Ahsante mume wangu kwa kuachana na mchepuko

Hahahaaa wanaume wapi hao !
Hapo anakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa
Siku akikumbuka kiuno kama cha wacheza shoo wa Twanga pepeta
Anamtxt tu baby am back...huyu fala nimeshamtuliza njoo tujilie mema ya nchi...
Nyumba ndogo hawanaga hiyana
Kweli Mkuu, hapo yeye amuombee tu mumewe ili MUNGU amnusuru na kadhia ya Nyumba ndogo na pia awaepushie Maradhi.
 
Mkuu , naomba tu nikushauri kuwa ( Usitukane Mamba kable hujavuka Mto;) Kwa unavyoongea ndoa yako bado mbich na Changa kikubwa jiangalie pale ulipokuwa na mapungufu yaliyopelekea yeye kuwa na Mchepuko upajaze na pajazike hasa ili iwe kweli ametoka moja kwa Moja... Kumbuka Mwanamke akimtaka mwanaume hashindwi kwa hiyo ukianza kuleta vijembe mapema huwezi jua Mbinu Mpya.. Kingine kumbuka hakuna Mwanaume Mjanja mbele ya mwanamke yeyote Duniani. Kwa hiyo Maadamu umeona anaelekea kujutia Makosa yake kisiwe kigezo cha Kuwadhihaki Nyumba Ndogo au Mchepuko?

Kikubwa ungejiuliza Kwa nini alikuwa na Huyo Mchepuko ? Walikutanaje? Kitu Gani kilichomvutia kwa huyo unayemuita Mchepuko? Kwa Hiyo Ugomvi wao ni Kwa kuwa anamuomba hela ya Matumizi? Je kama asingekuwa anamuomba ungejua? Unajuaje hizo status za Whatsapp nizakukuhadaa wewe usiendelee kumfuatilia?

Mama narudia Usitukane Mamba kabla hujavuka Mto.. Hakuna Kiumbe cha kuwa nacho kwa Uangalifu Kama hawa Viumbe ambao ni Zao za Mbavu za Mwanaume.

Ni hayo tu, Kuna wengine wanasema Tema Mate Chini.. Hayo yote ni Maneno ya Wahenga ambayo ya Maana Kubwa sana..

Ni hayo tu Mkuu Nakutakia Ijumaa Njema....
Alafu ukute hajasave number za mchepuko kwahiyo mchepuko wenyewe hauoni hyo status....kazi kweli kweli anapigwa changa la macho
 
Kinachonifurahishaga na kunipa raha ni pale wanaume wanaposema kuwa eti mpaka nimekuoa ujue nakupenda kuchepuka ni kutamani tu.
Kwani wanawake nao hawatamani,Mimi mpaka kukubali kuolewa na wewe ujue ninakupenda michepuko ni tamaa tu
 
Habari zenu wadau,

Wiki kama tatu zilizopita tulikuwa na mgogoro na mme wangu kuhusu kuwa na nyumba ndogo. Katika uchunguzi wangu nikagundua ni single mother. Alikuwa anajitahidi sn kumbembeleza mume wangu ili ampatie mahitaji mbalimbali kama kodi na ada ya mtoto wake.

So baada ya mie kugundua na kugombana na mme wangu (hapa niseme kujadiliana sijamtukana) kugombana kwa hekima, mume wangu alinibembeleza sana sio kwa kukiri moja kwa moja (wanaume hawaombi msamaha direct) akanishukuru kwa kumlinda na kanihakikishia mimi ndio chaguo la moyo wake kama ambavyo ameapa mbele ya Mungu.

Sasa basi huwa nafatilia status yake watsapp nikakuta anasikitikia mapenzi yamekufa. Akaja kuweka nyingine anasikitikia kuwa "mme wa mtu atakuchezea, atakugeuza na atafanya anavyotaka kisha atarudi kwa mkewe".Nilichogundua ni kuwa mume wangu kaachana na mchepuko wake.

Jamani michepuko mkiachwa msilalamike sana kwa kuwa nyinyi ni viburudisho tu, na ukimpata mume wa mtu usijione kuwa wewe ni zaidi sana ya mkewe.

NDOA NA IHESHIMIWE
Hongera ila wanaume naona huko kwenye michepuka huwa tunafanya mazoezi tu mechi kwa mkeo na wala hawakaagi moyoni.
 
Back
Top Bottom