Abiria washushwa kwenye ndege ya precision air

namaanisha kuna abiria wameachwa kisa over booking wakiwa wamekata tkt kama group ndipo wenzao waliotanguliwa wakapigiwa simu akuna kuonddoka wasimame kwenye ndege washuke..mkojo ukawabana ndugu zetu..manager nona amekula matusi ya kutosha..akika aaka kamchezo mnaitajji kuacha wote wa airline kama ndege imejaa unaachia wanauza ya nini???kilichofanyika kuna watu ambao awakuwa na tkt ya ok wakaingizwa mwanzoni kivip m na wewe sijui..yawezekana kuna mtu doller zitamtokea puani leo...naona wameamua kuwapeleka kwenye vi chata kule term 1..polen sana ndio ukubwa precissionair

Mmmh! Kunywa maji bro mbona mbio mbio sana? utavunja keyboard.... hatukuelewi!!
 
ujumbe umefika pdidi. Ila kibarua cha kutaka kujua kiswahili unacho bandungu
 
Unaweza hisi ni vituko lakini ndicho kinaendelea hivi sasa tatizo la ku overbook abiria linazidi kuwameza precissionair pale group la watu 48 liilipokata tkt na kuhakikishiwa safari ya Zanzibar matokeo yake leo wamekuta watu kadhaa wamepewa boarding pass ambao hawakuwepo kwenye list

Hivi sasa abiria 6 wamebaki walichoafanya ni kuwaambia wenzao sita wasimame na kushuka chini kwa habari zaidi tunaendelea kuwapa

Hili liwe fundisho kwa wenye tamaa kama hawa muweke wale waliolipa kwanza kunatabia cha hapa airport wafanyaakazi kupewa hela na kuchukua abiria tena wakisapotiwa na viongozi wao wa juu hili linafanya kutokuwa na maana ya kuwahi kufanya booking kwa nini wasifanye kama kalula air south mnakatia airport kabisa

Tunaitaji kuwepo na mashirika mengi ili urasimu kama huu uishe daima

Nadhani Pdidy anataka kuwasilisha kisa ambacho na mimi kilinitokea last week. Nilikuwa naelekea Mza na Ndege ya PA. Departure ilikuwa ni Saa 11.15 jioni. Tukiwa kwenye mstari (tumepita checking point) na tukiwa tumebaki abiria 4 majira ya Saa 10.30, mwenzetu aliyekuwa mbele yetu akionesha ticketi kwa wale mabinti wa PA akaambiwa amechelewa na ndege imeshaondoka na ujumbe ukaja kwa abiria wote waliobaki. Tulijaribu ku-struggle lakini haikuwezekana na ikabidi tupewe safari ya siku ya tatu yake tena kupitia KIA na tukalipa sh.20,000 kwa ajili ya non-show up. Tulichogundua baadaye ambacho nadhani Pdidy anasisitiza ni kwamba kuna abiria ambao hawakuwemo kwenye orodha ya kusafiri na ndege hiyo ambao waliwahi na kupewa nafasi. Kuna kitu ambacho wale mabinti walisema ambacho nilikuwa nakitafakari. Walisema kwamba ndege inaweza kuondoka wakati wowote hata kabla ya muda ulioandikwa kufika. Wakasisitiza kuwa cha muhimu ni kuwahi saa 2 kabla ya departure time. Hata hivyo, nikajiuliza kama abiria wote watafika saa 2 kabla ya muda wa ndege kuondoka, wataingia kwa wakati mmoja wote kwa pamoja? Mimi nilipata damage sana
1. Ilibidi nikae Hotelini Siku mbili zaidi
2. Nilikuwa nimeshaagiza gari toka Musoma ije ini-pick mwanza, ikabidi dereva alale siku mbili kunisubiri
3. Na karaha nyingine kadha wa kadha.
Kwa hiyo kama kuwa wengine wamekumbwa na mkasa huo basi nadhani kuna tatizo hapo
 
Huyu atakuwa Mnya Rwanda!

Sasa kama hajui kuandika Kiswahili anaandika nini hapa? Kwa kweli wachangiaji ndo mmeniua kuliko hata huyu bwana aliyetuleta hii taarifa, Mbavu sina!! Maana jamaa amejaribu kurudia ni yale yale tu yaani madudu ni mwisho sijapata kuona!! Nina mashaka na kisomo chake utafikiri jamaa katoka Ngumbaru?
 
Nadhani Pdidy anataka kuwasilisha kisa ambacho na mimi kilinitokea last week. Nilikuwa naelekea Mza na Ndege ya PA. Departure ilikuwa ni Saa 11.15 jioni. Tukiwa kwenye mstari (tumepita checking point) na tukiwa tumebaki abiria 4 majira ya Saa 10.30, mwenzetu aliyekuwa mbele yetu akionesha ticketi kwa wale mabinti wa PA akaambiwa amechelewa na ndege imeshaondoka na ujumbe ukaja kwa abiria wote waliobaki. Tulijaribu ku-struggle lakini haikuwezekana na ikabidi tupewe safari ya siku ya tatu yake tena kupitia KIA na tukalipa sh.20,000 kwa ajili ya non-show up. Tulichogundua baadaye ambacho nadhani Pdidy anasisitiza ni kwamba kuna abiria ambao hawakuwemo kwenye orodha ya kusafiri na ndege hiyo ambao waliwahi na kupewa nafasi. Kuna kitu ambacho wale mabinti walisema ambacho nilikuwa nakitafakari. Walisema kwamba ndege inaweza kuondoka wakati wowote hata kabla ya muda ulioandikwa kufika. Wakasisitiza kuwa cha muhimu ni kuwahi saa 2 kabla ya departure time. Hata hivyo, nikajiuliza kama abiria wote watafika saa 2 kabla ya muda wa ndege kuondoka, wataingia kwa wakati mmoja wote kwa pamoja? Mimi nilipata damage sana
1. Ilibidi nikae Hotelini Siku mbili zaidi
2. Nilikuwa nimeshaagiza gari toka Musoma ije ini-pick mwanza, ikabidi dereva alale siku mbili kunisubiri
3. Na karaha nyingine kadha wa kadha.
Kwa hiyo kama kuwa wengine wamekumbwa na mkasa huo basi nadhani kuna tatizo hapo

Ndege zetu ni taabu tupu yaani utaratibu hakuna kabisa utafikiri wanafanya kazi kwa kubahatisha. Na wewe mkuu kwa nini uagize gari kutoka Musoma si ungepanda bus tu kwenda Musoma mbona barabara ni nzuri tu? Hauoni kuwa huu ndo ufisadi tunaoupigia kelele kila siku tukiwalalamikia Mawaziri wetu wanapoagiza magari yawafuate?
 
presisheni.... mlichowafanyia ATC sasa kinawageuka......it will fire back to you
 
presisheni.... mlichowafanyia ATC sasa kinawageuka......it will fire back to you

umeonaaaa eeeehhhhhh na bado 540 wanakuja na DAR KIGOMA WIKI IJAYO
WACHA APRIL 15 JET LINK KUTOKA KENYA WANAKUJA NA DAR MWANZA,,KIGOMA,JRO BEI YA KUMWAGA
 
sasa kama hajui kuandika kiswahili anaandika nini hapa? Kwa kweli wachangiaji ndo mmeniua kuliko hata huyu bwana aliyetuleta hii taarifa, mbavu sina!! Maana jamaa amejaribu kurudia ni yale yale tu yaani madudu ni mwisho sijapata kuona!! Nina mashaka na kisomo chake utafikiri jamaa katoka ngumbaru?

katoa nyingine mpya leo kuhusu madiwani wa kimara vs manispaa ya kndoni . Nayo ni broken hii cha mtoto,mwisho asema afadhali arudi burundi!!!!! May be ni wakuja.
 
Back
Top Bottom