Aibu hii! Felix Tshisekedi kuzomewa mbele ya Papa Francis ni matokeo mabaya ya utawala wake

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,368
Juzi kwenye Uwanja wa Taifa (Stade des Martyrs) Kinshasa wananchi walimzomea Rais Felix Tshisekedi mbele ya Papa Francis wakiimba nyimbo ambazo zinasema (Fetshi oyebela mandat eseli) wakiwa na maana kuwa Rais Fatshi utawala wako umefika mwisho

Huku UN (umaja wa kimataifa) walitoa kauli kuwa mwaka 2018 Rais Felix hakuchaguliwa na wananchi wake

Papa naye alinukuliwa akisema kuwa hakuja kwasababu ya Siasa ambazo kuna baadhi ya viongozi ambao walipita kwa udanganyifu.

Sasa kosa la Rais wetu kuliko yeye kuonesha wananchi kuwa ana uwezo wa kuongoza nchi afanye vitu vya maana ili wananchi wawe na imani naye yeye muda wake wote alitumia kwa kusafiri tu huku chini ya utawala wake hakuweza kujenga hata barabara moja ya lami zaidi ya kudanganya wananchi wake kwa ahadi za uongo kuwa atafanya Kongo kuwa German ya Afrika halafu anataka tena apewe muhula wa pili.

Hivi kwanini viongozi wengi wa Afrika hawapendagi kuamini kuwa hawana uwezo wa kuongoza nchi kisa fahari tu ya kusifiwa na kuheshimiwa na watu ndo inafanya viongozi wengi wa Afrika kupenda madaraka hata kama hana uwezo wa kuongoza nchi.

Uongozi ni kipaji kutoka kwa Mungu sio kwa binadamu na sifa kubwa ya kiongozi bora anaonekana hata kwenye maendeleo yake binafsi tu.

Huwezi kumpa mtu ambaye hajui pesa zinatafutwa vipi au hajui jinsi gani ya kusimamia familia yake awe kiongozi wa nchi alafu utegee kuwa atakuwa kiongozi mzuri.

Mimi mimi sio mnafiki ninasema ukweli nchi ile apewa katumbi anaweza kuongoza vizuri na yeye mwenyewe Felix kabla hajawa Rais aliwahi nukuliwa akisema nchi hii akipewa Katumbi itaendelea kwanini tunamtenga na kumbagua kisa tu rangi yake, tuache ubaguzi.
 
Tabia ya waafrika kutafuta visingizio kwa umaskini wao ndio itafanya Afrika iendelee kuwa bara kichekesho.

Utawala mbovu na ufisadi uliokubuhu kamwe haiwezi kuiacha Afrika salama na kutafuta visingizio haitaisaidia hili bara.
 
Wao wazomee mpaka wafe. Mheshimiwa anapeta tu kwenye Mercedes
NB: Happy birthday CCM 46th anniversary.
 
Huyu tsesekedi amewahi ongoza nini au fanya nini cha maana, hadi mkampa nafasi hio kubwa.
 
Kuifanya congo kuwa ujerumani, hata mwanamke utongozwa kwa uongo Ili umpate, ukishampata shida ipo wapi. Hakuna mtawala wa kiafrika anaeweza mletea mwafrika maendeleo, kwao uongozi ni ajira na sio wito.
 
Kama ameweza ongoza timu ya mpira na makampuni yake ya madini yakafanya vizuri kwann asiweze
Sio makampuni tu ndugu yangu
Katumbi kipindi akiwa gavana wa Katanga
Aliweza kuongoza katanga vizuri saana
Kama katanga leo kuna barabara za lami kajenga katumbi
Kajenga hospitali nyingi
Kajenga madaraja mengi
Kajenga vitu vingi ndio maana unaona katumbi anapendwa na watu wengi kwasababu waliona alicho kifanya kipindi akiwa gavana
 
Huku UN ( umaja wa kimataifa) walitoa kauli kuwa mwaka 2018 Rais Felix hakuchaguliwa na wananchi wake

Papa naye alinukuliwa akisema kuwa hakuja kwasababu ya Siasa ambazo kuna baadhi ya viongozi ambao walipita kwa udanganyifu
Martin Fayulu ndio alishinda ule uchaguzi ila Kabila akafanya hujuma kumuweka Felix ila mwishowe vyama vyao vilikosana.

Moronight walker Nelson Jacob lushasi
 
Wewe utakuwa FPR maana mkaliwa vibaya mpaka baba yenu mnywa damu za watu juzi nimeona akishuka kwa ndege yake bujumbura anapepesuka sijuhi alikuwa ajapata drip ya walizomchomoa Ntwari Williams.
 
Huwa Naongea na Wacongo wengi tu shida kubwa Ya Congo ni NCHI ZA MABEBERU...China anaiba pale madini..Marekani anaiba pale Ulaya nzima inaiba pale Congo sasa huyu tshekedi atafanya nini kwa miaka 5 tu?>?? Joseph Kabila alikaa miaka 18 tufanye kama angekua anajenga Km 4000 za barabara Kila Mwaka nchi ingekua mbali sana...Wizi ni mkubwa kutoka kwa mabeberu wanafadhili vita zile kila mwaka...
 
Back
Top Bottom