ada za udsm postgraduate na masters zapaa juu maradufu!

abc2

New Member
Jul 23, 2013
4
0
Kwa waliopata admissions za hizo post ada imepanda zaidi ya nusu ya iliyokuwepo kwa sasa post graduate ni 4400000 kwa mwaka na masters ni 8000000! Kaazi kweli!
 
Mkuu nimepata admission letter leo nasikia kijasho chembamba. Hivi hawa jamaa wanawaza nini? Milioni 8.5 bila sponsor mtu unazitoa wapi? Halafu kudai 50,000 ya application wakati tushatoa 20,000 wakati wa kurudisha form si uhuni kabisa huu?
 
Ada ndogo sana hiyo. Watanzania jifunzeni kuthamini elimu.

Mtu unaona mil 8 ni ada kubwa wakati harusi yako imegharimu mil. 15 na unaendesha gari la sh. mil 12!
 
Kwani chuo ni UD peke yake jamani, acheni kulalama

Awali Mlimani ndio ilikuwa the cheapest. Inavyoonekana ada zimepanda across. Hakuna aliyesema hapa ndio bora kuliko kwingine. Tunazungumzia kupanda kwa fee.
 
Kwani
chuo ni UD peke yake jamani, acheni kulalama

mkuu kumbuka hiki ni chuo cha umma,watu wengi tunategemea ada iwe nafuu
ili wenye uwezo kielimu wamudu gharama,kama hawa ni hv je vyuo binafsi
wasemeje ukizingatia tunakichangia kupitia kodi zetu na hvi vya binafsi havipati ruzuku ya serikali,kweli tutasoma kweli mkuu??
 
Aisee nitakoma mbona, nimepa admission ya Msc.Renewable energy engineering, kiasi nilichoandaa kuisoma ni kidogo, sasa kama kweli imepanda itabidi nichukue ustaarabu mwingine.
 
Aisee nitakoma mbona, nimepata admission ya Msc.Renewable energy engineering hapo Coet, kiasi nilichoandaa kuisoma ni kidogo, sasa kama kweli imepanda itabidi nichukue ustaarabu mwingine.
 
Mbona sijaelewa, tufafanulie kwa Kiswahili postgraduate ni ipi na masters ni ipi. Nadhani sijajua methali za kiinglish.

kiswahili ndio kigumu zaidi, MASTERS ni SHAHADA ya pili wakati POSTGRADUATE ni STASHAHADA YA UZAMILI.
 
kiswahili ndio kigumu zaidi, MASTERS ni SHAHADA ya pili wakati POSTGRADUATE ni STASHAHADA YA UZAMILI.

Duh mkuu ukisema shahada ya uzamili ndo MASTERS yenyewe unaposema post graduate una maana shahada yoyote ya juu baada ya shahada ya kwanza inaweza kua post graduate diploma, masters au PhD ( Shahada ya Uzamivu ) labda wasomi wengine watatusaidia pia.
 
kiswahili ndio kigumu zaidi, MASTERS ni SHAHADA ya pili wakati POSTGRADUATE ni STASHAHADA YA UZAMILI.

Masters = Shahada ya Uzamili. PGD = Stashahada ya Uzamili.
Postgraduate = Masomo baada ya kupata Shahada.
 
Aisee nitakoma mbona, nimepata admission ya Msc.Renewable energy engineering hapo Coet, kiasi nilichoandaa kuisoma ni kidogo, sasa kama kweli imepanda itabidi nichukue ustaarabu mwingine.

Mkuu cheki ustaarabu wa ufadhili. Leave no room for despair.
 
Huo ni mkakati wa kupunguza wasomi wa elimu ya juu.hii c elimu ya wote ni kwa wachache tena wenye uwezo wa kifedha na c kiakili.
 
mkuu kumbuka hiki ni chuo cha umma,watu wengi tunategemea ada iwe nafuu
ili wenye uwezo kielimu wamudu gharama,kama hawa ni hv je vyuo binafsi
wasemeje ukizingatia tunakichangia kupitia kodi zetu na hvi vya binafsi havipati ruzuku ya serikali,kweli tutasoma kweli mkuu??
Kwa taarifa yako UD hawajawai kutoa ada za master na PHD kufuatana na km chuo cha umma, wanatoa undergraduate kama chuo cha umma lakini level zingine wanasema ni anasa ndiyo maana wanawakamua sana wanalalahoi.Nenda Mzumbe vodafasta so long as master zao zinatambuliwa hahahaha
 
Sina mpango wa kurudi pale tena;Hyo bacheror tu inanitosha wameshanikomesha sana wale jamaa;hapa bongo kwan hamna chuo kinatoa masters ya HR????? Ntaenda huko huko
 
Back
Top Bottom