phenomena MICROCHIMERISM, Mfano mwanamke kadri anapofanya tendo la ndoa kwa wingi na mwanaume zile DNA zake hubadirika na kuanza kuiga baadhi ya Mambo ya Yule mwanaume,Na hii ndiyo sababu pale watu wanapokuwa muda mrefu kwenye MAHUSIANO mwishowe hufanana kabisa, mpaka unajiuliza Hawa Ni mke na mume au Kaka na dada.

Mfano mwingine Ni pale mwanamke anapokuwa amejihusisha kingono na wanaume wengi, hivyo ndani yake kunakuwa Kuna DNA za wanaume wengi, hivyo ataanza KUBADIRIKA kuanzia tabia mpaka mienendo, kwa sababu tayari cell zake zimebeba taarifa za watu mchanganyiko.

Hapa utaona pia hata wale wanaojiuza wanakuwa na tabia tofauti tofauti Ni kwa sababu hii ya kufanya ngono na wanaume tofauti tofauti na kupelekea kubeba taarifa za watu tofauti tofauti.

Hii ndiyo kwa wale watu ambao wako kwenye masuala ya kiroho wanasema kwamba mwanamke akitendembea na wanaume tofauti tofauti Kuna Roho za wale wanaume anakuwa anazibeba na zitaanza kumpelekesha.

Mfano mwingine ambao sikupenda niuweke Ila Sina budi kuuweka Ni pale unashangaa kwenye familia yenu Kuna mtoto ambaye yeye Yuko tofauti kabisa na wengine kitabia, mpaka mzazi unajiuliza huyu hii tabia kaichukua wapi wakati kwenye Koo za mama na baba hakuna mwenye tabia hiyo.

Ukweli Ni kwamba mwanamke anahifadhi DNA za kila mwanaume aliyeshiriku naye tendo na hii kupelekea cells zingine kuingiliana pale mwanamke anapobeba ujauzito hat Kama ujauzito kapewa na mwingine. Yaani hapa namaanisha Kama umeoa na Ni wewe ndiyo uliyempa mke wako ujauzito lakini Kama mke wako aliwahi kulala na wanaume wengine Basi kunauwezekano mkubwa pia wa zile cells za wanaume waliopita kuingia kwenye uzao wako pia.

Hii inavutia si ndiyo au inachanganya, vipi nimeiweka mapema Sana au nimechelewa kuileta nondo hii.

Lakini pia Kama mwanamke wako anapenda kuimba kwa kutumia maiki/koni na ikatokea
amefanya hivyo kwa mwanaume mwingine na mchuzi wa koni ukaingia mdomoni hii Ni mbaya Sana, Kwa sababu Kama manii yakiingia mdomoni, yanaenda mpaka kwenye maeneo ya nasal( kisehemu Fulani hivi kipo maeneo ya pua kwa ndani, au nyuma ya macho na masikio), Kisha yanaingia kwenye mkondo wa damu na mwishowe yanaenda kujikusanya kwenye ubongo na kutiririka mpaka kwenye uti wa mgongo na hapo yanakuwa Ni sehemu ya huyo mwanamke milele.

Sasa jaribu kufikilia umempata mke ambaye siyo bikra, inamaanisha Ana DNA za mwanaume au wanaume wengine kwenye ubongo na uti wa mgongo wake, na kitakachotokea hizo DNA zao zinaenda kuwa sehemu za watoto wako.

Na hii ndiyo sababu wazazi wetu walituhusia tuoe wale ambao Ni mabikra na hii ndiyo sababu katika baadhi y jamii ukimtoa mwanamke bikra hata Kama Ni bahati mbaya Basi utake usitake huyo ndiyo anakuwa mke wako.

Ahsante.
Tutaona wakati mwingine.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
hatupo apa kwa ajili ya kubadilisha Dunia acheni watu wale vyupa kila mtu ataenda kubeba msalaba wake kwa namna ya imani yake kama wanawake watapigwa kibiriti sababu waligawa bikra watajua wao na kama Wanaume pia tupigwa kibiriti kwa sababu ya kuvunja bikra itajulikana huko huko kuna mda inabidi tuenjoy haya maisha hatupo hapa kubadilisha Dunia
 
Wengine zimetoka na baskeli hebu tuacheni bana argggghhhhh mfyuuuu!!
Baiskeli ya nyama au plastic ?
20240309_231821.jpg
 
Kuoa MWANAMKE bikira sio sababu au kigezo cha NDOA kua imara......!!! japo bikira kwa kijana wa kiume yeyote mwenye akili anaetaka kuoa lazima kitakua kigezo cha kwanza

NOTE 👉 "UBONGO UTAKUPA MWANAMKE ILA AKILI ITAMBADILISHA HUYO MWANAMKE KUA MKE"


Kuna tofauti kati ya MKE na MWANAMKE

Kijana wa kiume oa mke hutojuta milele, usioe MWANAMKE utajuta milele ✍️
 
Kwa sababu kama manii yakiingia mdomoni, yanaenda mpaka kwenye maeneo ya nasal( kisehemu Fulani hivi kipo maeneo ya pua kwa ndani, au nyuma ya macho na masikio), Kisha yanaingia kwenye mkondo wa damu na mwishowe yanaenda kujikusanya kwenye ubongo na kutiririka mpaka kwenye uti wa mgongo na hapo yanakuwa Ni sehemu ya huyo mwanamke milele.
Hapa umetupanga sana mkuu, kwann iwe manii tuu au hata wakila ugali inaenda huko.?
 
Baiskeli ya nyama au plastic ?View attachment 2936749
15 Mafarisayo walifanya mbinu za kumtega Yesu katika mafundi sho yake. 16 Wakatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode wakam wambie, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu wa haki na unafundisha njia za Mungu kwa uaminifu bila kumjali mtu, kwa maana cheo si kitu kwako. 17 Basi tuambie, wewe unaonaje? Ni halali, au si halali kulipa kodi kwa Kaisari?”


18 Yesu alifahamu hila yao kwa hiyo akawaambia, “Ninyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19 Nionyesheni sarafu mnayolipia kodi.” Wakamletea sarafu. 20 Yesu akawauliza, “Picha hii na sahihi hii ni za nani?” 21 Wakamjibu, “Ni za Kaisari.” Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kais ari; na ya Mungu mpeni Mungu.”


22 Waliposikia haya wakashangaa; wakamwacha, wakaondoka.
 
Mkuu hii elimu uliyoleta sijui umetokea wapi. Sayansi ya vinasaba Genetic+ uzazi haituambii hivyo kama ilivyoelekeza abadan.
Mtoto anatengenezwa kwa Chromosomes 46 tu, 23 toka kwa mama na 23 toka kwa baba. Chromosomes zimebeba DNA in cells ambazo kazi yake ni kutengeneza na kuumantain mwili na genes ambazo ni segments za DNA yako ndio zinafanya mtoto awe na sifa za tabia za kipekee.
Sayansi haituambii kuwa mbegu za mwanaume zinaenda kutunzwa ndani ya mwili wa mwanamke hata kidogo kwasababu manii/sperms/gametes inabeba meiosis ambazo zina life span yake tangia ziwe discarged na kumuingia mwanamke. Meiosis zenye sifa za kiume zina nguvu lakini hazina maisha marefu zaidi ya masaa 48 na meiosis zenye sifa za kike ni dhaifu lakini zinakaa kwa muda wa masaa 72 tangia zitolewe. Ukitaka niendelee kuishi lazima ziwe zimetengenezewa mazingira yenye sifa za kende za mwanaume kitu ambacho kwa mwanamke hakipo zaidi ya ile inayofanikiwa kupenya na kufika kwenye fallopian tube/oviduct na kulirutubisha yao la mwanamke na si kwenda KUKAA KWENYE UBONGO NA KUPENYA MPAKA KWENYE UTI WA MGONGO WA MWANAMKE na kuendelea kuishi. Itapendeza kama una supportive references uziweke hapa
Nikirudi kwenye mada yako kwanini wazee walitaka tuoe wanawake mabikra na kutoka koo fulani wanazozijua wao;
1- Wazee waliamini katika umoja(ONENESS) wa kimwili mwanaume na mwanamke katika kukuza ukoo, so mwanamke bikra ni ishara ya usafi wa ukuzaji wa ukoo, meaning mwanamke hajachafuliwa.
2- Bikra ni ishara ya submission kwa mwanaume anayekutoa. Wazee walisisitiza tuoe mabikra kwasababu mwanaume ndio atakayekuwa mwalimu, muongozaji wa kila kitu katika umoja mulioutengeneza.
Haya yalifanyika huku wakiangalia aina ya ukoo na taarifa za kigenetic zilizobebwa na ukoo na ukoo(GENETIC INHERITANCE). Hii ilifanyika ili kuepuka kurithi magonjwa au matatizo ya kurithi yanayobebwa katika Genes kama magonjwa ya ualbino, kisukari, pumu, sickle cells, ukoma, pressure, Kiafya nk.
Nimekujibu kifupi coz natumia simu, Ila ni somo refu na zuli sana ambalo likifahamika kwa watu wote tutakuja kuwa na familia bora hapo baadae tukiachana na environmental, cultural and technological interferences ambazo zinatubadirisha kila kukicha.
 
Unapata wapi uyo bikra dunia hii ndo ao wanakuambia imetoka na baskeli ila kiukweli zamani ht mm nilipenda ao adi nilipokutana na usmbf wao kwenye tendo siwatak tena
saiv mwendo wa kuvua samaki tu kwenye mabwawa
 
Mm mwanamke anaenipenda na kunijali anathamani ya bikra 100 .ntakana mabikra wote niwe na Mtu ambae wote tunaogopa kupotezana.
 
Back
Top Bottom