Ajali ya Precision Air: Ripoti yabaini hakuna Control Tower, Boti za Uokozi zilichelewa, Mhudumu na Abiria ndio waliofungua mlango

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,555
Imefahamika kuwa licha ya Jeshi la Wanamaji kujulishwa tukio la ajali, Boti rasmi ya uokoaji ya Kitengo cha Wanamaji ilichelewa kufika eneo la ajali na sababu ni kwamba haikuwepo katika Bandari ya Bukoba
-
Pia, pamoja na Askari wa Kitengo cha Wanamaji kuchelewa kufika, hawakuweza kufanikisha zoezi la uokoaji chini ya maji kwa sababu ya ukosefu wa oksijeni na mafuta ya kutosha Boti

Aidha, kabla ya kuwasili kwa Polisi Kitengo cha Wanamaji, mmoja wa wavuvi wa eneo hilo alianza mchakato ya uopoaji wa maiti kutoka kwenye mabaki Ndege.

======

Novemba 9, 2022, Ndege ya Precision Air iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba ilipata ajali pembezoni mwa ziwa Victoria, karibu kabisa na uwanja wa Ndege wa Bukoba.

Ajali hii iliyoua watu 19 ikiwemo wasafiri 17 na wahudumu 2 iliwasili Bukoba saa 8:25 asubuhi ambapo hali ya hewa ilikuwa mbaya, kukiwa na radi, mawingu mazito na upepo mkali.

Kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa na wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, ndege hii ilizunguka mji wa Bukoba mara mbili, kisha abiria walipewa taarifa kuwa ingegeuza kurudi Mwanza kwa kuwa hali iliyokuwepo hapo haikuwa rafiki.

Lakini wakati ikizunguka kwa mara ya tatu, rubani aliweza kuona sehemu ya kutua ndipo akaamua kuishusha. Kwa mujibu wa manusura, ndege hii ilishuka salama, lakini kabda haijakanyaga ardhi ndipo ilibadili uelekeo kuelekea upande wa ziwa.

Mhudumu mmoja wa ndege hiyo pamoja na abiria mwingine ndiyo walihusika kufungua mlango, kisha abiria huyo alisimama kuzuia mlango ili usijifunge ili abiria wengine waweze kutoka na kuingia kwenye mitumbwi ya wavuvi.

Boti ya uokoaji iliwasili saa 7:49 mchana sababu ilikuwa inafanya oparesheni zingine, hivyo haikuwa karibu na uwanja wa Ndege wa Bukoba.

Marubani wote wawili walishindwa kufungua mlango kutokana na nguvu kubwa ya maji, kama kungekuwa na msaada wa haraka, watu wengi wangeokolewa

Pia, ripoti imebainisha kuwa uwanja wa ndege wa Bukoba hauna mnara kwa kuongozea ndege (Control tower). Mawasiliano yote hufanyika kwa kutumia mnara wa Mwanza.

Uchunguzi wa kubaini chanzo halisi cha ajali hii bado unaendelea.

315E9DBE-F82B-4DD9-B044-D9A3CBDC68C6.jpeg
E4832698-180C-4719-B9DF-4865D452EB44.jpeg
 

Attachments

  • AIB_BULLETIN_ACC_6_22_5H_PWF_21_November_2022_1_221122_122008.pdf
    180.9 KB · Views: 15
Back
Top Bottom