Ahsante Wabunge Wa CCM, Ahsante JF!

Haya majina lazima yarudishwe na kupitishwa na cc yao; sasa kama ameanza sherehe kabla ya kutangazwa rasmi wanaweza kukata jina lake, irrespective of his surname!! Hiyo ndio mizengwe ya Magamba, lakini kwa vile baba yake wamemtesa sana watamuhurumia lakini angekuwa mtoto wa kabwela hiyo ilikuwa sababu tosha ya kumkata na wao kuweka mtu wanaemtaka. Huwa hawakosi sababu kupata wanachotaka hawa magamba.
 
Congats William,stay focused kusimama kidete kwenye kulinda interest za nchi ya tz (ndiyo tz,maana unaweza kuwa na uraia wa nchi mbili) na si za chama cha magamba.HONGERA MH.mtarajiwa WJM.
 
- Wakuu JF, heshima mbele sana ndugu zangu leo kwa mara nyingine tena tumepita kuelekea mwisho wa Safari ya mbio zetu za Ubunge wa EAC, we are almost there jamani bado kidogo sana, twende kwa mbele sasa I mean mwendo mdundo jamani twende kwa mbele!

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA, NA MUNGU AIBARIKI JF KUMKOMA NYANI!

William.

mbona wewe mbaguzi? Tena mapema kabisa! Unawashukuru tu wana ccm wenzako, why? Halafu una generalize huku jf. Mbona hujashukuru jf ccm? Si wanajulikana? Badili kwanza taito mkuu maana hata ukiipata hiyo post, huendi kuwatumikia ccm na jf tu
 
Hongera. Huu ubunge uwe maandalizi ya kulikomboa jimbo la Mtera na kumuondoa kichaa ndani ya bunge
 
Mkuu Willy once again, Congrats.

Kwa kweli sikudhani kama hao watu wenye makundi watakupitisha hizi hatua mbili za mwanzo. Sababu umefanikiwa kupita, kuwa macho sana, and YOU NEED TO CONSOLIDATE votes scientifically now. Usijipe nafasi kabisa ya kurelax, maana kuna watu wana hasira na yaliyotokea juzi, wanaweza kudhani success yako itareflect change in CCM, anyways najua unaelewa.

WANA JF, na ikiwezekana CHADEMA tumpe Willy support 100%, sababu kwa upande wa magamba, huyu ni way way better kwenye kututetea huko mbleleni kwenye EAC, sababu kwanza exposure yake ni ASSET na hawezi kubabaika na wabunge kutoka especially Kenya. Yuko accountable huku kwetu JF, na isiwe wakati wa kumpinga now, sababu who is better than WILLY kwenye hiyo list iliyopo?? Tusimpime kutokana na PERFECT Candidate criteria, No, tufanye comparison na hao wenzake wa CCM walioko kwenye hiyo hatua ya mwisho.

All the best Mkuu, na pse usiache angle yoyote open maana unajua tena kuna wale maadui Permanent.

Mhh!! kama kawaida ya magamba, watakuwa wameangalia tu sura ya mtu, jina na bila kufikiria umuhimu wa nafasi hizo kwa taifa letu, nakuhakikisia nafasi hii wanaweza kuwa wameacha vichwa vya maana kabisa ili kumpoza mtu, kama walivyofanya Arumeru, yaani mijitu haingalii maslahi ya taifa letu kabisa. Naamini kabisa kuna watu wazuri kabisa amabao wangeweza kutoa mchango muhimu kwa maslahi ya taifa letu huko EAC wanaweza kuachwa ili tukajaribu mtu, eti atajifunza kama alivyosema memba mmoja hapo juu.
 
umeanza dharau kabla hata hujaupata huo ubunge.Km ulijua unataka kupumzika kwa nini umeleta mada usiku huu? Si ungelala ukaja asubuhi?Jibu hoja hapa acha dharau za mapema!

Rugas,
Jamaa kasema kweli kachoka sidhani kama dharau, mpe muda kasema atarudi baadae.
 
Mi ninakuomba usije ukapata ubunge halafu ukajifunza matusi, maana nasikia mmfungua chuo cha matusi na Chancellor wake ni Lusinde na VC wake ni Mwigulu, sijui watakupatia cheo gani, chunga sana!!!!!!
 
As long as ni kwa tiketi ya magamba, sikupi sapoti. Inawezekana umeipata nafasi kama alivyopata Sioi, au ili chama kipate member wa jf maana Chiligati alikiri ni mtandao hatari kwa ccm! Vyovyote vile, sikupi sapoti maana naamini hakuna kiongozi anayeweza kufanya vizuri linapoja swala la maslahi ya taifa akiwa ccm! Waangalie akina Sitta, Mwakyembe! Jiulize alipo Aloyce Kimaro. Kukusapoti kwa kuwa tu ni member "mwenzetu" hapa jf ni upuuzi mtupu! Inawezekana huijui hata mtera. Unaishi marekani halafu unataka kuja kutetea maslahi yetu eac! Maslahi tunayajua sisi tuliopo huku siku zote au wewe uliyeona ukatafute maisha NY! Hao waliokupitisha nao hawana maono maana huitaji kufikiri sana kuhusu hilo! Wameshindwa kujifunza somo la haraka kwamba pamoja na mambo mengine Sioi ameshindwa sababu haishi Arumeru!? Kweli ccm sikio la kufa!
Yeyote wa ccm ashindwe na akafie mbali maana wanazidi kutucheleweshea mageuzi, ukombozi na maendeleo ya haraka nchini mwetu!
 
Huyu Mtu mbona alipokuwa anaomba support alikuwa anajibu kila comment? eti leo amechoka...kisa tu umeona kimwanga fulani kuwa huenda mambo yatakuwa mazuri...ukiupata huo ubunge si ndo utapata sababu tosha kuwa Upo Busy......Dalili za dharau umezianza mapema sana.....!!!
 
Back
Top Bottom