AIBU KWA CCM: Wanashindwa kuirudisha Arusha chini ya himaya ya CCM pamoja na kutumia polisi!

WanaArusha wanaweka historia ya ukombozi wa pili wa nchi hii. Hongereni sana.
 
Hivi lini vijana mtaacha ushabiki wa siasa za vyama hivi ambavyo haviwapi maslahi yeyote?

CCM wamekula nchi wamevimbewa, CHADEMA siyo wakombozi wa kweli wa taifa hili pindi watakapopata watakua ni zamu yao kula nchi.

Demokrasia katika nchi maskini yenye ujinga ni mchezo wa wajanja wachache wenye upeo huu au ule, walio nje wanapigana kuwatoa walio ndani ili wapate nafasi ya kumiliki nguvu za dola na faida zake kuzibinafsisha huku nyie mkitumiwa tu.

baada ya kupata madaraka vijana hutemwa na ukamanda huu upambanaji utupya nje kwa sababu hauna tija tena ukiwa mtawala, harakati ni pale ukiwa nje ya utawala kwa sababu ya kuona mabaya mengi na kutokuwepo kwako kwenye serikali.

Mimi ni mwanaharakati siyo shabiki wa kisiasa wa chama chochote, kuna mazuri na mabaya katika vyama vyote, na ubaya wa CCM ni obvious kwa sababu wametawala nchi na wameonekana walichoshindwa kufanya, ila tatizo linakuja kwa vijana kujipa matumaini ya hali juu sana juu ya uwezo wa CHADEMA kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa hapa nina matatizo napo kwani hili lina nafasi finyu sana angalieni nchi karibu zote za kiafrica wapinzani wamefanya nini baada ya kushinda na sisi siyo tofauti na hao)
kuweni na matumaini ya kawaida ya kupunguza hizi kero za CCM na siyo kushabikia kitu mpaka mnakua paranoid mkisia tu mtu anaisema CHADEMA mnahamaki, mishipa inawachachamaa na jasho la ghadhabu kuwatoka

Hizi nguvu ni vizuri mngezitumia pia katika ufahamu wa mambo na kuanzisha na kujiunga kwenye vyama vya kijamii ili tukuze zaidi demokrasia yetu na siyo ushabiki huu wa kihisia hisia unazuia mantiki kushika nafasi yake. Mtaendelea kutumia mpaka lini?

Nafikri hawa moderators hawatoitoa na hii thread maana wamekua PARTISAN sana bila ya kua na Uhakika na kilichoandikwa ni kinagusa nini haswa
 
Sidhani hata uwezo wa kukwepa risasi unao? Amani ikitoweka ndipo utajua nini maana ya kuwa na Amani! CCM endeleeni kulinda Amani Tanzania, Amani bado ipo ya kutosha ila kuna watoto wa shetani wanataka Amani itoweke!

Watoto wa shetani ni JK, watoto wake na CCM yake wanaodhani nchi hii ni yao pekee yao na wanaweza kufanya watakavyo kwa maslahi yao binafsi. Hata Gaddaf alidai kuwa Libya kuna demokrasia, amani na utulivu, wakati sio kweli na tumeshuhudia mwisho wake mbaya! Tanzania hakuna demokrasia, haki, amani na utulivu. Vyote vyote vya dola pamoja na Usalama wa Taifa wa CCM (UWTCCM) vimeacha kufanya kazi na majukumu waliopewa kwa mjibu wa katiba ya nchi badala yake vinawatumikia mabwana wao CCM!
 
Lakini mie nauliza -- kosa la Lema ni lipi? Mie nadhani polisi waliweke suala hili wazi.

Hivi mtu akienda kusikiliza kesi yake atangaze kwamba watu wengine wasiende kusikiliza kesi yake? Sheria hiyo imeanza lini?

Hivi mtu akitoka mahakamani kusikiliza kesi yake ni lazima aondoke hapo kwa gari? Sheria hii nayo imeanza lini?

Hivi mtu akikataa dhamana na kukubali kwenda rumande ni kosa? Sheria hii imeanza lini?

Hivi iwapo dhamana iko wazi na wadhamni wanataka kumtoa hakimu anakataa ni kosa? Hii sheria imeanza lini?

Hii sheria magamba wamei-copy na ku-paste toka kwa M7. kule ni marufuku kwenda kazini kwa miguu, ukionekana unatembea una ambiwa unataka kupindua nchi!
 
CCM inaamua kutumia ubabe kwa CDM na wananchi wa Arusha. Lakini CCM itambue kwamba wanazidi kujipalia makaa ya mawe. Wananchi wa sasa sio wa ile miaka ya zamani ambao walikuwa wanajua CCM tu. Watu sasa wanaona na wanatambua nini kinaendelea nchini.

CCM itambue kwamba inazidi kuimarisha umaarufu wa CDM.

Hongera CDM.
 
Kweli CCM vichwa nazi! Hivi hawaoni kwamba nchi ni muflisi, wameshindwa kusimamia fedha na matumizi, wizi wa hela za umma umekithiri, bado wanaanzisha bifu na CDM? Hivi hawajui timing?

Katika kisiasa huwezi kupigana na mwenzio wakati wewe uko mchafu sana. Haiwezekani!

Serikali ya CCM inaanza kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake, pia imeshindwa kulipa makandarasi wa barabara na construction ya barabara zote zimekwama.

Serikali imekopa benki kulipa wakandarasi lakini hela hizo zimepelekwa kwingine.

Pamoja na madudu yote hayo bado CCM wanataka bifu na CDM!

Au ndiyo ni katika kupoteza lengo la kuwaelezea wananchi wanavyoshindwa kuendesha nchi na hivyo kutumia polisi kwa singizio lao kubwa la "wanaleta vurugu?'
 
Leo alfajiri ktk purukushani za mabomu pale NMC kuna polisi wawili ambao hata kwa sura siwajui ila chakushangaza gafla baada ya mabomu kurindima FFU mmoja alitukuta tumejibanza (tulikua watatu) katika migomba na ukuta wa Arusha sport near arusha secondary na alikua kashika mtutu ila wenzake walivyomuuliza kwa mbali kama kuna watuhumiwa eneo hilo yeye aliwajibu kuwa hakuna mtu na akatuambia tusipite njia ya msikiti wa baniani kwani kuna polisi wenzake wengi sana ivyo tuelekee na njia ya town na tukiulizwa na askari wenzake tuwajibu kuwa tunaelekea sokoni na hatukua NMC, baaada ya hatua chache maeneo ya geti la shule ya msingi uhuru gafla mbele yetu akatokea FFU mwingine akiwa kavaa yale mavazi yao ya kazi na kashika mtutu akavua elemet yake akatuambia tukimbie kwa kupitia njia ya NSSF tuvuke mto then tutakuwa salama bila kutiwa nguvuni na askari wenzake.Askari wote hawa wawili hatuwafahamu wala hawatufahamu na wala hatukuwaomba msaada huu walioutoa pia hawakutuomba rushwa na hatukuwapa rushwa. Tulitimua kwa kupitia njia zile kama tulivyoelekezwa na polisi hao tusiowajua na tulifanikiwa kufika nyumbani salama na kupumzika kwa uchovu wa kukesha pale NMC.
Nashindwa kuelewa askari hawa waliopewa order kutukamata wakeshaji hapo NMC inakuwaje wanashiriki kututorosha tena ukizangatia askari hao wametoa msaada huo bila kuombwa wala kulaghaiwa na sisi wakeshaji.
 
Kwa nini serikali ya CCM haitumii busara? Mie nilifikiri yule Shamzi Nahodha ni mtu wa busara kumbe naye ni kama Mapuri tu.
 
Unaoneka hupendi amani na wenzio wapo kulinda watu na mali zao so wamekuonesha njia kwa usalama kabisa hawapo kishari,utii bila shuruti
 
Matukio ya jana na leo katika mji wa Ukombozi wa Arusha umeianika serikali ya CCM bila nguo mbele ya mgeni wao kutoka nchi tunakotembezea bakuli hali nchi yetu ni tajiri.

Kikubwa zaidi yanaonyesha mji huo ni kama vile CCM imekwisha kabisa hali iliyojitokeza tangu uchaguzi wa mwaka jana. Wanachofanya ni kutumia polisi kujaribu eti waonekane CCM bado ipo hapo.

Ni aibu kubwa sana kwa CCM kupoteza mji waliokuwa wanaringa nao wa kitalii na mikutano ya kimataifa.

Serikali ya magamba imejaribu kutumia nguvu kubwa tangu uchaguzi mkuu, uchaguzi wa meya, na hadi sasa lakini wanaArusha wako imara sana.

Ni kweli kabisa mkuu. Hasira zote za magamba ni kutokana na kuupoteza mji huo wa Arusha. Mwezi uliopita nikuwa Arusha kwa siku 5 hivi na kusema kweli sikuona iwapo CCM ipo. Honest -- CCM mmevurunda wenyewe kuupoteza mji.
 
Duu!! kama haya ni kweli!! basi haitajiki cdm kutumia nguvu nyingi kuisumbua serikali! vitendo vyao viovu vinatosha kabisa kuwamaliza mwenyewe!
 
CCM hawajagundua kuwa JK anaiuma chama kwa makusudi, kwasababu 2015 hatakuwa na lake. Ngoja aiongoze nchi mputa kama hana akili.
 
wameshaanza kuelewa somo, kwani unadhani wao rumba la ugumu wa maisha hawalioni, tupo nao huku mtaani wamepigika kinoma.
 
Back
Top Bottom