Afrika Kusini: Mchungaji Alph N Lukau afufua maiti na kuacha gumzo kubwa

Kwani shida ni kufufua mtu ama ? mbona maandiko yameweka wazi kwamba waamin wanaweza kufufua,MATHAYO 10:8,me nafikiri wakristo wasio amini kwamba mtu anaweza kufufuliwa ndio wa kuwaashangaa .
 
Hata kama ndio kutafuta pesa sio kwa dizaini hizi,.hawa manabii fake nadhani moto wao haujazimuliwa hata mara moja...shenzy zao mfyuuu!😏😏!!!
Unatumia kigezo ghani dada kuwaita feki ? wewe mwenyewe ulishashuhudia wakifanya mambo kwa ufeki ? au unasikiliza maoni ya watu ?
 
Hili jambo limewatia aibu karibu walokole wote duniani

View attachment 1032982

Bila shaka walokole wa Tanzania mna cha kujifunza
Tangia waujue wokovu walishatahadharishwa hayo ya kwamba zipo nyakati watumishi wa namn fulani watajitokeza . Ni watu wa mataifa ndiyo mambo hayo ni mageni kwao . Ila waamini wa kweli wa Yesu Kristo wanaijua dunia na mienendo yake (mabadiliko kulingana na wakati ) zaidi ya uwadhahaniavyo . HURUMA YAO NI KWENU NINYI AMBAE MUNGU WA DUNIA HII KAPOFUSHA MACHO YENU .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uislam hakuna cha nidhamu ya uoga wala hakuna mtu au sheikh au yeyote aliye juu ya mwenzake.Muislam anasali popote pale hategemei mtu kufikisha maombi yake kwa Mungu
FaizaFoxy
THE BIG SHOW
Ritz
Hata kwa Wakristo wanatakiwa kuomba wenyewe kwa Mungu. Hii mambo ya kuombewa inatuingiza mkenge sana. Watu wamejipa vyeo vya kuombea wengine.
1timotheo 2:5-6''Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;
6 ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake''
Mpatanishi ni mmoja
 
Bado wapo na Mungu anaendelea kuwatumia (Kwanini na wewe usitumike)

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajidanganya rafiki.
Yeremia 17:5''Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana''
Yesu anasema ombeni mtapewa, bisheni mtafunguliwa. Tatizo binadamu wenzetu wamejifanya wana uenyeji mbinguni na sisi wengine ni wageni. Jiulize wao uenyeji wameupata wapi na sisi tumeshindwa kuupata huo uenyeji . Wakristo mwenyeji wetu ni Yesu na tunapaswa kumuomba.
Usiwe mwepesi wa kumuamini mwanadamu.
Utakuta mtu anamuomba bikra Maria amuombee, huo ni upotofu , au unaenda kutubu kwa kiongozi wako ambaye naye ana madhambi yake ya kunajisi watoto na wajane.
Tujifunze kutegemea neon la Mungu
 
Ukimjua Mungu vizuri huwezi babaishwa na maigizo ya watu kwa kigezo cha dini. Mungu hufanya kitu ili utukufu apewe yeye na si apewe mwanadamu ila ukianglia watenda miujiza wa siku hizi wanafanya maigizo huku makamera yamejaa ili ulimwengu uwakubali kuwa wanaweza na kwa njia hiyo wajipatie waumini wengi na sadaka ziongezeke. Mungu muumbaji hawezi kufanya maigizo ya aina hii labda kama wana mungu wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom