ACT, Zitto Kabwe na Chadema

zig_charlzy

Member
Jul 24, 2014
92
23
Mi nasikia sikia tu, Zitto, Zitto, ACT, ACT, wasaliti ,wasaliti, CHADEMA CHADEMA, wabinafsi wabinafsi hebu nielezeni hii movie vizurii, mim na Watanzania wenzangu tuweze kuelewa vizuri tujue wapi pa kushika, wapi pa kuacha.
 
Swali zuri!majibu musharabu!!utamu wa kitu ukionje.Utamu wa yule mbunge wetu Joyce anaujua Mbowe,alifuatilia akaupata.Sasa nawe jitahid kufuatilia na kukudadavua utajua habari za ACT,Chadema na Zitto
 
Viongozi wa chadema wanamgwaya huyo kijana, kwahiyo wanajaribu kumpoteza katika siasa, lakini inaonekana wameshindwa.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Sasa kaka mgomyaa si ungenijibu huku huku wa tz nao wapate faida!? ananitumia sms anasema hivi
"Hii movie ina pande mbili.
1.WASALITI
huku jambaz mkuu ni zitto,na mugimba na stalling ni dr.silaa na mbowe
2.WABINAFSI
huku jambaz mkuu ni mbowe na slaa na stalling ni zitto na wenzie"
3.WENYE PESA ZAO
Stalling ni mbowe na slaa
Jambaz ni zitto……eti si unakumbuka watu waliojikopesha na wanajilipa kwa riba waipendayo.
4.WANYONGE
Jambaz ni slaa na mbowe stalling zitto ……… wanaonekana wasaliti wameamua kuanza upya na ACT yao.
Unajua kali kuliko yotee!!!??
kuna mjanja mmoja ambay ki sheria mahakaman ni mwanachama wa CHADEMA na inasemekana ndo mwenyekiti wa ACT…………"
………MOVIE haijaisha KAFULILA NAE ETI YUMO NDANI……,, MACHALI NAE DAAAH
AMA KWELI SIASA MCHEZO ……………!!
 
ACT-Tanzania inaamini katika elimu, uadilifu, kujitegemea na bidii katika kazi kama njia kuu ya kujikomboa dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi. Hii ndio misingi iliyoasisi Taifa la Tanzania. Hivyo basi falsafa ya ACT Tanzania ni UNYERERE, ikiwa ni ishara ya dhamira ya kurudisha na kuhuisha misingi iliyoasisi taifa la Tanzania. Kiitikadi ACT Tanzania imejikita katika MRENGO WA KATI KUSHOTO (Center Left Party) na itasimamia Demokrasia Jamii kama dira ya sera za maendeleo ya uchumi nchini Tanzania.

1.4.2MISINGI YA CHAMA
Uzalendo
Ili wananchi waweze kushiriki katika utumishi wa umma na kutoa michango yao mbalimbali kwa dhati na kwa moyo, ni muhimu mazingira yawepo ya kuhakikisha kwamba wananchi wanakuwa na mapenzi yasiyotikisika kwa nchi yao. Kwa msingi huu, ACT-Tanzania itajenga mazingira mwafaka ya wananchi kuipenda nchi yao ili wajitoe kikamilifu katika kuijenga na kuilinda.
Usawa
ACT-Tanzania inaamini katika usawa katika nyanja zote. Tunaamini kwamba mafanikio ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla yatatokana na bidii katika kazi. Kwahiyo, ACT Tanzania kitapigania kuwepo usawa wa fursa na mazingira mazuri kwa watu wote katika kuhakikisha kwamba kila mtu na kila kundi katika jamii linakuwa na fursa sawa ya kufanya kazi za kujiajiri au kuajiriwa, na kwamba kipato kitokanacho na kazi halali ndicho kitakuwa kipimo cha mchango wake katika jamii na taifa.
Uadilifu
Uadilifu katika maisha binafsi na katika jamii utakuwa ndio msingi na mwongozo mkuu wa viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania. ACT-Tanzania inaamini kwamba uadilifu ndio msingi na nguzo kuu ya mapambano dhidi ya rushwa na maovu mengine katika jamii. Kama wanachama wa ACT-Tanzania tutajitahidi wakati wote kutumikia na kuishi kwa uadilifu uliotukuka siyo tu kama taasisi bali pia katika maisha yetu binafsi.


Uwazi
ACT Tanzania inaamini katika uwazi kwenye mambo yote ya kijamii na kitaifa. Hivyo basi viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania wana wajibu wa kupigania uwazi katika mambo yote wanayofanya kwa ajili ya umma. Uwazi huu ni msingi wa kupambana na vitendo vya ukosefu wa maadili na ufisadi na hivyo tunaamini njia sahihi ni kuhakikisha kuwa wanachama na wananchi waliotupa dhamana ya uongozi wanajua yanayofanywa na chama na serikali yao.
Uwajibikaji
Sambamba na uwazi, ACT- Tanzania inaamini kwamba kila mwananchi na kiongozi mwenye dhamana katika umma ana wajibu katika jamii na Taifa kwa ujumla na ni jukumu lake kutekeleza wajibu huo bila kinyongo. Aidha, mwanachama na kiongozi atokanaye na ACT Tanzania anapaswa kuwajibika kwa maneno na matendo yake katika utumishi au nje ya utumishi wa chama au taasisi yeyote ya umma.
Demokrasia Raslimali
ACT-Tanzania inaamini kuwa demokrasia ndiyo msingi wa kujenga fikra pevu na kueneza uhuru wa mtu, jamii na Taifa kwa ujumla. Hivyo basi, viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania watapigania uwepo wa demokrasia ya kweli katika kila ngazi, ndani na nje ya chama. Hata hivyo, ACT Tanzania inaamini kwamba umaskini na ufukara ni kikwazo kikubwa katika kufikia fikra huru. ACT Tanzania inaamini kwamba wananchi kuwa na sauti katika umiliki na uendeshaji wa raslimali za Taifa ndio njia sahihi na ya haraka ya kumaliza umaskini. Chama kinaamini katika demokrasia raslimali ikiwa ni imani kuwa utajiri wa Maliasili ya Afrika kwa ujumla na Tanzania hususani; ni lazima utumike kwa maendeleo ya watu wa Afrika na Tanzania. Hivyo basi, sera za chama zitaelekeza mfumo wa umiliki wa utajiri wa Nchi kuwa ni mali ya wananchi na uendelezwaji wake utafanywa kwa faida ya wananchi kwa ruhusa yao, yaani demokrasia raslimali.
Haki ya Kupata Hifadhi ya Jamii
Chama cha ACT - Tanzania kinaamini kuwa kila mtanzania ana haki ya kupata hifadhi ya jamii na hivyo sera zake zitaelekeza serikali kuwajibika katika kutoa haki hii kikatiba. Hifadhi ya jamii ni pamoja na pensheni, bima ya afya, ulinzi wa kijamii kwa wazee, watu wenye ulemavu na wananchi waliofukarishwa na mfumo wa uchumi wa kibeberu.

Utu
ACT-Tanzania inaamini kuwa sera, mipango na shughuli zozote za kichama au za kiserikali zitakuwa hazina mafanikio ya kudumu kama hazitatambua, kuheshimu na kulinda utu wa kila Mtanzania. Ni kwa sababu hiyo tunu kuu itakayotuongoza katika utumishi wa umma ni kuheshimu, kutambua na kulinda utu wa kila mtu bila kujali tofauti zozote ambazo zinawatofautisha watu.
Umoja wa Afrika
Chama cha ACT - Tanzania kinaamini katika umoja wa bara la Afrika na itikadi ya umajumui wa Afrika. Sera za chama zitajengwa katika kuelekeza nchi yetu inachukua uongozi katika kujenga Shirikisho la Afrika Mashariki kama msingi wa kujenga Afrika moja imara na yenye sauti kwenye mataifa ya ulimwengu.
Kujitegemea, Bidii na Weledi katika Kazi
ACT Tanzania inaamini kwamba kujitegemea, bidii na weledi katika kazi ndiyo njia pekee ya kujipatia maendeleo. Hivyo basi wajibu mkuu wa mwanachama wa ACT Tanzania utakuwa ni: BIDII NA WELEDI KATIKA KAZI.
 
Vyovyoye iyakavokuwa,mimi ninaimani kubwa sana na ZITTO KABWE(kwa sasa). Aende ACT,TADEA au kokoye kule,of course me sitamfuata(labda ikibidi). Lakini ninaimani kubwa katika yeye.
 
Back
Top Bottom