William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
JF Senior Expert Member Join Date: Tue Feb 2007
Re: A vote of confidence for Mama Anne-Kilango Malecela
Nipe popote ANNE alipowahi kusema lolote juu ya hili jambo kama ulivyosema hapo awali.....But naamini kuwa binadamu huwa wanabadilika kulingana na wakati, matukio, mazingira, na hata matukio. Ninachosisitiza ni kuwa tunahitaji muda wa kujua na pia anatakiwa kuonyesha dhahiri kuwa hakuna politics of revenge.
Mkuu Mheshimiwa
1. Heshima mbele mkuu wangu, ninaomba kukwambia neno moja muhimu, mimi binafsi nipo hapa JF, na sehemu mbali mbali za taifa za habari kwa wananchi, kwa sababu moja muhimu, nayo ni taifa langu na lako, Tanzania, mimi nina tatizo na viongozi wabovu, wahuni, wezi, na wasiokuwa na heshima kwa wananchi, na the most important of all, sipendi unafiki, kuanzia kwa viongozi mpaka sisi wananchi wenyewe.
2. Sasa ninaomba nikuambie wazi kuwa ninajua nyuma ya jina lako kuna nani, sasa kama wewe kweli ni mkweli, na usiyependa unafiki, unayelipenda taifa lako kama ninavyofahamu unavyopenda kufahamika:-
Naomba useme wazi hapa JF, mbele ya wananchi wakiwa mashahidi, kwamba nguvu unayoitumia kumshambulia Mama Kilango kwa kutetea wanyonge, mbona toka uingie hii forum JF, hujawahi kuwakemea kwa nguvu zote viongozi wafuatao, Mkapa, Chenge na Lowassa? WHY? mbona una nguvu sana ya kumshambulia huyu mama likini huna nguvu ya kuwashambulia hao niliowataja huko juu? Kwa nini Mkapa, Chenge, na Lowassa, wakishambuliwa huonekani kabisaaa hata comment? WHY? Je katika uhai wa maisha yako, kuna wakati wowote uliwahi kuwa mbunge? Ulifanya nini hasa?
3. Ninaomba kuwakumbusha wale wote ambao pamoja na wewe, mnaomshambulia Mbunge Shujaa Mama Kilango, ninasema hivi Mama Kilango, na wabunge kama Zitto, Dr. Slaaa, na Dr. Mwakyembe, kuna kitu kiomoja cha maana wanachotufanyia wa-Tanzania, ni kwamba wametupandia mbegu za mapinduzi, ambazo huenda hawataishi long enough kuona matunda yake, lakini ninawahakikishia kuwa hakuna atakayeweza kuzing'oa, au kuzizima hizi mbegu,
Ni m-Tanzania asiyekuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri ndiye anyeweza kuamini kuwa itatokea kwa urahisi viongozi mafisadi kufungwa, au kusumbuliwa na serikali yetu, lakini one thing guaranteeed hapa ni kwamba mbegu wanazozipanda hawa viongozi, Mama Kilango included, tutazipokea na kuziendeleza when the time comes, hawa wametuwekea msingi mzito ambao haukuwepo kwenye taifa letu, leo viongozi wote wa taifa hakuna anayekubali kusaini mkataba wowote kwa urahisi, infact juzi kiongozi mmoja aliniambia kuwa yeye hakubali mkataba wowote mpaka aupitishe kwa mawakili kama watatu kwanza,
alisema "...mambo yamebadilika kijana......."
Kwa wale tunaongalia a big picture ya taifa letu, tunawashangilia, na kuwafagilia, kwa sababu ya mbegu nzito wanazozipanda kwa ajili ya the future ya taifa letu, only small mind people ndio wanajali sifa za kina Mama Kilango, either viongozi hawa wanayafanya haya kwa kujua au kutokujua, lakini matokeo ni makubwa sana ambayo hayawezi kuzimwa na kiongozi yoyote yule hata awe na nguvu au hela kiasi gani hawezi kutununua wa-Tanzania wote, labda hao kina Serukamba tu!
Mungu Awabariki Viongozi Wote Wanaolala Macho Kwa ajili Ya Taifa Letu, na awalegeze wale wote wenye nia mbaya na taifa letu!
Ahsante Mkuu!
Field Marshall ES: Sauti Ya Umeme!