Afrika Kusini: Mchungaji Alph N Lukau afufua maiti na kuacha gumzo kubwa

Kama hatutasoma maneno ya Mungu wenyewe na kumuomba roho mtakatifu msaada hakuna namna ni ni kupotea maneno ya Mungu yanasema ijaribuni kila roho mpate kujua kama ni ya Mungu au shetani Badilisha maisha yako soma sana neno na sali sana Mungu atakuongoza ila ukiwa na nguvu za roho mtakatifu unaweza ukafufua wafu hata wewe maana nguvu iliyomfufua Yesu kristo inakaa moyoni mwako lakini hujui njinsi ya kuitumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo sio wanaodanganya. Tatizo ni watu kupenda kudanganywa.

Kizazi hiki alikiona nabii Yeremia.
'' Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake? '' Yeremia 5:31.

Haya unayoona ni rasharasha tu, yajayo yatakufurahisha.
Wajanja wamerudi kwenye kusoma Bibilia wenyewe na kutii maagizo yake, sio kusikiliza Manabii mabarabarani.
 
Ukristo wenyewe ni biashara ya wajanja tu. Mambo kuzidiana.

Hata ubora wa Wakristo ni kwa mali si kwa ucha Mungu.
Wekeza muda wako mwingi katika kuijua vyema imani yako..Ukristo sio biashara ila wapo wanaotumia ukristo kutapeli wenzao. Tujaribu kuvumiliana katika imani zetu kwani siku zetu ni chache kabisa. Jifunze yasiyofunza nawe utakuwa mstaarabu zaidi.
 
Hivi kwanza mtu unajuaje kama huyu ni nabii ?

Pili,unawezaje kutofautisha kati ya miujiza,mazingaombwe na kiini macho ?
 
Kumbe marehemu huyu aliyefufuliwa juzi alishawahi kuwa cameraman kwenye show nyingine Ambayo pastor huyu alimfufua huyu mama...
Screenshot_20190226-145020.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom