Victor: Niliwatoa Watu kwenye Ndege na Wavuvi walinisaidia kuwapakia kwenye Mitumbwi ajali ya Precision Air. Amsifu mhudumu wa ndege kufungua mlango

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,035
Abiria aliyenusurika kwenye ajali ya Precision Air iliyozama anasema yeye ndio alikuwa wa pili kutoka baada ya Muhudumu wa Ndege kufanikiwa kufungua mlango

Victor anasema alipotoka nje aliona wavuvi Wanne kwa mbali wanakuja na mtumbwi na walipomfikia yeye alianza kuwavuta abiria akiwa pale mlangoni na Wavuvi waliowapokea na kuwaingiza kwenye Mitumbwi

Victor anasema alishiriki zoezi la uokoaji kwa zaidi ya Saa 1 kabla hajaenda nchi kavu ambako alikaa hadi jioni lakini hakupenda ajulikane kama naye ni abiria manusura

Ameeleza mengi nikifanikiwa nitaweka clip hapa
Source Ayo tv

Sabato njema!

=========

WASIFU
Victor Laurian ni manusura kwenye ajali ya ndege ya Precision iliyotokea Bukoba mkoani Kagera na kuua watu 19. Victor ni mzaliwa wa Kagera, kitaaluma ni injinia na anafanya kazi kampuni ya ujenzi ya Esteem Construction LTD.

KWENDA KAGERA
Victor amesema alikuwa anaenda Kagera akitokea Dar kuendelea na majukumu ya kikazi, kampuni yao ya Esteem ina mradi kwenye kiwanda cha uzalishaji sukari cha Kagera Sugar. Victor anasema mke wake alimuomba aondoke Jumatatu lakini walijaribu kubadili tiketi ikashindikana na kusafiri Jumapili.

SAFARI
Victor anasema walisafiri salama mpaka Bukoba na kufika saa 2:20 asubuhi. Rubani alitangaza wameshafika Bukoba lakini hawataweza kutua, ataangalia mazingira na ikishindikana watarudi Mwanza, alipopata taarifa Victor alimtumia ujumbe mfupi mkewe.

AJALI
Victor anasema baada ya muda ndege ililala upande wa kushoto na kutumbukia kwenye maji na maji yalianza kuingia kwenye ndege muda huohuo ilipozama ndani ya maji na alijaribu kuinuka mara tatu akashindwa lakini baadae aliweza kuona mkanda na kuufungua.

UOKOZI
Victor anasema alienda nyuma na kuuona mlango lakini alipojaribu kuufungua alishindwa na maji yalianza kujaa kwenye eneo hilo pia, Victor alipiga kelele kuuliza kama hakuna anaeweza kufungua mlango na baadae akamuona mchina ambae anadai alikuwa 'sharp' kidogo na mhudumu wa ndege 'Air hostess' wakielekea upande wa mlango.

Victor anasema mhudumu wa ndege aliinama chini akagusa kitu na mlango ukaachia na kuwa wazi kwa upenyo mdogo, Victor anasema huyo dada hawezi kumsahau. Pressure ya maji kutoka nje ilizuia mlango kufunguka lakini waliongeza pressure na kuweza kufungua mlango na yeye, mhudumu na mchina walikuwa wa mwanzo kutoka.

Kutokana na pressure ya maji, mlango ulitaka kujifunga na Victor aliweka mguu na mama mmoja alimuomba amuokee mwanae na jitihada ziliendelea.

WAVUVI KUFIKA
Victor anasema wavuvi walifika kama dakika 5 na anamsema Mchina kama mtu aliyekuwa 'sharp' kwenye uokoaji na alianza na yule mtoto kwa kumuweka kwenye mtumbwi na watu waliendelea kutoka na kuingia kwenye mtumbwi.

Baadae Victor aliomba anaeweza kuogelea aingie ndani kuona kama kuna mtu amebaki na alipoangalia hakuona na akarudi kwenye mtumbwi.

Baadae Victor alitoka kwenye mlango na baada ya kutoka mlango ukajifunga. Victor anasema alirudi nchi kavu baada ya kama dakka 45 tangu ajali ilipotokea na hakuna aliyejua kama ni msafiri, wengine wakajua ni mvuvi.

KUSEMWA AMEFARIKI
Anasema kwasababu hakuwa na simu, majina yalizunguka mtandaoni kwamba amefariki lakini anashukuru hospitali kwa umakini kwani jina lake halikuwepo katika waliofariki. Anasema taarifa ya kufariki kwake ilichanganya watu.

NENO LAKE
Victor amesema watu wamche Mungu kwani kuna msemo unaosema 'There is no tomorrow' hivyo kama mtu ana muda wa kumshuru sasa afanye hivyo. Victor anasema Mungu yupo na anasaidia na yeye yupo hai, hajafariki.

Abiria aliyenusurika kwenye ajali ya Precision Air iliyozama anasema yeye ndio alikuwa wa pili kutoka baada ya Muhudumu wa Ndege kufanikiwa kufungua mlango

Victor anasema alipotoka nje aliona.wavuvi Wanne kwa mbali wanakuja na mtumbwi na walipomfikia yeye alianza kuwavuta abiria akiwa pale mlangoni na Wavuvi waliowapokea na kuwaingiza kwenye Mitumbwi

Victor anasema alishiriki zoezi la uokoaji kwa zaidi ya Saa 1 kabla hajaenda nchi kavu ambako alikaa hadi jioni lakini hakupenda ajulikane kama naye ni abiria manusura

Ameeleza mengi nikifanikiwa nitaweka clip hapa

Sabato njema!
Majaliwa Ni mchongo 👇
Screenshot_20221111-122634.png
Screenshot_20221111-122710.png
Screenshot_20221111-205632.png
 
Abiria aliyenusurika kwenye ajali ya Precision Air iliyozama anasema yeye ndio alikuwa wa pili kutoka baada ya Muhudumu wa Ndege kufanikiwa kufungua mlango

Victor anasema alipotoka nje aliona wavuvi Wanne kwa mbali wanakuja na mtumbwi na walipomfikia yeye alianza kuwavuta abiria akiwa pale mlangoni na Wavuvi waliowapokea na kuwaingiza kwenye Mitumbwi

Victor anasema alishiriki zoezi la uokoaji kwa zaidi ya Saa 1 kabla hajaenda nchi kavu ambako alikaa hadi jioni lakini hakupenda ajulikane kama naye ni abiria manusura

Ameeleza mengi nikifanikiwa nitaweka clip hapa

Sabato njema!
Hizo mzee baba ni tango pori
 
Hizo ni habari za ziada...
Kila mtu atakuja na zake...
Mimi nilishiriki kuwaombea mlango ufunguke..ukafunguka!.
Hadithi ni tele.....
 
Back
Top Bottom