A vote of confidence for Mama Anne-Kilango Malecela

Tumpe sapoti lakini tuwe makini ili tusijiingize kwenye vita vya ndani kwa ndani vya CCM.
Kama ni kweli yeye ni mpiganaji...Afanye mambo na si rhetorics amabazo zimekuwa zikiwa rewarded na mikamati inayoendelea kula pesa zetu!

...cool but let's see and hear what best she can stand for then we line behind her.

Mkuu unajua mbwembwe za kuongea na kutoa povu mdomoni haziwezi kuondoa shida zetu, we need action not promise.
we are dying kwa shortage ya huduma za afya, we are killed na dawasco kwa mimaji michafu wanayosuply kutokana na uzembe wa usimamizi, we are the victims of our own cast (votes). we dont need help from them (wabunge) we demand their actions to rewards our votes
 
Msanii,

I will only answer this part of your question by a simple question:

Do you know who in ccm was outrageusly outraged (using Pundit's gramma) when the parliament voted to suspend Zitto from the parliament?

Can i answer on be half please?

It Was Stella Manyanya ,she was also a member of Mwakyembe Richmond team.

Eng, Manyanya she was the only one within CCM who she stood up in the Parliament and said no to suspension to Zitto but not this MAMA Please.

The one who puts the last nail in Zittos coffin was mzee TINGATINGA,.
 
Can i answer on be half please?

It Was Stella Manyanya ,she was also a member of Mwakyembe Richmond team.

Eng, Manyanya she was the only one within CCM who she stood up in the Parliament and said no to suspension to Zitto but not this MAMA Please.

The one who puts the last nail in Zittos coffin was mzee TINGATINGA,.

Check your facts MK ..... Go back (and if you can) get yourself through all speeches from ccm members during and after the debate to suspend zitto to get Mama Malecela's take on the issue.
 
Mwafrika wa Kike,

I missed u a lot! ... In fact I nilikuo...

welcome back!
 
Check your facts MK ..... Go back (and if you can) get yourself through all speeches from ccm members during and after the debate to suspend zitto to get Mama Malecela's take on the issue.

nisije nikawa mvivu wa kusoma nitaenda ktk hansard za bunge nikasome kule....
But i believe i was there and you know the vote casted and the majority (ccm) had their best to hammering Zitto out.

About Anne Kilango, she was also a minister ktk serikali fa fisadi then lini amekuwa mlokole mpaka amkane shetani na mambo yake yote??? Just think think and not stink..... shehe yahaya hutumia majini kuagua watu lakini anamcondem shetani.... inakuja hiyo??? isije ikawa changa la macho.

Lakini kwa ccm (wakali wa propaganda) yote yawezekana. mchanga unaweza kuwa sukari
 
nisije nikawa mvivu wa kusoma nitaenda ktk hansard za bunge nikasome kule....
But i believe i was there and you know the vote casted and the majority (ccm) had their best to hammering Zitto out.

About Anne Kilango, she was also a minister ktk serikali fa fisadi then lini amekuwa mlokole mpaka amkane shetani na mambo yake yote??? Just think think and not stink..... shehe yahaya hutumia majini kuagua watu lakini anamcondem shetani.... inakuja hiyo??? isije ikawa changa la macho.

Lakini kwa ccm (wakali wa propaganda) yote yawezekana. mchanga unaweza kuwa sukari

Msanii ... una hakika na hicho kwenye bold hapo juu?
 
Keep it up Mama,divine support is with you now and forever together bila kusahau wazalendo wa kweli wa Tz.
 
nisije nikawa mvivu wa kusoma nitaenda ktk hansard za bunge nikasome kule....
But i believe i was there and you know the vote casted and the majority (ccm) had their best to hammering Zitto out.

About Anne Kilango, she was also a minister ktk serikali fa fisadi then lini amekuwa mlokole mpaka amkane shetani na mambo yake yote??? Just think think and not stink..... shehe yahaya hutumia majini kuagua watu lakini anamcondem shetani.... inakuja hiyo??? isije ikawa changa la macho.

Lakini kwa ccm (wakali wa propaganda) yote yawezekana. mchanga unaweza kuwa sukari


Msanii, huo ndio mjadala wote-utaona humu mchango wa Stella Manyanya na Malecela, mmoja alitetea-mwingine alipiga msumari:

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita mtoa hoja ambaye ni Mheshimiwi Zitto Kabwe nilikuwa na taarifa tu kwamba ilikuwapo pia hoja binafsi ya Mheshimiwa Dr. Slaa inayohusu anayodai yeye matumizi mabaya ya fedha katika Benki Kuu ya Tanzania lakini hoja za namna hiyo na hasa inapogusa Taasisi nzito kama Benki Kuu ya Nchi ilikuwa inabidi nijiridhishe mimi mwenyewe kwamba yanayosemwa humo katika hoja angalau yanaushahidi wa awali. Kwa sababu tabu ya Waheshimiwa Wabunge jina la mtu au la Taasisi huwa linachafuliwa mara hoja ikifika mezani. Sasa itakapogundulika kwamba yaliyosemwa si sahihi bado haisadii kwa sababu taasisi au mtu anakuwa amekwisha chafuliwa. Kwa hiyo katika hali hiyo Maspika huwa waangalifu sana, maspika huwa waangalifu sana wanataka ushahidi zaidi ambao uendane na hizo hoja.

Kwa hiyo nilimwomba Mheshimiwa Dr. Slaa na sasa hivi naambiwa imeandaliwa ni book kubwa sana, sasa mpaka nitakapolitathimini na kuona kama linalingana na hoja anayoitoa ndipo nitaweza kupanga hoja yake katika orodha ya shughuli. Kwa leo tutakuwa na hoja hii ya Mheshimiwa Zitto kabwe, kwa hiyo namwita ili aweze kuwasilisha hoja yake.

Mheshimiwa Zitto tunafuata taratibu zilezile za hoja za kawaida mtoa hoja dakika zisizozidi 60 hii siyo ya Bajeti hii ni hoja ya kawaida. Kwa hiyo inakwenda na utaratibu wake dakika zisizozidi 60 hala nitaita upande wa Serikali Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, kwa muda ambao hauwezi ukakadiriwa kwa sababu atakuwa anajibu hoja zote za ile hoja kwanza. Nitaita wachangiaji kadiri ambavyo mtakuwa mnaleta majina. Kwa hiyo sasa Mheshimiwa Zitto Kabwe.

UCHUNGUZI WA MAPITIO YA MIKATABA YA MADINI

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, Maelezo yangu kuhusu Hoja ya kuundwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya Mikataba ya Madini na mazingira ya kusainiwa kwa Mkataba (MDA) mpya wa madini wa Buzwagi kulikofanywa na Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Nazir Karamagi (Mb) huko Uingereza Mwezi Februari 2007. Nawasilisha maelezo haya kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kanuni 104(2) Toleo la mwaka 2004

Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipatia fursa ya kuleta hoja hii hapa kwenye Bunge lako Tukufu kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge. Kuletwa kwa hoja hii, bila kujali maamuzi ya kuhusu hoja yenyewe, ni ishara tosha ya ukomavu wa demokrasia yetu ambayo inakuzwa na mijadala ya Bunge lako Tukufu. Nakupongeza kwa dhati kabisa kwa juhudi zako za kuliimarisha Bunge letu na kujenga muhimili imara wa ulinzi wa demokrasia ya vyama vingi nchini kwetu.

Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16/7/2007 mara baada ya hoja ya Waziri wa Nishati na Madini kuamuliwa na Bunge lako Tukufu nilisimama mahala pangu na kutoa taarifa ya kukusudia kuleta hoja ya kuunda Kamati teule ya Bunge. Nilisema kama ifuatavyo (kwa mujibu wa kumbukumbu sahihi za Mijadala ya Bunge), ninanukuu ‘…… naomba kutoa Taarifa Rasmi …… kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda Kamati Teule kuchunguza mkataba mpya wa Madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya kupitia mikataba aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe 30 Desemba, 2005. Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, nimeshawasilisha hoja yangu hii kwa maandishi kwa Katibu wa Bunge na sasa nawasilisha rasmi katika kikao hiki cha Bunge kwa uamuzi. Nimezingatia kanuni 104 (2) katika kuwasilisha hoja yangu.

Mheshimiwa Spika, katika maelezo yangu niliyowasilisha Bungeni wakati wa mjadala wa Hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini siku ya tarehe 16/7/2007 nilihitaji maelezo kutoka serikalini katika masuala makuu mawili yafuatayo:

(i) Kusainiwa kwa Mkataba mpya wa wa Madini wa mgodi (mradi) wa Buzwagi kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick na sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi, London Uingereza na vilevile kwa nini mkataba huo umesainiwa wakati bado serikali inafanya durusu (review) ya mikataba kufuatana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.

(ii) Kuondolewa kwa kipengele katika Sheria ya Kodi ya mapato ya mwaka 1973 kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ bila ya kibali cha Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja zangu Waziri wa Nishati na Madini alijenga hoja zake kama ifuatavyo,

Kusainiwa kwa Mkataba wa Mgodi (Mradi) wa Buzwagi.

Mheshimiwa Spika, Wakati akijibu hoja yangu kuhusiana na suala la Mkataba mpya wa mgodi wa Buzwagi, Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema kama ifuatavyo, nanukuu,

“Mheshimiwa Spika, katika tathmini ya Migodi, Mgodi wa Buzwagi ni Marginal Mine ambao uhai wake si wa muda mrefu. Bila ya kutumia fursa ya bei ya Dhahabu uwekezaji wake usingeweza kuwa wa faida. Hata hivyo, Mkataba wa Buzwagi hauna mapungufu yaliyokuwamo kwenye mikataba ya zamani”. Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Waziri alikiri mbele ya Bunge lako Tukufu kwamba amesaini Mkataba huo jijini London Uingereza.

Mheshimiwa Spika, Mapitio ya Mikataba ya Madini ni mchakato ambao mwisho wake ni kuletwa kwa sheria ya madini hapa Bungeni na kuifanyia marekebisho ili kuiboresha na kuondoa mapungufu. Hivyo, mpaka hapo sheria itakaporekebishwa ndipo tutasema tumemaliza zoezi la kupitia mikataba ya madini na hivyo kusaini mikataba mipya na makampuni yote ya madini yaliyopo nchini na yatakayokuja kuwekeza.

Mheshimiwa Spika, suala ambalo linanipelekea kuomba kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mkataba huu mpya ni kuhusu uharaka uliopelekea Waziri wa Nishati na Madini kusaini Mkataba huu. Sheria ya Madini bado haijarekebishwa, je Waziri anatumia vigezo gani kusema mkataba mpya wa Buzwagi aliousaini London hauna mapungufu?

Mheshimiwa Spika, Waziri wa Nishati na Madini aliliambia Bunge lako Tukufu kuwa Buzwagi ni marginal mine. Vile vile Waziri anasema kuwa Kampuni ya Barrick inamiliki migodi mitatu tu kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Bulyanhulu Gold Mine, North Mara Gold Mine na Pangea Minerals Limited Tulawaka. Kwa maelezo haya ya Waziri Karamagi, Buzwagi sio Mgodi.

Mheshimiwa Spika, hoja hii ya kuwa Buzwagi sio mgodi inashabihiana kabisa na hoja ya Kampuni ya Barrick kwamba Buzwagi ni Project. Taarifa ya kampuni hii ya Barrick Gold Corporation-Global operations - Africa - Buzwagi, inaonesha kuwa Buzwagi ni mradi. Taarifa hii nimeiambatanisha katika hoja hii.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya Barrick, Annual Review 2006 inasema ifuatavyo katika ukurasa wa 23, ninaomba kunukuu. “A major milestone was reached in February 2007 when we signed a mineral Development Agreement (MDA) with the Tanzanian Government. In 2007, we expect to complete a detailed construction design and receive Environmental Impact Assessment Approval approval”.

Mheshimiwa Spika, suala ambalo vile vile linanisukuma kuomba Bunge lako Tukufu kuunda Kamati Teule ni kwamba, iwapo Buzwagi sio mgodi bali ni mradi, ni kwa nini tumesaini Mineral Development Agreement (MDA) mpya? Kwa kuwa Pangea Minerals Tulawaka ndio inaonekana kumiliki mradi huu, Je serikali imefanya marekebisho tu ya MDA na kampuni ya Barrick?. Naomba Kamati Teule ichunguze ni nini kilichosainiwa, marekebisho ya mkataba wa Tulawaka au MDA mpya ya Buzwagi?

Mheshimiwa Spika, Buzwagi inashika nafasi ya pili kwa uwekezaji wa Barrick katika migodi hapa nchini. Wakati kampuni hii inawekeza dola za kimarekani 400 milioni katika Buzwagi, imewekeza dola za kimarekani 600 katika Bulyanhulu. Je ni kwa vipi Buzwagi iwe marginal mine wakati uwekezaji wake unashinda uwekezaji wa Migodi ya Tulawaka na North Mara?

Mheshimiwa Spika, chini ya kifungu cha 47 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 (Na.5/98), pamoja na mambo mengine kinataka leseni yeyote isitolewe mpaka taarifa ya mazingira iwe imetolewa na kuruhusu mgodi kuendelea na kazi.

Mheshimiwa Spika, wakati Waziri wa Nishati na Madini ameweka saini Mkataba wa Buzwagi juma la mwisho la mwezi Februari 2007, Baraza la Mazingira nchini limetoa kibali (Environmental Impact Assessment- EIA approval) tarehe 11 mwezi Mei 2007. Ni kwa nini Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Nazir Karamagi alisaini MDA ya Buzwagi na Kampuni ya Barrick kabla Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) halijatoa ruhusa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Madini, niliyoitaja hapo awali, imeunda Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining advisory Committee). Kabla ya Waziri kusaini mkataba wowote ni lazima apate ushauri kutoka kamati hii. Kwa taratibu za Kiserikali, kama kamati ikimshauri Waziri na Waziri akakataa ushauri huo, inampasa Waziri atoe sababu ni kwa nini anakataa ushauri. Je, Waziri alifuata ushauri wa kamati ya Ushauri ya Madini kuhusiana na wakati mwafaka, narudia, kuhusiana na wakati muafaka wa kusaini Mkataba huu?

Mheshimiwa Spika, inawezekana kabisa MDA ya Buzwagi kusainiwa Uingereza sio tatizo. Kwa mfano, Mwaka 2006 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini mikataba kadhaa. Ni mingapi kati ya Mikataba hii imesainiwa nje ya nchi? Nini madhara ya kisheria kwa Mkataba kusaniwa Uingereza? Je, Mkataba ambao umesaidiwa wa Buzwagi umeandikwa “signed in London” au “signed in Dar es Salaam”, yaani umesainiwa London au umesainiwa Dar es salaam? Kamati Teule ya Bunge ndio chombo pekee kitakachoweza kutoa majibu ya maswali haya.

(b) Kuhusiana na asilimia 15% ya capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema, naomba kunukuu “…kwa hiyo pamoja na kwamba ninamheshimu sana Mheshimiwa Kabwe Zitto na sote tunamheshimu ni msomaji mzuri, lakini wakati mwingine lazima kuangalia vitu gani unasoma. Ni kwamba kipengele hiki cha sheria kililetwa hapa Bungeni mwaka 2001 kwenye Bajeti kikabadilishwa” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, katika kuandaa hoja yangu hii, ilinibidi kupitia upya kumbukumbu za majadiliano ya Bunge ili kujiridhisha na maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, maelezo ambayo mimi nililitaarifu Bunge lako tukufu tarehe 16/7/2007 kuwa sio sahihi.

Mheshimiwa Spika, Kumbukumbu hizo zinaonesha kwamba, sheria ya fedha ya mwaka 2001 (Finance Act. No.14, 2001) ilifanyiwa marekebisho kadhaa ikiwemo marekebisho ya sheria ya madini kifungu cha 87 ambapo kifungu kidogo cha (3) cha kifungu cha 87 kiliongezwa. Kifungu kidogo hicho kinasema, ninaomba kunukuu kwa Kiingereza. ‘(3) The provisions of subsections (1) and (2) shall not apply to any person who, immediately before the first day of July, 2001 was not the holder of a mineral right granted under this Act’

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 87 cha Sheria ya Madini ya mwaka 1998 (No.5/1998) kinazungumzia Mrahaba wa Madini (Remission and deferment of royalties). Hivyo, kama sheria ya fedha ya mwaka 2001 haikubadili kipenge hiki, Mheshimiwa Waziri ametoa wapi jibu aliloliambia Bunge? Mheshimiwa Spika, suala hili linahusu haki, kinga na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa sheria namba 3 ya 1988.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika hotuba ya Waziri wa Fedha Mheshimiwa Basil Mramba, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti mwaka 2002, tarehe13 mwezi Juni, alizungumzia kipengele hiki. Ninaomba kunukuu sehemu ya hotuba ya Waziri wa Fedha Mheshimiwa Basili Mramba katika hotuba ya bajeti ya Kiingereza;

“Amendment to the Income Tax structure, (44) Mr. Speaker, in this area I propose to take the following measures: (v) I propose to reinstate (Naomba kurudia) the additional 15 percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure as set out in the Mining Act. No. 5 of 1998” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, nilipopitia sheria ya fedha ya mwaka 2002 nimekuta sehemu ya 8 inazungumzia mabadiliko katika kodi ya mapato ya 1973 ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2004. Na hata katika ukurasa wa kwanza wa sheria hii (Arrangement of Contents), sheria ya Madini haitajwi.

Mheshimiwa Spika, maelezo haya ya Waziri wa Fedha ya mwaka 2002 yanaonesha dhahiri utata wa kipengele hiki. Ni kwa vipi kifungu cha sheria ambacho hakijafutwa kirejeshwe? Mheshimiwa Spika, tuchukulie kuwa maneno ya Waziri ni ya kweli. Je, kwa nini makampuni ya Madini ambayo yameingia Mkataba na serikali kuanzia Julai mosi 2001 hayajaanza kulipa kodi ya mapato kama Waziri alivyosema?

Mheshimiwa Spika, utata huu ambao umegubika sekta hii ya madini unaweza kufafanuliwa na Bunge lako tukufu kupitia Kamati Teule. Kamati teule ya Bunge ichunguze upitiaji wa mikataba hii na kuona kama kuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria za nchi na kupotea kwa mapato ya Serikali na ufisadi.

Mheshimiwa Spika, suala hili ni suala la Kitaifa. Halina hata chembe ya itikadi za kivyama. Ninaamini Wabunge wataamua kwa maslahi ya Taifa letu. Uundwaji wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini na mazingira ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa Buzwagi utatoa msaada mkubwa kwa azma ya Rais wetu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ya kuona rasilimali za madini zinafaidisha nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.

(Hoja Ilitolewa Iamuliwe)

SPIKA: Asante sana Mheshimiwa! Hoja hiyo imetolewa na imeungwa mkono. Lakini kwa saba bu inahitaji majibu, sasa tutaendelea na utaratibu wa kuijadili ili tuweze kufikia uamuzi sahihi. Baada ya kumwita Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, ninao wachangiaji 13; labda nitaje watatu wa mwanzo, ah! Acha niwataje wote ili wajiandae. Wa kwanza ni Mheshimiwa Khalifa Suleiman Khalifa, Mheshimiwa Ruth Msafiri, Mheshimiwa Maulida Komu, Mheshimiwa Mhonga Ruhwanya, Mheshimiwa Suleiman Kumchaya, Mheshimiwa Chacha Wangwe, Mheshimiwa Susan Lyimo, Mheshimiwa Adam Malima, Mheshimiwa Magdalena Sakaya, Mheshimiwa Siraju Kaboyonga, Mheshimiwa Manju Msambya, Mheshimiwa Mudhihir Mudhihir na atakayehitimisha ni Mheshimiwa HafidH Ali Tahir. Kuna mwingine! Mheshimiwa Phares Kabuye naye ameomba, baasi kwa mpangilio nitamchomeka labda kati kati ya Mheshimiwa Manju Msambya na Mheshimiwa Mudhihir hapo. Kwa hiyo, watakuwa 14. Ni dhahiri mjadala huu utaendelea hadi jioni, kwa hiyo tujiandae hivyo. Sasa, namwita Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini. (Makofi)

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Maoni ya Serikali kuhusu Kuundwa Kamati Teule ya Bunge Kuchunguza Mapitio ya Mikataba ya Madini na Mazingira ya Kusainiwa kwa Mkataba Mpya wa Madini wa Buzwagi kama Ilivyowasilishwa na Mheshimiwa Kabwe Z. Zitto mbele ya Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kuchangia kwa niaba ya Serikali hoja ya kuundwa Kamati Teule ya kuchunguza Mkataba Mpya wa Madini wa Mgodi wa Buzwagi.

Mheshimiwa Spika, mtoa hoja amejielekeza katika masuala makuu mawili ambayo anadai wakati nayaelezea, aidha sikuwa sahihi au nilidanganya.

Kwanza, Licha ya maelezo ambayo nilikwisha yatoa kwa niaba ya Serikali juu ya kuondolewa kwa kipengele katika Sheria ya Mapato ya mwaka 1973 kuhusiana na Nyongeza ya asilimia 15 kwenye Mtaji wa Uwekezaji ambao Haurejeshwi kwa kila mwaka (Additional capital allowance of 15% per annum applied to the balance of unredeemed qualifying capital expenditure) Mheshimiwa Kabwe Zitto anaendelea kusisitiza kuwa kuondolewa kwa kipengele hicho kulifanyika bila ya kupata kibali cha Bunge.

Mheshimiwa Spika, Katika kujaribu kuthibitisha hoja yake, Mheshimiwa Kabwe Zitto amenukuu kumbukumbu za Bunge ambazo zinaonyesha marekebisho yaliyofanyika kwenye Sheria ya Fedha ya mwaka 2001 (Finance Act. No. 14 of 2001), kwa kutaja marekebisho ya Sheria ya mwaka 1998 ya madini kifungu cha 87 ambapo kifungu kidogo cha (3) cha fungu la 87 la Sheria ya Madini liliongezwa.

Mheshimiwa Spika, naomba Bunge lako tukufu litambue kuwa hapa Mheshimiwa Kabwe Zitto anachanganya Sheria mbili tofauti; Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 na Sheria ya Kodi ya Mwaka 1973. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kipengele kinachozungumziwa hakiko chini ya Sheria ya Madini ya mwaka 1998, bali kipo chini ya Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973. Ukweli kuhusu suala hili ni kwamba kipengele hiki cha Nyongeza ya asilimia 15 kwenye Mtaji wa Uwekezaji ambao Haujarejeshwa kiliondolewa na Bunge kupitia Sheria ya Fedha ya 2001. Kama Mheshimiwa Zitto angesoma kwa uangalifu, narudia, kama Mheshimiwa Zitto angesoma kwa uangalifu; Finance Act No.14 of 2001 aliyoinukuu angebaini kuwa marekebisho ya kipengele hiki yalifanyika katika fungu la 16B ya Jedwali la Pili la Sheria ya Mapato ya Mwaka 1973 na siyo fungu la 87 la Sheria ya Madini ya mwaka 1998 kama anavyodai Mheshimiwa Kabwe Zitto. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kunukuu marekebisho kama yalivyoletwa Bungeni kwa manufaa ya Bunge lako tukufu:

16B. Paragraph 16 of the second schedule to the Principal Act is amended.

(a) by deleting the definitions of the words “additional capital allowance” and qualifying capital expenditure” which appear in sub-paragraph (1) of paragraph 16.

(b) By deleting the definitions of word “expenditure” and substitution for it the following definition. “Expenditure” means the sum of prospecting capital expenditure and development capital expenditure incurred in the United Republicof Tanzania by any person carrying on mining operations. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, maana ya mabadiliko haya ni kwamba fungu la 18 (1) la Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 1973 linaloweka masharti ya kipengele cha nyongeza ya asilimia 15% kwenye mtaji wa uwekezaji ambao haujarejeshwa liliondolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya Bunge kupitisha marekebisho hayo, matokeo yake yalikuwa kwamba Bunge liliafiki kuondolewa kwa 15% ya additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure bila ya kujali mikataba ambayo baadhi ya makampuni ya madini yalikuwa yameingia na Serikali kwa mujibu wa fungu la 10 la Sheria ya Madini ya mwaka 1998 kabla ya mabadiliko haya.

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua kwamba mikataba ambayo Serikali iliingia na kampuni za madini kabla ya mabadiliko ya sheria hiyo ilikuwa inaifunga (binding) Serikali kutofanya mabadiliko ya sheria ambayo yataondoa vivutio vya kodi vilivyokuwepo wakati mkataba unatiwa saini, Serikali kwa kutambua hili, ilileta mapendekezo kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2002 (The Finance Act, 2002) ambayo yalipitishwa na Bunge ili kurekebisha kasoro hiyo.

Mheshimiwa Spika, maana ya mabadiliko hayo ni kwamba 15% additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure ilirudishwa kwa makampuni ya madini yaliyoingia mkataba na Serikali kabla ya tarehe 1 Julai 2001. Ndio sababu migodi iliyokuwa na mkataba na Serikali kabla ya tarehe 1 Julai, 2001 ilieendelea kuwa na kivutio 15% additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure hata baada ya kuondolewa kwa fungu hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili kuthibitisha kauli yangu, nimewasilisha kwako nakala ya Hansard ya tarehe 14 Juni, 2001 na nakala ya Ibara ya 16 ya Finance Act No.14 of 2001 ilivyowakilishwa Bungeni ili igawiwe kwa Mtoa hoja na Waheshimiwa Wabunge wengine wanaotaka kujiridhisha na ukweli huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali makini kama ilivyo Serikali yetu, haidanganyi. Uthibitisho huu ni kielelezo tosha kuwa mtoa hoja ndiye aliyedanganya Bunge na Watanzania waliomsikiliza kwa…., Mheshimiwa Spika, nitarudia; Uthibitisho huu ni kielelezo tosha kuwa mtoa hoja ndiye aliyedanganya Bunge na Watanzania waliomsikiliza kwa kutokuwa makini na kauli yake Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nataka kuchukua nafsi hii, kuwasilisha kwako ile Hansard niliyoizungumzia ambayo mwaka 2002 iliondoa kipengele hicho. (Makofi)

(Hapa Hansard Husika na Viambatanisho
vyake vilikabidhiwa kwa Spika)

Mheshimiwa Spika, Pili Mhe. Zitto anahoji kusainiwa kwa mkataba mpya wa Madini wa mgodi wa Buzwagi kati ya Serikali na kampuni ya Barrick na uhalali wa Mkataba huo kusainiwa mjini London, Uingereza. Vile vile, Mhe. Zitto anahoji kwa nini Mkataba huo umesainiwa wakati Serikali bado inafanya durusu (review) ya mikataba ya Madini kufuatia maagizo ya Rais.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Mkataba kusainiwa Uingereza, kama nilivyolielezea Bunge lako Tukufu wakati nahitimisha hoja ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2007/08, mkataba huo uliandaliwa Tanzania na wataalamu wetu na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining Advisory Committee) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika viambatanisho nilivyokupatia sasa hivi, vile vile nimeambatanisha wa kauli yangu hii. Vile vile uamuzi wa kuingiza mradi wa Buzwagi kwenye miradi ya Barrick Gold Corporation ambayo ni kampuni mama, ulihitajika kufanyika kabla ya Machi, 2007, vinginevyo fursa ya uwekezaji katika mradi huu ingepotea.

Mheshimiwa Spika, Kwa kuwa maandalizi yote ya kusaini mkataba yalikamilika nikiwa ziara ndefu ya nchi za nje, niliona si busara kuhatarisha uwekezaji wa mradi huu jambo ambalo lingeathiri maslahi ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nataka kutoa faida inayotarajiwa kutokana na Mgodi wa Buzwagi katika kipindi cha uhai wake ambayo kama usingesainiwa na Barrick wasiwekeze kwenye mradi huu ingepotea:-
(i) Mrabaha na kodi nyingine zinatarajiwa kufikia kiasi cha USD198.9 milioni.
(ii) Pay As You Earn kwa wafanyakazi inatarajiwa kufikia USD50.3 milioni.
(iii) Ujenzi wa laini ya umeme na matumizi ya Umeme ya mgodi na maeneo yanayozunguka mgodi yanategemea kutumia USD30 milioni.
(iv) Kununua huduma mbalimbali za wakati wa kujenga miundombinu mingine kwenda mgodini, ujenzi wa mitambo na wakati wa uzalishaji ambao unatarajiwa kugharimu takriban USD568.4 milioni.
(v) Jumla ya mapato yote yatakayoingia kwenye uchumi wa Taifa katika kipindi cha uhai wa mgodi yanatarajiwa kufikia takriban USD818.3 milioni.
(vi) Mgodi unatarajia kutoa ajira katika fani mbalimbali kwa jumla ya watu 696 watakaopata ajira ya kudumu. Kati yao, 630 au asimilia 91 watakuwa Watanzania; ikiwa ni pamoja na maafisa waandamizi.
(vii) Mgodi utaongeza mapato ya taifa ya fedha za kigeni kutokana na mauzo ya madini nje.
(viii) Mgodi utaendeleza miundombinu ya kiuchumi na kijamii, hasa huduma za jamii kama vile shule na zahanati katika maeneo yanayozunguka mgodi.
(ix) Kufunguliwa kwa mgodi huo kutafungua fursa nyingine za kiuchumi katika maeneo mengi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe Zitto anauliza kwenye mkataba huo, Je, kipengele kimekuwa signed in London ama signed in Dar es salaam?

Mheshimiwa Spika, hali ya maendeleo tuliyoyafikia dunia ya kileo, si muhuimu tena kwenye mikataba kuweka kipengele cha kubainisha mkataba kuweka kipengele cha kubainisha mkataba umewekwa saini eneo gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Format ya mkataba wa Madini wa Buzwagi hauna kipengele anachokiuliza Mheshimiwa Kabwe Zitto. Hiki si kitu cha ajabu kwa mikataba ya siku hizi ambapo mkataba unaweza kusainiwa na pande zaidi ya mbili zikiwa nchi tofauti. Mkataba unaweza ukasainiwa upande mmoja na ukatumwa kusainiwa na upande mwingine nchi nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu muhimu katika mkataba ni kuonyesha kwenye mkataba ni sheria ya nchi gani itaongoza mkataba. Mkataba wa Mgodi wa Buzwagi unataja kuwa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo itaongoza mkataba huo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe Zitto anahoji kama kabla ya kusaini Mkataba wa Buzwagi nilifuata Sheria inayonitaka kwanza kupata ushauri wa Kamati ya Ushauri ya Madini. Kama nilivyokwishasema mkataba ulipitia taratibu zote zinazohitajika ikiwa ni pamoja na kupata baraka za Kamati ya Ushauri ya Madini. Kivuli cha idhini ya Kamati hiyo nimekwisha wasilisha kwako kama kielelezo cha kuthibitisha kauli yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe Zitto anazungumzia eti maagizo ya Rais yalikiukwa, kauli anayoitoa bila ya kutafakari maagizo hayo yalikuwa ya aina gani. Mheshimiwa Rais aliagiza mikataba yote ya madini kufanyiwa mapitio ili kubaini maeneo yanayoweza kurekebishwa kwa faida ya pande zote mbili – faida ya Nchi na faida kwa Mwekezaji (win-win situation). Kamati iliundwa kwa ajili hiyo na baada ya kukamilisha kazi iliyopewa, iliwasilisha mapendekezo yake Serikalini tarehe 14 Septemba, 2006. Baadhi ya mapendekezo ya Kamati hiyo yalitumika katika majadiliano na makampuni ya madini yenye mikataba ya zamani. Mafanikio ya majadiliano hayo niliyataja kwenye hotuba yangu wakati nawasilisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka 2007/08 kuwa ni:-

• Kuondoa nyongeza ya asilimia 15 kwenye mtaji wa uwekezaji ambao haujarejeshwa (15% additional capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure). Hatua hii itawezesha kampuni hizi kukomboa gharama zao za uwekezaji mapema na hivyo kuweza kulipa kodi ya mapato (corporation tax). Kwa hili, ningependa kumsahihisha Mheshimiwa Kabwe Z. Zitto kwamba kuondolewa kipengele hicho siyo automatic kwamba kampuni inaanza kulipa kodi, isipokuwa inaharakisha muda wa kampuni kulipa kodi.

• Kulipa kiasi cha Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka kwa Halmashauri zinazohusika na migodi hiyo. Kampuni ya Barrick Gold Corporation imekubali na imeanza kulipa Dola za Marekani milioni 7 kila mwaka kama malipo ya awali ya kodi ya mapato ya kampuni hadi migodi yake itakapoanza kulipa kodi stahili.

• Kampuni ya Resolute (Tanzania) Limited imeondoa kipengele kwenye mkataba wake kilichokuwa kinairuhusu kutokulipa kodi ya mapato kwa wafanyakazi wake wa kigeni. Kuondolewa kwa kipengele hiki kutailazimu kampuni hii kulipa takriban Dola za Marekani milioni 2.2 kila mwaka kama malipo ya kodi ya mapato. Katika mwaka 2006/07 kampuni hiyo imelipa Dola za Marekani milioni 2.3.

• Kampuni ya AngloGold Ashanti inayomiliki mgodi wa Geita imekubali kulipa kiasi cha Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Aidha, majadiliano katika maeneo mengine ya mkataba wake, yanaendelea.

Mheshimiwa Spika, hivyo, si kweli kuwa zoezi la kudurusu mikataba ya madini bado linaendelea.

Mheshimiwa Spika, nilisema kuwa mkataba mpya kuhusu Buzwagi hauna upungufu uliokuwemo kwenye mikataba ya zamani – Ikiwa na maana kuwa kwa kutumia ushauri wa Kamati niliyoitaja hapo juu, mkataba wa Buzwagi umeboreshwa kwa maslahi ya Taifa ukilinganisha na mikataba ya zamani.

Mheshimiwa Spika, naomba ninukuu baadhi ya vipengele vilivyoboreshwa:-
• Depreciation ya gharama ya uwekezaji ni asilimia 80 mwaka wa kwanza, na baadaye asilimia 50 miaka inayofuata, katika Mikataba ya awali depreciation allowance ni asilimia 100 mwaka wa kwanza.
• Withholding taxes zimeongezwa kiwango kama ifuatavyo:-

• Technical services kodi ya zuio itakuwa asilimia 5 badala ya asilimia 3 zilizoko kwenye Mikataba (MDAs) ya zamani na hii ni kwa kila malipo yanayozidi asilimia 2 ya gharama za uzalishaji.

• Service fees kwa ajili ya gharama za utawala itakuwa asilimia 15 ikilinganishwa na asilimia 3 za Mikataba (MDAs) ya awali na hii ni kwa gharama ya uzalishaji. (Makofi)

• Kuna masharti ambayo hayakuwemo kuhusu kununua bidhaa na huduma mbalimbali hapa nchini.

• Kuna masharti kuhusu kuchangia mfuko wa uwezeshaji (empowerment fund) ambao haukuwepo katika mikataba ya zamani, kupitia Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, USD 125,000 kwa mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, utaona kuwa kuna vipengele vilivyowekwa kwenye mkataba huu ambavyo utekelezaji wake utafanyika baada ya kuleta Bungeni mapendekezo ya kurebisha vifungu husika kwenye sheria inayohusu mfumo wa kodi katika sekta ya Madini.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe Zitto, anasisitiza kuwa zoezi la kudurusu mikataba bado linaendelea. Mtoa hoja labda anachanganya tena zoezi la kudurusu mikataba na zoezi linaloendelea na kudurusu Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 na Sheria zinahusu mfumo wa kodi katika sekta ya madini kitu ambacho ni kipana zaidi na kinawahusu wadau wote yaani, wawekezaji wakubwa, wawekezaji wadogo na wote wanaojihusisha na utafiti katika sekta ya madini. Akielewa hili mtoa hoja atabaini kuwa maagizo ya Rais yalitekelezwa kikamilifu na matokeo yake yameishaanza kujitokeza kama faida nilizozieleza hapo juu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe Zitto anahoji kama Buzwagi ni mradi (project) au ni mgodi (mine). Nafikiri hili ni suala dogo ambalo naamini ni la uelewi tu. Hadi sasa mradi wa Buzwagi haujafikia hadhi ya kuitwa mgodi. Kama ilivyo miradi yote, Buzwagi utapata hadhi ya kuitwa mgodi baada ya Waziri wa Nishati na Madini, kutoa leseni ya uchimbaji, ujenzi wa mgodi kukamilika na shughuli za uchimbaji kuanza. Kwa hiyo, nazidi kusisitiza kwamba Buzwagi ni mradi kama tulivyo hapa kwenye Bunge tukufu, tulipokuwa hapa tusingeliweza kuliita Bunge ama jengo ilikuwa inaitwa mradi mpaka ilipokamilika tukaingia ndiyo likaitwa jengo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mgodi wa Buzwadi kuwa ni Marginal mine. Nilisema kwamba katika tathimini ya migodi, Mgodi wa Buzwagi ni Marginal Mine ambao uhai wake si wa muda mrefu na kwamba bila ya kutumia hela fursa iliyokuwepo hususan bei kubwa ya dhahabu uwekezaji wake usingekuwa wa faida. Wizara ya Nishati na Madini ilifanya uchambuzi wa taarifa ya uwekezaji katika Mgodi wa Buzwagi na kuonekana kuwa mgodi huo ni marginal project na ukianza kuendelezwa wakati huu ambapo bei ya dhahabu ni kubwa wastani wa zaidi ya dola za Marekani 600 kwa wakia, ndiyo utatoa marginal profit na kuwezesha mwekezaji kuendeleza mradi wa Buzwagi hadi kufikia hadhi ya kuwa mgodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kabwe anasema kuwa mgodi wa Buzwagi hauwezi kuitwa marginal mine kwa kigezo utashika nafasi ya pili kwa migodi inayomilikiwa na kampuni ya Barrick kwa kulinganisha moja kwa moja gharama za uwekezaji kati ya Mgodi wa Bulyanhulu uliofanyika miaka ya tisini na mgodi wa Buzwagi unaotarajiwa kujengwa mwaka ujao 2008.

Mheshimiwa Spika, mtoa hoja inaelekea anazungumzia suala la utaalamu wa fedha ambalo inaonyesha wazi hana ujuzi nalo. Hata hivyo mtu hahitaji kuwa mtaalamu ili kuelewa kuwa kama mwekezaji alitumia thamani ya dola za Kimarekani milioni 600 kujenga mgodi wa Bulyanhulu miaka kumi iliyopita, akitaka kujenga mgodi kama huo kwa sasa thamani yake itakuwa kubwa maradufu. Labda kwa manufaa ya Bunge lako tukufu, naomba nito ufafanuzi wa ziada ili kuonyesha kuwa gharama za uwekezaji siyo kigezo pekee cha kupima ubora wa mgodi. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, vigezo vingine vinavyotumika kujua ubora wa mgodi ni pamoja na mashapo yaliyopo na kiwango cha upatikanaji wa dhahabu kwa tani ya miamba (ore grade per tonne). Kiwango cha upatikanaji wa dhahabu katika mgodi wa Bulyanhulu ni wastani wa gramu 11 za dhahabu kwa tani ikilinganishwa na Buzwagi ambapo ni gramu 1.8 za dhahabu kwa tani. Mashapo yaliyopo Bulyanhulu ni kiasi cha wakia milioni 12 inayoweza kuchimbwa kwa miaka karibu 25 wakati Buzwagi ni wakia milioni 2.2 inayoweza kuchimbwa kwa miaka 10. Kutathiminiwa Mgodi wa Buzwagi kama Marginal mine ni suala la kitaalamu lenye takwimu za wazi ambalo halipingiki wala halipindishwi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuhuma kwamba sheria imevunjwa kwa kusaini Mkataba kabla ya Baraza la Mazingira kutoa kibali. Mheshimiwa Kabwe Zitto amenukuu kifungu cha 47 cha Sheria ya madini ya mwaka 1998 kinachotaka leseni yeyote ya uchimbaji madini isitolewe mpaka taarifa ya mazingira iwe imetolewa.

Mheshimiwa Spika, Kabwe Zitto anachanganya tena vitu viwili tofauti yaani Mkataba wa Madini na Leseni ya Madini. Mkataba wa Madini kati ya Serikali na kampuni za madini unaingiwa chini ya kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini ya mwaka 1998 na hicho kitu cha kwanza kinachoanzishwa mchakato wa uwekezaji. Hivyo, tathimini ya mazingira (environmental impact assessment study) inafanywa baada ya mwekezaji kuwa na mkataba. Mwekezaji anaweza kuomba leseni ya ya uchimbaji wa madini wakati wowote lakini hawezi kuipata mpaka awe na kibali cha Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC). Kwa maneno mengine kwa mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 1998, maombi ya leseni ya uchimbaji wa madini (mining license) lazima yaambatane miongoni mwa mambo mengine na tathimini ya mazingira kuhusu mradi huo (environment impact Assessment Study). Mpaka sasa leseni ya uchimbaji kwa mradi wa Buzwagi bado haijatolewa. Kwa kupata kibali cha Bazara la Mazingira la Taifa (NEMC), mwekezaji atakuwa ametimiza sharti mojawapo la kupata leseni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kumshauri Mheshimiwa Kabwe Zitto ajielimishe zaidi juu ya sheria zinazosimamia sekta ya madini hapa nchini. Vile vile namshauri Mheshimiwa Kabwe Zitto kujiepusha na hulka ya kutoa kauli nzito ambazo hazikufanyiwa utafiti wa kutosha kama hili analodai kuwa Serikali imevunja sheria za nchi na kulidanganya Bunge wakati ni yeye mwenyewe hajajielimisha vya kutosha kuhusu sheria anayoizungumzia kwamba imevunjwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtoa hoja amedai kuwa suala analolizungumzia eti ni la kitaifa na halina hata chembe chembe za itikadi za kivyama. Pamoja na kuwa hoja alizozitoa hazina ushahidi wowote, tayari hoja hizo zimekwisha dakwa na kubebewa bango na Mwenyekiti wa Chama chake cha CHADEMA na wamezigeuza kuwa propaganda ya kisiasa kupitia vyombo vya habari. Labda angalizo alilolitoa Mheshimiwa Kabwe Zitto, analilenga kwa Chama chake mwenyewe. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kuna msemo wa Kingereza usemao (No Research no Right to speak) bila utafiti huna haki ya kuzungumza. Hivyo vile vile Chama makini kinahitaji kufanya utafiti kabla ya kujihusisha na mambo ya kuzua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja ya Mheshimiwa Kabwe Zitto, imeonyesha mapungufu makubwa ya tafsiri ya sheria anazozinukuu na vifungu anavyo vilenga ili kuthibitisha kuwa Serikali imelidanganya Bunge. Ni dhahiri hoja yake imejengwa katika mazingira ya uzushi yenye malengo makuu mawili, kwanza kuchonganisha Bunge lako tukufu na Serikali na pili ni kuwapotosha wananchi juu ya sheria zinazotungwa na Bunge lako tukufu kwa nia ya kujitafutia umaarufu. “Nataka kurudia ni dhahiri hoja yake imejengwa kwa mazingira ya uzushi yenye malengo makuu mawili, kwanza kuchonganisha Bunge lako tukufu na Serikali na pili kuwapotosha wananchi juu ya sheria zinazotungwa na Bunge lako tukufu kwa nia ya kujitafutia umaarufu usiokuwa na msingi (cheap popularity)”. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtoa hoja anaomba Bunge lako tukufu kuunda Kamati teule ya Bunge hili Kamati imfanyie kazi ya kuhalalisha mambo ya kuzua au kumsaidia kumfafanulia sheria ambazo yeye mwenyewe kashindwa kuzielewa. Hii si kazi ambayo Bunge hili linaweza kutumia fedha za walipa kodi kuifanya. Tabia ya namna hii ikiruhusiwa kuendelea inaweza kulipunguzia Bunge lako tukufu heshima na hadhi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nijielekeze yaliyojitokeza tarehe 16 Julai, 2007 mara baada ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kupitishwa na Bunge, Mheshimiwa Kabwe Zitto alisimama na kutoa tuhuma nzito kwangu kama Waziri wa Nishati na Madini, kuhusiana na mkataba mpya wa Buzwagi. Akinukuliwa na hansard ya tarehe 16/07/2007, ambayo mwenyewe ameinukuu bila kuikamilisha, Mheshimiwa Kabwe Zitto alisema nanukuu “kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na mkataba mpya wa mgodi Buzwagi ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi, amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli sivyo ambavyo vipo katika mkataba ambao ameusaini mwisho wa kunukuu”.

Kutokana na tuhuma hizo, Mheshimiwa Zitto kwa kutumia kanuni ya 104 (1) ya Bunge alitoa taarifa rasmi ya mdomo ya kusudio la kuleta hoja ya kuunda Kamati Teule kuchunguza mkataba mpya wa Madini wa Buzwagi. Leo ametoa hoja aliyoitolea taarifa, lakini mbali ya kujikanganya kwenye sheria alizodai zimevunjwa, hajaonyesha wazi pasipotiliwa mashaka wapi nililidanganya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuhuma Mheshimiwa Kabwe Zitto alizozitoa kwangu kama Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Nishati na Madini na kudakwa na vyombo vya habari ameniathiri mimi binafsi kwa kunichafulia jina langu bila sababu za msingi kwa kutoa taarifa za uzusi tena uzushi wa hatari. Nina hakika wewe mwenyewe pamoja na Waheshimiwa Wabunge wenzangu makuwa mashuhuda jinsi magazeti mbalimbali yalivyokuwa yakitoa vichwa vya habari vyenye kutoa lugha za kejeli kwangu kutokana na tuhuma Mheshimiwa Kabwe Zitto alizozitoa hapa Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa vielelezo na maelezo ya Serikali niliyoyatoa, sasa naomba kupitia kwako kuliomba Bunge lako tukufu vile vile liangalie vielelezo alivyovitoa mtoa hoja kama vipo ili liweze kupima na kuamua ni nani, mwongo ni nani aliyelidanganya Bunge mimi au Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge, ni dhahiri tuna kazi kubwa hapa ya kufanya ili tufikie haki. Sasa kwa mpangilio nitamuita mchangiaji Mheshimiwa Khalifa S. Khalifa halafu atafutiwa na Mheshimiwa Ruth Msafiri na wakati huo huo Mheshimiwa Maulidah Anna Komu ajiandae.

MHE. KHALIFA S. KHALIFA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fura hii ili na mimi nichangie machache katika hoja hii ambayo ipo mbele ya Bunge letu tukufu.

Mheshimiwa Spika, na mimi niungane na wenzangu kwanza kwa kukupa pole sana wewe binafsi, familia ya marehemu mzee Fundikira na wananchi wote wa Tanzania kwa kuondokewa na mzee wetu ambaye sote tuliomjua tuliona busara zake na mchango wake. Aidha, nitumie fursa hii kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Gando pia kumpa pole Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa kifo cha mzee wake na nampa pole kwa sababu siku mbili tu kabla yake tulikuwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli, akaniambia hali yam zee wake kumbe alikuwa anabashiri kifo cha karibu cha mzee huyu. Mwenyezi Mungu awape malipo yanayostahili watu hawa kwa mujibu wa madi zao.

Mheshimiwa Spika, hoja iliyopo mbele yetu mimi ninavyoitazama ni ndogo sana, udogo wake ni kuwa inazungumziwa suala la kuunda tume teule ya Bunge. Sasa udogo wake ama kukubali au kukataa. Mwisho, katika maneno ya mwisho ya Mheshimiwa Waziri hapa ninayemheshimu sana amesema maneno yafuatayo: kuwa vielelezo alivitoa Mheshimiwa mtoa hoja kama vipo na vielelezo alivyovitoa yeye ambavyo naamini na vipo vinahitaji kutazamwa. Chombo cha kutazama vielelezo hivyo na kuthibitisha nani muongo ni hiyo Kamati teule ya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, imezuka shutuma hapa ya kuwa Mheshimiwa Rais amesema kwa nia nzuri tu suala la kupitiwa mikataba. Ni kweli Mheshimiwa Rais amesema hivi na mimi naamini amesema kwa nia safi. Sasa sisi hatukulazimisha kama Wabunge kuwa tuione mikataba. Lakini kama kumbukumbu ni sahihi ni Bunge hili hili na Wabunge hawa hawa katika mijadala mbalimbali wamekuwa wakilizungumzia jambo hilo labda wayafute maneno yao hayo leo. Wamezungumza sana kuhusu mikataba ya madini. Kama tutakuwa tunakwenda katika mwenendo huo hiyo ni hatari mno. Kwa sababu ni sisi Wabunge, Bunge hili hili tumesema mikataba ya madini ina matatizo tunahitaji tuione ina mambo mengi. Sasa kama leo imetolewa hoja ya kuundwa tume ya Bunge kutazama issue moja tu ya mkataba mmoja tu ilishakuwa tatizo kubwa nasikitika tatizo kubwa nasikitika sana. (Makofi)

Tumeambiwa hapa mfano mzuri tumeambiwa kampuni ya Barrick kuwa inachingia shilingi bilioni 7 au dola milioni 7. Lakini maneno hayo tunaambiwa leo baada ya kauli ya Mheshimiwa Rais ya kupitiwa mikataba. Hivi kwa nini haikuwepo mwanzo? Na ni kwa nini ni kampuni ya Barrick tu je, hizi nyingine? Sasa yote hayo ni mambo ambayo Wabunge kama wawakilishi wa wananchi wanapaswa kuyajua.

Mheshimiwa Spika, zaidi ya hilo mitandao wewe mwenyewe ulisema hapa kuwa tuiitumie sana na taarifa za mitandao mingine si sahihi sana. Ruling yako ambayo mimi naiheshimu kweli kweli kwa sababu ruling yako ni kubwa mara nyingine hata kuliko kanuni zetu za Bunge kwa mtu anayeelewa taratibu za hapa. Lakini PRC ambayo ni taifa lililotulia karibuni tu wamechukua miezi minne kupitia mikataba yao. Sasa sisi ni muda mrefu ni miezi 18 ni kimya inakuja taarifa tena inakuja taarifa ndogo tu kama hiyo Barrick inachangia makampuni mengine yatakayochangia dola 250,000 sijui dola 200,000 kwa Halmashauri kwa ufupi ufupi namna hii.

Sasa nije kwenye hoja ya Mheshimiwa Mbunge, Bunge hili katika kipindi kilichopita kiliwahukumu Wabunge wa Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa kosa kutia sahihi taarifa ya Kamati ya PAC kantini. Ndani ya yetu Bunge hili likawaadhibu kwa kosa hilo. Sasa mimi nastuka sana inaposemwa kuwa kumbe jambo zito unaweza ukalifanya vyovyote kwa sababu unataka hivyo. Je, tuliwaadhibu nini wale kama lile lilikuwa si kosa kwani kantini si mahali, si Tanzania hii hii? Lakini tukawaadhibu wakakosa Ubunge. Kama wanaokumbuka. (Makofi)

Sasa tunapoambiwa tu ni jambo la kawaida tu kwenda kusainiwa nje jambo zito kama hili linalohusu maslahi ya wananchi, nje ya nchi na halafu inajengwa hoja ya kuwa hapana haja ya kujua kinachofanyika ndiyo kinachosemwa katika hoja hii kuundwa Kamati maana yake ni kuwa kijulikane kilichofanyika kwa nini iwe nje isiwe ndani? Sasa mimi napata tabu kidogo kuona kuwa tunayajadili mambo yanayohusu Watanzania tena mara nyingine mimi nasikitika kidogo kwa sababu lugha ambazo zimetumika hapa si nzuri hata kidogo hatuwezi kupingana na kanuni tukaelezana na nini kwa sababu si utaratibu na tunaheshimiana sana humu ndani. Hii kanuni si wengine tunaijua vizuri kweli kweli. Lakini si vizuri anasimama mtu mzima unampiga kanuni kaa kitako lugha si nzuri. Lugha ilikuwa ikisemwa hapa kama lugha iliyozungumzwa katika hoja ya mtoa hoja hapo mwanzo tarehe 16 ilikuwa ina maneno ya kukera na hii ya leo waliosikia ni maneno ya kukera sana. Sasa katika busara ya kawaida, katika watu tulioendelea kama sisi na tena bahati nzuri tunajisifu kuwa tumesoma sana tunasheria nyingi tusitukanane kabisa kwa sababu wananchi wetu wanasikia na hawapendi vitu hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi narudia kwenye hoja yangu ya msingi ipo haja ya kuundwa Kamati Teule ya Bunge na naunga mkono kwa asilimia kubwa kabisa asilimia mia moja na zaidi kuwa Bunge hili tukufu kuangalia hali hii nzima ilivyokwenda na utata huu lazima iundwe Kamati Teule ya Bunge na kama hoja ni kutumia fedha za wananchi, fedha za wananchi zimetumiwa katika majadiliano madogo tu ya hapa. Wewe Mheshimiwa Spika, ofisi yako imeunda Kamati Teule na zimetumika fedha Serikali haikuwa na maneno, je hili jambo linalohusu maslahi ya wananchi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)

MHE. RUTH B. MSAFIRI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii, ili nipate nafasi ya kuchangia machache katika hoja iliyoko mbele yetu. Hoja iliyowasilishwa asubuhi hii na Mheshimiwa Kabwe ni ya kuona uwezekano wa kuunda Tume teule ya Bunge kwa mujibu wa kanuni za Bunge toleo la mwaka 2004 ibara ya 104 (2).

Mheshimiwa Spika, naomba mimi nitamke moja kwa moja kwamba hakuna haja ya kuunda tume hii. Nasema hivyo kwa sababu mto hoja alifuata taratibu zote ambazo alitakiwa kuzifuata kwa mujibu wa kanuni. Asubuhi ya leo amepata nafasi ya ziada, ametoa maelezo yake yeye mwenyewe alikwishawasilisha vielelezo vyake mapema tu na vile vile tumepata nafasi ya kumsikiliza mjibu hoja na vile vile mjibu hoja ametoa vielelezo vyake mbele ya Bunge hili tukufu.

Mheshimiwa Spika, Bunge letu limekuwa na kawaida ya kupokea hoja na kuzijadili kwa kupima nguvu ya hoja yenyewe. Kwa mujibu wa hoja iliyotolewa na majibu tuliyokwisha kuyapata nimeridhika kabisa kwamba mjibu hoja ameweza kujibu hoja zote vizuri. Hali ambayo inaondoa dhumuni la kuwa na tume teule kama ambavyo mtoa hoja alipendekeza. Yako mambo mengine ambayo ni madogo madogo ambayo kimsingi wala hayakutakiwa hata kuonekana. Kwa mfano anaposema mkataba ulisaini wapi? Ulisainiwa London au ulisainiwa Dar es Salaam mimi nashindwa kujua kwamba aliyeusaini ni nani kwa sababu mimi sijui Mheshimiwa Waziri akishakuwa amekula kiapo ni wakati gani anapoacha kuwa Waziri, anapokuwa yupo ndani ya nchi, ama nje ya nchi? Ni wakati gani ambapo hatumii madaraka yake ipasavyo? (Makofi)

Kwa hali hiyo, mimi sikuona mahali ambapo Mheshimiwa Waziri kwa kusaini mkataba huu alipokuwa yuko nje nchi alifanya makosa. Alifanya hivyo kwa kutumia mamlaka aliyopewa na mamlaka iliyomteua. Mamlaka hiyo haijamlalamikia imeridhika kwa kazi aliyoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile, tumekwisha kufanya mikutano sisi wenyewe Wabunge, sielewi labda Mheshimiwa Kabwe lakini sisi tumekwishafanya mikutano tunakaa Dar es Salaam tuko ndani ya Ukumbi wa Mkutano kwa kutumia mtandao, tunafanya mkutano na wenzetu ambao wako katika nchi zingine, wako Afrika ya Kusini, wako Uingereza, wako New York tunaongea nao tukiwa tuko katika kumbi ambazo zimeandaliwa.

MBUNGE FULANI: Visual Conference.

Wamenipa jina rasmi basi nilitamke sikuwa napenda kulisema inaitwa Visual Conference mnaonana mnazungumza mnajibizana na mnaweza kuzungumza na kufikia muafaka wa jambo lolote na yale mnayoyafikia yanachukuliwa kwamba ni maazimio rasmi ambayo mmeyafikia hamkuonana uso kwa uso lakini kwa kutumia vyombo mmeweza kuonana. (Makofi)

Sasa ikiwa katika mkataba huu hili jambo linashangaza labda tu niunge mkono kwamba maneno ya Waziri kwamba mtoa hoja ajielimishe zaidi pamoja na mitandao ya kisasa kwa umri bado anaweza kufanya hivyo na akafanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia kuna maneno mengine ambapo mimi nadhani tumepata darasa kidogo kwa Mheshimiwa Waziri kwa kutuelimisha tofauti ya mkataba na tofauti ya leseni ni wakati ambapo mkataba unasainiwa wakati gani tathimini ya mazingira inafanywa? Hakuna tathimini ya mazingira inaweza ikafanywa wakati huyu mwenye kuingia mkataba hajaonyesha nia na hajaingia makubaliano. Sasa baraza litakwenda kutazama nini kati ya nani na nani maana mimi sijapata kusikia ndoa inaandaliwa kati ya watu wawili ambao hawajakubaliana. Kwa hiyo, haiwezekani baraza likaenda kufanya tathimini ya mazingira wakati Serikali haijakubaliana na yule mwenye kutaka kuingia mkataba ule. Katika hili ndicho kitu kilichofanyika kwa hali hiyo, mimi sijaona tunaiunda Kamati teule kwenda kuchunguza nini na kitu gani ambacho hasa ni kigumu katika hili.

Lakini kinachonikera zaidi mimi nataka nijirejeshe kwenye hansard kuna mazingira ambayo yameendelea kujengeka kwa namna ambavyo inatisha. Naomba ninukuu hansard, mtoa hoja anaposema Mheshimiwa Spika, kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na mkataba mpya wa Mgodi Buzwagi, ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli sivyo ambavyo viko katika mkataba ameusaini.


Mheshimiwa Spika, naomba kutoa taarifa rasmi ya mdomo kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda Kamati Teule kuchunguza mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini. Ninapenda nisisitize pale ambao ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais ya kupitia mikataba ya madini aliyoitoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe 30 Desemba mwaka 2005.

Mheshimiwa Spika, mimi naona hapa jina la Rais limetumika tu labda kuvuta hisia kwamba kuna hoja hapa ya msingi. Lakini halikutumika kueleza kwamba hoja yenyewe ni hoja gani na mjibu hoja ameeleza vizuri.Kwa hali hiyo mimi nisingelipenda tabia inayojengeka ya kupenda kutumia jina la viongozi wakuu kuonyesha kwamba hili jambo ni zito wakati uzito wenyewe haupo. (Makofi)

Lakini vile vile inanikera kuona kwamba ndani ya chombo hiki tukufu, ndani ya ukumbi huu mtukufu, tunaanza kujengeana mazingira ya kuwajengea wenzetu kutokuaminiwa. Kuwajengea wenzetu hisia za kuonyesha kwamba wanadanganya. Inasikitisha kweli kweli kuona kwamba kiongozi aliyeaminiwa na wananchi akaaminiwa na kiongozi wa nchi akapewa mamlaka kubwa ya kusimama akawa miongoni mwa watendaji kuwa Serikali anaweza akaelezwa kwamba amedanganya. Hiki ni kitu ambacho hakika mtoa hoja anaposema kwamba haizui hisia za kisiasa. Mimi nakataa kwamba anayetaka atumie ukumbi huu kuonyesha kwamba sasa yeye ana hisia zake za kisiasa na anataka kuzijenga ndani ya ukumbi huu kwa kudhalilisha watendaji wazuri walioteuliwa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu hiki si kitu kizuri. Wote tunamfahamu vizuri Mheshimiwa Nadhir Karamagi, ni kipindi chake cha pili kuwa Bungeni, amefanya kazi zake kwa uaminifu na uadilifu na hata mabadiliko ya Mawaziri yalipokuja bado aliendelea kuwa ndani ya Serikali. Amefanya kazi yake ambayo ni nzuri, na Wizara aliyoshika tunajua ilivyo nzito na nyeti. Inashikilia Nishati na Madini ambayo ni maeneo ambayo ni nyeti katika Taifa letu na sisi tunapenda kuona kazi hii inafanyika vizuri.

Mheshimiwa Spika, kwa hali hiyo mimi kabisa naona kwamba maelezao haya ya mtoa hoja yamekusudia kumdhalilisha mjibu hoja ambaye ni Mheshimiwa Waziri na nikisoma ibara ya 50 kipengere kidogo cha 8(a) na (d) ambapo inasema ni marufuku kwa mtu yoyote kutumia lugha ya kuudhi, vile vile kujiingiza katika mambo ya kuwasema wenzake au zaidi mno ni kutaka kuleta malumbano ndani ya kisiasa ndani ya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii sasa imezoeleka kuwa ni tabia Mheshimiwa Mbunge ananyanyuka anazungumza maneno, anasema futa, anafuta. Lakini akishafuta anarudia neno la kusema kwamba message sent and delivered. Hii inaonyesha kwamba ni madhumuni yanayotumika kuutumia ukumbi huu vibaya ili kupeleka ujumbe usiokuwa sahihi kwa wanaosikiliza, kwa wananchi ambao wanadhani kwamba hapa ni mahali pa watu kuja kutoa hoja zao ambazo hazijibiwi. Ninapenda kuishauri Bunge lako Tukufu kwamba sasa liongeze kipengele kingine ndani ya Kanuni kwamba Mbunge yoyote anayezungumza maneno ya uongo hana ushahidi, hata kama ametakiwa kuyafuta na akayafuta, bado apewe adhabu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kusudi kuzuia tabia ya kusema uongo na kutumia Bunge hili kusema uongo kisha kufuta na kuongeza maneno, message sent and delivered hiki ni kitu ambacho ni dharau kubwa na kwa kweli hakijengi heshima ya Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kuyasema hayo, naomba niseme kwamba hakuna haja ya kuunda Kamati Teule, maelezo yaliyotolewa yanatosha. Serikali yetu ni aminifu, inatenda kazi zake kwa umakini mkubwa, na maelelzo yaliyotolewa yanatosheleza.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Nitoe tu taarifa Mheshimiwa Ruth Msafiri, amezungumzia Kanuni. Kanuni ipo. Sio kwamba haipo, Kanuni ya 59 fasili ya 3. Nainukuu, iwapo hadi kufikia mwisho wa muda aliyopewa Mbunge aliyeamriwa kuthibitisha ukweli wa usemi wake, atakataa au atashindwa kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge basi Mbunge huyo atachukuliwa hatua na Spika, kwa mujibu wa Kanuni wa 59(2). (Makofi)

Lakini bado tunaendelea. Sasa namwita Mheshimiwa Maulidah Anna Komu, ajiandae Mheshimiwa Mhonga Ruhwanya na atafuatia Mheshimiwa Suleiman Kumchaya.

MHE. ANNA M. KOMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuiona note yangu ya kutaka kuchangia hoja hii na kunipa nafasi hii adhimu ya kuchangia. Kabla sijaanza hata mchango naomba kusema naunga mkono hoja kama wenzangu husema mia kwa mia mimi naunga kwa mamilioini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea kwanza nikupe pole kwa kifo cha Mzee wetu sisi wote na pia niungane na wenzangu kumpa pole Mheshimiwa Waziri Magufuli kwa kifo cha mzee wetu kwa sababu mzee wake ni mzee wetu. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amini.

Mheshimiwa Spika, naomba tukumbushane kidogo japokuwa wenzangu wanasema kwamba tusitumie majina ya viongozi kwenye ukumbi huu kwa kujinufaisha, lakini mimi kamwe kwenye maisha yangu sitasahau kauli za Baba wa Taifa Mzee wetu Julius Kambarage Nyerere, na kila nitakapokuwa natoa mchango nikikumbuka kauli yake nitamtaja. Tena ninapomtaja huwa ninamtaja kwa uchungu mkubwa sana. Ama kweli kama Mwenyezi Mungu ameleta kitu kibaya duniani au kitu ambacho kinatuchosha kuleta kifo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuondokewa kwa baba yetu, tumeondokewa sana na nina hakika kwamba majadiliano haya yaliyopo leo katika Bunge lako yasingekuwepo. Mali ya nchi hii, madini ya nchi hii, alikabidhiwa yeye kutoka kwa Wakoloni. Lakini hakuna kitu alipenda kukihifadhi na kitu alichopenda kukienzi kama madini na mali kwa ajili ya kutuwekea sisi Watanzania. Leo ninapoona kwamba tunatumia mali hizi zote kwa kusema kwamba ati tunataka kufanya haraka kwa ajili ya mustakabali wa Watanzania, sikubali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ari mpya, kazi mpya na nguvu mpya tuzitumie kwa vitu ambavyo tunaviona kwamba havitaleta mjalada kwa Watanzania pindi wakivipokea. Mimi sioni tabu kabisa kwa nini Mheshimiwa Waziri amesaini mkataba Uingereza. Asaini mkataba Uingereza, asaini mkataba Somalia, asaini mkataba Ethiopia popote atakapopaona yeye kwamba ana uharaka wa huo mkataba asaini. Tatizo langu linakuja kimoja tu, kuna tatizo gani wakati madini ya dhahabu tunayotafutia wafadhili yako Tanzania. Waziri wetu ni Waziri wa Wizara ya Serikali ya Tanzania. Muwekezaji anayekuja kuwekeza anakuja kuwekeza kwa madhumuni na mintarafu na misaada na yote yaliyozungumzwa na mashule na ma-dispensary kwa ajili ya Mtanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna haraka gani ya kuchukua mikataba hii ikasainiwe nje ya Tanzania, wakati tunajua kwamba wenzetu walio wengi Watanzania ambao wananisikiliza naomba wanisamehe wengi wetu hatuelewi nini maana au faida ya mikataba juu ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kila siku nitakuwa nakuambia na nikiwaambia ukumbi huu, tujitahidi sana kuwa wa wazi. Tujitahidi sana kuweka hivi vitu visilete maswali kwa sababu jambo hata likiwa zuri, lakini ukayajengea maswali mengi katika jambo lenyewe linakuwa si zuri tena. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nimesema ninaunga mkono mamilioni kwa sababu sikioni hata kimoja kilicho tatizo katika karatasi hii au katika hoja hii. Mheshimiwa Zitto kama alivyoambiwa kwamba hana anachokijua akasome, sawa! Lakini anachotaka kusoma ndiyo masuala zaidi ya 11 aliyoyatoa katika karakatasi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nimejaribu kupitia hii karatasi ninaona mengi ni maswali anauliza, na kwa sababu hajui ndiyo alitaka kujulishwa. Sasa kuna tatizo gani la yeye kutaka kujua maana yake mtatutisha hata sisi wengine ambao siyo wacharukaji humu ndani. Mtakapoona kuna jambo huko nje nikasema ngoja niende Bungeni kwa sababu nina uwezo huo nikaulizie nitakuwa ninaogopa ninakaa kwa sababu nikiuliza nitaambiwa Mama Komu kajifunze zaidi hujui. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nina hakika sisi wote wote hapa hata tuliomaliza miaka 30 katika Bunge hili kila siku mwanadamu anataka kujua zaidi. Sikuambii sisi wengine ambao ndio kwanza tumekuja na pengine tusirudi. Sasa miaka yangu mitano nisiitumie kweli kwa kuuliza kitu ambacho sikijui. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nafikiri ustaarabu wa mtu siyo kunyamaza kuuliza, ustaarabu wa mtu ni kuuliza ili apate jibu. Sasa maswali yaliyomo humu ndani mwanangu Zitto anachokitafuta hapa ni kutaka kujua je, katika haya masuala aliyoyauliza nikikupa mfano swali moja, anasema je, Waziri anatumia vigezo gani kusema mkataba mpya wa Buzwage uliosainiwa London hauna mapungufu? Anataka kujua tu, amweleze hivyo vigezo. Lakini sasa tukianza tena na kupeana maneno ya kashifa humu ndani tutakuwa kweli hatutendeani haki na hasa nikirudi tena, hii Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu kisisi tunasema ni Msahafu au Biblia ni nini lakini ndiyo mwongozo wetu.

Mheshimiwa Spika, inasema hivi ibara ya 100, kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano, na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano. Au katika Mahakama, au mahali pengine popote nje ya Bunge. Kwa hiyo, swali lolote lile mtakaloliona linanikita nakuja kuliuliza kwa sababu sitapelekwa Mahakamani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namaliza kwa kumalizia kitu kidogo tu ambacho nimekinukuu hapa. Shule, zahanati pia zimetajwa kwamba wawekezaji hawa wanakuja hapa katika kuchimba hayo madini, wakati tunazungumza kila siku hapa, tujitahidi sana mali hizi tuzishike wenyewe Watanzania. Mimi nitarudia tena na tena kwa kusema tena na tena kwamba huwezi kumpa mgeni mali kama hizi za dhahabu, almasi na nini na nini achume akuachie wewe vyote. Lazima atahakikisha atapeleka kwao. Anachochukua yeye ni kingi zaidi atachukua anakupa wewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hizi shule na hizi zahanati basi mimi ningetaka zisiwe shule tu na zahanati na shopping centre kama wenzetu wanavyoendelea. Tusidanganye kwa sababu kama ni shule basi hata Watanzania tunachangishana tunajenga shule, kama zahanati ilizungumzwa hapa kwamba tumemaliza shule sasa tutaingia kwenye zahanati. Mimi nakwenda Mererani kila siku. Hali ya Mererani si nzuri na nina hakika kwamba na wewe pengine ulishapitia njia ni mbovu, maisha ya watu wa pale ukiwaona unawaona kwamba maisha haya si mazuri. Tumeanza lini kuchimba Tanzanite miaka mingapi sasa Tanzanite inachimbwa. Kiko wapi hicho mwekezaji ambacho atatutishia kwamba ametuletea baada ya yeye kunufaika, kiko wapi? Hii ni mifano midogo tu.

Mheshimiwa Spika, sasa tunapokuja pahala kama hapa tukawa tunataka kujua zaidi, lakini tukaleteana kashfa, tukaambiana maneno yasiyokuwa na maana, Mheshimiwa nasisitiza tena kwamba itakuwa siyo vizuri. Mimi ni Mbunge na wenzangu wote hapa ni Wabunge wa Majimbo, wameletwa na wananchi.

SPIKA: Mheshimiwa, itapendeleza na itausaidia mjadala kama na wewe utatathmini majibu ya Mheshimiwa Waziri. Kwa sababu na wewe unaanza kusema vitu na kupuuza bila kuzitaja hoja zenyewe. Mheshimiwa Zitto katoa hoja. Mheshimiwa Waziri kazijibu hoja na kwa taarifa Waheshimiwa Wabunge kwa sababu mimi ni fair kabisa nimeagiza zimechukuliwa photo copy Dr. Slaa kama Kiongozi pale na mtoa hoja wanayo majibu ya Mheshimiwa Waziri. Sasa tukielekeze kujibu tusiseme tu kwamba kuna kashfa, inakuwa ni malumbano tu hayana maana. (Makofi)

MHE. ANNA M. KOMU: Ahsante Mheshimiwa Spika nakusikiliza. Narudia tena samahani, kwamba alichokijibu Mheshimiwa Waziri sijapingana nacho na wala alichouliza Mheshimiwa Zitto sijapingana nacho. Isipokuwa narudia tena kusema kinachotakiwa hapa ni kuundwa kwa Tume tu kwamba Mheshimiwa Zitto aweze kujiridhisha na maswali yake 11 na zaidi ambayo aliyouliza kwenye hoja yake na Mheshimiwa Waziri kama alivyomjibu inawezekana kwamba Mheshimiwa alivyojibu yeye mimi nimeona nimeridhika kwa sababu amejibu vizuri. Je, mtoa hoja ameridhika? Sasa ninarudia pale pale kusema kwa hiyo hoja hizo zilizoletwa katika Ukumbi huu isiishie hapa tu kwa vyovyote vile naunga mkono tena kusema kwamba Tume Teule iundwe na ichunguze jambo hili mpaka upatikane ukweli ili na wananchi wa Tanzania na wao waridhike kuona kwamba kweli Tume imeundwa na jibu limekuja zuri. Sio kwamba kwa jinsi alivyouliza Mheshimiwa Zitto na jinsi alivyojibu Waziri tumeridhika sisi. Je, wananchi wote wameridhika. Tume iundwe huru kabisa Tume ije ichunguze jambo hili jibu lije hadharani na wananchi waridhie kwamba kweli Zitto kasema uongo, Waziri kasema kweli au Waziri kasema uongo Zitto kasema kweli.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja mamilioni. (Makofi)

MHE. ANNA M. ABDALLAH: Mwongozo wa Spika.

SPIKA: Mheshimiwa Anna Abdallah mwongozo wa Spika.

MHE. ANNA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, naomba mwongozo wako. Hivi hii sasa ni hoja ya Bunge ama bado ni hoja ya mtu binafsi. Yeye ameitoa mbele ya Bunge, Bunge tunajadili. Sasa hii hoja ni ya nani? Sio ya ndani ya Bunge? Inatakiwa sisi ndiyo tujiridhishe wote? Lazima aridhike mtoa hoja ndiyo nilitaka kujua tu hilo Mheshimiwa Spika.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge hilo nilitaka kulisema. Lakini nadhani Mheshimiwa Anna Abdallah ameniwahi tu. Hoja ikishawasilishwa hapa, uamuzi wa usahihi wa yoyote yatakayosemwa ni uamzi wa Bunge. Hatumfurahishi mtu, hatumfurahishi mtoa hoja, hatumfurahishi Waziri aliyejibu, hatuwafurahishi wananchi. Jambo linaweza kuwa gumu. Lakini tunaotakiwa kuamua ni sisi humu Wabunge. Kwa hiyo, mjadala ujiekeleze katika hoja na majibu halafu Wabunge turidhike. Maana yake hatima yake tunapiga kura kuiamua. Kwa hiyo, jibu ni kwamba hoja hii ni ya Bunge sasa kuweza kufikia maamuzi. Mheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya, atafuatiwa na Mheshimiwa Suleiman Kumchaya wakati huo huo Mheshimiwa Chacha Wangwe ajiandae. (Makofi)


MHE. MHONGA SAID RUHWANYA: Ahsante Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kutoa pole kwako wewe na familia yako na familia ya marehemu na vile vile napenda kutoa pole kwa Mheshimiwa Magufuli kwa kufiwa na baba yake mzazi. Kabla sijatoa mchango wangu kuhusiana na hoja iliyowasilishwa hapa mbele yetu. Naomba nikumbushe tarehe 28 mwezi wa 12, 2005 ulitoa picha katika ule Ukumbi wa zamani na tulishika Katiba ya nchi na tulishika Quoran na wengine walishika Biblia na tukasema kwamba tutailinda na tutaitetea Katiba ya nchi. Kwa hiyo naamini kabisa tuko humu kwa mujibu wa Katiba na tunafanya kazi hii kwa kutumia Katiba. Kuna mtu anasema kwamba nani hajui ni katika kujenga hoja ndiyo nimeanza hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba unilinde.

SPIKA: Wewe unaongea unamwa-address Spika, hao wengine hawana hoja yoyote ya maana. Wangekuwa na hoja wangejiorodhesha kusema. (Makofi)

MHE. MHONGA SAID RUHWANYA: Ahsante Mheshimiwa Spika. Kama nilivyosema kwamba tuko humu kwa mujibu wa Katiba na hili Bunge sio letu sisi ni la wananchi kwa sababu limepewa madaraka na wananchi kwa mujibu wa Katiba yenyewe inavyosema. Katika ibara ya 63 ya Katiba yetu.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka ya Bunge. Naomba kunukuu, kifungu cha 3 cha 63 ya Bunge kuna vipengele mbalimbali ambacho cha kwanza kinaweza kuwa kumwuliza Waziri yoyote swali lolote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake. Kwa hiyo, sijaona kutokana na jinsi dira inavyokwenda unaonekana kama kuna makosa yaliyofanyika kwa mtu kutoa hoja ya binafsi. Hii inakubalika kikatiba, kwa hiyo hakuna mtu aliyevunja Katiba kwa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile kuna kipengele cha ibara ya 63 kifungu kidogo cha pili, hii tunaruhusiwa kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa. Ingawa siku zote tunaambiwa kwamba mikataba ni siri haturuhusiwi kujadili, lakini Katiba inaturuhusu kufanya hivyo. Kwa hiyo sidhani kama kuna ubaya wowote kwa sisi kujadili hili suala. Kwa hiyo, nilikuwa naweka msingi wangu vizuri.

Mheshimiwa Spika, vile vile hapa tumeambiwa kwamba tunatumia jina la Rais lakini tunakumbuka kwamba tarehe 30 mwezi wa 12, 2005 Rais alisema kwamba mikataba itakuwa reviewed. Kwa maelezo ya Mheshimiwa Waziri amesema kwamba kwa leo ametueleza kwamba mikataba imekuwa reviewed na kuna baadhi ya vipengele ambavyo vimebadilishwa na vitaletwa hapa Bungeni. Lakini tatizo ni kwamba kama kweli haya yote yamefanyika ni kwamba taarifa ilikuwa haijafika na tulikuwa hatujaambiwa vipengele gani vilikuwa vimebadilishwa katika usainishaji mikataba upya. Labda ndiyo maana mikataba mingine imeendelea kusainiwa kama labda Ritchmond, na kadhalika.

Lakini kulikuwa hakuna taarifa yoyote ya Bungeni kuambiwa kwamba kuna taarifa italetwa ya Muswada ili ije kuwa Sheria ya Madini mpya baada ya kufanyia marekebisho. Ndiyo kitu ambacho ninakiona kwamba hakuna kosa lolote limefanyika kwa kuuliza chochote kwa sababu hatujapewa taarifa kwamba tayari wameshafanya review ya kitu chochote. Wala Rais hajasema kwamba tumeshafanya review kile nilichosema tayari kimeanza kufanyika. Kwa hiyo naweza kuiweka hiyo sawa.

Mheshimiwa Spika, sasa mimi naona bado kuna matatizo kidogo pamoja na kwamba tulikuwa hatujajua tayari mikataba imefanyiwa reviewed na wala Rais hajatuambia kama tayari mikataba imeshafanyiwa reviewed sasa tunaweza kuanza mikataba mipya. Ninachoweza kusema ni kwamba nina maswali kidogo. Swali langu la kwanza ni kwamba kwa nini mkataba huu wa Buswagi umesainiwa kiharaka yaani kulikuwepo na uharaka gani wa kusainiwa kiasi kwamba naweza nikarejea ukarasa wa 148 kulingana na majibu ya Mheshimiwa Waziri tarehe 16 Julai, alisema kwamba naomba kunukuu.

Mheshimiwa Spika, mgodi wa Buswagi katika tathmini ya mgodi, ni marginal mine ambao uhai wake si wa muda mrefu, bila kutumia fursa ya sasa ya bei ya dhahabu uwekezaji wake usingeweza kuwa wa faida. Kwa hili mimi ninavyofahamu kwamba dhahabu inapanda thamani yake kila siku. Kwa hiyo ule uharaka wa kusema kwamba alikuwa anajitahidi kuwahi soko la bei ya dhahabu mimi sioni kama lina usahihi ingawa sitaki kujaji alichosema Waziri kwa sababu dhahabu siku zote inapanda thamani. Haiwezi kurudi nyuma yaani kama bei ya leo haiwezi kuwa sawa sawa na miezi sita ijayo. Mimi ndivyo ninavyofahamu. Kwa hiyo, inawezekana labda angeweza kusaini baadaye ingeweza kusaidia kwamba labda dhahabu ingeweza kuwa na bei kubwa na nchi ingepata pato kubwa zaidi.

Mheshimiwa Spika, vile vile nikienda kwenye Hansard naomba kunukuu jibu lingine kwa jinsi Mheshimiwa Waziri alivyosema ni kwamba yeye ametoka katika private sector kwa hiyo anajali muda katika masuala ya biashara. Kwa hiyo, inawezekana kwamba hakuwa na ubaya wowote katika kusaini ule mkataba. Yaani kuusainia huko London, maana yake inaonekana hapa tatizo ni kusaini London. Lakini mimi naomba Wabunge wenzangu tukubali Kamati Teule iundwe ili kuondoa doubt yoyote kwa sababu wakati anajibu pale watu wamechukua tofauti tofauti, majibu yaani hoja iliyoulizwa na jinsi Waziri alivyojibu, katika kuweka tu ile wazi, clear kwa sababu nchi inavyosema kwamba tunatawala kwa ukweli na uwazi na ni sehemu mojawapo ya uwajibikaji kwa kiongozi yoyote kukubali kama kuna doubt yoyote labda Kamati Teule iundwe ili iweze kufanyiwa au ku-clear.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hili suala mimi naliona sio la kiitikadi. Maana yake hapa inaonekana kama limejengwa kuwa ni la kiitikadi. Mimi sioni kama ni la kiitikadi. Bali ni kwa maslahi ya Taifa na tunafanya kazi hii kama nilivyosema kwa mujibu wa Katiba na Katiba inaturuhusu kufanya hivyo, katika Ibara ya 100 tunaruhusiwa kutoa mawazo yetu na vile vile katika ibara ya 63 tunaruhusiwa kuuliza swali au kuuliza jambo ambalo linaonekana labda lina utata kwa Waziri au swali lolote. Kwa hiyo, naomba naendelea kusisitiza hatutakuwa tumevunja Katiba wala Kanuni za Bunge kwa kuunda Kamati Teule. Nilikuwa naomba Kamati iundwe ili tuweze kujiridhisha yaani tuweze kujiridhisha hata kama siyo sisi basi wananchi huko nje kwa sababu kila mtu atalichukua kivyake na Mheshimiwa Waziri amesema kwamba inaonekana hapa palikuwepo na nia ya kuchafua jina lake. Saa nyingine amewaza tu kwamba kulikuwa kuna nia lakini mimi sioni kama kulikuwa kuna kitu kama hicho, kwa sababu paper nzima jinsi ilivyo inauliza tu maswali ambayo yalikuwa yanahitaji majibu.

Hakuna sehemu yoyote ambayo mimi nimeona lugha iliyotumika ambayo ni ngumu au mbaya kwa Mheshimiwa Waziri. Vile vile ninachoona mimi kwa upande wa Mheshimiwa Waziri yeye ndiyo ametumia lugha ngumu zaidi. Sasa mimi nilichokuwa naomba, naendelea kusisitiza kwamba ili jina lake lisichafuke kama alivyosema kwamba limechafuliwa, akubali Kamati Teule iundwe na nchi yetu hii tunasema kwamba inatawaliwa kwa mujibu wa sheria kuna utawala bora kuna taratibu. Kwa hiyo, ninaomba kabisa ili haki hiyo iwepo na huo
utawala bora uonekane Waziri aonyeshe uwajibikaji wake na uwazi ikubalike Kamati Teule iundwe na hili siyo suala la kiitikadi ili kuondoa utata ni suala tu la kitaifa kwa sababu hata katika Katiba yetu imeonyeshwa kwamba tunaruhusiwa kufanya hivyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo sina zaidi, naomba kuunga mkono hoja zaidi ya asilimia 100. (Makofi)

MHE. SULEIMAN O. KUMCHAYA: Mheshimiwa Spika ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niweze kuchangia katika hoja hii iliyotolewa na Mheshimiwa Zitto Kabwe na kujibiwa vizuri sana na Waziri wa Madini na Nishati, Mheshimiwa Karamagi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naanza kwa kusema hivi hakuna haja ya kuunda Tume Teule ya kuchunguza utaratibu nzima wa mikataba na sheria ya madini kutokana na hoja iliyotolewa na Mheshimiwa Zitto Kabwe. Ninasema hivyo kwa sababu gani kwa sababu majibu yaliyotolewa yako wazi kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu chochote ambacho kinaeleweka kisichokuwa na utata hivi kuna haja gani tena ya kuunda Kamati Teule. Tunataka tuunde tupate nini? Tupoteze pesa za wananchi bila sababu yoyote. Juzi hapa tumetumia karibu milioni 400 bila sababu yoyote narudia tena hivi kweli leo turudi huko huko kwa kitu kinachooeleweka. Mimi ningekubaliana na Mheshimiwa Zitto Kabwe kama Mheshimiwa Waziri asingekuja na kutoa ushahidi tena ushahidi tosha ulioandikwa. (Makofi)

Lakini tuunde tu, hiyo si kweli hata kidogo. Mheshimiwa Zitto Kabwe anasema hivi, naomba kunukuu ukurasa wa tatu wa hoja yake. Kwa kusainiwa kwa mkataba mpya wa madini wa mgodi katika (mradi wa Buzwagi) kati ya Serikali na Kampuni ya Serikali na Kampuni ya Barick na sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi, London Uingereza. Na vile vile kwa nini mkataba huo umesainiwa wakati bado Serikali inafanya durusu reviw ya mikataba kufuatana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.

Mheshimiwa Spika, mimi hapa inanishangaza kidogo, na inanishangaza hasa baada ya kupata maelezo kamili kutoka kwa Mheshimiwa Waziri. Hapa tunachozungumza ni maudhui ya mkataba huu sio wapi mkataba umesainiwa hata kidogo. Kama kungekuwa na maelezo nani ya mkataba huu uliosainiwa London yanayohatarisha maslahi yetu hapo ingekuwa jambo lingine. (Makofi)

Lakini kule kusainiwa London tu iwe ni hoja ya kuunda Tume Teule, si kweli hata kidogo. Na sababu zilizotolewa na Mheshimiwa Waziri zinatosha kabisa kuonyesha kwamba hakukuwa na madhara yoyote ya kusainiwa mkataba huu huko London Uingereza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 5 wa hoja ya Mheshimiwa Zitto Kabwe, anasema hivi, Mheshimiwa Spika, kumbukumbu hizo zinaonyesha kwamba sheria ya fedha ya mwaka 2001 Finance Act No. 14 ya 2001 ilifanyiwa marekerisho kadhaa ikiwemo marekebisho ya Sheria ya Madini Kifungu cha 87, ambapo kifungu kidogo cha 3 cha kifungu cha 87 kiliongezwa kidogo hicho kinasema ninanukuu. Akanukuu kama alivyonukuu. Alipokuja Mheshimiwa Waziri ameeleza kinaganaga ukweli wa kifungu hiki, kwamba hivi ilivyokuwepo katika hoja yake si kweli. Na mabadiliko haya yalifanyika rasmi, ushahidi umetolewa. (Makofi)

Leo tunang’ang’ania tuunde Tume, ya nini Tume hii. Mimi wasi wasi wangu kwamba ndani ya Bunge hili panaweza kuwa uwanja wa siasa badala ya kuwa uwanja wa kuwatumikia wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, uchaguzi tulimaliza nje hapa ndani sote sisi ni Wabunge kazi yetu kubwa ni kuwatumikia wananchi na ndivyo viapo tulivyoapa tarehe 28 Desemba, 2005.

Mheshimiwa Spika, hakuna hata Mbunge mmoja humu hata mmoja ambaye yuko hapa hajali maslahi ya wananchi hata kidogo hayupo hapa, na ndiyo maana kila tunaposimama tunazungumza maslahi ya wananchi, naomba twende tufike mahali tukaanza kutumia ukumbi huu kama jukwaa la kujijenga kisiasa, tutafanya makosa makubwa kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, lazima niseme ukweli, binadamu ni binadamu awe mtu wa kawaida, awe kiongozi, awe Waziri, Naibu Waziri, Mbunge anahitaji heshima, anahitaji kulindwa ili heshima yake isiharibike. Tunapokuja kuzungumza mambo haya hilo lazima tulijue kwamba hichi ninachokizungumza hakitamshushia heshima yake huyu binadamu mwenzangu kama mimi. Na ndipo tunapotakiwa tuseme ukweli katika mambo yetu yote ambayo tunazungumza hapa katika Bunge letu hili Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa tisa, Mheshimiwa Zitto Kabwa anasema hivi naomba kunukuu, Mheshimiwa Spika, suala ambalo linanipelekea kuomba kuundwa kwa Kamati teule ya Bunge kuchunguza mkataba huu mpya ni kuhusu uharaka uliopelekea Waziri wa Nishati na Madini kusaini mkataba huu. Sheria ya Madini bado haijarekebishwa, je Waziri anatumia vigezo gani kusema mkataba mpya wa Buzwagi aliousaini London hauna mapungufu.

Mheshimiwa Spika, tumepata majibu yake, nia yetu wa Watanzania ni kutaka kwenda kasi huyo Baba wa Taifa ambaye wenzetu wanamtumia hapa bila utaratibu alisema hivi wakati wenzetu wanatembea sisi tukimbie. Huku ndiko kukimbia kwetu, Mheshimiwa Waziri amekuwa na safari London ameikuta Board ya Bariki inafanya mkutano nafasi ndiyo ile ile Watanzania tunataka kukimbia, hivi arudi Tanzania awaite waje huku tena, Tanzania tuko peke yetu hapa duniani si kweli maana yake nini huku maana yake kuto kujali hamu ya wananchi wanaotaka kupiga hatua katika maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hakuna baya alilolifanya Mheshimiwa Waziri kusaini mkataba huu London, alichofanya ni kujali maslahi ya Watanzania ametueleza hapa jinsi tutakavyofaidika, mambo chungu mzima.

Mheshimiwa Spika, nataka niseme jambo moja, ni kweli kabisa Baba wa Taifa alitulindia madini haya, ili tufike mahali tuyatumie vizuri. Nataka kusema hivi na ndiyo maana tumefika tumewaambia makampuni haya makubwa makubwa kwa sababu ya elimu hiyo ambayo Baba wa Taifa aliisubiri kwamba jamani eeh, na sisi tunataka kufaidika na madini haya, hiyo ndiyo elimu tuliyokuwa huko nyuma tusingeweza kufanya hivyo lazima tujivunie kwamba sasa tunaweza kusema hapana. Huko nyuma tulikuwa hatuwezi kufanya hivi.

Mheshimiwa Spika, naomba kurudia tena sisi tunakazi moja tu ya kumtumikia Mtanzania na ndiyo kiapo chetu na ndiyo kazi yetu, kwa hiyo tunapokuja hapa tuje na uhakika na yale ambayo tunayazungumza ili tuifanye kazi hiyo vizuri na wananchi wakisikia wajue kweli Wabunge wanafanya kazi yetu. Tuko hapa kwa niaba ya milioni 36, nawaomba wadau wote wa maendeleo katika Tanzania walikubali hili tuache tabia ya kujengana bila sababu yoyote, tutafika mahali tutahesabiana nani alikuwa anatumikia wananchi na nani alikuwa anataka kujijenga yeye mwenyewe. Na haya mambo tunayasema hayakuwahi kutokea tu Tanzania hapa yametokea katika nchi nyingine nyingi tu.

Mheshimiwa Spika, kengele ya kwanza imelia ya pili karibu italia nasema hivi kwa hili ambalo limeeleweka kwa majibu sahihi ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini hatuna haja hata kidogo ya kuunda Tume teule bila sababu za msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. (Makofi)

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, asante sana kwa kunipa nafasi kuchangia hoja hii muhimu, kwanza kabisa napenda kukupa pole kwa msiba wa mjomba wako ambaye Tanzania inamtambua kama mwana harakati wa kweli ambaye alitumia muda wake mwingi sana kuwapigania wananchi na hakuona kama chama kilikuwa ni kigezo kikubwa ndiyo maana aliweza kuwa hata upande wa wapinzani. (Makofi)

Pia napenda kumpa pole Waziri wa Ardhi Mheshimiwa Magufuli kwa kifo cha Baba yake Mpendwa, Mheshimiwa Magufuli ameonyesha kwamba na yeye anauwezo wa kusimamia ukweli, na ndiyo maana wakati anakuwa na maadui wengi. Kwa sababu haki siku zote inaposimamiwa ni lazima wale wasiopenda haki wafanye uadui, na waweze kukejeli ili kuifunika haki. Lakini mimi nasema ya kwamba nikiwa kama Mbunge ambaye nimechaguliwa na nimekuja hapa pamoja na Wabunge wenzangu tukala kiapo kwa sababu sisi Wakurya na waafrika kwa ujumla tunaogopa sana kiapo. Unapoinua mkono wako hapa na kusema ya kwamba nitailinda na nitasema kweli daima, kinyume chake ni kwamba hivyo hicho kiapo kitakumaliza wewe, kwa hiyo wale ambao wanaikiuka viapo vyetu hapa kwa kutaka kugeuza uwongo uwe ukweli basi wananchi wanaona, Mungu anaona na wenyewe dhamiri ndani yao zinawashitaki kwamba haya wanayoyasimamia ni mambo ambayo hayana ukweli wowote.

Kwa kuwa Mungu ni Mungu wa haki na wananchi wa Tanzania wanachokitaka ni haki mimi naunga mkono hoja hii mia kwa mia kwamba ili tujiridhishe na pia Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye mimi namheshimu sana ni msomi mzuri na anafanya kazi kwa bidii ili hiki kiwingu cha kusema ameharibiwa jina kiondoke ni lazima kuwe na Tume ambayo itachunguza haya mambo na kuyaweka bayana ili wananchi wote wafahamu na Wabunge pamoja na mtoa hoja aridhike ya kwamba kweli hayo mambo yamechunguzwa, sababu tumeunda Tume nyingi tu hapa, na suala la select committees hizi Tume teule ni la kawaida katika Bunge lolote la common wealth, na tumeunda Tume hata za kumchunguza Mheshimwa Chacha Zakayo Wangwe kama amesema ukweli zimetumia fedha zikakaa huko Mara na zikagundua ya kwamba amesema ukweli. Tumeunda Tume hapa hata za kumchunguza Mheshimiwa Malima hizi Tume zinaundwa ni jambo la kawaida, kwanini hapa Wabunge Waheshimiwa kweli muone uzito sana na muone shida sana kwamba hii Tume itaundwa. (Makofi)

Kwanza kabisa...

SPIKA: Mheshimiwa Chacha Wangwe unachanganya mambo bure, kanuni ya 104 inaunda Kamati teule, hata neno Tume sijui mnalipata wapi hayo yote mengine unayoyataja Spika alikuwa anateua Wabunge wachache kwenye Kamati kuweza kumshauri juu ya ukweli wa jambo ni tofauti kabisa na Kamati teule chini ya Kanuni ya 104. Ningeomba Waheshimiwa Wabunge tunavyokwenda tunayo hoja ya Mheshimiwa Zitto, tunayo majibu ya Mheshimiwa Waziri yanasambazwa kwenu hivi sasa. Hivi kuna ugumu gani kwenda kwenye hoja mbona mnazungumza mambo, mnajaribu Baba wa Taifa muende wapi, twende kwenye hoja tujaribi kuzijibu ili tuzifafanue.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, asante nashukuru katika yote uniongezee dakika zangu tatu ili nimalizie. Hii ni tatizo la kiswahili mimi ni lugha yangu ya tatu, Tume, Kamati mimi nazungumzia select committee basi tuseme ni Kamati teule ndiyo maana yake na ndiyo tunayoizungumzia hapa Mimi nasema hili si liliagizwa na Rais siku alipozungumza hapa Bungeni akasema ya kwamba mikataba itapitiwa kwa hiyo sio lazima tumsubiri yeye aje kutuambia hapa, ameshatoa order agizo tayari kwamba mikataba ichunguzwe na hapa naona imeandikwa ya kwamba ni Tume teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini mazingira.

Kwa hiyo ni wakati umefika sasa ili haya mambo yachunguzwe kwa sababu wanataka kuyajua na sio hayo tu mimi naweza nikakupa mfano hayo, kwamba Waziri Karamagi si yeye wa kwanza kufanya kitu ambacho kinaonekana kiko kinyume hata waliotangulia na wote vilevile wa Wizara hiyo ni lazima wachunguzwe vilevile wengine wanashika nafasi za juu sana sasa hivi ni kwamba hata katika mwaka 1980 Sheria ya Madini inatamka bayana ya kwamba maeneo yaliyo kwa ajili ya wachimba wadogo wadogo na yale yaliyo wachimbaji wakubwa yatakuwa hivyo na wasiingiliane. Lakini tunaona ya kwamba maeneo ya Mara yote yalitengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo kuanzia mwaka 1980 na Mawaziri waliyalinda hadi mwaka 1996 lakini ilipofika tarehe 14 Juni, 2006 alikuja Waziri ambaye aliyageuza yale maeneo na kuwapa wachimbaji wakubwa bila ridhaa ya wananchi na bila vilevile kuzingatia sheria inakataa hilo nalo linahitaji kuchunguzwa ni sehemu ya haya.

Kuna mengi sana ambayo yanahitaji kuchunguzwa katika migodi yote ambayo imepewa makampuni makubwa na pamoja na hii kampuni ya Barick ambayo sasa hivi tunaamini ya kwamba ina ukaribu sana na Serikali na mikataba inaweza ikasainiwa hata Motrio Cananda lakini hiyo mikataba basi iletwe hapa tuione wananchi nao wajiridhishe kwamba kweli hiyo mikataba ilikuwa ni sahihi kuna tatizo gani, kwanini inakuwa hofu kubwa sana halafu Wabunge hapa wanataka kufanya kitu kama ushabiki hii ni kazi ya wananchi tumepewa hapa kesho na kesho kutwa watakuja wengine tunataka iwe on record kwamba hayo mambo ambayo yanasemekena yalikuwa ni kinyume yamekuwa straight.

Kwa hiyo mimi navyoona ni kwamba tusiwe tunatumia Bunge kama sehemu ya ku-justify mambo ambayo si ya kweli, tumeapa kwamba tutailinda Katiba, na ningependa kutumia hii nafasi kusema ya kwamba katika viongozi wetu ambao ni Mawaziri wawe wanasimama kutetea kiapo chetu na wasitake kugeuza hili Bunge kama sehemu yao ya kupinda sheria za Katiba ya nchi. Kwa mfano natoa mfano hai hivi majuzi niliuliza swali kwanini Tarime kwa mfano itawaliwe kinyume cha Katiba na Sheria, akasimama Waziri wa Utawala Bora, akasema kwamba wale watu sio Watanzania kama Watanzania wengine tangu ukoloni bila Katiba, akasimama Waziri Mkuu naye akathibitisha hivyo hivyo kwamba...

SPIKA: Mheshimiwa nenda kwenye hoja tuna hoja ya Mheshimiwa zito vinginevyo nitakuzuia kabisa kusema kwa sababu huelekei kuchangia hoja.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, nilikuwa natoa mfano jinsi Mawaziri wetu wanavyokiuka Katiba hapa Bunge na ingefaa waombe radhi kwa hayo waliyoyatamka kwa ajili ya watu wa Tarime, mimi nasisitiza ya kwamba kwa sababu mimi kitu cha kuogopa mimi sina bwana, nasikia mimi nawakilisha wananchi hapa. Nasema hivi hii Tume yaani hii Kamati teule ya Bunge iundwe ili ukweli uonekane...

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU: Muongozo wa Spika.

SPIKA: Muongozo wa Spika, Kanuni.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU: Kanuni ya 55, naomba muongozo wako Mheshimiwa Spika, kwa sababu mchangiaji wa hoja hii naona sasa hivi anageuza hoja hii kuwa ni kama uwanja wa kuanza kuleta malumbano na hoja ambazo hazina msingi na kutoa matamshi ambayo kwa kweli yanaendana na kupotosha watu kwamba kwanza naomba umtake aeleze na atoe ufafanuzi kwamba ni kwa vipi Mawaziri wanavunja Katiba na wanakwenda tofauti ya Katiba inavyoagiza. (Makofi)

Lakini pili tunamuomba Mheshimiwa Mbunge anavyozidi kuchangia aende kwenye hoja na asianze kutafuta mambo ambayo hayasiki, hapa Bunge hili sio mahali pa kuhalalisha uwongo kama anavyodai kwamba sasa hivi tunageuza uwongo kuwa ukweli sio kweli, ukweli umewekwa wazi na Mheshimiwa Waziri na kama hoja basi hoja itolewe kupinga yale yaliyozungumzwa na Mheshimiwa Waziri katika kujibu hoja za mtoa hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tatizo sio kuuliza swali, kila mtu anafursa ya kuuliza swali na akajibiwa tatizo ni jinsi lilivyoulizwa kwa kuuza kwamba Mheshimiwa Waziri amedanganya, ukianza na shutuma umejibiwa ukweli sasa Bunge linatakiwa hapa kusema kwamba je hiyo shutuma ilikuwa ni ya ukweli? Nashukuru. (Makofi)

SPIKA: Kwanza nikuhakikishie kwamba dakika zako tunazihifadhi, lakini ni wewe mwenyewe unajisababishia matatizo kwa kwenda nje kabisa ya mada na kanuni haziruhusu. Namshukuru sana Waziri wa Nchi anatukumbusha hilo tuhuma ya kusema kuna Mawaziri kadhaa wanavunja Katiba ndani ya Bunge ni nzito sana lakini hazihusiani na mada hii kilicho mbele yetu hapa ni Serikali kutiliana sahihi mkataba wa mgodi wa Buzwagi wala sio sera ya madini kama wengine mnavyoendelea mimi napenda Waheshimiwa turudi kwenye mada yenyewe ili tuweze kujua ukweli uko wapi na uwongo uko wapi iko wapi kabisa. Mheshimiwa Zitto ametoa hizo tuhuma kama 11 Waziri amezijibu kwa mpangilio moja baada ya nyingine, semeni majibu yanatosheleza wapi hayatoshelezi, tutafikia mwisho vizuri tu, kwa hiyo Mheshimiwa Chacha Wangwe kwa maelekezo hayo hebu endelea sasa kwenye mada.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, mimi naheshimu maelekezo yako na ninaamini kabisa ya kwamba unaongoza Bunge letu kwa njia nzuri, mimi nilikuwa najaribu kuelezea kile ambacho kimezungumzwa hata na Wabunge wenzangu hapa ya kwamba Mheshimiwa Waziri kwamba hadanganyi, na hoja iliyopo hapa ni kwamba anadanganya na mimi nikawa natoa mifano hai ambayo nimeishuhudia hapa na Wabunge wakaishuhudia na wananchi jinsi ambavyo Mawaziri wanadanganya hapa Bungeni.

MHE. HAROUB S. MASOUD: Mheshimiwa Spika, kuhusu utaratibu.

SPIKA: Mheshimiwa Masoud.

MHE. HAROUB S. MASOUD: Mheshimiwa Spika, natumia kanuni Na. 50(8)(b) na naisoma kama ilivyo, inasema hivi kutumia haki yake ya kusema kwa madhumuni ya kutaka kuchelewesha shughuli za Bunge. Mhusika amefahamishwa na Mheshimiwa Waziri wa Nchi lakini bado anaendelea na kwa nia hii ina maana anataka kusababisha shughuli za Bunge zisiendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na wewe mwenyewe umemfahamisha vizuri sasa sielewi kama hajui kanuni au anataka kuibeza kanuni hii, naomba kuwasilisha. (Makofi)

SPIKA: Nampa nafasi ya mwisho Mheshimiwa Chacha Wangwe kurudi katika mada yenyewe, tafadhali rudi katika mada iliyo mbele yetu, ukirejea tena kwenye njia zako hizo ambazo hazielewiki itabidi nikusitishe.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kutambua kwamba wewe preciding wa ku-guide debate hapa Bunge. Na hawa wanaojaribu kunishika koo wangeacha nimalize kujenga hoja lakini basi kwa hivyo mimi narudi kwenye hoja maana mimi tunafahamiana hapa. Ni kwamba hoja iko pale pale kwamba ningeomba Waheshimiwa Wabunge ambao tunawakilisha wananchi waruhusu Kamati teule ya Bunge iundwe kwa ajili ya kuchunguza hii mikataba yote na mambo ambayo yamekuwa ni kero kwa wananchi kuhusiana na mambo ya migodi kuanzia mikataba na yale yaliyojitokeza juzi ya kuendelea kusaini mikataba mingine wakati ile aliyoisema Rais haijachunguzwa.

La kwangu ni hilo, lakini pia naomba uendelee kufanya nguvu ili hili Bunge lizindikuwa la kidemokrasia na lisiwe ni Bunge la mashabiki ambao wanakuja hapa kufanya kama kijiwe cha chama chao hapa. Nashukuru sana. (Makofi)

MHE. SUSAN A. J . LYIMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi ili na mimi nichangie katika hoja hii muhimu iliyo mbele yetu. Awali ya yote nami niungane na Wabunge wenzangu kukupa pole wewe binafsi na familia yako pamoja na familia ya Mheshimiwa Mzee wetu Chifu Abdallah Fundikira ambaye kwa kweli amelitumikia taifa hili kwa muda mrefu na kwa uaminifu wa uadilifu mkubwa, pole sana.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nadhani tayari umetuongoza hayo jinsi gani ya kujielekeza katika hoja hii na mimi nadhani nitatumia yale ambayo umetuambia. Awali ya yote naomba niunge hoja hii mia kwa mia kwamba Kamati teule iundwe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, labda nianze kwa majibu ambayo Mheshimiwa ametuambia na labda nianzie tu hili la kwake ambalo amesema kwamba awali amesema amechafuliwa sana jina lake, kimsingi nakubaliana naye, lakini pia hapo hapo akasema haoni haja ya kuundwa kwa hii Kamati teule.

Mheshimiwa Spika, mimi naona hapa kuna contradiction kama kweli amechafuliwa jina lake kiasi hicho alichosema na naamini ni kweli kwa sababu ni mtu mzima anauzoefu mkubwa na ameona kwamba amechafuliwa. Njia pekee ya kusafisha jina lake ni Kamati teule iundwe kwa sababu itaangalia ama ni Zitto kweli amesema uwongo ama ni yeye kwa hiyo Kamati teule peke yake ndiyo itaweza kumsafishia jina. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naelewa kwamba hapa kama itapigwa kura ni ukweli uliowazi kwamba Serikali itashinda kwa sababu hata tunavyosimama kujielekeza katika hizi hoja imeonekana kabisa kuna mpasuko kwamba upande wa Serikali wanatetea kusiwe na Kamati teule lakini upande wetu tunasema kuwe Kamati teule. Kwa hiyo mimi nilikuwa nashauri kwa kweli kama ni mwenzetu alichafuliwa jina, njia peke yake ya kumsafishia ni kuundwa kwa Kamati ambayo itatoa taarifa kamili ya nani amesema ukweli na hapo wananchi wataelewa kwa sababu tukipiga kura hapa nakubali kabisa kwamba wananchi hawataelewa kama kweli Mheshimiwa Waziri anasema kweli au ni Zitto amesema kweli. Kwa hiyo nilikuwa nafikiri Waheshimiwa Wabunge wenzangu tukubaliane kama kweli tunataka kumsafishia Mheshimiwa Waziri jina lake Kamati teule iundwe kama tunataka kumsafisha jina. (Makofi)

SPIKA: Hatua ya kwanza Mheshimiwa ni kujadili ama majibu ya Waziri yanatosheleza ama hayatoshelezi, logic mantiki inataka tutathimini majibu ya Mheshimiwa Waziri, kila saa nawarudisha huko hamkubali, kama huna hoja wala usijiorodheshe tu maana yake kama huwezi kusema tathimini ya aliyosema Mheshimiwa Waziri sasa tutaridhika vipi Bunge zima kuunda ama sivyo itakuwa kila anayejisikia anaomba Kamati teule, hili litakuwa Bunge la Kamati teule tu sasa. (Kicheko)

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa muongozo wako, lakini nadhani nilichokuwa nakisema nikujibu kile alichosema Mheshimiwa Waziri kwamba haoni haja ya kuundwa kwa Kamati teule, lakini mimi nasema kuna haja. Kwa sababu kama kweli yeye anaona hamna sisi pia tunaona kuna haja sababu ya hizo hoja ambazo wamezileta ambazo mimi nadhani hazijajibu hoja zote za Mheshimiwa Zitto.

SPIKA: Zitaje sasa hizo hoja.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Spika, labda niende kwenye suala zima la ajira, Mheshimiwa Waziri wakati anajibu amesema kwamba kampuni hiyo ya Buzwagi itaweze kuajiri wafanyakazi 696. Tutakubaliana kwamba kumekuwa na wawekezaji wengi katika madini na siku zote ajira hazijapatikana wengi wanaoajiriwa wamekuwa ni makampuni kutoka nje, kwa hiyo bado nadhani hii si hoja. Lakini pia kwamba amezungumzia suala la tofauti kati ya kudurusu sheria na kudurusu mikataba.

Mheshimiwa Spika, mimi naaamini kabisa mikataba hii inaandikwa kisheria sasa nashangaa hii contradiction iliyoko inatoka wapi, kwamba yeye anadai kwamba mikataba imeshafanyiwa review lakini hapo hapo anasema sheria ndiyo hazijafanyiwa review sasa mimi najiuliza hivi hii mikataba inafanywa bila sheria kwa sababu naelewa mikataba mingi inafuata sheria, sasa kama sheria hazija-.... hii mikataba inakuwaje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini labda niende kwenye hoja za Mheshimiwa Zitto, kama nilivyosema awali naunga mkono lakini mimi nadhani tatizo hapa sio suala la mkataba umesainiwa lakini mimi nadhani tatizo hapa sio suala la mkataba umesainiwa wapi, kama alivyosema mwenzangu ni kwamba hata ungesainiwa Nairobi, ungesainiwa Marekani sisi hatuoni tatizo. Lakini tatizo tunaloliona sisi ni ule uharaka wa kusaniwa kwa huu mkataba wakati tulishaambiwa kwamba bado kuna review bado zinafanyika. Kwa hiyo mimi nilikuwa nadhani hoja hapa ni Waziri atuambie ni kwanini amesaini mkataba whether ni Dar es Salaam au ni Uingereza lakini tunataka kujua ni kwanini umekuwa na uharaka kiasi hicho cha kusaini mkataba huo.

Mheshimiwa Spika, lakini lingine nililotaka kulizungumzia kuna ile methali inayosema kizuri chajiuza kibaya cha jitembeza. Ninaamini kabisa sisi migodi yetu ni mizuri, kwa hiyo kama Waziri ni Mtanzania ni hii kampuni iko Tanzania hatuoni sababu ni kwanini aende mpaka nje huko kwenda kusaini, na je gharama hizo zilikuwa za watu gani kwa sababu hapa tumeambiwa kwamba hii Kamati itachukua hela nyingi lakini bado je, gharama walizotumia wao kwenda nje zilikuwa sio kodi za wanchi?

Mheshimiwa Spika, jingine ambalo nataka kuzungumzia ni kwamba naomba niunge hoja mkono kwamba Kamati teule iundwe ili tuweze kupata ukweli wa mambo yote asante. (Makofi)

MHE. ADAM K. A. MALIMA: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba kukushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia hoja hii binafsi.

Mheshimiwa Spika, mimi pia kama walivyofanya wenzangu, nianze kwa kukupa salamu za pole kwa msiba wa mzee wako na mzee wetu, mzee Abdallah Fundikira, Mungu amlaze mahali peponi, Inshallah.

WABUNGE FULANI: Amen.

MHE. ADAM K.A. MALIMA: Mheshimiwa Spika, hoja iliyoletwa hapa mimi jana nilisikia na wakati nazifanyia tafakari kama nitachangia au sitachangia, nadhani katika mambo niliyosikia moja ilikuwa ni suala la kwa nini mkataba huu ulisainiwa London na kulikuwa na uharaka gani halafu kwa yale ambayo niliyapata mimi sijui kama nimekosea nadhani kulikuwa na hoja kwamba Waziri wangu wa Nishati na Madini anatuhumiwa kwamba alikiuka sheria na taratibu. Katika majibu yake aliyoyatoa humu ndani ya jumba lako hili Tukufu kwamba alisema uongo.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa mujibu wa kanuni zako za Bunge na sisi wengine tumepata bahati by necessity kuzisoma hizi kanuni na kuzielewa vizuri tumepata kuzielewa sasa hivi na kusema kweli tuhuma ya kumwambia Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambaye anaapa mbele ya Rais kwamba anakuja katika Bunge hili na kusema uongo ni tuhuma nzito. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi naungana na wenzangu ambao wanasema kwamba kama kuna hoja basi ziletwe. Kama ninavyosema baada ya kupata ule mtihani kidogo huwa siachi mbali kanuni zangu, naomba nisome yafuatayo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Kamati teule, kanuni ya 104(1), kamati teule yaweza kuundwa na Bunge kwa madhumuni maalum, kwa hoja mahususi itakayotolewa kwa ajili hiyo na kuafikiwa. Hapa pana suala la madhumuni maalum, hoja mahususi hoja zenyewe ndio zimeletwa kama ndio hizo mahususi zimeshajibiwa. Sasa hoja zimeshajibiwa tunazijengea hoja bado tunataka kamati teuli, ya nini tena jamani? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi naomba kubwa zaidi kwamba mwaka huu mwezi wa tatu au wa nne sikumbuki ilifanyika semina ya viongozi waandamizi wa Serikali na mashirika ya umma na katika hilo ambalo nadhani alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi wakati anatoa mada yake alisema kwamba lazima tuwe na utaratibu Tanzania hatuwezi kuendesha kama business as usual, kama kuna opportunity ambayo inayojitokeza ya kwamba tuna emergency investor anatokea tunataka tuanze kurudi tuende wapi, turudi hizi, tufanye nini opportunity inapotea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi namuomba Waziri wangu wa Madini mimi nina-guess Mkuranga bado suala linajadiliwa ikitokea opportunity ya kuja na investment namna hiyo mimi naomba afanye haraka, hata ikiwa kusaini huko New York au wapi afanye. Lililokuwa linanisumbua mimi ni manufaa ya dhahiri ya mradi huo yapo? Au tumefanya haraka kwa sababu kuna jambo lilitaka kufichikana. Waziri ametoa maelezo kwamba alisaini one kwa sababu kulikuwa na window of opportunity ambayo ilikuwa inaisha Machi 2007, lakini baada ya kupata ushauri wa mining advisory committee akaa na kusema kulikuwa na mrahaba na kodi ya milioni zinazotarajia kufikia 198 milioni US Dollars, pay as you earn milioni 50, mambo ya investment za umeme na infrastructure zingine totalling to 800 milioni US Dollars. Sasa opportunity kama hiyo kweli unaiacha tu ili jamani hebu njooni tukazungumzie Dar es Salaam, mimi sijaelewa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo mimi naomba niseme nimeridhia majibu wa Mheshimiwa Waziri na kwa mujibu wa tafakari ninayoifahamu mimi tangu tukiwa katika kampeni hari mpya na kasi mpya ndiyo hii. Sasa kama kuna watu wanataka kuturudisha nyuma kama anavyosema Waziri Mkuu hao wako kwenye boti lingine siyo boti hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni suala hili nimeona hapa kidogo kulikuwa na hoja ya kusema kwamba mtoa hoja ameuliza swali ameomba muongozo, lakini mimi nadhani kwenye ile hoja ambayo ilisema kwamba Waziri amelidanganya Bunge pale sidhani kama kulikuwa swali kwa sababu sikuona mfumo wa swali nimeona suala la shutuma direct iliyoenda kwa Waziri wa Serikali na hapa hatuko by partition lazima tukubaliane kwamba lile halikuwa swali bali lilikuwa shutuma na hivyo Waziri ana kila haki ya kujisikia kwamba amekuwa defend na sababu ya sisi kuzungumza humu ndani ni kuliweka sawa, sasa sijui kwa nini mtu anasema tunaomba tena Kamati teule ichunguze kama Waziri a-feel aggrieve, jamani mtu akitukanwa si lazima ajisikie vibaya kwa hiyo mpaka iundwe Kamati teule ndio ujisikie, kama ametukanwa na alijisikia vibaya anajisikia vibaya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi tumo humu ndani na sisi tuna uwezo wa kusema uongo tumeuona dhahiri au kweli tumeuona dhahiri tukikubaliana basi tumekubaliana na lichukuliwe hatua nyingine. Kwa mujibu wa Bunge lako Tukufu na kanuni zilizopo kwa hivi sasa, kwa hiyo mimi nataka kusema kwamba kwenye upande wa economic opportunity iliyokuwa imejitokeza, kwa maelezo haya labda kama mtoa hoja anataka kusema kwamba maelezo haya hayako sawa, lakini kama maelezo haya yako sawa mimi nampongeza Mheshimiwa Waziri na ninamkaribisha Mkuranga atufanyie hivi hivi kwenye suala la gesi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nijikite pale alipozungumza kaka yangu Mheshimiwa Suleiman Omar Kumchaya kwamba tunaraji kwamba tunapozungumzia masuala kama haya tutambue kwamba tunataka tuwe by partition na pia tuheshimu origin za watu wote humu ndani tunakotoka. Kwa hiyo mimi naomba niseme tu kwamba kama alivyosema Mheshimiwa Suleiman Omar Kumchaya tunapozungumza humu ndani tukae tukijua kwamba Watanzania chungu nzima wako wako huko nje wanatuangalia tuna obligation ya kusema yale ambayo tunaamini ndani ya nafsi kwanza, pili kama ndio kuna hoja nyingine ambazo ni za kujengewa basi nazo zifanyiwe tafiti na sisi kama wachumi na Wabunge na wanasheria tuna specialization nyingi humu ndani obligation yetu ni kufanya utafiti wa kina.

Mheshimiwa Spika, mimi naomba nimshukuru Mheshimiwa Nazir M. Karamagi sikuona chochote ambacho amefanya ambacho kinaenda kinyume na maagizo aliyopewa kama kiongozi wa Chama cha Mapinduzi, naomba nimshukuru kwamba katika ku-promote investment hiyo ndiyo sehemu ya Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi na sisi wengine ambao tunaraji tumuunge mkono hapa Bungeni, kila atakaposimama yeye na Mawaziri wenzake kuuhami uchumi wa nchi hii sisi ni wajibu kuwatetea kwa kila hali.

Mheshimiwa Spika, lakini la mwisho, naomba niseme tu kwamba haya mambo ya kuleta hizi fitina na ghasia watu wakae na kujua kwamba tunatazamwa nje, sasa mnapojenga hoja hizi na mnatumia fursa hizi za viwanja vya Bunge kuleta maneno ya uongo namna hii mimi naomba Bunge lako litumie kanuni zilizopo ili mambo haya ya kuliongopea Bunge hapo tutakapothibiti na tutathibiti hapa hapa mchana tutajua uongo uko wapi, tukapolithibiti basi Bunge lako lichukue hatua hapa hapa ili liwe mfano kwa atakayekuja baadaye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa na mengi ya kusema lakini nimezidiwa, mengi yamesemwa na walionitangulia, naomba kumpongeza sana Waziri wa Nishati na Madini kwa majibu yake mazuri sana na naomba kuwasilisha, ahsante sana. (Makofi)

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika, na mimi nashukuru pia kwa kunipa nafasi niweze kuchangia kidogo hoja iliyopo mbele yetu.

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nichukue nafasi hii kukupa pole wewe mwenyewe, familia ya mzee Chief Abdallah Fundikira pamoja na Watanzania wote kwa msiba mzito uliotupata. Pia naomba kumpa pole Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa John Magufuli kwa kifo cha mpenzi baba yake Mungu aziweke roho za marehemu wote peponi. Amen.

Mheshimiwa Spika, kwanza naanza mchango wangu kwa kuunga mkono hoja kwamba kuna kila sababu ya kuundwa Kamati itakayoangalia nini kilichosainiwa kwenye mkataba uliosainiwa huko nje wa madini. Suala la mikataba mibovu hapa Tanzania ni tatizo kubwa sana na kila mmoja ameona hili suala siyo Wabunge, siyo Watanzania wanaotuangalia wamekuwa wakiangalia wamekuwa wakiangalia ni jinsi gani mikataba mibovu imepelekea Taifa hili pasipoeleweka mikataba mingi imetupeleka pabaya Serikali wakati mwingine imekuwa inaingia hasara kubwa kwa sababu mikataba inayoingiliwa inakuwa haina utaratibu mzuri, haina umakini na hivyo kuletea Taifa hasara kubwa.

Mheshimiwa Spika, hasa suala la mikataba ya madini ni suala ambalo ni la msingi kabisa Watanzania na sisi Wabunge tukiwa kama wakilishi wa Wananchi tusilichukue kirahisi rahisi hivi hivi, nina imani kabisa hapa Bungeni hakuna Mbunge ambaye hajawahi kuona ubovu wa mikataba ilivyopelekea Taifa hili pasipoeleweka. Watanzania tuna rasirimali nyingi sana, tuna madini mengi sana lakini kila siku hapa Bungeni tumekuwa tunasema kwamba rasilimali zetu hazitumiki ipasavyo matumizi yake siyo mazuri wanaofaidika ni wawekezaji wageni ambao wanaenda kujenga nchi yao na watu wao na sisi Watanzania tunabaki kuwa maskini. Kwa hiyo tungependa kujua kwa nini Waziri aharakishe kusaini huo mkataba ndio kinachotia wasiwasi pale ni kwa nini ameharakisha huo mkataba?

Mheshimiwa Spika, kulikuwepo na uharaka gani wa kumchukua mwanasheria hapa amfuate kule London kwenda kusaini mkataba jambo ambalo rasilimali yetu najua ipo hapa nchini tunajua kwamba madini yapo hata mwakani, thamani ya kitu inapanda siku baada ya siku huwezi kuniambia kwamba leo madini pengine labda kilo Sh.5,000/= labda kesho kutwa itakuwa Sh.2,000/= haiwezekani thamani ya shilingi inapanda dola inapanda kila siku tukiangalia kila mwaka jana na mwaka huu ni tofauti na hivyo hata thamani ya madini yetu inazidi kupanda, kulikuwa hakuna ulazima huo ndio maana inatia wasiwasi kumesainiwa nini huko ndani. Kwa hiyo mimi kwenye hii naunga mkono ninaomba kwamba Wabunge pamoja na wananchi ili waweze kuridhishwa na mkataba huu uliosainiwa Mheshimiwa Waziri katoa vielelezo akiwa kama ni mjibu hoja, mtoa hoja Mheshimiwa Kabwe Zitto na yeye atakuwa ametoa vielelezo vyake basi vielelezo vyote viwekwe pamoja vipitiwe na hii kamati huru na kupitia huu mkataba ili ijulikane kwamba haki iko wapi na Watanzania wote tuweze kujiridhisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri kasema kwamba kazi ya kupitia mikataba imekamilika mwaka jana Novemba lakini ningependa kujua sisi Wabunge kama tunaotetea wananchi kila siku tunajadili kwamba mikataba ipitiwe, tulijulishwa hilo? Hatujajulishwa na mpaka sasa hivi kama kweli mwaka jana mwezi wa 11 ni mwisho wa kupitia mikataba mabadiliko yaliyofanyika tunayajua mpaka sasa hivi kwa sababu ninavyofahamu hata hivi karibuni tu yamekamatwa makontena bandarini yanasafirisha mchanga wa madini, limetangazwa kwenye vyombo vya habari kila mmoja amesikia, mchanga ule umeyeyuka kwa mazingira yasiyoeleweka yote haya tunasema ni kwa sababu ya mikataba mibovu ya madini. Je, kama kweli imemaliza kupitiwa mbona bado kuna kasoro nyingi sana?

Mheshimiwa Spika, mimi kwa hapa sina mengi ninaomba sana iundwe Kamati tuweze kujua kwa kuanzia na huu mkataba mmoja pengine tutajua na mingine ambayo inaingiwa pasipo kujua nini kilichosainiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nashukuru kwa kunipa nafasi hii, ahsante sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)

MHE. MANJU S. O. MSAMBYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuniruhusu na mimi nichangie hoja iliyoko mbele yetu, hoja ya mdogo wangu Mheshimiwa Zitto Kabwe Zubeir kwanza siiungi mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nilifuatilia mjadala uliokuwepo Bungeni siku ile Waziri anawasilisha makadirio ya Wizara yake na yale mengine yote yaliyojiri siku ile, kwa bahati nzuri mimi nimekuwepo kwenye Wizara hiyo lakini kwa bahati nzuri vile vile sheria hii imetungwa mimi nimekuwa Naibu Waziri pale. Sasa nilipata hofu na kwa kweli nilikuwa nashawishika nimuunge Zitto Kabwe mkono kama mkataba huu ungekuwa umesainiwa na Mheshimiwa William Ngeleja kwa sababu kwa mujibu wa sheria hana instrument za kusaini mkataba kama Naibu Waziri, kwa sababu hata mimi nilipokuwa Naibu Waziri sikuwa na instrument za kusaini au kufuta chochote kwa mujibu wa sheria. Sasa nilikuwa napata hofu pengine William Ngeleja ndio alisaini nikafikiri pengine hilo ndio kosa, kumbe kosa ni Waziri Nazir Karamagi kusaini mkataba huu London, lakini waliotanguliwa kusema wameeleza na Mheshimiwa Waziri mwenyewe kaeleza sababu zipi zilizopelekea yeye na uharaka gani uliopelekea mkataba ukasainiwa kwa wakati ule na huko ulikosainiwa.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Lucy Msafiri alipokuwa anazungumza hapa ametueleza tumekuwa nazo video conference zingine zinaitwa tele conference mtu mmoja yuko Tokyo mwingine anaweza kuwa hata yuko kwetu Ujiji na mwingine akawa yuko London na mkutano ukaendelea umeme uko Ujiji japokuwa wa kubabaisha na mkutano ukaendelea na watu wakafikia uamuzi ambao waliukusudia au kukubaliana au kutokukubaliana. Sasa kwa Mheshimiwa Waziri kusaini mkataba London lilikuwa si tatizo, maudhui yaliyoko kwenye mkataba na kwa bahati nzuri mkataba huwa ni document ambayo mtu mwenye mashaka anaweza akaipitia ile document na akaisoma akaona upungufu uliopo kwenye mkataba ule,mimi nilidhani mdogo wangu Mheshimiwa Zitto Kabwe angeomba auone mkataba ule je, una upungufu mkataba kama mkataba au hauna? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini lingine lililoko kwenye hoja ambalo Mheshimiwa Waziri amelijibu vizuri ni suala la environmental impact assessment ambayo ni moja ya hoja ambayo Mheshimiwa Zitto Kabwe ameitoa hapa. Mheshimiwa Waziri ameeleza vizuri kabisa kwamba hatua hiyo inafikia wakati mtu kapewe mining licence, leseni ya kuchimba ambayo mpaka leo tunavyozungumza Mheshimiwa Waziri kaeleza vizuri kwamba leseni hiyo haijatolewa sasa haya mashaka ya invironmental impact assessment kwamba kibali kimetolewa, mashaka haya yanatoka wapi. Lakini Mheshimiwa Waziri vile vile ameeleza nashukuru sisi tumegawiwa maelezo yake hata kabla hatujatoka kaeleza vizuri faida itakayotokana na kusaini mkataba huo na vitu gani ambavyo kama alivyosema Mheshimiwa Adam Malima hapa ni vitu gani tungevikosa kama mkataba huu ungechelewa kusainiwa.

Mheshimiwa Spika, mimi nilidhani tungekuwa na kila sababu ya kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa uharaka aliouchukua kwa kuweza kutafakari kwa haraka kwa sababu angechelewe ndio unakuja ule usemi wa kiswahili chelewa chelewa utamkuta mtoto si wako. Sasa Mheshimiwa Waziri hakutaka amkute mtoto si wake, aliona apeleke posa achumbie tayari apate mtoto huyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, document hii ambayo Mheshimiwa Waziri ametupa hapa ina vielelezo vyote kuna viambatisho ambavyo Mheshimiwa Waziri kafanya juhudi kaviweka ili kwa yoyote mwenye mashaka kwa yale ambayo Waziri mwenyewe ameyaeleza kutetea yale aliyoyafanya, kujibu ambayo Mheshimiwa Zitto Kabwe ameyaeleza aweze kupitia ili tutakapofika kwenye majumuisho Bunge hili kama walivyotanabaisha wasemaji waliotangulia lipate kuchukua uamuzi kwa sababu hoja hii si ya Mheshimiwa Zitto Kabwe tena, hoja hii ni hoja ya Bunge na Bunge ndio lenye mamlaka ya kuamua hoja hii tuipeleke wapi, kumekuwa kuna mashaka hapa mtu amesimama anasema najua tayari tukisimama kupiga kura unaanzaje kuwa na mashaka kabla haujafikia hatua hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapoeleza kwamba tunawatumikia Watanzania ni kweli, sisi wote hapa kwa pande zote tunawatumikia Watanzania ni katika kuwatumikia Watanzania hao ndio maana mimi naamini Mheshimiwa Waziri pengine ili kuandaa kujibu hoja hizi hakupata usingizi na katika kuwatumikia Watanzania amejinyima usingizi ili awatumikie Watanzania atoe majibu yaliyo sahihi. Kama hivyo ndivyo na ni kweli ndivyo ilivyo haya aliyotoa Mheshimiwa Waziri kwa maoni yangu na ninaamini ni kwa maoni wa wengi na hasa wale walionitangulia kuzungumza yamekidhi na yamejibu hoja ambazo Mheshimiwa Zitto Kabwe ameeleza na kwa misingi hiyo hakuna sababu ya kuunda kamati teule ya kuchunguza kwa sababu unaanzisha kamati kama Mheshimiwa Waziri asingekuwa ametoa majibu ya kujibu yale ambayo tuhuma zimetolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo mimi sina ya ziada ninaamini kabisa Mheshimiwa Zitto Kabwe atakuwa ameelewa, amefuatilia na waswahili wanasema muungwana akivuliwa nguo anachutama, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Sasa Mheshimiwa Manju Msambya baada ya mazungumzo yake umeketi au umechutama, namtania tu jirani yangu yeye ni Kigoma Kaskazini na mimi ni Urambo Mashariki. (Makofi/Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge bado ninao wachangiaji watano ambao tutaweza tunao muda wa kuweza kuwasikiliza jioni, nisisitize tu hapa hoja hii ya Mheshimiwa Zitto Kabwe inajadiliwa sasa na Bunge, ametoa maswali na hoja mbalimbali ndani ya ile hoja yake Mheshimiwa Waziri kwa mujibu wa utaratibu wetu wa kanuni kuhusu masuala kama haya ya hoja binafsi Mheshimiwa Waziri mhusika Waziri wa Nishati na Madini ametoa majibu na yamesambazwa. Ninawaomba nyie wa jioni maana yake ndio tutafikiwa hatma ya kupiga kura mjielekeze kwenye hayo yanagawiwa, Mheshimiwa Kabuye hajapata na ni mchangiajia basi tafadhali yagawiwe ili jioni tuna kazi ambayo wananchi wanaitazama hapa nayo ni kuamua kama yale maswali ya Mheshimiwa Zitto Kabwe yamejibiwa na kama yamejibiwa na Bunge itakuwa hatua ya kamati teule haina maana, lakini kama mkiridhika hayajajibiwa hapo ndio unaanza kuzungumzia sasa kuunda kamati nyingine nje na nikumbushe tu kamati teule kwa mujibu wa kanuni ya 105 Spika anaiunda kutoka miongoni mwa Wabunge kwa hiyo sisi hawa hawa siyo kwamba utatafuta utaalamu mwingine ni Wabunge kwa hiyo kama kwa umoja wetu tutaridhika njia moja au nyingine basi hatua inayofuata ni dhahiri kabisa, yaani kama tukiona majibu yanatosheleza tuna uamuzi, tukiona hayatoshelezi tuna uamuzi.

La pili nilikuwa nakumbusha tu kwamba vijana wetu hawa wanaogawa karatasi page boys and page girls mara nyingine mnawapa vitu vingine ambavyo ni binafsi kabisa na kuwalazimisha kwenda mpaka kantini picha sijui vitu gani, sasa wanatakiwa wahudumie shughuli za Bunge humu naomba sana wakiyaona mambo yenyewe ni binafsi kwa kweli nimeshawaambia wakimbie tu waweke kwenye pigeon hole basi inatosha. Lakini kumfuata Mheshimiwa Mbunge mpaka kwenye jengo la utawala kwa karatasi ambayo ina mambo binafasi ni kudhoofisha huduma ndani ya mkutano huu. Kwa hiyo Katibu wa Bunge asimamie na twende na utaratibu huo tu, tuwape kazi ambazo zinaendeleza shughuli za Bunge badala ya hayo mengine ambayo hayahusiki.

Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge baada ya kusema hayo na muda uliosalia hautuwezeshi kuita mchangiaji yoyote kwa hiyo sasa nasitisha shughuli za Bunge hadi saa 11 jioni leo.

(Saa 06.53 Bunge Liliahirishwa Mpaka Saa 11.00 Jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

(Majadiliano yanaendelea)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mtakumbuka zilipositishwa shughuli za Bunge pale saa saba, nilikuwa bado ninao wazungumzaji watano. Nitaona kama wote wanaweza kupata muda kwa sababu inabidi tena na mtoa hoja hatimaye apate nafasi ili aweze kuhitimisha hoja yake. Eeeh mtoa hoja hayupo? Ana udhuru eeh. Basi vema.

Sasa ninao wafuatao, Mheshimiwa Siraju Kaboyonga, Mheshimiwa Phares Kabuye, Mheshimiwa Mudhihir Mudhihir, Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir na Mheshimiwa Waziri wa Miundombinu. Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed ameniletea ombi la kuchangia, tutaona kadri inavyokwenda maana yake wengine wanachangia dakika tano wanamaliza, kumi sasa inanishinda kuweza kutabiri kabisa.

Lakini kwa sasa namwita Mheshimiwa Siraju Kaboyonga wakati huo huo Mheshimiwa Phares Kabuye ajiandae.

MHE. SIRAJU J. KABOYONGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami kuwa mmoja wa wachangiaji wa hoja iliyo mbele yetu mchana huu ambayo imeanza toka asubuhi.

Awali ya yote, napenda nianze kwa kusema kwamba baada ya majibu ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, kwa kweli nimeridhika kwamba hakuna sababu ya Bunge hili kuunda Kamati Teule kwa ajili ya kufuatilia mambo aliyoyasema mtoa hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, moja ya hoja za mtoa hoja ni kwamba anadadisi kusainiwa mkataba nje ya nchi. Sasa suala hapa si kusaini mkataba nje ya nchi au ndani ya nchi isipokuwa la msingi ambalo mtoa hoja angepaswa kutuambia ni kwamba je katika kufanya hivyo kuna sheria yoyote ya nchi iliyovunjwa? Kama hakuna sheria ya nchi iliyovunjwa kwa sababu mkataba umesainiwa nje au umesainiwa mahali popote, basi sioni kama kuna sababu ya kuendelea na malumbano juu ya jambo hili kwa ajili tu mkataba ulisainiwa nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ni kwamba kwa nini mkataba huu ulisainiwa wakati zoezi la kudurusu mikataba iliyotangulia bado linaendelea. Kwanza ni vizuri tufahamu kwamba kampuni ya Barrick ni miongoni mwa kampuni zinazochimbwa madini hapa nchini na ambayo mikataba yao au mikataba yake ni miongoni mwa mikataba ambayo tayari Serikali inaidurusu. Kwa hiyo, kutokana na uzoefu ambao Serikali imepata wakati wa kudurusu mikataba mingine ya nyumba ya Barrick ni dhahiri Serikali itatumia uzoefu huo au imetumia uzoefu huo katika kuingia mkataba huu wa maendeleo yaani Mining Development Agreement ambao kwa kweli ni mwanzo tu wa kuiwezesha kampuni hii ya Barrick kutengeneza feasibility study, design na mambo mengine yanayohusiana na mradi huo kabla ya kupata mining licence na kuanza kuchimba. Kwa maana hiyo, ni kwamba utakapofika wakati wa kupata licence ya kuchimba itatolewa hiyo licence pamoja na mkataba ambao utaonyesha terms and conditions ambazo ni lazima Barrick azifuate katika utekelezaji wa mkataba huo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini la msingi hapa ni kwamba Serikali yetu imefanya jambo zuri la kiungwana hata baada ya kufahamu kwamba kulikuwa na matatizo katika mikataba iliyotangulia huo ambao ni sehemu ya majadiliano ya leo, hatukuivunja hivi hivi tu baada ya kufahamu kwamba ina matatizo na hatukuitengeneza vizuri. Tulifanya hivyo kwa kuzingatia jambo moja kubwa pamoja na mengine kwamba Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa inayojulikana kwa kifupi kama MIGA (Multiletaral Investment Guarantee Agency). Ukishakuwa mwanachama wa MIGA unawapa matumaini makubwa sana wawekezaji kutoka nje kwamba nchi hiyo ambayo ni mwanachama wa MIGA inafaa kwenda ku-invest kwa sababu hawawezi wakukufanyia mambo ya kihunihuni, humuwezi kuingia mkataba leo kesho wakaubadilisha, haiwezekani. Kwa sababu tukifanya hivyo tutakuwa tunajiharibia sura yetu mbele ya international community kuifanya Tanzania kama destination ya investors. Kwa hiyo, kwa sababu hiyo ndio maana tumezungumza nao hao wenye makampuni ambapo Barrick ni mojawapo ambayo yalitangulia katika kuwekeza katika eneo hili la madini.

Mheshimiwa Spika, eneo la 15% interest on unredeemable capital, hili nalo mtoa hoja amelivalia njuga na kusema kwamba ni tatizo. Sasa mimi kabla sijaendelea zaidi nilitaka nitumie fursa hii kulielezea Bunge letu Tukufu kwa maana ya kuelimishana tu na kuliweka jambo hili wazi zaidi ni kwamba kwa kweli kile kitendo tu kwamba hii 15% unredeemable capital ilikuwepo kama interest juu ya capital ambayo haijakuwa unredeemed ilikuwa ni kosa. Kosa lenyewe lilikuwa linaifanya Taifa hili liendelee kulipia gharama za mwekezaji ambazo initially zilikuja hapa nchini au zinapaswa kuja hapa nchini kama mtaji (equity). Malipo au reward ya mtu anayeleta equity kama risk capital ni dividends sio interest. Hapo awali Serikali ilipokuwa imeweka kwamba kama katika mwaka wa kwanza na wakati ule kabla hatujafanya review ya mikataba iliruhusu recovery ya 100% ya capital iliyokuwa invested. Katika review exercise Serikali ikaona kwa kufanya hivyo tungechelewa sana kuanza kupata faida kutoka kwenye miradi hii kwa sababu depreciation ya 100% ni kwamba unamfanya yule mtu aliyeleta mtaji wake kwanza a-recovery yeye kwa asilimia 100 akishamaliza ndio tunaanza kufikiria na gharama nyingine. Serikali imelibadilisha hili na sasa chini ya taratibu ambazo Serikali imefanya mwekezaji atakuwa amepewa ruhusa ya ku-recovery 80% mwaka wa kwanza na 50% subsequent years. Dhamira ya kufanya hivyo ni kuwezesha yale mapato ambayo kampuni iliyokuja hapa nchini kuchimba madini inapotoa gharama zake zile gharama za depreciation zisiwe kubwa sana kiasi cha kupunguza kiasi kinachobakia ambako huko ndiko tunakoweza kuona kama na sisi kama nchi tunaweza kufaidika kupata cooperate tax. Haya ndio yaliyofanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye 15% of unredeemable capital hoja ni hiyo hiyo, mantiki yake ni kwamba imeondolewa ile 15% kwenye unredeemable capital ili ile unredeemable capital isizaliane tena kwa kutumia asilimia 15. Kwa sababu kadri inavyoendelea kuzaliana ile unredeemable capital haitalipwa hiyo siku zote sisi tutakuwa tunamlipa yule mchimba madini tu ndio maana imeondolewa. Kwa kufanya hivyo, mimi nilidhani mtoa hoja angeipongeza Serikali kwa kuja na utaratibu huu wa kuiondoa kabisa ile unredeemable capital. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja yake ni kwamba haikuja Bungeni ili iweze kuondolewa. Nyaraka za Waziri zimeonyesha dhahiri kwamba iliondolewa kwa kupitia Bunge letu Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kwanza ni kitendo kizuri kinamfanya mwekezaji wa nje aanze kulipa kodi mapema. Pili, kiliondolewa kwa kupitia Bunge lako Tukufu kwa kupitia Acts na Financial Bills ambazo zilikuja humu kama tulivyoonyeshwa leo na miongoni mwa hizo tunazo hapa kama vielelezo. Kwa hiyo, hiyo nayo sio hoja ya kusema kwamba tuunde Kamati Teule ili tuweze kuitazama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kuelezea haya, nataka kusema kwamba huyu Barrick ambaye ndiye amepewa mradi huu tunaouzungumza leo yeye alikuwemo katika mazungumzo ya awali kwenye miradi ya nyuma. Kwa hiyo Serikali imeshazungumza naye huyu na inafahamu matatizo, maeneo yenye matatizo katika mikataba Barrick anaelewa na Serikali inaelewa. Kwa hiyo tumeingia naye katika mkataba huu sote wawili tukiwa tunajua kwamba hata kabla ya sheria mpya ya madini kuja tena na kupitishwa upya maeneo yenye matatizo yamekwishaeleweka na kwa maana hiyo huu mradi wa Buzwagi nao umefaidika katika yale majadiliano yaliyokwishafanywa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hivyo na kwa sababu muda wetu hautoshi wote kuendelea na haya mambo, nadhani nitumie fursa hii kusema kwamba baada ya kutoa hoja hizo sioni sababu za msingi za kukubali kuunda Kamati Teule ya Bunge kwa ajili ya suala hili kwa sababu mtoa hoja ameshindwa kudhihirisha kwamba kweli aliyoyasema ni kweli na sisi kupitia Waziri wetu wa Nishati na Madini amemjibu kikamilifu na kumuonyesha kwamba hoja yake haina msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Msemaji wangu anayefuata hayupo kwa hiyo ninamwita wa upande wa Upinzani, Mheshimiwa Kabuye hayupo, kwa hiyo namwita Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed.

MHE. HAMAD RASHID MOHAMED: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza naunga mkono hoja mia juu ya mia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Zitto. Mheshimiwa Zitto alichokifanya kwanza ametujulisha Watanzania kwa mara ya kwanza kwamba kuna mkataba umesainiwa nje ya nchi ambao hatukuwa na taarifa nao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hicho ni kitendo kimoja kizuri kwamba taarifa ambayo Serikali haikutupatia kwa kupitia kwake sasa Serikali imetupa taarifa rasmi. Namshukuru sana kwa hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pili, nimekuwa naangalia maelezo ya Mheshimiwa Waziri, namshukuru sana na nampongeza sana yeye ni rafiki yangu sana lakini kuna moja ambalo amelisema kwamba bila ya utafiti basi hupaswi kuzungumza. Sasa ili ufanye utafiti lazima upate taarifa. Kwa mujibu wa Katiba kifungu cha 63 na sheria ya Immunities and Privileges Act, kifungu cha 10 kinatupa mamlaka sisi Wabunge kuomba nyaraka zozote Serikalini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi mwenyewe binafsi tarehe 17/7/2007 nilimwandikia Waziri Karamagi nikimwomba taarifa ya miaka mitatu ya Alex Stewart na nikanakili barua hii kwako na kwa Waziri Mkuu. Waziri Mkuu ndani ya Bunge hili alisema kwamba Serikali haikutoa nyaraka. Kwa taarifa yako Mheshimiwa Spika mpaka leo hata barua kujibiwa sijajibiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Zitto Kabwe alimwandikia Waziri akiomba apatiwe mkataba wa Buzwagi tarehe 17/7/2007 lakini mkataba huo hakupewa mpaka leo. Sasa, hivi Mheshimiwa Kabwe afanyeje research wakati umemnyima nyaraka wakati sheria na Katiba ya nchi inamruhusu Mheshimiwa Mbunge yeyote kupata nyaraka hizo! Sasa mnaweza kutulaumu kwamba hatufanyi utafiti, ni kweli utafiti tunaofanya ni finyu kwa sababu Serikali inatunyima nyaraka na tunazidai kwa mujibu wa sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa nini tunaomba sasa Kamati Teule iundwe? Pengine kwa kupitia Kamati Teule hizi nyaraka zitapatikana na sisi tuna experience na hiyo. Tuliunda Kamati Ndogo ya PAC tukapata nyaraka ya Williamson Diamond lakini kwa njia ya kawaida ndani ya Bunge hili ilishindikana kupata nyaraka. Kwa sababu hiyo tunaungana kabisa umuhimu wa kupata nyaraka na hasa huu mkataba uliosainiwa nje ya Tanzania upatikane uje hapa tuone ukoje na tutaupata kwa kupitia Kamati Teule. Hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, katika majibu ya Mheshimiwa Waziri ameeleza manufaa ambayo tutayapata baada ya kusainiwa mkataba huu na mradi huu utakapokuwa umeanza. Kwa taarifa tulizonazo sisi hapa alizotupa Waziri kwamba mradi huu ni mdogo sana unatoa ounce 1.8 kwa tani moja ya mchanga lakini kampuni hii imewekeza kwenye mradi unaotoa ounce 12 kwa tani. Experience tuliyonayo sisi, Williamson kila siku walikuwa wanasema hawapati faida lakini wanaendelea kuwekeza. Waziri katika maelezo yake humu wanasema faida tutakayopata ni dola 198 milioni. Ukiangalia kitabu cha revenue kwa Wizara hii kwa miaka mitatu mapato yaliyopatikana ni 77 bilioni. Sasa unajiuliza hizi 198 milioni zinazosemwa baada ya mradi huu kuwekezwa zitatoka wapi ikiwa mradi utakaowekezwa unatoa 1.8 ounce kwa tani moja hizi 198 bilioni zitapatikanaje? Haya ni maswali yanayotakiwa kujibiwa ndani ya Kamati na si mahali pengine popote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nasema pamoja na majibu haya ya Mheshimiwa Waziri kuna maswali bado 100 unaweza kujiuliza. Tunaambiwa juu ya uwezekano wa kupata ajira 600 kwa mradi mdogo huo mradi mkubwa je unatoa ajira ya watu wangapi? Maana inatakiwa unapoleta maelezo lazima uleta na comparing notes zinazosema kwa mradi huu mkubwa basi tumepata ajira hizi na kwa mradi huu mdogo tutapata ajira hizi, ndio itatusaidia. Sasa ni Kamati tu itakayotusaidia kutupatia majibu haya hivi hivi hatuwezi kupata majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine tumeambiwa kwamba faida tutakayopata ni kubwa sana dola 568 kwa ajili ya miundombinu na kadhalika lakini hatuelezwi kilomita ngapi zitajengwa, hatuelezwi megawatt ngapi za umeme na kadhalika. Kwa hiyo kuna masuala mengi tu hii Kamati Teule ikiundwa ndio itapata majibu kama haya ni sahihi au siyo. Kwa hiyo sitaki kusema Mheshimiwa Waziri Karamagi hakusema sawasawa lakini nasema bado kuna utata wa taarifa. Kama taarifa ya Zitto ina utata hii ina utata zaidi maana yake ina figures ambazo lazima u-clarify kwamba ni figures sahihi zilizoletwa hapa. Bila kutushawishi sisi na kusema tu kwa ya juu juu kwamba aah kuna manufaa wakati experience yetu ya madini, nasoma taarifa zote za Bunge hili za Wabunge, za Kamati za Bunge wanalalamika mapato yanayopatikana kutokana na madini. Sasa kama leo tutapata manufaa makubwa kwa mradi mdogo tu min tiger tu naambiwa basi itakuwa faida kubwa sana, tutashukuru sana sisi lakini nasema hayo majibu yatatoka kwenye Kamati Teule. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika viambatanisho vya Waziri ameleta barua iliyoandikwa na Kamati iliyomshauri. Kamati inamshauri hivi, inasema:

“Hivyo Kamati inapendekeza ni vema mkataba huu usainiwe kwa mfumo wa kodi uliopo ili kuwezesha mgodi huu uanze kufanya kazi”.

Huku tunambiwa kuna review mpya imefanyika ya mikataba lakini kauli zinakuwa tofauti, Kamati inasema isainiwe kwa mfumo wa zamani, contradiction Mheshimiwa Spika ni kitendawili kabisa kabisa. Sisi wenzenu jamani bahati mbaya tunaambiwa hatuna uzoefu na na nini lakini nasema mtusaidie huu utata unapotokea tunahitaji hizi information zitusaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tatu, ninaomba Serikali itusaidie best practice ni Serikali kusaini mikataba nje ya nchi? Serikali itueleze mikataba mingapi ya madini imesaini nje ya nchi. Itueleze kama ndio best practice kwamba Serikali ina uharaka wa kusaini mikataba na kampuni siyo Serikali na Serikali, Serikali na kampuni kwamba best practice ni kusaini mikataba huo nje ya nchi kwa sababu tu mgodi huo eti unawezekana usiwe na market baadaye. Hivi dhahabu kubaki pale kwenye ardhi kwani Watanzania wana hasara? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hiyo ndio argument pale mapema tuliposema juu ya habari ya Mwalimu pamoja na kwamba tunaambiwa tunam-quote vibaya lakini nafikiri tuna-m-quote vizuri tu kwamba aliona Watanzania bado hatujaweza kukamata rasilimali hii ya madini, tujielimishe basi angalau. Serikali hii inasema sasa tumechangamka tunafahamu ndio maana tumekubali lakini Serikali hii hii ndio ina-review mikataba kwamba haikufanya vizuri. Kwa hiyo, hiyo ile dhana ya kwamba tumeelemika juu ya jambo hili sio kweli kama tungeelimika tusingeingia kwenye mikataba yenye makosa. Hatujaelimika na tumeambiwa ndani ya Bunge hili hili kwamba mambo haya yanahitaji utaalam mkubwa na kadhalika. Kwa hiyo sisi tuka-caution katika Bunge hili ni vizuri Serikali ikawa waangalifu katika suala zima la kuingia kwenye mitakata. Leo tunakwenda kusaini mkataba nje ya nchi perception tu sitaki kusema kuna kasoro ni perception kwa madhambi haya yaliyoko tayari kwenye madini unakwenda kusaini mkataba nje ya nchi wala hutoi taarifa kwa wananchi taarifa imetoka baada ya Mheshimiwa Zitto kuibua hoja. Naomba sana kabisa kabisa Watanzania wenzangu tuiunge mkono hoja hii tuunde Kamati Teule itusaidie kwa sababu tutaibua mambo mengi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika Bunge hili Mheshimiwa Karamagi alituahidi, niliomba taarifa mbili ya Alex Stewart na ripoti ya Dr. Kipokola na akaahidi ndani ya Bunge hili hili kwamba atatupa, mmepata Waheshimiwa Wabunge? (Makofi)

WABUNGE FULANI: Badoooo! (Makofi)

MHE. HAMAD RASHID MOHAMED: Halafu tunaambiwa hatufanyi utafiti, utafiti gani tufanye sasa na vitabu hamtaki kutupa? Taarifa hamtaki kutupa sasa tufanye utafiti gani? Kwa hiyo, tutakachofanya tutaambulia hizi hizi mnazotupa hapa tutafanya nazo kazi basi hatuna nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wenzangu wengine wamesema ooh kuna internet siku hizi na nini hapana mikataba hii ya madini hairuhusiwi kusainiwa kwenye internet mkatazame sheria vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii na naomba kabisa Waheshimiwa Wabunge kwa kuwasaidia Watanzania wetu hawa tukubali kabisa tuunde Kamati Teule ya Bunge. Experience tuliyoiona sisi tulipounda Kamati Ndogo ya Public Accounts Committee tumegundua mambo mengi sana toka mwaka 1994 mkataba umesainiwa mpaka leo kampuni husika haijalipa kodi ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilipokuwa nauliza swali la nyongeza kuhusu Williamson Mheshimiwa Waziri akasema pale Williamson kuna mambo mazito pale huwezi kuingia hovyo hovyo sisi tulikwenda na Kamati yetu na Wabunge wengine wako hapa tumekwenda mpaka kwenye hicho chumba unaambiwa huingii tumeingia na tukatia mkono tukakamata almasi. Mimi nikauliza nyie mnasema mtu haingii humu mbona sisi Wabunge mmeturuhusu kuingia na tumechukua almasi tukatizama? Pamoja na kwamba Serikali ina hisa hakuna Mtanzania yeyote pale ni wao wenyewe wageni watupu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumekwenda London, Valuer aliyewekwa na Serikali kutathmini almasi zetu tulipomwambia Williamson haijalipa kodi yule Mchecoslovakia alianguka chini akasema siamini huku Serikali inasema inafuatilia kwa undani na kadhalika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaomba Waheshimiwa Wabunge kwa maslahi ya Taifa hili, kwa maslahi ya Watanzania kweli tuungane na Mheshimiwa Rais kwa kauli yake aliyoitoa ya kupitia mikataba hii kwa kusaidiana na Wabunge. Tuliiambia Serikali peke yenu kazi hii hamtoiweza lazima mlishirikishe Bunge na na njia ya kulishirikisha Bunge ni kuunda Kamati Teule tutapata mambo mengi ndani yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)

MHE. MUDHIHIR M. MUDHIHIR: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangia hoja binafsi ya Mheshimiwa Kabwe.

Mheshimiwa Spika, yaliyopo mbele yetu hapa ni mambo mawili tu. Moja la msingi ni tuhuma ambayo aliitoa Mheshimiwa Zitto tarehe 16/7/2007 ambayo ningependa niinukuu katika Hansard ukurasa 181 alisema hivi:

“Mheshimiwa Spika, kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na Mkataba mpya wa Mgodi wa Buzwagi ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo sio sahihi, amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli sivyo ambavyo vipo katika Mkataba ambao ameusaini”

Mheshimiwa Spika, hii ndio hoja ya msingi. Kwa mkataba ambao ameuona yeye hayo yaliyosemwa na Waziri sivyo vilivyomo mle. Sasa mnataka taarifa gani na mkataba anao na amesema aliyoyaona yeye mle sio aliyosaini Waziri. Mnatafuta taarifa gani tena? Kwa hiyo, mkataba huu alikuwa nao ndio maana akaweza kufananisha kwamba yaliyosemwa na Waziri siyo yaliyomo mle, hii ndio hoja ya msingi kudanganya. Sasa hii habari ya Kamati Teule ilikuwa ni mtoto wa hoja ya msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tunazungumza habari ya Kamati Teule tunaacha hoja ya msingi iliyotukusanyisha hapa leo kwamba Waziri alidanganya. Waziri asubuhi ametoa majibu. Tulitarajia wanaounga mkono hoja hii waeleze basi katika yale majibu ya Waziri la uongo lipi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hakuna ubishi kwamba Ibara ya 8 ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa mamlaka ya msingi kabisa ya Serikali kuwa ni wananchi. Hapana ubishi vile vile kwamba mamlaka haya ya wananchi….

MHE. KABWE ZUBERI ZITTO: Mheshimiwa Spika, kuhusu utaratibu.

SPIKA: Mheshimiwa Zitto kuhusu uratibu.

MHE. KABWE ZUBERI ZITTO: Mheshimiwa Spika, kanuni ya 43(7), “Mbunge yeyote hataruhusiwa kufufua jambo lolote ambalo Bunge lilikwishakuamua ama katika mkutano huo uliopo au ule uliotangulia”.

Mheshimiwa Spika, hoja iliyopo Mezani kwako ni hoja yangu ambayo nimeisoma hapa na sio hoja iliyotolewa tarehe 16/7/2007. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba utupe utaratibu ili Wabunge wachangie hoja ambayo nimeitoa Mezani.

SPIKA: Mheshimiwa Wabunge, hoja aliyoitoa Mheshimiwa Zitto Kabwe iliyombele yetu sasa ina chimbuko lake hata yeye mwenyewe ukisoma katika hoja yake inaanzia kule kule. Kwa hiyo leo Mheshimiwa Zitto hawezi kusema ameleta hoja mpya kabisa ambayo haina msingi wa nyuma na wakati wote ananukuu maneno aliyosema Waziri, Mheshimiwa Hamad naye amesimama hapa wote wananukuu yaliyosemwa na Waziri basi pande zote zina haki ya kuanzia kwenye mzizi mpaka tufike mwisho kwenye matawi. (Makofi)

Endelea Mheshimiwa Mudhihir.

MHE. MUDHIHIR M. MUDHIHIR: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Ukiona Mpinzani wako hafurahishwi na jambo lako usiliachie ukiona anafurahiwa nalo hilo baya liache mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nafikiri vile vile kwamba hakuna ubishi kwamba mamlaka ya wananchi waliopewa katika Katiba Ibara ya 8 kwa kiasi kikubwa yanapitia kwa sisi Wabunge wao. Sina ubishi vilevile kwamba Ibara ya 100 ya Katiba inatupa Wabunge uwezo wa kutoa maoni yetu kujadili kwa ukubwa kabisa, lakini ninapenda tukumbushane lakini ninapenda tukumbushane uhuru huo tunaopewa ni Ibara ya 100 ya Katiba na siyo uhuru holela. Bunge haliwezi kugeuzwa kuwa kijiwe cha mambo ya hisia, majungu na kupakana matope, huu siyo uhuru wa kukiuka haki na wajibu kama vinavyoainishwa katika Ibara ya 12 – 30 ya Katiba. Uhuru usiokuwa na mipaka siku zote ni kuingilia uhuru wa mtu mwingine. (Makofi)

Nimesikia hoja ya Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto leo, nimesikia na majibu ya Mheshimiwa Waziri, kwa maoni yangu ushahidi uliotolewa na Mheshimiwa Waziri hapa kujibu hoja 11 za Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto unaonyesha kabisa bila wasiwasi kwamba hutuma za Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto zilikuwa ni hoja hewa. (Makofi)

Zimechukuliwa zilikochukuliwa tuhuma hizo zikaingizwa Bungeni bila kufanyiwa uchunguzi wa ukweli na usahihi wake, alipotoa hoja hii tarehe 16/07/2007 tulimsikiliza na kweli wengi tulisisimkwa kwamba Waziri wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi anathubutu kufanya ufisadi wa namna ile. Tulimpa benefit of doughty Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto pengine alikuwa na hoja za kwelikweli na angeweza kuleta ushahidi kwa tuhuma hizi na siku hiyo ni leo ndiyo maana hata siku ile hatukumpiga stop kwa kutumia kifungu cha 50(1) maana benefit of doughty ilikuwa ni haki yake ya msingi.

Mheshimiwa Spika, Leo ni mwezi mmzima toka Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto atoe tuhuma hizi dhidi ya Mheshimiwa Nazir Mustafa Karamagi, kipindi chote hiki wananchi wamekuwa wakisikia na kusoma kwenye vyombo vya habari juu ya matope haya, Waziri wa Nishati na Madini kwamba si muadilifu, si msafi kwa kushindwa kuthibitisha tuhuma zake leo ndugu yangu Kabwe Zuberi Zitto amemvunjia heshima, kamvunjia sifa, kamvunjia na hadhi Waziri Naziri Mustafa Karamagi.

Haya yangesemwa nje ya Bunge hapana shaka kuwa ingekuwa ni kesi nzuri sana ya defamation Mahakamani, kwa bahati mbaya haya yamesemwa Bungeni ambapo Kanuni zetu hazimruhusu Mheshimiwa Naziri Mustafa Karamagi kudai fidia.

Mheshimiwa Spika, ni Bunge lenyewe tu ndiyo lenye Mamlaka ya kuona hatua ipi ichukuliwe baada ya mjadala huu kuisha na lazima hatua zichukuliwe ili mchezo wa aina hii wa mtu kukusanya taarifa nje kuzileta humu ndani, mchezo huu ukome mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Short Spear anasema katika author na ninaomba kumnukuu;

“Jina zuri kwa Mwanamke na Mwanamume ni Johari, ni tunu. Anayeniibia mkoba wangu wa fedha anaiba takataka lakini anayening’anya jina langu lililo zuri ananifilisi kabisa” mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, mimi namthamini sana ndugu yangu Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto bali ninaithamini sana heshima ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, kutokana na ukiukwaji huu sijui taratibu zinakuwa wa Kanuni ya 50(1) ya kumsemea mwenzake uongo, ya kumpaka matope nahisi aliyedanganya ni huyu mtoa hoja kuliko yule aliyebambikiwa tuhuma hizi na kwa msingi huo utanielekeza kama nitakuwa nakosea ninaomba mimi nitumie kanuni ya 59(3) kwamba kwa tabia hii ambayo imefanywa na ndugu yetu Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto asimamishwe kazi ya Ubunge kuanzia leo na mkutano wote wa tisa unaokuja, tukutane naye hapa Bunge la Januari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

SPIKA : Waheshimiwa Wabunge mwenzetu Mheshimiwa Mudhihiri M. Mudhihiri amewahi mno, kwanza wachangiaji bado wapo hatuna haraka jambo ni kubwa na zito tuende bila papara, bila jazba na tuende vizuri tu tutafika maana bado wasemaji ninao na ni wasemaji wazuri mtawasikia mtafika mahali ambapo inafaa kuona tunafanya nini kabla sijamuita mtoa hoja.

Kwa hiyo, sasa namwita Mheshimiwa Phares Kashemeza Kabuye atafuatiwa na Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba ajiandae.

MHE. PHARES KASHEMEZA KABUYE : Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Mimi kama mwalimu utaniwia radhi nianze na utangulizi.

Ndugu zangu mambo ya madini ni mambo ya kuangalia sana na waliofanya mchezo leo hii wanalia, Afrika ya Kusini imeboresha miundombinu kwa sababu dhahabu zote na almasi zimechimbwa na wale wazungu waliojiita wenyeji zikatengeneza nchi. Leo hii rand yao ni sawasawa na dola 7 hadi 6, Ghana ambao almasi zao na dhahabu zilipelekwa na watu wa nje kama tunavyofanya leo hii sen ya Ghana 9000 ndiyo sawasawa na dola, muiangalie sana. Kongo nao mali yao imepelekwa, nimezaliwa nasikia kwamba kuna Mgodi Geita sisi tunaita Keita akasezia Keita bandu. Leo hii wananchi wa Geita ndiyo wanaoambiwa kwamba wana hali mbaya ya maisha. (Makofi)

Mambo ya mali tuliyopewa na Mwenyezi Mungu lazima tuisimamie na wananchi wana matumaini na Bunge hili hawana popote pale pa kwenda. (Makofi)

Sasa naanza, ni kweli kabisa kusaini mkataba wa dhahabu, dhahabu kuisainia London una mashaka. Hivi alikuwa anatembea nchi za nje alikwenda na mkataba huo? Gharama iliyoita mkataba watu waliompelekea mkataba huo gharama hiyo nani anailipa? Hivi kweli tumefikia hali ya kwenda kubembeleza wawekezaji kwa dhahabu na almasi? Bwana Mkubwa anasema Waziri wa Tanzania leta mkataba hapa, unakimbia! Nasema tuunde Kamati kuna wasiwasi hapa kwa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunagawa mali, tunabembeleza njoo tukugawie mali? Hakuna haraka, ninafahamu kabisa mgodi huo ulianza zamani hawahawa walikuwa wameanza eti wamewapa tarehe mwezi wa tatu ndiyo mgodi ulikuwa umeanza wameanza mambo mengi, ulikuwa unatakiwa kufunguliwa wasingeacha hiyo mali tu. Kwa hiyo, wasiwasi wa kwenda kusaini London ulitokana na Waziri na wala siyo wawekezaji walikuwa wameshawekeza pesa nyingi wasingeacha. Sasa wanakimbiakimbia London, kwa nini saini isisainiwe Kahama na ndugu yangu Kabuzi Faustine Rwilomba wakaangalia, lakini London? Kuna kitu hapo. Ndiyo Kabwe Zuberi Zitto anasema Kamati teule iende ikaangalie kisa cha kwenda London. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Barrick mimi nafahamu mgodi wa Tulawaka umekwisha ile open cutting imekwisha sasa wanafanya underground wana haja ya kutafuta migodi hawawezi kukupa kwamba tarehe fulani usipokuja hatuwezi kufungua migodi, haiwezekani haya ni mambo ya kufumba tu. Taratibu zilifuatwa kama zilifuatwa angalieni kile kibali kilichotolewa na Mwanasheria Mkuu halafu angalieni na yale maazimio ya Halmashauri inayoshauri Madini ni tarehe 1, tarehe 16/02 wote kweli walikuwa wanakimbia . Mheshimiwa ulikuwa na haraka kweli aaah! sijui mlifanyaje, tarehe 16 wote, Mwanasheria Mkuu ameandika harakaharaka kikao kikakaa aaaaah! Kwa kweli ulikuwa na haraka na hicho kitu kilichokuwa kinakufanya haraka kipo ndicho tunachotaka Kamati iende ikajue, haraka ya nini? (Makofi)

Angalieni tarehe moja hiyo sijui walifanyaje hayo mambo, kwa nini tusiwe na wasiwasi wananchi waliotuleta hapa tuwe na wasiwasi kwa niaba yao haraka ya nini hiyo? Siku moja angalieni.




Mheshimiwa Spika, lakini pia ukiangalia ushauri wanasema kabisa kwamba wafanye kabla ya mfumo wa Kodi kuboreshwa soma, aliruhusiwa kabla ya mfumo wa Kodi kuboreshwa asaini. Hivi kweli wewe unasimamia Madini yetu ndugu yangu? Kabla ya mfumo wa kodi kuboreshwa? Jamani someni amesaini kabla ya mfumo wa kodi kuboreshwa ndiyo anatuambia ulikuwa umeboreshwa labda baada ya kusaini alikaa sana baada ya ushauri.

Lakini pia anasema kwamba wale wanaohusiana na mkakati wa kupitia mikataba ya Madini kama angesubiri wao walihitaji muda mrefu kwa hiyo alifanya kabla ya mkakati wa kupitia mikataba ya Madini haijafanyika, ile inaitwa GNT ilikuwa haijakaa kujadiliana. Sasa anasema utaratibu ulifuatwa hakuna upungufu haya si mapungufu ndugu yangu? Si mapungufu haya? Mfumo wa kodi haujaboreshwa, mikataba haijapitiwa, sasa unasema hakuna upungufu upungufu unataka uweje? Uangushe Mbingu? Akaambiwa atumie mfumo uliopo, ule wa zamani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lazima tuangalie haya ya kudanganywa wakati ile ya kumshauri ilipokaa yeye ndiye alikwenda kuwashawishi kwamba soma kawaambie kwamba hiki kitu kina faida mnishauri haraka pitisheni, someni ushauri wao. Wanasema yeye ndiye aliyetoa hoja, siwezi kusema maana nitatakiwa kudhibitisha, ndiyo! walishauri wao yeye alikuwepo anawaambia huu mgodi una faida wanasema wenyewe kwamba baada ya kuhakikishiwa kwamba mgodi una faida na mgodi mdogo una faida kuliko Tulawaka mambo haya ndiyo Kamati Teule inataka iangalie, hiyo faida inayosema mimi ninao mgodi wa Pangea, Tulawaka! Tumehangaika na wananchi kujenga shule Mheshimiwa Waziri Mkuu amepata dosari kwamba aliamrisha watu tuwapige wajenge shule hivi migodi tuliyonayo yote mbona haikuleta pesa za kujenga shule? Huu mgodi mdogo ndiyo utakaokomboa Tanzania? Lazima tuangalie. (Makofi)

Tumejenga Zahanati, lazima wananchi tuende kuwahangaisha migodi tunayo mingi haka kamgodi haka tu ndiko katakaoleta neema? Nina mashaka na wasiwasi yaani Question Mark! Hii Question Mark inahitaji Kamati iende ikatafute ituletee sasa jawabu tusije kwa kweli tukaambiwa ambiwa tu mambo watu wakaaanza kuja kuchukua Madini na wanachukua kama kweli wangesema mwekezaji wa kuja kupeleka muhogo wa Mtwara hapo tungekimbia kwa kweli kumtafuta. Lakini dhahabu? Dhahabu? Unakwenda kumbembeleza mpaka ndiyo unakwenda London? Sasa Kabwe Zuberi Zitto akiwa na wasiwasi ni matatizo wewe huwezi kuwa na wasiwasi kama Mtanzania? Huwezi kuwa na wasiwasi juu ya haya?

Kama mtu anasema Phares Kashemeza Kabuye mtu anasema nyumbani kwako kuna kitu cha wizi mimi nikisema usije kusachi hivi kweli hakuna mashaka?

WABUNGE FULANI: Yapo!

MHE. PHARES K. KABUYE: Hivi kweli Kamati inaogopa? Huna tatizo lolote nenda uje utukejeli Kamati iseme hakuna kitu tulidanganya mjisifu, sasa unaogopa nini ndugu yangu na Serikali yetu tukufu?

Mheshimiwa Spika, u wapi utawala bora sasa? U wapi uwazi wa Serikali yetu? Toa Kamati ije mtusimange hapa Kamati iseme hakuna kitu ni uzushi, sasa wewe uzushi unauota wewe mchangiaji hapa umefanya utafiti mpaka unasema ni uzushi ni uzushi gani? Tuhuma inaamuliwa na Mahakama sasa ni tuhuma tutengeneze Kamati ambayo itakwenda ndani. Mimi huo mkataba sijauona lakini hii Kamati itauona na mtu anasema tena Kabwe Zuberi Zitto alikuwa nao hivi Serikali yetu imeshatangaza kwamba imeibiwa nyaraka? Walipata wapi huo mkataba? Mheshimiwa Waziri umeibiwa nyaraka bwana? Walipata wapi sasa? Ni lazima tuangalie. (Makofi)

Mimi nilikuja kwamba kwa kufa na kupona kwa ajili ya wananchi, mkiona nimefunga virago nimefukuzwa Ubunge msishangae ni kwa ajili yenu.

Kwa hayo machache naunga mkono asilimia elfu kumi, ahsante sana. (Kicheko/ Makofi)

SPIKA: Bado nawasihi Waheshimiwa Wabunge twende kwenye hoja, kuna hoja imetolewa na Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto majibu yametoka sasa mchango kama wa Mheshimiwa Phares Kashemeza Kabuye unafurahisha lakini hauingii katika maudhui, hauingii kabisa katika maudhui ya hoja. (Makofi)

Kama hoja itakuwa ni kwamba tusipouona mkataba wowote tunaunda Kamati teule itakuwa ni Bunge la kitoto kabisa, kwa hiyo suala hapa siyo kuona mkataba lakini pima majibu ya Waziri kama yanatosheleza hiyo ndiyo hoja yenyewe.

Haya, msemaji anayefuata ni Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba wakati huohuo na Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir ajiandae.

MHE. PETER JOSEPH SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, na mimi nianze kwa kukushukukru kwa kunipa nafasi ili niweze kutoa mchango kwa hoja iliyo mbele yetu.

Kwanza nianze kwa kusema hoja hii siiungi mkono kabisa lakini jambo la pili nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri sana. Ni majibu ambayo hakuishia kwenye kueleza ameweka na viambatanisho. (Makofi)

Lakini ukiangalia mtoa hoja katika hoja zake ana mambo makuu mawili ambayo yeye ndiyo anataka leo tuyajadili. Anasema na nitaomba nimnukuu;

“Kusainiwa kwa Mkataba mpya wa Madini wa mgodi wa mradi wa Buzwagi katika Serikali na Kampuni ya Barrick, sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi yaani London Uingereza na wakati unasainiwa na wakati review zinaendelea na kuondolewa kipengele cha 15% Capital Allowance on redeemable qualifying capital expenditure bila kibali cha Bunge laki tukufu ”

Majawabu haya na hoja zake zimejibiwa vizuri sana na Mheshimiwa Waziri lakini yapo mambo kwanza Rais wetu aliagiza review zifanyike, review zimefanyika Barrick ndiyo watu wa kwanza waliokubali wakafanya hizo review na wakasaini MDAs. Kwa kweli concerns za Rais zimetekelezwa katika hii MDA mpya na new understanding ambayo ipo sasa kati ya Barrick na Tanzania ni kulingana na tulivyo negotiate na kwa kweli hili mimi lazima nimpongeze Waziri na niipongeze Serikali na niwapongeze wenye makampuni ya Madini yote kukuli kufanya review na masharti ya tuliyosaini Mkataba ni kwa kufuata masharti mapya.

Lakini linakuja suala la pili ambalo ni la msingi mkubwa wa hoja yake yaani Mkataba kusainiwa London. Nimewasikiliza wote hasa rafiki zangu wa upande wa upinzani wanaounga mkono hoja hii hakuna hata mmoja amabaye amesimama akatuambia ni sheria ya namba ngapi ya nchi hii ilivunjwa kwa kusaini Mkataba London? Hayupo hata mmoja aliyetuambia kwamba kwa kusaini Sheria ya Nchi imevunjwa, nani asimame hapa atuambie? Lakini cha muhimu hapa jamani kilichofanyika London ni ceremony tu lakini negotiations zote za Mkataba huu zimefanyika Tanzania, Kamati zote zimekaa Tanzania, Mkataba ukaandaliwa Tanzania lakini Waziri wetu ndiye mwenye Mamlaka na ndiye mwenye instrument ya kusaini mwisho wa siku. Imemkuta kila kitu kiko tayari already yuko safarini kwa sababu tuna ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya akasema lete nisaini. (Makofi)

Sasa ni mikataba mingapi sijui wenzetu watuambie tumesaini nje ya nchi mbona hawajalalamika?

Mheshimiwa Spika, lakini pia ninachotaka kusema ni kwamba wanasema Buzwagi ni Marginal Mining, mimi nasema Buzwagi ni Marginal Mining kwa sababu deposits zake ni kidogo sana lakini kwa sababu tumefanya review mgodi huu utatusaidia na Waziri ametuambia hapa kwamba tutapata dola za kimarekeni milioni 818.3. Kuna mtu amesema hapa atuambie hela hizo zitafanya kazi gani lakini ni suala la hesabu tu akiamua sasa atajua ni kiasi gani zitafanya kwa maendeleo ya nchi yetu akiamua tupige hesabu inawezekana tu. (Makofi)

Lakini pia tunakuja suala la 15%, 15% hii ya hili redeemable kwa capital allowance ndugu zangu hebu tulielewe hili jambo maaana yake nini?

Waziri ametoa majawabu yake hapa lakini akaenda mbali zaidi ametupa na sheria na watu wote waliosimama hapa ambao ni wapinzani sikumuona hata mmoja ambaye ana question hii sheria tuliyoipitisha kwenye Bunge hili. Matokeo yake tunakwenda kuchagua sentensi moja wana capitalize on that, tunayo Sheria hapa nani ameikataa? Tuliipitisha hapa na Waziri amesema kwa bahati mbaya Mheshimiwa Mbunge hakuelewa kwamba kuna Sheria ya Madini na kuna Sheria ya Income Tax Act ya mwaka 1973. Tunachokiongelea hapa ni sheria ya mwaka 1973 siyo Sheria ya Madini, unless watu hatuelewani vizuri. Lakini katika hili huyu bwana amejichanganya. (Makofi)

Lakini lililofanyika ni haya yafutayo;

Kwanza, hiyo Capital allowance and Redeemable Qualifying Capital Expenditure haimo katika Sheria ya Madini lakini hii imerudishwa kwenye MDAs zote maana yake ni kwamba sasa Serikali yetu ita benefit kwa hiki kipengele kuondoka unless watu waniambie kwamba hawataki Serikali yetu i-benefit. Kama mtu alikuwa umempa Allowance Relief ya 15% leo unaiondoa maana yake wewe unafaidi. (Makofi)

Kwa hiyo, katika hili mimi ninachosema kilichofanyika hapa kwanza ni kumpongeza Waziri kwa kuhakikisha hii relief ya 15% inaondoka.

Mheshimiwa Spika, kuna mtu alikuwa anaongea hoja hapa kwamba Madini yana bei kubwa sana duniani hatupaswi kuyaa……

Lakini ngojeni niwaambieni Gold Price duniani ina fluctuate. Nataka niwaeleze ni kwa nini essence ya kusaini mkataba huu ilikuwa ni muhimu sana sasa hivi baada ya Septemba 11 na Afghanistan, Iraq War na terrorism bei ya gold ndiyo ikapanda, kwa hiyo kukishatokewa instability kwenye global scale ile bei ya gold inapanda. Kwa hiyo, economies of scale ambazo huyu bwana alikuwa anatuambia ukiangalia Buzwagi tunapata 1.8 gram katika tani moja kwa vyovyote mtu kama ingekuwa price ya Gold haiku juu hakuna ambaye angesaini mkataba huo. Lakini leo bei ya gold ni kubwa sana duniani kwenye financial markets zote duniani stocks ambazo ni expensive ni stocks za gold katika hali ambayo kuna instability duniani na ndiyo maana investors wote wanakwenda kwenye hii wanayoiita ni self of heaven yaani gold ni self of heaven.

Kwa hiyo, ninachotaka kusema hii ndiyo maana kwa kweli tulicho benefit kutokana na mradi wa Buzwagi ni kikubwa sana kama nchi. Sasa mimi najiuliza hivi tunataka tuunde Selective Committee ifanye kazi gani? Yameulizwa maswali, maswali yamejibiwa tena siyo kujibiwa peke yake na viambatanisho lakini bado mtu hataki anataka nini sasa? (Makofi)

Wenyewe mmesema asubuhi hapa kwamba tuondoke kwenye suala la siasa na mimi nasema tuondoke huko twende kwenye ukweli, Waziri amejibu maswali na ameweka na ukweli sasa tunataka Kamati ya nini? Ifanye kazi gani?

Mheshimiwa Spika, Bunge lako hili hatuwezi kufanya kazi za mtu akikaa akifikiri jambo akalitangeneza sisi tunalibariki tu, haiwezekani! Haiwezekani tuipake matope Serikali inayoafanya kazi kubwa namna hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi naomba kwa hoja alizoleta Mheshimiwa Kabwe Zuberi Zitto hakuna hoja hata moja na bahati nzuri hata yeye alisema anauliza maswali amepata majibu yake lakini on top of it amepewa na viambatanisho vya majibu pale ambapo alikuwa haelewi ameelekezwa, sasa tunataka nini? Mimi naamini alighafilika tu na tumemsaidia vya kutosha, mimi ndicho ninachoamini tu hapo.

Kwa hiyo, mimi nataka kumpongeza Mheshimiwa Waziri Nazir Mustafa Karamagi kwa kweli leo ametusaidia sana. (Makofi)

Lakini pia napenda kuipongeza Serikali na kuyapongeza Makampuni ya madini yaliyokubali tumefanya review zetu na sasa nchi yetu inafaidika na madini yetu. H oja hizi tumesaini London ni hoja ambazo hazina justification kwa sababu hakuna aliyesema tumevunja sheria gani.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nakushukuru sana.

MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Spika, kwanza nami nikushukuru kwa kunipa nafasi hii adhimu. Pia nami niungane na wenzangu kukupa pole kwa mambo mbalimbali yaliyotokea.

Mheshimiwa Spika, lakini pia niwapongeze wenzangu wote ambao wameikataa hoja hii na bila kusahau na mimi nasema kwamba siungi mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unapokataa kitu uwe na sababu na mimi nina sababu zangu, lakini naomba kwa ruhusa yako nianzie pale katika kipindi ambacho Mheshimiwa Mudhihir alifanywa akae kitako baada ya kuitaja tarehe 16 na ikakataliwa kwamba tarehe 16 siyo. Bado narudia kwamba mtoa hoja amelidanganya Bunge tangu tarehe 16/7/2007 pale aliposema na naomba kunukuu: “Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16/7/2007 mara baada ya hoja ya Waziri wa Nishati na Madini kuamuliwa Bungeni. Sasa ninakwenda chini kidogo, kwamba, nakusudia kuleta hoja ya kuunda Kamati Teule kuchunguza Mkataba mpya wa Madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais”. Katika tamko hili bila kuzingatia maagizo ya Rais Mheshimiwa Waziri ameshalitolea tamko na imethibitishwa kwamba Mheshimiwa Waziri hakukiuka agizo la Rais. Hapa tunasimama pale pale kwa Mheshimiwa Mudhihir kwamba Mheshimiwa Kabwe amelidanganya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini mimi nimekwenda mbali zaidi na hasa hoja hii ilivyokuwa inatoka upande huu. Lililofanywa na Mheshimiwa Karamagi kwa niaba ya Serikali ni kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeweka wazi kwamba itahakikisha pato la Taifa linakua kwa kiwango kinachotakiwa. Sasa anapotwambia kwamba Mheshimiwa Karamagi katika Mkataba ule kuna dola milioni 818, hizi zinawasaidia Watanzania hazimsaidii mtu mwingine yeyote, lakini Mheshimiwa Karamagi alipozungumzia suala la ajira kwa Watanzania 696, tupo kwenye Ilani ya Uchaguzi na tumeweka ahadi hapa kwamba tutatoa ajira kwa Watanzania milioni moja. Bado yupo kwenye mstari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini naomba nirudie matamshi yafuatayo, Serikali makini huwa na Wabunge makini wenye kufuata maadili ya kutodanganya wananchi wake. Lakini hiyo hiyo igeuzwe, Mbunge asiye makini ambaye anakurupuka, asiyefanya utafiti, asiyetaka kujua undani wa mambo ulivyo ni hatari katika Taifa hili. (Makofi)

MHE. PHARES K. KABUYE: Mwongozo wa Spika.

SPIKA: Mwongozo wa Spika, kanuni.

MHE. PHARES K. KABUYE: Kanuni ya 50.

MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Spika, suala la mwongozo halipo hapa.

SPIKA: Nimeruhusu kuhusu utaratibu, tumsikie tu.

MHE. PHARES K. KABUYE: Mheshimiwa Spika, Kipengele cha Nane (8) kinasema: “Ni marufuku kwa Mbunge yeyote kutoa lugha ya kuudhi”. Mambo ya kukurupuka nadhani yanaudhi sana na si lugha nzuri ya Bunge na legelege, hakuna kipimo cha kupima Wabunge hapa, wote tuko sawa. Nashukuru.

SPIKA: Sasa sikuelewa Mheshimiwa ulichohitaji ufafanuzi ni nini, kwamba neno kukurupuka linaudhi ama?

MHE. PHARES K. KABUYE: Mheshimiwa Spika, neno kukurupuka linaudhi kwa sababu Wabunge wamechaguliwa kwa makini na watu waliowaleta hapa. Legelege pia linaudhi, Mbunge legelege maana yake waliomchagua ni legelege. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa sikubaliani na tafsiri hiyo kwa sababu inawezekana kabisa Mbunge akakurupuka hata akiwa na busara. Kukurupuka ni neno la kawaida tu la Kiswahili na isitoshe tumpe haki Mheshimiwa Hafidh naye amalize, ataeleza hilo, maana yake ameanza tu kusema mwenzie amekurupuka, tunataharuki, hakuna haja, huu ni mjadala wa afya kabisa, kila mtu apewe nafasi aseme lile analoweza. Mheshimiwa Hafidh hebu endelea. (Makofi)

MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na kanitia wasiwasi kidogo Mheshimiwa Mbunge aliyekaa hivi sasa, kwa sababu katika maelezo yangu sikumtaja Mbunge yeyote, nimetoa aina ya Wabunge, sasa kwa nini anaingia wasiwasi yeye tu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, nilichosema mimi ni kwamba, Mbunge asiye makini anayekurupuka, asiyefanya utafiti, asiyetaka kuujua undani wa mambo yalivyo ni hatari kwa Taifa. Sijamtaja Mbunge yeyote hapa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, katika maelezo yaliyotolewa na pande zote mbili, mtoa hoja na Mheshimiwa Waziri kuna suala ambalo limezungumzwa hapa, suala la hoja linalotenganisha Bunge na Serikali ambalo limo katika maelezo ya Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Spika, naomba nikupe nasaha kidogo, usiwe unatulea kama babu na mjukuu. Unajua unapokuwa na mjukuu kama unampenda sana, basi unafika mahali anafanya mambo wakati mwingine yanaondoa utaratibu. Unapotuachia tukafanya baadhi ya mambo yaliyokuwa nje ya kanuni inakuwa matatizo. Kwa mfano, kama hili la sasa hivi Mheshimiwa, ninachosema, babu unatakiwa umruhusu mjukuu wako achezee ndevu na kifua, lakini kuna sehemu nyingine unamzuia na halafu unachukua hatua. (Kicheko/Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Hafidh naomba urejee katika hoja. (Makofi)

MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na nazungumzia suala hili kwamba ni la Kitaifa si la kisiasa. Mbona hatutaki kuwa wakweli? Lazima tuwe wakweli. Hili ni suala dhahiri ni la kisiasa na haliondoki kwenye siasa, mtoa hoja ni mwanasiasa, Mheshimiwa Waziri ni mwanasiasa, tumekuja hapa kutoka katika Vyama vyetu vya Siasa, tunachotakiwa sisi upande wa Chama Tawala kutekeleza shughuli za Kitaifa tulizokabidhiwa na wananchi. Sasa unapolizungumza kwamba, suala hili si la kisiasa, huna haja ya kuleta hoja hii hapa. Hili ni suala la kisiasa, sote tumeingia humu katika Bunge hili tumetokea katika nyanja za kisiasa hakuna atakayekataa hapa, kama si mwanasiasa huji hapa. Kwa hiyo suala hili liko dhahiri ni suala la kisiasa.

Mheshimiwa Spika, mengi yamezungumzwa, kutokana na misingi ya mtoa hoja ya kuunda Kamati Teule, mimi naungana mkono na wenzangu wote waliosema hakuna haja ya kuundwa Kamati Teule katika kushughulikia suala hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, sasa pamoja na tuhuma zote zilizotolewa na Mheshimiwa Waziri na zile ambazo zimetolewa sehemu nyingine, tunafika mahali sasa niombe ruhusa ya kutoa hoja kama ifuatavyo. Kwa sababu ya mambo yote yaliyokuwa yamefanyika na Mheshimiwa Waziri kulithibitishia Bunge letu Tukufu kwamba yaliyosemwa yote ni uongo, mtoa hoja amedanganya, kuna kauli Mheshimiwa Waziri kasema ni uzushi. Kwa hiyo narudia katika ombi la Mheshimiwa Mudhihir na mimi naomba kutoa hoja kwamba kitumike kifungu namba 59(3) para ya (2) naomba ninukuu:

“Lakini endapo Mbunge mwingine yeyote ataona kwamba uongo uliosemwa na Mbunge huyo ni mkubwa kiasi cha kuathiri heshima ya Bunge anaweza hapo hapo kutoa hoja kwamba Mbunge huyo asimamishwe kazi za Bunge kwa kipindi maalum atakachokitaja katika hoja yake”.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Mheshimiwa Zitto Kabwe asimamishwe hadi Januari mwakani ndiyo aingie katika Bunge hili. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge msije kunifikisha mahali nikasema mnakurupuka. (Kicheko)

Hoja hii tayari tunayo, imetolewa taarifa na Mheshimiwa Mudhihir. Kwa mujibu wa kanuni ya 59 hiyo hiyo uliyoinukuu kama kweli itaendelezwa na nitampa nafasi Mheshimiwa Mudhihir, inaishia hivi: “…….. kama kuna hoja nyingine inayojadiliwa wakati huo basi hoja ya kumsimamisha Mbunge huyo aliyetajwa itatolewa mara baada ya hoja iliyokuwa ikijadiliwa kuamuliwa. Mmeelewa sasa?

WABUNGE: Ndiyo.

SPIKA: Kwa hiyo tuchangie hoja tu kwa hivi sasa.

WAZIRI WA MIUNDOMBINU: Mheshimiwa Spika, napenda sana nikushukuru kwa kunipatia fursa hii ili na mimi niweze kuchangia kwa kifupi katika hoja iliyo mbele ya Bunge lako Tukufu. Lakini kwanza nianze kukupa pole sana kwa msiba uliokusibu wa kupotelewa na mjomba wako Chifu Abdallah Fundikira, Chifu wa Unyanyembe. Taifa limepoteza kiongozi shupavu ambaye alikuwa ni mfano wa kuigwa. Ana historia ndefu sana katika nchi hii na wale ambao tunatoka maeneo ya Maswa, Maswa iliyokuwa kabla ya kugawanywa katika maeneo ya Wilaya mbili za Bariadi na Meatu, marehemu alikuwa Afisa Kilimo wa Wilaya ya Maswa kwa kipindi kirefu sana. Alifanya kazi nzuri sana kuboresha kilimo katika Wilaya ya Maswa. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Hapo hapo napenda nimpe pole sana mdogo wangu Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa kupotelewa na baba yake mzazi. Naye tunaomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Mheshimiwa Spika, ukiona fisi baada ya mvua kubwa ameteleza kwenye kichuguu, basi ujue mvua ilikuwa kubwa sana. Unaelewa nataka kusema nini. Lakini nina kitu kimoja, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Karamagi, Waziri wa Nishati na Madini kwa maelezo fasaha ambayo ameyatoa mbele ya Bunge lako Tukufu kujibu hoja iliyowasilishwa na Mheshimiwa sana Zitto Kabwe. Mheshimiwa Waziri amejibu kwa kituo kila tuhuma au swali, yeye anasema swali au maswali lakini yote yamejibiwa kwa ufasaha kweli kweli. Nampongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa kukamilisha rekodi ya Bunge lako Tukufu, wewe unafahamu na Watanzania wote wanafahamu, mimi nilibahatika kuwa Mwanasheria Mkuu wa nchi hii kwa kipindi takriban cha miaka kumi na tatu. Inapoletwa tuhuma nzito kama hii inayohoji utaratibu wa maamuzi ya Bunge lako. Mimi kipindi kile nilikuwa humu nikiishauri Serikali kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiyo maana nimeona ni vizuri nikalisaidia Bunge lako katika eneo moja ambalo Mheshimiwa Waziri Karamagi hakulikamilisha. Nalo linahusu ambayo Mheshimiwa Kabwe amesema kwamba Serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha alisema kuwa anarejesha ile asilimia kumi na tano ya Depreciation Allowance kwa unredeemed capital expenditure. Sasa hoja yake amekuwa akisema nimepitia hadi Sheria ya Finance Act ya mwaka 2000, eti hakuona hayo. Eti tunakwenda kinyume na sheria kwa kuruhusu hayo ambayo Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mramba wakati ule aliyasema humu Bungeni.

Mheshimiwa Spika, sasa nimekuletea nakala ya majadiliano ya Bunge ya Mkutano wa Nane sehemu ya kwanza ya tarehe 11 Juni, 2002 hadi 17 Juni, 2002 kuhusiana na eneo hili. Mheshimiwa Waziri anasema: “Napendekeza kurejesha kipengele cha additional fifteen percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure kwenye Sheria ya Madini Na. 5 ya mwaka 1998 kwa wawekezaji waliokuwepo hadi Julai Mosi, 2001 na akaendelea.

Sasa Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu wote maamuzi yanayoletwa na Waziri wa Fedha kupitia hotuba yake yale ambayo yanahitaji Sheria hatua zake zinapitia kwenye Finance Bill na baadaye inakuwa ya Finance Act. Sasa nimewasilisha kwako Finance Act, No. 18 ya mwaka 2002 ambayo ilikuwa inafanya marejesho hayo kwa makampuni ambayo yalikuwepo yalikuwa na leseni, yalikuwa na Mikataba na Serikali kabla ya tarehe 1 Julai, mwaka 2001. Kwa sababu ya muda nisingependa kuwasomea hili, lakini itapendeza iwapo mtoa hoja atapewa naye nakala ya sheria ya nchi ili aweze kuliona hili kwa sababu ni hoja ya msingi sana hii.

SPIKA: Nilimpatia nakala mara uliponipa, kwa hiyo anayo.

WAZIRI WA MIUNDOMBINU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, kusema kweli Serikali imehitimisha kwa kusema uwazi kabisa kwamba kwa makampuni ambayo ni mapya yaliyoingia kuanzia tarehe Mosi, Julai, 2001, kipengele ambacho kilikuwa kinaruhusu wapate asilimia kumi na tano ya ziada kwa mtaji ambao haujarejeshwa kwa hao sasa hakuna. Lilifanyika kosa katika uandishi wa mwisho wa sheria hiyo, tukaingiza na makampuni ambayo tayari yalikuwa na Mikataba ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria pia unafahamu kwamba haiwezekani ukachukua uamuzi unilaterally, wa kiimla, kama Serikali unaweza lakini madhara yake ni makubwa sana kama unataka kuvutia wawekezaji waje nchini kwako na ndiyo maana sheria zote zinatambua haki ambayo ilikuwa imetolewa. Ukiamua kubadilisha sheria lazima uheshimu hayo au uweke mechanism ambayo itamfidia yule ambaye sasa unataka kumwondolea hicho alichokuwa amepata. Kwa hiyo hilo ni la msingi sana na Serikali yetu ni Serikali inayoheshimu mikataba ambayo imeingia. Lakini tuseme mapitio ya Mikataba ya Madini na Petroli ambayo ni ya muda mrefu sana ni kitu cha kawaida sana duniani. Someni maandiko haya mtayaona, lakini aliyetoa maelekezo ya kufanya mapitio ya mikataba ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, si mtu mwingine na alisema itafanywa na Serikali yake kwa kuongea na makampuni ambayo tunayo. Mheshimiwa Rais hajasema kwamba tukimaliza zoezi hilo tutakuja kutoa taarifa Bungeni, kazi hiyo aliituma Kamati, Kamati hiyo ni Kamati yake na ripoti hiyo iliwasilishwa kwake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitakachotokea kwa maeneo ambayo katika kudurusu sheria. Yale ambayo tutaelewana na makampuni haya kama alivyosema Mheshimiwa Karamagi, tumeanza vizuri, mengine itabidi tuyalete Bungeni ili yaendane na sheria na kusema ukweli hoja za mkataba kusainiwa nje ya Tanzania si hoja ya msingi na nataka kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba hakuna sheria iliyovunjwa katika kusaini mkataba huo nje ya nchi. Imeelezwa vizuri sana na baadhi ya waliochangia kwamba la msingi hapa ni yale majadiliano, mnakamilisha mazungumzo yanakuwa mazungumzo mazito kweli. Ndiyo mnasema katika hatua ya kwanza, naamini mkataba huo unasema wazi kabisa kwamba, kila page ya kwanza tuna initial mpaka ile page ya mwisho ambayo tunataka kuweka saini, normally hatu-initial, maana hiyo ndiyo inaonyesha kwamba haya ndiyo tumekubaliana. Haya mimi ningemwelewa sana Mheshimiwa Zitto kama angesema tu kwamba kuna ushahidi Mheshimiwa Waziri angekwenda akaingiza mambo ambayo hayakuwa yamekubalika na Serikali kabla ya kwenda kule. Lakini kama ataweza kututhibitishia hayo atutolee hapa hadharani kwenye Bunge lako Tukufu tuyaone hayo.

Mheshimiwa Spika, lakini kuna moja la msingi sana lililosemwa la kutumia jina la viongozi. Sawa, litumie vizuri basi. Baba wa Taifa marehemu Julius Kambarage Nyerere, Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, ni kiongozi shupavu, mahiri, anayeheshimika sana Tanzania na nje ya Tanzania na duniani kote. Kusema kwamba yeye alisema madini ya nchi hii yasiendelezwe mpaka Watanzania watakapokuwa wameelimika jamani tusimsingizie mzee wa watu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika uongozi wa Mheshimiwa Mwalimu mimi nimebahatika sana kulelewa katika Sera ya kwanza ya Madini ya nchi hii ya Mwaka 1979 na ndiyo iliyozaa Sheria ya Madini ya Mwaka 1979 na ndiyo iliyozaa Sheria ya Kutafuta na Kuendeleza Petroli ya Mwaka 1980. Yote haya yana vivutio, wakati ule mwalimu aliliona hili mbali sana. Mheshimiwa Rais na Serikali yake wakati ule wanasema kwamba lazima tujenge mazingira mazuri ya kuleta wawekezaji. Sasa leo mnaposema kwamba Mwalimu angekuwepo mikataba hii isingekuwepo, ni upuuzi mtupu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme lingine, kipindi kile kile tunaongea kuhusiana na Sera ya Madini na Sheria ya Madini tuliongea na Wajerumani, Kampuni ya kwanza ambayo tuliwekeana Mkataba wa kutafuta madini ya Uranium katika maeneo mengi ya nchi hii hasa sehemu ya Selou ilikuwa ni kupitia sera hizo. Nimeona niliweke wazi hilo, liwe sahihi kwa sababu kuna picha inayoanza kuonekana kwamba Mwalimu yeye hakusema tutumie rasilimali hii kuendeleza watu wetu, nchi yetu na kupambana na umaskini.

Mheshimiwa Spika, naelewa kengele ya kwanza imelia, lakini nimalizie kwa kusema kweli Bunge lako limesikia hoja ya Mheshimiwa Zitto namheshimu sana. Tumesikia hoja nyingi ambazo zinapinga hoja iliyo mbele yetu na mimi napenda niungane na wote waliosimama na kuchangia kusema hawaungi mkono hoja hiyo kwa sababu haina tija, ukweli wote umeshawekwa hadharani. Isipokuwa kama mtu anataka kwenda kuganga njaa kupitia posho ya Bunge, mimi siamini kama huo ni utaratibu mzuri wa kutumia fedha za walipa kodi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kusema kwamba, mimi ningependa sana Mheshimiwa Zitto atakapoanza kujibu...........

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, kuhusu utaratibu.

SPIKA: Ahaa, sasa namwita tu mtoa hoja kwa sababu naona jambo lenyewe limefikia mwisho. Nadhani tumwite mtoa hoja kwa sababu na muda nao unakwenda.

Mheshimiwa mtoa hoja, Mheshimiwa Zitto Kabwe.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naomba nirejee kukushukuru kwa dhati kabisa kwa kuruhusu hoja hii kujadiliwa na Bunge na jambo la kufurahisha sana leo, watu wote ambao kwa kawaida wananchi wamezoea kuunga mkono hoja mia kwa mia, leo walikuwa wanapinga hoja. Watu waliokuwa wanaopinga hoja leo wameunga mkono mia kwa mia na hii inaonyesha ni jinsi gani ambavyo demokrasia yetu inakomaa. The House at work, Bunge linafanya kazi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kweli nimeridhishwa na mijadala mbalimbali ambayo imeendelea ndani ya Bunge na naomba kuchukua fursa hii sasa kwanza kujibu hoja za wachangiaji mbalimbali. Hoja yangu imechangia na jumla ya wachangiaji kumi na wanane na hapakuwa na mchango wa maandishi na naomba niwatambue kama ilivyo desturi ya wenzangu wa upande wa pili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wa kwanza alikuwa Mheshimiwa Nazir Karamagi, Mheshimiwa Ruth Msafiri, Mheshimiwa Maulidah Annakomu, Mheshimiwa Khalifa Suleiman Khalifa, Mheshimiwa Mhonga Ruhwanya, Mheshimiwa Suleiman Kumchaya, Mheshimiwa Chacha Wangwe, Mheshimiwa Suzan Lyimo, Mheshimiwa Adam Malima, Mheshimiwa Magdalena Sakaya, Mheshimiwa Manju Msambya, Mheshimiwa Siraju Kaboyonga, Mheshimiwa Hamad Rashid Mohammed, Mheshimiwa Mudhihir M. Mudhihir, Mheshimiwa Phares Kabuye, Mheshimiwa Peter Serukamba, Mheshimiwa Hafidh Ali na wa mwisho kabisa ni rafiki yangu sana Mheshimiwa Andrew Chenge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nianze na hii hoja ya mwisho ya Mheshimiwa Andrew Chenge kuhusiana na fifteen percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure.

Mheshimiwa Spika, nilichokisema katika hoja yangu na naomba Bunge lako Tukufu linielewe. Nilisema Mheshimiwa Waziri wa Fedha mwaka 2002 ali-reinstate fifteen percent na alisema hivi na naomba kunukuu kwa sababu umenipatia nakala halisi ya majadiliano ndani ya Bunge:

“Napendekeza kurejesha kipengele cha additional 15% capital allowances on unredeemed qualifying capital expenditure kwenye Sheria ya Madini. Narudia haya ni maneno ya Waziri wa Fedha ndani ya Bunge kwenye Sheria ya Madini Na. 5 ya Mwaka 1998 na hoja imeendelea. Hoja yangu namwomba Mheshimiwa Chenge anielewe, yeye ni Mwanasheria na nisingependa atumie uzoefu wake wa ndani ya Bunge kupotosha. Nilisema hivyo na naomba kunukuu.

Mheshimiwa Spika, naomba kunukuu. “Nilipopitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2002, nimekuta sehemu ya 8 inazungumzia mabadiliko katika Kodi ya Mapato ya mwaka 1973”. Hata katika ukurasa wa kwanza wa Sheria hii yaani Arrangement of contents, Sheria ya Madini haitajwi.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Kigoma Kaskazini hawakukosea kunichagua. Hapa nina sheria na ukurasa unaoelezea content ninao hapa na naomba nitaje content moja baada ya moja ili Bunge lako Tukufu liweze kuona.

Mheshimiwa Spika,

1. Preliminary Provisions
2. Amendment of Business Licensing Act 1972
3. Repeal of Car Benefits Tax acts 1991
4. Amendment of the Commodity of Import Supports Regulations Act 1992
5. Amendment of the Customs Tariffs Act 1976
6. Amendment of the Excess Tariffs Ordinance Cap. 332
7. Amendment of the Executive Agencies Act 1997
8. Amendment of the Income Tax Act 1973
9. Amendment of Pools and Lotteries Act 1967
10. Amendment of the Road and Fuel Tools Act 1985
11. Amendment of the Stamp Duty Act 1972
12. Amendment of the Value Added Tax 1997

Hakuna Amendment of the Mining Act, naomba nirudie Waziri Mramba alivyosema Waheshimiwa Wabunge na mnielewe, napendekeza kipengele cha additional 15%.

WAZIRI WA MIUNDOMBINU: Mheshimiwa Spika, naomba mwongozo wako kuhusiana na hayo anayoyasema Mheshimiwa Zitto Kabwe. Sheria ya nchi iko katika vitabu vya nchi, mambo ya utangulizi wa Hansard, Hansard sio sehemu sheria za nchi. (Makofi)

Pili, anayotueleza yawezekana Mheshimiwa Waziri mtoa hoja wakati ule kwa sababu yeye sio Mwanasheria hoja ya msingi pale ni nini kilichokusudia kufanyika, sasa tuongoze kwa sababu …..

SPIKA: Order, order !!!!! Utaratibu jamani.

WAZIRI WA MIUNDOMBINU: Kwa sababu unayo na wewe nakala ya sheria ya nchi kama maudhui ya kurejesha kile kifungu hayamo katika sheria ya nchi, mwongozo wako Mheshimiwa Spika.

SPIKA: Nitamwomba Mheshimiwa Zitto aendelee kidogo niweze kupata nafasi ya kuangalia na nitalitolea mwongozo.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, nilichokizungumza katika hoja yangu nimezungumzia, naomba kurudia nilichokizungumza katika hoja yangu.

Nilipopitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2002 nimekuta sehemu ya 8 inazungumzia mabadiliko katika Kodi ya Mapato na hata katika hoja ya kwanza ya sheria hii ambayo nimeitaja content zote arrangements of contents Sheria ya Madini haitajwi na ninachofahamu mimi Hansard ni Taarifa Rasmi za Bunge na baadhi ya vielelezo ambavyo Waziri alikuja kujibu hoja ametumia Hansard kujibu, kwa hiyo tunataka kuambiwa kwamba tusiamini Hansard?

Mheshimiwa Spika, katika hoja hii ambayo Wabunge kadhaa wamechangia kwa sababu nimeshataja Wabunge waliochangia nisingependa kuweza kurudia majina, ingawa baadaye naweza nikarudia majina. Mantiki ya hoja yangu ilikuwa ni kwamba mwaka 2001 Sheria ilibadilishwa na katika hili napenda nieleze Wabunge wote tulivyoingia hapa Bungeni tuligaiwa CD zenye sheria zote za nchi toka mwaka 1961 na tumetumia CD hizi ambazo zimegawiwa na Ofisi ya Spika kwa ajili ya kufanyia kazi utafiti wetu. Nitakuwa mtu wa ajabu sana niende nizushe tu mambo ambayo sijayafanyia kazi. Kwa hiyo CD zote zimeeleza na nimeeleza katika hoja yangu ya msingi mwaka 2002 Waziri ali-reinstate sheria hii na Mheshimiwa Spika, wakati hoja zinajibiwa tumeambiwa kwamba mwaka 2006 makubaliano yamefikiwa na watu wachimbaji wa madini kwamba kipengele hiki kiondolewe na wala mimi sijahoji mantiki ya kuondoa kipengele, nimehoji mantiki ya utaratibu wa uondoaji wa kipengele, ndicho nilichohoji mimi ambalo ni jukumu la Serikali kuweza kujibu.

Mheshimiwa Spika, katika maelezo Waziri aliyejibu hoja amesema kwamba mkataba wa Buzwagi uliandaliwa Tanzania na wataalamu wetu na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuata ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri wa Madini na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Pia Mheshimiwa Waziri Nazir Karamagi akawasilisha vielelezo vya ushahidi wa maneno yake. Barua yenye kumbukumbu Na. CDB 14301 ya tarehe 16 Februari, 2007 iliyotoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Madini kwenda kwa Waziri wa Nishati na Madini. Barua nyingine yenye kumbukumbu Na. JCA1305016 ya tarehe 16 Februari, 2007 ya kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenda kwa Kamishna wa Madini.

Kwa mujibu wa barua hiyo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Madini inaonyesha wazi kabisa ukiisoma ile barua Waziri ndiye aliyeanzisha kusudio la kutaka Mkataba wa Buzwagi usainiwe. Namshukuru sana Mheshimiwa Kabuye, ameli-raise suala hilo. Inavyoonyesha ni kwamba vikao viwili vya Kamati ya Ushauri vilikaa, kikao cha kwanza kilikaa tarehe 6 Februari na kikao cha pili kilikaa tarehe 16 Februari, 2007.

Hoja yangu ya Kamati Teule ya Bunge ni kwamba kumbukumbu za vikao vya tarehe 5 na tarehe 16 zipitiwe ili Bunge lijiridhishe na kumbukumbu hizo Mheshimiwa Waziri hajazileta hapa minutes za Kikao cha tarehe 5 na cha tarehe 16 zipitiwe ili kuweza kujiridhisha kama Waziri alifuata ushauri ambao ulitolewa na Kamati.

Mheshimiwa Spika, kwa utaratibu ulivyokwenda kabisa kabisa ni dhahiri kwamba Waziri alifahamu kwamba kuna kusainiwa kwa mkataba. Mosi, Waziri anajenga dhana kuwa tukio la kusainiwa kwa mkataba huu lilijitokeza kwa dharura na wakati yeye akiwa safarini ndiyo wanavyotaka Wabunge waamini na wengine wameamini na wanavyotaka jamii iamini.

Mheshimiwa Spika, dhana hii ambayo Mheshimiwa Waziri alitumia nguvu zake zote kuijenga bado mimi kama mtoa hoja naona haina nguvu na nina sababu zangu. Kukamilika kwa maandalizi ya utiaji saini mkataba kunamaanisha pia uwepo wa watiaji saini na kama maandalizi yalishakamilika basi watu wabariki wangekuwa tayari wapo Tanzania kwa ajili ya kusaini mkataba huo. (Makofi)

Kwa hiyo inaonyesha kuwa kitendo cha Waziri kusaini mkataba huu London, Uingereza hakikujitokeza kwa dharura kilipangwa. Waziri alisaini mkataba huu Uingereza, juma la mwisho la mwezi Februari. Vikao ambavyo nimevieleza vimekaa tarehe 5 na tarehe 16 kwa taratibu zozote zile, Waziri hakurupushwi kusafiri, lazima kulikuwa kuna schedule ambaye inafahamika kabisa kwamba Waziri atasafiri. Kwa hiyo alipanga kukutana na watu wa Barrick London, it is very clear na wala huhitaji Mbunge awe makini sana kuweza kufahamu usawa huo.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la uharakishaji, Waziri amejieleza kwamba ilipasa tuharakishe tusipoteze uwekezaji naomba niulize kitu hapa. Hivi nani amesema dhahabu ni ndizi inaoza, kwamba ukiacha kusaini itaoza itaharibika Taifa litapata hasara, nani amesema? Dhahabu ni madini na yanakaa pale. Kwa hiyo mimi sipati mantiki ya uharaka wowote ule wa kusaini mkataba huu na kwa kweli bado naamini kabisa kuna sababu ya msingi kabisa, Bunge lako Tukufu kuunda Kamati Teule ili kuweza kuondoa mashaka haya ambayo yamezungumzwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la kusaini London na kutokusaini London ambao watu wameeleza sio sababu haina maana yoyote na vitu kama hivyo. Mheshimiwa Waziri anasema si muhimu kwamba mkataba umesainiwa London au kutokusainiwa London, anatuonyesha kwamba format ya Mkataba wa Buzwagi haionyeshi mkataba ulisainiwa wapi. Kwa mujibu wa hali ya teknolojia ilivyo hili hatulikatai na wala hamna mtu anayelikataa. Mtu anaweza kuwa Buenos Aires, Argentina akaweka sahihi mkataba na kuutuma kwa huko Laspalma, Spain na mwingine akaweka saini. Hili halihitaji kuelezwa ndani ya Bunge lako Tukufu kwani hivi sasa watoto wa Sekondari wanafanya scanning na pia attachments za E-mail kilichotofauti hapa ni kwamba Waziri wetu wa Nishati na Madini hakuwa Dar es Salaam na kupeleka Mkataba London, naomba hii concept ieleweke. Concept ya kwamba mkataba unaweza ukatumwa kwenye e-mail ni pale ambapo mimi leo niko Dodoma, Mheshimiwa Hamad Rashid yupo Bujumbura nachukua mkataba nasaini na-scan signature nautuma Bujumbura anasaini signature, yeye anakuwa na kopi yake na mimi nakuwa na kopi yangu.

Mheshimiwa Spika, katika hili la Buzwagi haikuwa hivyo, katika hili la Buzwagi part zote to the contract zilikuwa London. Kwa hiyo ni lazima unaposaini mkataba huo ionyeshe kama umesainiwa London useme signed in London tarehe hii na hii, ebu Waheshimiwa Wabunge waangalie sheria zetu zinapowasilishwa hapa Bungeni. Katika sheria yoyote, katika hoja yoyote ambayo Waziri anaileta ni mfano tu wa kawaida pale chini mwisho pale anaandika Dar es Salaam ama Dodoma na kuweza kugaiwa. Sasa hapa tunazungumzia mkataba wa nchi. Mkataba kati ya dola na Kampuni binafsi. Kwa hiyo tulikuwa tunaomba kwa mujibu wa maelezo haya ambayo Waziri ameeleza ninaendelea kuwashawishi Waheshimiwa Wabunge wenzangu kukubali kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge ili Bunge lako Tukufu lijiridhishe na kuliridhishe Taifa kwamba Mkataba huu upo sawa sawa Watanzania watatushangaa tunapoacha maeneo yenye utata bila ya kufanyiwa kazi. (Makofi)

Katika suala hili pia watu wanaweza kusainiwa London au Dar es Salaam haijalishi wapi. Juzi mzee mmoja aliniambia vitu vya maana sana siwezi kusahau katika masuala ya majadiliano na kusainiwa kwa mikataba. Aliniambia unapokuwa katika majadiliano yoyote au unapotarajia kusaini makubaliano yoyote uzingatie vitu vitatu kwa Kiingereza power, time and information, katika hali ya kawaida naanzia power. Katika hali ya kawaida unapokuwa unataka kukubaliana kitu na mimi ukaja kukubaliana hicho kitu na kuwekeana sahihi nyumbani kwangu you are weak. (Makofi)

Kwa hiyo Waziri anapotuambia kwamba ilibidi atekeleze matakwa ya wawekezaji tena kwenye uwanja wao wa nyumbani kwa vyovyote vile lazima watakuwa weakened. Ndiyo maana bado pamoja na majibu haya Waziri naomba Kamati Teule iweze kuangalia labda kwa sababu ya nadharia hii ya power inawezekana kabisa kwamba Waziri wetu kwa kwenda kwenye uwanja wa nyumbani wa wenyewe alikuwa weakened. Nataka Kamati iweze kuangalia kama maslahi ya Taifa yalizingatiwa.

Mheshimiwa Spika, katika maelezo yangu nilihoji masuala kadhaa kuhusiana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuna baadhi wamesema kwamba tusitumie tumie majina ya viongozi wetu, mimi kama Mbunge nina wajibu wa kufuatilia matamko ya viongozi wakuu wa nchi. Vile vile ninamheshimu sana Rais wetu wa sasa na siwezi hata kidogo kutokutafakari maagizo yake kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 17 Julai, 2006, akisoma hotuba ya bajeti Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo Mheshimiwa Msabaha, alisema kuwa Serikali imesitisha kusainiwa kwa mikataba mipya ya madini. Tazama Hansard ya tarehe 17 Julai, 2006 ukurasa wa 41 mpaka 42. Serikali haijatamka ndani ya Bunge lako Tukufu kuwa usitishaji huu umeondolewa na wala hii haikuwa kauli ya Rais tena ni kauli ya Waziri ndani ya Bunge. Bajeti iliyopita na Waziri wa sasa alikuja kwenye bajeti hii hakuliambia Bunge hili Tukufu kwamba kuna mkataba mpya umesainiwa na Wabunge wengi leo hii wanaizungumzia Buzwagi baada ya ku-raise hoja hiyo Buzwagi. Vinginevyo hoja hiyo ilikuwa kimya na Wabunge wote wanajua kwamba leo hii hoja ya Buzwagi inazungumzwa kwa sababu niliizungumza. Waziri hakuliambia Taifa na alikuwa na nafasi katika hotuba yake ya bajeti kuliambia Taifa. Kwa sababu mgodi huu utaanza utekelezaji wake ndani ya mwaka huu wa fedha. Ndiyo, kwa hiyo ilikuwa ni jukumu la Waziri kuweza kulieleza Taifa.

Serikali kama nilivyosema haijatamka tena, kwa hiyo tulio Wabunge makini, narudia kusema tulio Wabunge makini tulipopata tetesi kuwa kuna mkataba mpya umesainiwa tukaja kuhoji hapa Bungeni. Mimi kama Mbunge nisingekwenda kuhoji mtaani as a forum, forum yangu ni Bunge ndiyo nimekuja kuhoji ndani ya Bunge, sasa kulikoni? Waziri lazima ajibu masuala haya kikamilifu na Taifa limuelewe ni lini usitishaji huu uliondolewa ambao Waziri Msabaha alisema. Mathalani Waziri ameweka saini mkataba huu takribani miezi sita tu tangu tamko hilo la Serikali na isitoshe mkataba huu umesainiwa wakati Bunge la Februari lilikuwa tu limemaliza mkutano wake, Bunge halikutaarifiwa kama kuna uamuzi mzito kama huu jambo hili linatia shaka na shaka yoyote hamna namna ya kuiondoa isipokuwa kwa uchunguzi wa kina na uchunguzi wa kina unafanywa kupitia Kamati Teule.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri katika majibu yake anasema kuwa Kampuni ya Barrick Gold Corporation imekubali kulipa kodi ya mapato naomba watu warudi kwenye ukurasa wa 5 wa Waziri. This is very serious. Waziri anasema Kampuni ya Barrick Gold Corporation imekubali kulipa Kodi ya Mapato, Kodi ya Mapato yaani Corporate Tax, Waziri hajasema, Provisional amesema kodi ya mapato na nakala ambayo imewasilisha ndani ya Bunge amesoma. Waziri anataka kutuambia kuwa hizi Dola za Marekani milioni 7 wanazolipa Barrick ni Kodi ya Mapato. Naomba Waziri aangalie vizuri majibu yake maana yanaweza kuzaa hoja mpya kabisa. Kodi ya Mapato ina Sheria maalum Income Tax Act 2004 na kwa wale Wabunge wengine ambao labda walipewa hoja waseme Income Tax Act 1973 tulii-repeal to 2004. Hizi Dola milioni 7 kutoka Barrick …

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, naomba kuuliza na uniongoze anafuata yale aliyosoma ama niliyoyasema nilipokuwa nimesimama pale. Kwa sababu nangoja Hansard kusudi aone niliyoyasoma pale ama niliyoyasema nilipokuwa nimesimama pale. Kwa sababu nangoja Hansard kusudi aone niliyoyasoma pale ama anasimama aliyoyasoma kwenye karatasi.

SPIKA: Nimemsikia na nanukuu ukurasa wa 5 na mimi nilikuwa nautazama wa hotuba yako. Lakini sijaliona hilo.

WAZIRI WA MIUNDOMBINU: Bullet ya 3 katika ibara ya 2 kutoka juu. Lakini Mheshimiwa Spika, hoja yetu ni kwamba malipo ya awali ya kodi.

SPIKA: Ndiyo, Tusubiri, tusubiri.

Namwomba Mheshimiwa Zitto kwenye mambo haya ambayo ni mazito aache technicalities zinaleta taabu, kwa mfano nirudi ile ya kwanza nimeisoma sasa. Ni kweli Waziri Mramba alipokuwa Waziri wa Fedha alizungumza na akanukuliwa moja kwa moja kwa Hansard kama ulivyo utaratibu, akaelezea nia yake “Napendekeza kurejesha na akaitaja Sheria ya Mining ya mwaka 1998”. hatma yake hakufanya hivyo, lakini ukweli sasa ukisoma katika ile Finance Act mwaka 2002, kodi hiyo aliishughulikia kupitia Finance Act. Sasa katika madini vyote viwili vina-apply Finance Act ikikugusa lazima ulipe kodi. Sasa kutofautisha ili mradi haikuingia kwenye Sheria ya Madini basi ni kosa kwa sababu tu Waziri alikusudia hivyo, hiyo tunafanya kama.

Ni kweli kiufundi ufundi unaweza kusema ni kosa lakini unafika pahala ambapo. Ndiyo, lakini hapa hatukai kufanya mchezo wa debating society ya shule hapa. Hatuko Secondary School kusema kwamba una score point kwa kutofautisha Serikali inatoza kodi ama kwenye Sheria ya Sekta ama kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato. Kodi hii imerejea sasa nongwa ni ipi. Kwa hiyo mwongozo wangu kwa ile ya kwanza aliyosema Waziri wa Miundombinu ni kwamba hakuna kosa lolote kwa Waziri kueleza makusudio yake au nia na baada ya hapo kutumia sheria tofauti kutoza kwa sababu hatma yake kodi hiyo inabidi ilipwe kwa nchi yetu.

Hili la pili hili namrudisha tena Mheshimiwa Zitto, malipo ya awali ya Kodi ya Mapato kwa Kiingereza ni Provisional Tax. Kwa Kiingereza hicho hicho na kwa masuala ya taaluma ya kodi huwezi kusema Provisional Tax ni sawa sawa kabisa na Income Tax. Kwa hiyo sijui, mimi nadhani Mheshimiwa mtoa hoja nenda kwenye majibu ya Mheshimiwa Waziri utusaidie pale ambapo wewe unaona tatizo la kikweli. Lakini kwenda kwenye matatizo ya kiufundi kama tulivyokuwa tunafanya kwenye High School kwa kweli haistahili hapa katika Bunge. (Makofi)

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa maelekezo napenda tu niweke wazi kabisa kwamba katika hotuba ya Waziri amezungumza Kodi ya Mapato, angeishia kodi isingekuwa tatizo, kwa sababu Serikali inaweza kutengeneza kodi ya aina yoyote ile. Lakini amezungumzia Kodi ya Mapato na naomba msome hiyo hotuba.

Mheshimiwa Spika, mmoja wa Wabunge waliochangia amesema ni vyema ningeomba kupatiwa mkataba ili niuone na nijiridhishe, Mbunge yeyote makini, hili ndilo angelifikiria la kwanza, yoyote yule. Mheshimiwa Kiongozi wa Upinzani wakati anachangia amezungumza tarehe 17 Julai, 2007, siku moja tu baada ya kuchangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini niliandika barua kwa Waziri wa Nishati na Madini ili anipatie mkataba huo niuone na kopi ya barua ninayo hapa na Mheshimiwa Spika, nilikuletea kopi. Nilitumia kifungu cha Sheria ya Kinga za Bunge, Sheria Na. 3 ya Mwaka 1988 kifungu cha 10, mpaka hapa ninapozungumza si tu sijapatiwa mkataba huu bali hata jibu la kupokea barua yangu sijalipata. Nilitoa nakala ya barua yangu kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu na kwako Mheshimiwa Spika, sishangai kutojibiwa kwani kuna uharaka kumjibu Mbunge tena chini ya sheria zetu au kuna uharaka kwenda kusaini mkataba London?

Kama kungekuwa na nia njema, Mheshimiwa Waziri angenijibu barua yangu na kunionyesha mkataba chini ya kiapo. Kufichwa kwa mkataba huu inathibitisha kuwa labda kuna mapungufu ambayo Bunge lako Tukufu halitakiwi kuyaona. Hata pale nilipoomba kwa mujibu wa sheria.

SPIKA: Mheshimiwa Zitto nikusaidie, tafadhali keti. Waheshimiwa Wabunge suala hili la mikataba na kudai taarifa mbalimbali nilizungumza na Mheshimiwa Zitto na viongozi wakuu wawili, Kiongozi wa Upinzani na Dr. Slaa. Nikawaambia hivi pamoja na sheria ile inavyosema utaratibu ni Ofisi yangu kudai kwa niaba ya Mbunge sio kila Mbunge atakuwa anakwenda ofisi yoyote unadai nyaraka. Ikiwa hivyo sisi watu 300 hata tukiondoa Mawaziri 60, Wabunge 240 ebu fikirieni Waheshimiwa kama kutakuwa hakuna utaratibu, yeyote anakwenda ofisi yoyote anadai karatasi anayoitaka na lazima apewe na mkumbuke Waheshimiwa Wabunge baadhi yenu mnafanya biashara tunajuaje wewe unataka kwa ajili ya maslahi ya nchi au unataka kwa ajili ya biashara zako. Niliwaarifu na wakatae hapa kwamba kwa njia hii kweli hamjajibiwa, tunaomba mpitie ofisi yangu mimi nisidai, Katibu wa Bunge adai nyaraka Serikalini kwa niaba yenu na mtazipata mkatae. Mnaposimulia mambo haya muwe mnasema na hayo ya ziada.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, wakati Mheshimiwa Waziri ananijibu, alisema eti mimi natafuta cheap popularity. Mimi sipo, hivyo hata kidogo, sihitaji cheap popularity. Nafanya kazi yangu iliyonileta hapa Bungeni na wananchi wa Kigoma Kaskazini. Sasa kama wananchi wanaona mimi ni maarufu huu ni uamuzi wao wananchi na kama kuna watu wanachukizwa na umaarufu wangu sina cha kuwasaidia. Ninachowashauri ni kufanya kazi kwa bidii ili wananchi watambue kazi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri katika majibu yake amekihusisha chama changu eti kwamba ninaleta siasa. CHADEMA ni chama kilichosajiliwa kihalali kabisa kwa mujibu wa sheria CHADEMA kama chama cha siasa kina haki zote kufuatilia mijadala ya Bunge na kutoa matamko. Matamko ya Chama cha Siasa ni jukumu la kisiasa la kila Chama.(Makofi)

Matamko ya Chama cha changu waulizwe viongozi wangu wa Chama. Lakini matamko yangu kama Mbunge niulizwe mimi. Ni kuunganisha mambo mahali pasipo husika.

Mheshimiwa Spika wakati akichangia Mheshimiwa Kumchaya amesema kuwa kuunda Kamati ya Bunge ni kupoteza fedha za wananchi. Nimeshtuka sana kusikia kauli hii Bunge limepewa Mamlaka ya na Katiba ya kusimamia Serikali. Njia moja wapo ya kuisimamia Serikali ni kuunda Kamati Teule ya Bunge. Tena hapa tunaunda Kamati teule ili kujadili suala la madini ambayo mchango wake katika Taifa si kupuuzwa. Kamati teule kwa taarifa ya Mheshimiwa Kumchaya inaundwa na Wabunge takribani watano tu. Hivyo wasiwasi wa fedha za wananchi anautoa wapi? (Makofi)

Inashangaza eti leo tunaona taabu kutumia fedha za nchi. Tumesahau kuwa tumetumia fedha nyingi za nchi huko nyuma tena kwa sababu ya mmoja wa Watuhumiwa kuleta mashahidi wengi hata wasiohusika katika kesi husika, inashangaza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Kumchaya amesema pia kuwa baadhi ya Wabunge wanatumia Bunge kama uwanja wa siasa na Mheshimiwa Hafidh Alli ameizungumza hiyo lakini kwa tofuati. Sipati mantiki ya hoja hii. Kwanza Wabunge ni wanasiasa kwa vyovyote vile mjadala wa Bunge haiwezi kukwepa siasa. Lakini wananchi ndiyo wanaojua, ni Wabunge gani wanageuza Bunge kuwa uwanja wa Siasa.(Makofi)

Mimi nilichokifanya ni kuleta hoja yangu, imejadiliwa itafanyiwa maamuzi nimetekeleza wajibu wangu. Moyo wangu mweupe kabisa uwamuzi ni wa Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Msambya na Mheshimiwa Msafiri wamezungumzia Video Conferencing, naomba wakajifunze vizuri jambo hili. (Makofi)

Video conferencing ni Mkutano tu, si kusaini Mikataba ya Kisheria na wala mifano hii haiendani kabisa na hoja iliyo mbele yetu. Video conferencing haliingizii Taifa katika mfangamo wa Kimkataba. Kwa hiyo kulinganisha kusainiwa kwa Mkataba na Video Conferencing ni kuchanganya mambo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naungana kabisa na Mheshimiwa Mhonga Ruhwanya aliposema kuwa Katiba na ametaja vipengele vya Katiba inatupa Mamlaka ya kujadili mambo haya. Nimalizie hoja yangu kwa hoja mbili muhimu.

Mheshimiwa Mudhihir, na baadae Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir ni baadae maelezo yako wamenijibu na kusema kwamba niadhibiwe.

Mheshimiwa Spika, Hoja mahususi iliyombele yetu ni Hoja ambayo nimeisoma hapa Bungeni. Narudia Hoja mahususi iliyo mbele yetu ni hoja ambayo nimeisoma hapa Bungeni. Kanuni za Bunge ziko wazi kabisa. Kama Mbunge ameona nilimzushia Waziri kuna taratibu za Kikanuni tena Mbunge Mwenyewe anaweze, Mnadhimu wa Serikali anaweza angeweza kutoa hoja.



Mheshimiwa Spika, kuchanganya mambo haya mawili kwa maoni yangu mimi ni hoja mbili tofauti kabisa kabisa. Lakini Katiba inatoa uhuru Kanuni zetu zinatoa uhuru Kanuni zetu zinatoa uhuru, Mbunge anaweza akaleta hoja ya mahususi kuhsiana na suala ambalo Mheshimiwa Mudhihir amelizingumza na Mheshimiwa Hafidh amelizungumza. Hata hivyo naomba kurejea mwaka 1978.

Mwaka 1978, pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kulikuwa na Jarida linaitwa Cheche, Serikali ikalifungia Jarida hili. Katika toleo la mwisho la mwisho la Jarida hili la Cheche walisema hivi. You Can Burn Organisations, You can Liquidate People, But Revolutionary Ideas Never Die.” (Makofi)

Inaweza ikatolewa Hoja, nimetimiza wajibu wangu, maamuzi ni ya Bunge, Moyo wangu ni mweupe, ni jukumu la Bunge kuweza kuamua na kutoa uamuzi. Ninachoomba tu nitendewe haki, nipewe haki ya kusikilizwa kwa sababu haki ya kusikilizwa ni haki ya msingi kabisa kwa hiyo kama kuna hoja yoyote ya kuniadhibu kwa vyovyote vile na bahati nzuri Mheshimiwa Spika ni Mwanasheria; kwa vyovyote vile nitapata the right of hearing. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya Maelezo haya bado nalishawishi Bunge lako Tukufu njia pekee ya kuweza kuondoa ukungu wote kuhusiana na hoja ambazo nimezieleza ni kuunda Kamati Teule ya Bunge.(Makofi)

Mheshimiwa Spika naomba kutoa hoja. (Makofi)

SPIKA: Hoja hiyo imetolewa na tutaiamua lakini naomba nitoe maelezo yafuatayo hususan kuhusu hiki alichosema Mheshimiwa Zitto hapa mwisho. Kanuni ya 59 Fasili (3), inaruhusu hoja nyingine kuweza kujadiliwa baada ya kuamua ile ya awali. Naomba nisome ile sentensi ya mwisho. Ikiwa kama anavyodai Mheshimiwa Mudhihir anadhani kwamba Mheshimiwa Zitto katika mwenendo mzima na mimi nasema lazima tuyachukue tangu tulikoanzia na ndiyo maana reference zote mpaka nakala za miswada na nakala za sheria na kadhalika ni mlolongo ule ule wa kutufikisha, leo ni kuhitimisha tu, Kwa hiyo huhesabu unapoangukia lazima uanzie kuhesabu pale ulipojikwaa ndiyo kawaida. (Makofi)

Kwa hiyo niliiweka kiporo hoja ya Mheshimiwa Mudhihir Kanuni ya 59 ambayo inasema kwamba endapo Mbunge mwingine yoyote ataona kwamba uongo uliosemwa na Mbunge huyo mwingine ni mkubwa kiasi cha kuathiri heshima ya Bunge aweza papo hapo kutoa hoja kwamba Mbunge huyo asimamishwe kazi za Bunge kwa kipindi maalum atakachokitaja katika hoja yake. Hoja ya aina hiyo yaweza kutolewa bila taarifa na itajadiliwa na kuamuliwa kama hoja nyingine yoyote. Sasa hili ndilo la muhimu kama kuna hoja nyingine kama hii ya Mheshimiwa Zitto inayojadiliwa wakati huo basi hoja ya kumsimamisha Mbunge huyo aliyetajwa itatolewa mara baada ya hoja iliyokuwa ikijadiliwa kuamuliwa. Kwa hiyo sasa tuiamue hoja ya Mheshimiwa Zitto.

Hoja iliyombele yetu ni kutaka iundwe Kamati teule ya Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 104 ili kuchunguza itiwaji sahihi wa Mkataba baina ya Serikali na Barrick kuhusu Buzwagi Mine na mazingira yote yanayoizunguka hiyo. Hoja hiyo imetolewa na imeungwa mkono. Sasa nitawahoji.

Hoja ya Ukaguzi na Mapitio ya Mikataba ya Madini Uliyowasilishwa
na Mheshimiwa Kabwe Z. Zitto ilikataliwa na Bunge

SPIKA: Wasioafiki wameshinda na kwa kura hizo Bunge limekataa kuundwa kwa Kamati teule kuchunguza ule Mradi wa Buzwagi.

Sasa tunaingia awamu ya pili na awe makini maana yake hapa si jambo jepesi kumuadhibu Mbunge, mimi nafuata Kanuni tu kwa sababu siwezi kuzuia hoja zinazoletwa mbele yetu lakini tuwe makini. Kwa sababu katika kufanya hivi tusije tukajifikisha pahala Wabunge wasiwe na wepesi wa kuyasema yale wanayolindwa na Katiba katika Ibara ya 100 Fasili ya (1) kwamba wawe na hofu. Lakini kama ukidhihirika uongo basi Kanuni nazo zinachukua hatua yake. Basi Mheshimiwa Mudhihir nakuomba uendelee pale ulipoishia.

MHE. MUDHIHIR M. MUDHIHIR: Mheshimiwa Spika, hoja hii iliyotukutanisha hapa leo, mzizi wa hoja iliyotukutanisha hapa leo unaonekana katika Hansard ya tarehe 16/7/2007 ukurasa wa 181 na kwa mara nyingine napenda niikukuu.

Mheshimiwa Zitto alisema mambo yafuatayo; “Mheshimiwa Spika, kutokana na Majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na Mkataba mpya wa Mgodi wa Buzwagi ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo si sahihi amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli sivyo ambavyo vipo katika Mkataba ambao ameusaini.” Kudangaya Bunge ni kosa, kwa mujibu wa Kanuni zetu lakini kwa kushindwa Mheshimiwa Zitto leo kuthibitisha kwamba yale maelezo aliyoyatoa Mheshimiwa Karamagi kwamba yalikuwa ni ya uongo maana tumemsikiliza na hakuna hata neno moja alilobisha ina maana maneno yake kusema kwamba amedanganya ameeleza vitu ambavyo kwa kweli si ambavyo vipo katika Mkataba ambao ameusaini ni kosa kwa mujibu wa Kanuni ya 50(1) ya Kanuni zetu za Bunge.

Mheshmiwa Spika, kwa faida ya wengine wanaotusikiliza ningeomba kunukuu hiyo. “Ni marufuku kabisa kusema uongo Bunge kwa sababu hiyo Mbunge yoyote anapokuwa akisema Bungeni atawajibika kuwa nahakika kwamba maelezo anayoyatoa ni sahihi na si mambo ya kubuni au ya kubahatisha tu na Spika au Mbunge mwingine yoyote aweza kumdai Mbunge huyo atoe uthibitisho wa usemi wake. Mbunge aliyetakiwa kufanya hivyo atawajibika kutoa uthibitisho huo katika muda atakaopewa na Spika.”

Kwa ajili hiyo mtoa hoja alipewa muda huo na Spika na leo ametoa maelezo yake na ameshindwa kuthibitisha uongo wa Mheshimiwa Karamagi, kwa msingi huo Kanuni ya 59 (3) inasema iwapo hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa Mbunge aliamuliwa kuthibitisha ukweli wa usemi wake kwa mujibu wa Kanuni 50 (1) atakataa au atashindwa kutoa uthibitisho huo kwa kiwango cha kulilidhisha Bunge basi Mbunge huyo atachukuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni 59(2).

Mheshimiwa Spika, lakini mimi naona uongo huu ni mkubwa zaidi ndiyo maana naomba kitumike kifungu 59(3). Kwa hiyo naomba kutoa hoja kwamba Mheshimiwa Zitto asimamishwe kazi ya Ubunge kuanzia leo na Mkutano wa Tisa. Nasema hivi si kwa nia ya kumkomoa yeye au wapiga kura wake, nasema hivi ili kuzuia vitendo hivi vya kuzuliana zuliana visiendelee ndani ya ukumbi wako wa Bunge. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika naomba kutoa hoja.

(Hoja ilitolewa Iamuliwe)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge nataka niwarejeshe kwenye maneno ya Kanuni ili tujue uamuzi tunaotakiwa kuchukua uchukuliwe katika mazingira yepi. Kanuni inasema 59 (3) ameinukuu mpaka pale katikati akaicha. Ili Mheshimiwa Mbunge aadhibiwe katika namna aliyomalizia Mheshimiwa Mudhihir inabidi tulidhike kwamba uongo uliosemwa na Mbunge huyo ni mkubwa kiasi cha kuathiri heshima ya Bunge. Ndiyo hayo yanafuata. Kwa hiyo sasa mjadala uko wazi hoja ya Mheshimiwa Mudhihir ya kumsimamisha Mheshimiwa Zitto Kabwe kwa kipindi alichokitaja sehemu iliyobaki ya Mkutano huu na Mkutano wa Tisa imeungwa mkono sasa tunaingia katika hatua ya kuijadili. Nitaomba wale wanaotaka kujadili wasimame na nimeletewa karatasi na Mheshimiwa Dr. Slaa.

Mheshimiwa Waziri unaanza au unataka kuchangia. Sekretarieti hebu andikeni majina sasa. Sasa kwa kuzingatia hali halisi ningemwomba Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu atoe hoja kwa sababu tumebakiza dakika 25 na sioni kama zitatuwezesha kulimaliza suala hili. Kwa hiyo atoe hoja ili tuweze kuendelea kwa muda usiozidi nusu saa. Baada ya saa mbili kasarobo.

HOJA YA KUTENGUA KANUNI ZA BUNGE.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU BUNGE: Mheshimiwa Spika, naomba kwa mujibu wa Kanuni ya 124 naomba Bunge lako Tukufu likubali kutengua Kanuni ya 21 (3) ili tuweze tukaendelea na hoja iliyopo mbele yetu mpaka hapo tutakapo hitimisha hoja hii.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO: Naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)
(Hoja iliamuliwa na kuafikiwa)

Hoja ya Kutengua Kanuni ya 21 ilipitishwa na Bunge

SPIKA: Hoja hiyo imekubaliwa kwa hiyo tutaendelea hadi ikibidi hasi saa mbili na robo. Sasa Mheshimiwa Dr. Slaa

MHE. DR. WILBROD P. SLAA: Mheshimiwa Spika, labda muongozo tu kwa sababu muda ni huo mdogo. Tunaongea muda wa Kawaida au tunaongea kwa muda gani.

SPIKA: Nadhabi ni kwa sababu suala la utaratibu tu kuthibitisha kitu pengine dakika tano inaweza kutosha.

MHE. DR. WILBROD P. SLAA: Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru kwa kunipa nipate nafasi hii ya kwanza kuchangia hoja hii ya kwanza ambayo Mheshimiwa Mudhihir ameitoa. Kwanza niseme kwamba sikubaliani na hoja ya kumsimamisha Mheshimiwa Mbunge kwa sababu kilichokuwepo hapa mbele yetu ni suala la kujadili hoja ya kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge; na ushahidi wote uliokuwa unatakiwa ni wa kwenda kwenye hoja hiyo. Lakini ushahidi wa uongo na ukweli bado ni suala halijajadiliwa. (Makofi)

Ni kweli kwamba Mheshimiwa Waziri amewasilisha hapa nyaraka mbalimbali alichowasilisha kwetu ni nyaraka ambazo zinaonyesha jinsi mchakato ulivyofanyika hadi kufikia yeye kusaini. Kilichowasilishwa ni zile zinazoonyesha kodi ile asilimia 15 kama ilirejeshwa au hapana. Lakini hoja ya Mheshimiwa Zitto ilienda mbali zaidi ilienda kwenye kutafuta kama Mkataba wenyewe upo. Mheshimiwa Waziri hajawasilisha ndani ya Bunge hili. (Makofi)

Unapochukua uamuzi wa kumsimamisha mtu ni lazima tuwe na uhakika beyond reasonable doubt kwamba Mheshimiwa Zitto amedanganya Bunge. Hoja ya kudanganya haiwezi kujengwa kwa sababu tu tumejibiwa hapa au kwa sababu tu imepigwa kura. Kura imeweza kupigwa na ushahidi wa jengi hili ni kwamba tunapiga kura kwa wingi kwa misingi ya watu walivyokaa kiitikadi si kwa misingi ya ukweli. (Makofi)

Sasa unapofika kwenye uwamuzi wa kwenda kumsimamisha mtu kwa sababu ya matokeo ya kura hatumfanyii huyo haki. Kwa hiyo kinachotakiwa sasa ili Mheshimiwa Zitto aweze kuchukuliwa hatua na mimi nakubali achukuliwe hatua kama kweli amedanganya Bungeni na kama kweli amesema uongo na kama kweli amemchafuliwa jina Mheshimiwa Waziri ni lazima Mbunge yoyote wa upande wowote ule achukuliwe hatua kama kweli inathibitika hivyo. Sasa ili hiyo iwe kweli mimi ninaomba sasa hatua zote zichukuliwe za document zote muhimu katika suala hili kama alivyoomba Mheshimiwa Zitto ziwasilishwe ziangaliwe na Kamati Maalum ndiyo tujue kwamba amedanganya au hakudanganya. (Makofi)

Lakini dhidi ya kupitia kwenye hiyo kwa misingi tu ya kura zilizopigwa nadhani ni kwenda kinyume na utaratibu wowote wa demokrasia katika nchi hii na itakuwa ni kinyume na utaratibu wa demokrasia popote duniani. Kwa kuwa muda ni mfupi naomba niseme tu kwamba katika misingi ya aina hii.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, muongozo wa Spika.

SPIKA: Mwongozo wa Spika, Mheshimiwa Manyanya mwongozo.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, naomba kurejea mazungumzo ya msemaji ambaye alikuwa akiendelea katika kifungu cha kusema uongo kwamba humu ndani tunapiga kura kwa kufuata makundi yetu na si kufuata ukweli. Naomba athibitishwe.

SPIKA: Tumpe nafasi aongee kila mtu ana haki ya kuongea. Kama unapingana nae basi inabidi. Sasa kwa kuwa aliomba mwongozo, mimi siwezi kuwakadilia Waheshimiwa Wabunge wanapiga kura kwa hisia zipi hilo ni suala la kila mmoja katika nafsi yake na si vizuri tukakadiliana au tukasema nia ya fulani iko hivi mimi nadhani hilo tuliache tuendelee na hoja iliyombele yetu hapa. Hebu niifafanue, hoja iliyombele yetu tena hapa si kuingia kwenye hoja ya kama Mkataba wa Madini upo ama sijui una ubovu gani nakadhalika si hoja hiyo. Hoja hapa ni kama Mheshimiwa Zitto amesema uongo kwa kumsingizia Waziri kwamba Waziri alilidanganya Bunge. Ndiyo hojo.

Waheshimiwa naweza kuwachukulia hatua kali kabisa hatuna mchezo hapa. Endelea Mheshimiwa Dr. Slaa.

MHE. DR. WILBROD P. SLAA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, sasa sina hakika muda wangu uliobaki lakini niendelee pale tu nilipokuwa nimefikia. Nilikuwa narejea uzito wa Kanuni tunayoizungumzia. Kanuni tunayoizungumzia ina maneno mazito, hoja ya aina hiyo yaweza kutolewa bila taarifa na ikajadiliwa na kuamuliwa kama hoja nyingine yoyote. Kwa hiyo kimsingi hoja hii inaturejesha kwamba majadiliano yatakwenda kwenye utaratibu wa kawaida unavyotakiwa na majadiliano katika Hoja yaani Kanuni ya 43. Sasa kwa ajili ya muda tunakubali tu hapa tujadili katika dakika tano; lakini kimsingi ninachosema kinachosemwa kwamba kasema uonga hakuna ushahidi wowote katika hotuba iliyotolewa hapa kwamba kasema uongo, wala hakuna ushahidi wowote kwamba Waziri alichesema ndicho sahihi. Kwa sababu tunahitaji kupima document mbili ambayo moja inaonyesha ndiyo ukweli na moja inaonyesha uongo sasa hicho huwezi kuipata kwa kujadiliana kama tunavyofanya ndiyo maana ninaomba kuwe na document hizo mahali na Bunge lako likubali kuwa na Kamati ndogo au kwa maelekezo utakayotoa wewe Kamati hiyo ichambue na ikushauri kama kuna uongo au hapana. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge labda nirudie tena kilichopo mbele yetu hapa na alicholeta Mheshimiwa Mudhihir ni kurejea kauli ya Mheshimiwa Zitto ya tarehe 16 mwezi wa saba ambapo alimtuhumu Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Jamhuri kwamba amelidanganya Bunge na kutokana na hilo Mheshimiwa Zitto akaleta hoja hapa kujaribu kuthibitisha kwamba Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini alilidanganya Bunge. Waziri wa Nishati na Madini leo ameeleza mtiririko wote wa mchakato wa Mkataba wa Buzwagi. Sasa wawili wote mmewasikia na wengine mmechangia sasa hapa jambo ni rahisi tu. Je, Mheshimiwa Zitto alisema uongo kwa kusema kwamba Mheshimiwa Waziri alilidanganya Bunge wakati ule na la pili haliishii hapo lazima ujibu. Uongo huo ni mkubwa kwa maneno ya 59 hapa uongo unatakiwa uwe mkuwa kiasi kwamba umeathiri heshima ya Bunge. Ndiyo hicho tunachosema sio ule uongo mdogo mdogo wa Kanuni ya 50 ule. Ni ule uongo ambao umeathiri Heshima ya Bunge. Hilo ndilo mlijadili na mnipe maamuzi. Anayefuata Mheshimiwa Ponsiano Nyami.

MHE. PONSIANO D. NYAMI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa nafasi hii adimu ili nami niweze kuchangia hoja hii kwamba Waziri alilidanganya Bunge. Mheshimiwa Waziri si kwamba amelidanganya Bunge. Bali Mheshimiwa Kabwe Zitto ndiyo ambaye amesema uongo unaoweza au ambayo tayari umekwisha athiri Heshima ya Bunge tayari.

Anaposema Waziri amesema uongo na kwa matamshi yake mwenyewe alipokuwa anaelezea hoja yake amesema pia baadhi ya mawazili wamekuwa wakisema uonga hapa Bungeni. Maana yake ni kwamba Serikali ndiyo imekuwa ikisema uongo na kwa sababu kiongozi wa Shughuli za Bunge ni Waziri Mkuu anataka kumpaka pia Waziri Mkuu matope kwamba yeye ndiye anayesema uongo.

SPIKA: Mheshimiwa Nyami, jamani hebu tafadhalini turudi kwenye hoja. Ni fupi kabisa inahusu matamshi ya Mheshimiwa Kabwe Zitto ya tarehe 17 kwa sababu hayo ndiyo yametufikisha hapa. Na ndiyo siku aliyotoa taarifa kwamba ataleta hoja ya kuundwa kwa Kamati teule. Sasa yale kwa mujibu wa Hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini aliona kwamba ameonewa kwa sababu kasingiziwa kwa kusemekana kwamba yeye alilidanganya Bunge kwa kutoa uongo huu ni hilo tu. Tusiende kwenye makando kando. Sasa tuseme juu ya Mheshimiwa Zitto, Mheshimiwa Nyami hebu endelea.

MHE. PONSIANO D. NYAMI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa mwongozo huo. Kutokana na uthibitisho alioutoa Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini kulithibitishia Bunge na mpaka dakika ya mwisho, Bunge limekubali kwamba Mheshimiwa Waziri hakusema uongo. Kwa hiyo, ni wazi kuwa Mheshimiwa Kabwe yeye ndiiye ambaye ameweza kulidhalilisha Bunge kwa kusema maneno ya kashfa kwa Mheshimiwa Waziri ambaye amethibitisha ukweli kwamba hakulidanganya Bunge. Na kwa maana hiyo naunga mkono hoja kwamba Mheshimiwa Kabwe anastahili adhabu hiyo ili iwe funzo kwa kila Mbunge asiweze kusema maneno au kulidanganya Bunge. Naunga mkono hoja!

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, asante, nashukuru kwa kunipa hii nafasi. Mheshimiwa Spika, mimi ningependa kulirejesha Bunge lako tukufu katika Kanuni ya 50(1) ambayo inajieleza bayana hapa. Katika hii Kanuni, Bunge lako tukufu nasikia linaendelea na review, ni Kanuni ambayo vile vile nadhani pengine itakuwa reviewed, kuhusu the burden of proof ilivyo hata katika sheria kwamba; kama kuna Mbunge ambaye anaona ya kwamba Mbunge mwingine anasema uongo…Sasa anayetakiwa kuthibitisha ni yule anayedai kwamba huyo Mbunge amesema uongo au ni yule ambaye anasemekana amesema uongo? Hii kidogo ina contradiction, lakini ninachotaka ku-prove hapa ni kwamba; ulichotuuliza Mheshimiwa Spika, ni nani anaunga mkono na nani anapinga na huo ndio utaratibu wa kawaida ambao kila siku tunaufuata hapa. Sasa, kama ni hivyo basi, aliyeleta hoja ya kusema ya kwamba Mheshimiwa Zitto aadhibiwe ni Mheshimiwa Mudhihir. Na Kanuni aliyoi-quote ya 59(3) inayosema ya kwamba; “lakini endapo Mbunge mwingine yeyote ataona kwamba uongo uliosemwa na Mbunge huyo ni mkubwa kiasi cha kuathiri heshima ya Bunge, aweza papo hapo kutoa hoja kwamba Mbunge huyo asimamishwe kazi ya Ubunge kwa kipindi maalum”. Sasa, Mheshimiwa Mudhihir ametoa hoja, lakini hiyo hoja yake, hajaithibitisha, ndio maana hoja ya Mheshimiwa Mudhihir bado iko subject to 51 kwamba yeye Mheshimiwa Mudhihir athibitishe kwamba Mheshimiwa Zitto aliyoyasema yalikuwa ni ya uongo. Kwa hiyo, yeye anabeba the burden of proof kulingana na hii Kanuni ya 50(1). (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo mimi ningeomba ya kwamba hili suala kwa sababu lilikuwa liko kwenye mchakato wa kawaida wa ki-Bunge, tungeacha, tuendelee na mambo mengine, badala ya kuadhibiana hapa. Lakini, kama ni hivyo, basi Mheshimiwa Mudhihir a-prove kwamba Mheshimiwa Zitto amesema uongo. Na akishindwa ku-prove na yeye pia achukuliwe hatua zinazostahili. Mheshimiwa Spika, mimi ya kwangu ni hayo! (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Hiyo ni upotoshaji tu, kwa sababu aliyeanza na hoja ya kutuhumu uongo humu ndani ni Mheshimiwa Zitto ndiye alimtuhumu Waziri. Tuachoamua leo ni tofauti. Anachosema Mheshimiwa Mudhihir ni kwamba; Kauli ya Mheshimiwa Zitto kwamba Mheshimiwa Waziri wetu wa Nishati na Madini alilidanganya Bunge, haikudhihiri na pengine ni uongo. Na kwa maana hiyo, ninalowaomba kuamua ni uongo mkubwa kwa mujibu wa Kanuni 59(iii)? Msilikwepe hilo, hilo ndilo lililopo mbele yetu. Sasa Mheshimiwa Mudhihir yeye ameridhika hivyo. Sasa ni juu ya kila mmoja wenu mliojiorodhesha kutoa maoni yenu. Kwa hiyo, namwita sasa Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Masuala ya Bunge.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU – BUNGE: Mheshimiwa Spika, naomba kwanza nami niungane na wenzangu ambao tunaunga mkono hoja hii ya kuweza basi kumpa adhabu mwenzetu ili iwe fundisho katika shughuli zetu za utendaji hapa Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba tu niseme kwamba Mheshimiwa Zitto ni Mbunge kijana, hodari kama walivyo Wabunge wengine vijana kama vile Mheshimiwa Vita Kawawa, Mheshimiwa Lucy Mayenga, Mheshimiwa Faida Bakari na wwengine ambao kwa kweli wamekuwa na mchango mkubwa na kuwakilisha vijana ndani ya Bunge lako tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jamii na hasa vijana wetu walioko mashuleni, walioko majumbani wamekuwa ni mashabiki wakubwa wa kuangalia Bunge letu katika vipindi mbali mbali na hasa vinavyorushwa hewani siku zote katika shughuli zetu. Na kwa kweli vijana wamekuwa ni mashabiki wa Wabunge Vijana walioko humu ndani. Sasa basi, kauli zinazoletwa na vijana Wabunge, tunategemea viongozi hawa wawe ndio role model kwa vijana wetu waliopo mashuleni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Jambo hapa naomba lieleweke na wanaonisikia, hatuhoji Mheshimiwa Mbunge kuhoji Serikali yake na kutaka maelezo na kutaka ufafanuzi. Ninachohoji kama Mnadhimu Mkuu wa Serikali, nasimamia nidhamu, nahoji kauli ya Mheshimiwa Mbunge. Mheshimiwa Mbunge amekuwa na matamshi ya aina kama hii. Hii siyo mara yake ya kwanza. Mheshimiwa Mbunge wakati Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki anahitimisha hoja yake, Mheshimiwa Mbunge katika vifungu wakati wa Kamati ya Bunge zima, alidiriki kusema kwamba…naomba ninukuu, nakumbuka alisema: “ Mheshimiwa Spika, nasikitika sana, Mheshimiwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, hawajui wanachokizungumza”. Kauli hiyo, ilisikitisha Watanzania wengi. Mheshimiwa Spika, wengi niliokutana nao, walisema “hatukufurahia”. Pale tulipokwenda Uwanja wa Jamhuri wakati wa mpira kati ya NSSF na Bunge, nilikutana na baadhi ya Watanzania waliokuwepo pale katika match na ninaweza kusema kwamba nilikutana na kijana mmoja ambaye ni mlemavu wa miguu, akaniambia “Mheshimiwa Waziri nilifurahi sana ulivyomsimamisha Mheshimiwa Mbunge yule, kauli yake haikuwa nzuri kabisa na watu wengi tulikasirika sana kwa jinsi alivyoweza kusema”. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kweli mimi naomba niseme kwamba, Mheshimiwa Mbunge bado alikuwa na fursa leo hii kuweza kutoa kauli yake hiyo, kwa sababu gani; katika Kanuni za Bunge ya 59(iii), inasema “Mbunge yule anaweza akafuta usemi wake”. Bado alikuwa na nafasi ya kufuta usemi wake leo hii wakati ahitimisha hoja yake hiyo. Lakini kwa makusudi kabisa, hakutaka kufuta, aliona kama vile itampunguzia heshima.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tusimamie nidhamu, tufanye hili suala liwe ni suala ambalo litatoa fundisho kwa watu wetu ambao wanatusikiliza kule. Bunge isiwe mahali ambapo mtu atakuja tu kudiriki na kusema kwamba Mheshimiwa Spika, naomba ninukuu…maneno aliyoyasema yalikuwa ni maneno makali sana na ni maneno ya kuudhi. Naomba nimnukuu Mheshimiwa Mbunge akitoa taarifa ya kutoa hoja yake hiyo, alisema: “Mheshimiwa Spika, kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri kuhusiana na Mkataba mpya wa Mgodi wa Buzwagi ambao Mheshimiwa Waziri ameeleza maelezo ambayo siyo sahihi, amedanganya na ameeleza vitu ambavyo kwa kweli siyo ambavyo vipo katika mkataba huo”.

Mheshimiwa Spika, Mbunge angeweza kusema maneno haya haya bila kumtuhumu Mheshimiwa Waziri amesema uongo na tusingefika hapa leo. Angeweza kusema tu “Mheshimiwa Spika, mimi naomba kutoa hoja ya kumtaka Mheshimiwa Waziri atoe ufafanuzi wa kina kuhusu mkataba huo aliousaini huko Uingereza. Hii ingetosha!

Lakini, anapokwenda na kumtuhumu Mheshimiwa Waziri, “amedanganya”, amesema mambo yasiyo sahihi! Waziri ni Kiongozi katika jamii, kiongozi ambaye ana heshima siyo tu hapa Tanzania, lakini kwa watu wote ambao wanafanya naye kazi; viongozi wa nchi za nje, Mawaziri wenzake (counterparts) katika nchi zingine wanatakiwa waone kwamba Mheshimiwa huyu anapata heshima katika nchi yake. Sasa pale tunapoanza kumburuza Mheshimiwa Waziri na kuonyesha kwamba Mheshimiwa Waziri ni muongo kabla hata hatujampa nafasi ya kutoa hayo maelezo, kwa kweli hiyo haikuwa nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi naomba tu niseme kwamba maneno aliyoyasema Mheshimiwa Mbunge, mimi nasema ni mazito, yameudhi na yamemsononesha Mheshimiwa Waziri. Naomba kusema kwamba adhabu hiyo, naunga mkono itolewe. Asante sana. (Makofi)

MHE. WILLIAM J. KUSILA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Lakini, kwa heshima zote kabisa, naomba niseme kwamba msemaji aliyenitangulia sasa hivi, amenifilisi yale yote niliyotaka kusema, na kwa misingi hiyo, sioni sababu ya kuchelewesha shughuli za Bunge lako, bali naunga mkono hoja iliyotolewa. (Makofi)

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, asante. Kimsingi naungana na waliotangulia kwamba maneno yaliyokuwa yamezungumzwa na Mheshimiwa Zitto, yalikuwa ni maneno ambayo hayaridhishi na ninaona kuna uongo ndani yake kutokana na hasa pale aliposema kwamba mkataba unaonekana uko tofauti kwa maana kwamba alikuwa anaongea kama mtu tayari alishaona mkataba, kumbe baadae tumekuja kugundua kwamba alikuwa bado katika kuomba mkataba. Kwa hiyo, mimi naona hiyo ni uongo.

Mheshimiwa Spika, lakini, kwa sababu kwa sisi tunaoamini Biblia, inasema kwamba “Mwenyezi Mungu alipoudhika na Godoma…

SPIKA: Siyo Dodoma! (Kicheko)

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, Sodoma na Gomola, alipokuwa amesikitishwa, amewatuma wale Malaika, lakini kuna waliokuwa wanahuzunika, wakaomba kama unaweza ukapataikana msamaha. Akasema hata wangekuwa watano, ningesamehe. Akashuka mpaka akatokea Bwana Rutu na Familia yake. Sasa na mimi najiuliza, katika yale yote ambayo kijana huyu Mbunge anayachangia, Je, hatuwezi kuona hata moja ambalo ni jema? Kwa hiyo, ninaomba kwamba badala ya kumsimamisha kwa sababu Chama cha Mapinduzi (sasa niko kwenye siasa) ndicho kilichosababisha kuwa na Vyama vya Upinzani, kilikubali chenyewe kwamba tuwe na hali ile ya kubadilishana mawazo, kwa hiyo kwa misingi hiyo kwa kutumia nafasi hiyo ya Chama, naomba siyo nia yangu kupingana na hali iliyopo, nina uchungu sana na mambo yaliyojitokeza, lakini naomba kama kuna uwezekano wa kupunguza adhabu hiyo, basi nitakuwa nimefarijika zaidi. Mheshimiwa Spika, asante!

SPIKA: Pendekeza adhabu mbadala, ndio Kanuni zinavyosema!

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, adhabu mbadala ninayoiona ni yeye kusema kwamba hatarudia tena kusema maneno kama hayo Bungeni.

SPIKA: Naona hiyo, haikuungwa mkono!

MHE. ABUBAKAR KHAMIS BAKARY: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii. Mimi nina mambo mawili tu:

(Hapa Minong’ono ya Wabunge Ilisikika)

SPIKA: Order, order, tusikilizane! Tumsikilize mwenzetu!

MHE. ABUBAKAR KHAMIS BAKARY: Mheshimiwa Spika, suala la mwanzo ni kwamba Je, ile kauli ya Mheshimiwa Zitto aliyozungumza ya kusema kwamba alimtuhumu kwamba alidanganya. Je, kauli hii kuna athari yoyote katika kulivunjia heshima Bunge letu? Nafikiri hili ndilo suala ambalo ni muhimu.

Mheshimiwa Spika, sasa tukitizama katika Katiba, Kifungu cha 63(2), moja ya kazi za Bunge ni kusimamia Serikali. Na unaposimamia Serikali, unapokuwa na honest belief kwamba kuna kitu ambacho kimefanyika na honest belief ile ukaitoa katika Ukumbi huu wa Bunge, Mheshimiwa Spika, hiyo ni kuonyesha kwamba unataka kujua hali ya Serikali inavyotendeka. Kwa hiyo, mimi nasema kwamba Mheshimiwa Zitto alikuwa na honest belief ingawa baadaye ilitolewa na kuonekana kwamba siyo kweli, hizo ni moja katika kazi za Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ikiwa kila mtu atakuja hapa, atakuwa na honest belief, atasema kitu, halafu kikaonekana kwamba honest belief ile si kweli, tukamtia adhabu, Bunge lako Mheshimiwa Spika, ninaweza kusema kwamba litakuwa ni rubber stamp, litataka kila mtu anayesema ndio hicho hicho kiungwe mkono, kitu ambacho kitakuwa ni kinyume kabisa na haki za Wabunge na utaratibu wa Bunge kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa maana hiyo, mimi nahisi maelezo aliyoyazungumza Mheshimiwa Zitto hayajaathiri heshima ya Bunge katika mantiki ya kufanya kazi. Kwa maana hiyo, mimi ningelishauri kwamba Mheshimiwa Zitto ni kuonywa tu kwamba yale maneno aliyoyatumia yalikuwa ni mazito kidogo, basi mara nyingine angalau atumie maneo laini. Lakini, ninachoogopa ni kwamba ikiwa kila mtu anatoa maelezo kwa belief katika roho yake kusema kwamba hiki ninaamini kwamba kimefanyika, kikawa proved kwamba hakikufanyika, halafu tukampa adhabu, Mheshimiwa Spika, Bunge lako litakuwa ni rubber stamp ambayo hiyo siyo kazi ya Bunge. Mheshimiwa Spika, nakushukuru! (Makofi)

SPIKA: Nifafanue tu, haki ya kusema au kuchangia humu Bungeni inalindwa na Katiba. Lakini, katiba hiyo hiyo ambayo imeturuhusu kuunda Kanuni, imeweka mipaka ya namna ya kuitumia haki. Kwa hiyo, uangalifu kuhusu lugha umesisitizwa sana humu, ndiyo maama mnaona Mabunge ya wenzetu watu wanatupiana viti, watu wanapigana ngumi kama Bunge la Italia ilitokea mwaka jana! Kauli ikiwa mbaya tutashindwa. Sasa mimi nataka mjielekeze hapo tu. Siyo suala la haki, haki ya kusema ipo. Lakini, sasa nini kinasemwa, wakati gani, kwa ushahidi upi, ndio suala lenyewe hilo. Kwa hiyo tuendelee. (Makofi)

MHE. ADAM K. A. MALIMA: Mheshimiwa Spika, naomba niseme yafuatayo katika hoja hiyo:- Kwanza kabisa, naomba niseme kwamba labda sisi wengine tunamfahamu Mheshimiwa Zitto kuliko wengine kwa sababu tunapata fursa ya kukaa naye kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi na pale taratibu za mjadala ni tofauti na hizi, kwa hiyo, tunaufahamu mchango wake, tunaufahamu uwezo wake. Na katika hili ambalo linaamuliwa, hakuna mtu anayeweza kusema kwamba kuna mtu ana–doubt kuhusu uwezo wake.


Mheshimiwa Spika, lakini, tunachosema, umesema wewe “imeathiri heshima ya Bunge”. Mheshimiwa Spika, sasa umenitangulia kidogo, lakini mimi nilitaka kusema wale wanaokwenda mbali huko Italy na Japan na Israel, Kenya tu hapa! Walikuja Wabunge wa Kenya kwenye Kamati ya Fedha wiki iliyopita, wamekaa kule juu. Tulivyokutana nao Dodoma Hotel jioni yake, wanasema “Your Parliament is very Civilized”, Wabunge wa Kenya tu hapo! Sasa sisi tunachosema ni kwamba ile civilized nature ya Parliament yetu inatokana na kuheshimiana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na kaka yangu Waziri Mkuu anajua, katika watu wanaoihoji Serikali wanapopata nafasi, mimi ndiye ninakuwa wa kwanza. Lakini, ukitaka kuihoji Serikali, uihoji kwa taratibu na nidhamu ambazo sisi katika Bunge hili tumejiwekea. Suala linaloingia hapa siyo kuihoji Serikali, suala linaloingia hapa ni kumvunjia heshima Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tunajiuliza Je, yale maneno ya kumwambia amelidanganya, amelipotosha na yeye ni Waziri, ana nafasi yake. Kwa hiyo, na magazeti yakalichukulia hapo na watu wengine na nini…. Kusema kweli mimi naungana na Mheshimiwa Mudhihir anaposema kwamba Mheshimiwa Waziri amedhalilishwa na kauli hiyo. Na baada ya kudhalilishwa Mheshimiwa Waziri kwa nafasi yake na kwa kauli yake kwa kuwa ameisema Bungeni, kumtuhumu kwamba amesema maneno yale ndani ya Bunge ni kulivunjia heshima Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi nakubaliana na adhabu ya Mheshimiwa Mudhihir na naomba isiwe hiyo tu, kuna mwingine amenong’ona viwe vikao vinne. Mheshimiwa Spika, lakini, mimi ni katika watu ambao tutaathirika na kutokuwepo kwake kwa sababu tunamhitaji kwenye Kamati ya Fedha. Lakini, hatuhitaji watu ndani ya Bunge hili ambao watakuwa hawana nidhamu kiasi cha namna hii. Mheshimiwa Spika, naomba niunge mkono hoja ya kaka yangu Mheshimiwa Mudhihir. Asante sana. (Makofi)

MHE. PHARES K. KABUYE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi niseme machache. Mheshimiwa Spika, mimi nashindwa kusema kwamba kasema uongo na huo uongo kwamba ni mkubwa. Amehoji mkataba kusainiwa London na ni kweli na hakuna aliyekwishakwenda kuona kwamba yale yalikuwa safi au hapana. Yote aliyoyasema, nadhani wengine tumesema si kweli, hapa tumegawanyika. Kuna aliyesema ni kweli, lakini na sisi tukasema si kweli. Lakini, yeye alileta hoja, katoa taarifa kwamba nitakuja nitaleta hoja. Hoja ameileta, kama inaonekana ameshindwa, hivi shitaka linazua lingine pale pale? (Kicheko)

SPIKA: Mheshimiwa Kabuye, unaturudisha nyuma. Tunafuata Kanuni. Kesho na keshokutwa tutazungumza upungufu na jinsi ya kuboresha Kanuni zetu. Sasa hapo, unaweza kuyazungumza na tukarekebisha. Lakini, sasa hivi hizi ndio Kanuni tulizonazo hazijabadilishwa na ya 59(iii) inamruhusu Mbunge bila taarifa kusimama na kutoa hoja kwamba Mbunge mwenzie aadhibiwe kwa kiwango ambacho atakitaja kwa sababu alichokifanya au kukinena kabla huyo mhusika, Mbunge kimeathiri heshima ya Bunge. Sasa wewe jadili hilo.

MHE. PHARES K. KABUYE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwanza mtu, si mahakamani, lakini mtu anaweza akajiuliza Bunge ni Waziri? Waziri anaweza akasema nimevunjiwa heshima, akatoa hoja! Maana ya Bunge ni nini? Kamsema mtu na mtu huyo hajalalamika, sasa kavunjia Bunge heshima namna gani?
Mheshimiwa Spika, lakini naomba tu niseme kwamba uamuzi wa watu wengi unakuwa hivyo kwa sababu, utanisamehe, wakati najifunza Literature, nakumbuka mambo ya Socret, alisema (msinichukulie kwamba nawasema) “kwamba ninyi mwafanya hivyo mkifikiri kwamba mtakwepa kutoa hesabu ya maisha yenu, bali mimi nawaambia kwamba matokeo yatakuja kinyume chake, watu wengi watawataka kutoa hesabu ya maisha yenu nao watakuwa vijana zaidi kuliko mimi. Na ninyi mtawakasirikia sana”

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo uamuzi wa wengi…aliposema hiyo, wakampigia kura, alipojaribu kujieleza, hata kura zikapungua. Kwa hiyo, uamuzi wa namna hiyo, ninaomba kama ingekuwa Kamati ikakaa, ikachekecha, tungepewa kwamba kweli ukubwa wa uongo unalingana na huu au uongo haupo. Lakini, kwa sababu ni umati, uamuzi wa watu wengi, eeh, hapa ni mambo mengi. Kwa hiyo, mimi ninaomba mwisho kwamba angepewa fursa ya kutafuta hivyo vielelezo, inawezekana hakujua kwamba mambo yangelifika hapa. Nakushukuru sana!

SPIKA: Kabla sijamwita Mheshimiwa Mbunge, Mzee Malecela, ninapenda kuuliza kama Mheshimiwa Zitto anapenda kusema kitu chochote katika mchakato wote huu kwa sababu hakujiorodhesha kusema, pengine anacho cha kuongea.

MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, I am a democrat. Niko tayari kwa maamuzi yoyote Bunge litakayochukua! (Makofi)

MHE. DR. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Spika, kwanza ningependa nichukue fursa hii kusema naunga mkono hoja mabyo imetolewa na ndugu yetu Mheshimiwa Mudhihir. Ninaunga mkono hoja hii na ninataka niseme hili kwa uchungu sana kwamba Bunge hili lazima liwe Bunge lenye heshima ambayo tumeachiwa tangu miaka mingi iliyopita. Mimi sijapata kukuta debate ikawa kama ya leo. Na lilipoanzia, kwanza yeye alianza kusema Waziri amelidanganya Bunge hili. Sasa wengine tunajaribu kusema labda tunasema Karamagi, hapana, siyo Karanmagi, ni Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Taznania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo hili alilolisema, kwanza limemdhailisha Waziri, limedhalilisha Serikali. Pili, linaleta hisia kwamba Mawaziri wa Chama cha Mapinduzi waongo. Na wana-CCM, tukumbuke, tunapoapa tunasema “nitasema kweli…”

WABUNGE FULANI: Daima.

MHE. DR. JOHN S. MALECELA: Hapa tumeona Mheshimiwa Karamagi akaisema kweli na wote hapa katueleza na tukaamini na tukakubali kwamba kweli hakudanganya Bunge hili. Kwa hiyo, mimi ningependa kwamba katika hili tusiwe na huruma kwa sababu wanasema “mdharau mwiba ataota nini…?”

WABUNGE FULANI: Tende.

MHE. DR. JOHN S. MALECELA: Sasa huu mwiba tuuondoe leo. Wengine watasema kwamba ooh labda hii itampa sifa kwa watu, hapana! Tusipomuadhibu, kwa watu itaonekana Serikali ya CCM, Mawaziri wa CCM wanasema uongo kwenye Bunge ambayo si kweli. Hii ni Serikali ambayo imechaguliwa na Mheshimiwa Rais Kikwete, Serikali tunayoiamini chini ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Edward Lowassa. Na kweli, tuseme kweli kwamba Serikali yetu kila mara inajitahidi. Mawaziri wanapojibu hapa, wanajitahidi kweli kweli, kutoa mambo ya kweli na wakiona haitoshi, huwa wanasema au tuwafuate tuwaongezee au wanasema watatuandikia barua baadaye. (Makofi)

Makeshimiwa Spika, kwa kweli baada ya kusema hayo, mimi ningewaomba Wabunge wote pamoja na hata Wapinzani kwamba….shauri yenu, mimi mradi naomba tu, cha hakika sibembelezi! Ila ninachosema yeyote atakayepita katika njia ambayo Kabwe amepita, lazima tumuadhibu na kwa hiyo nakubalina na hoja ya Mheshimiwa Mudhihir kwamba Kabwe aadhibiwe na ni leo. Mheshimiwa Spika, Asante! (Makofi)

SPIKA: Kabla sijamwita mtoa hoja, nalazimika nifafanue hii adhabu imekaa kaaje kama ndiyo itaamuliwa. Tukiamua Waheshimiwa Wabunge leo kwamba imethibitika kuwa Mheshimiwa Zitto alimsingizia Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini na kwa hiyo alisema uongo, maana yake hatahsiriki kwa mujibu wa Azimio ama hoja iliyoletwa na Mheshimiwa Mudhihir, hataruhusiwa kushiriki shughuli za Bunge kuanzia Azimio litakapochukuliwa na adhabu hiyo itaendelea kwa maana ya Vikao vya Bunge na Kamati zake hadi mwaka ujao. Ndio, kwa sababu na mkumbuke Mkutano wa Januari ni wa wiki tatu na Kamati zake wiki mbili na kwa kipindi chote hicho atakuwa…Ni Novemba, ndio, ni Novemba samahani. Hatuna Mkutano mwingine mpaka Januari mwaka ujao. Adhabu ikichukuliwa inayohusu Mkutano huu na ujao…si ndio alivyosema! Maana yake huu na ule wa Novemba. Mimi naifafanua tu adhabu ili tuielewe. Kwa hiyo adhabu ni kwamba arejee Januari mwakani. Au sivyo? …huku akilipwa nusu mshahara na bila posho. Sasa, basi mmeiona uzito wake na wakati huo huo sauti ya wananchi wa Kigoma Kaskazini iwe kama imezima. Sasa, ni zito, mimi niseme tu kuna nafasi hapo ya marekebisho, inaruhusiwa kabisa. Kuna mnafasi ya marekebisho na ningemuomba Mheshimiwa Mudhihir kulitazama hilo kama inawezekana…. Mimi ndiye ninayeongea sasa, kuguna wala hakusaidii, vinginevyo wewe mwenyewe ndiye unaweza kupata matatizo bure, ndio tabu ya Kiti hiki. Kwa hiyo, mtulie ninapotoa maelezo, kwa sababu ipo Kanuni nayo ambayo ukionyesha dharau kwa Spika, yatakupata makubwa kuliko ya Zitto! Kwa hiyo, Mheshimiwa Mudhihir unayo nafasi ya kupendekeza kwa sababu wewe ndiye mtoa hoja, kwa kuzingatia uzito huo niliousema. Kwa hiyo, namwita sasa mtoa hoja! (Makofi)

MHE. MUDHIHIR M. MUDHIHIR: Mheshimiwa Spika, niliipenda sana hekima yako ya kumtaka Mheshimiwa Zitto kama ana lolote aseme, nilijua kwa utu uzima wako ulikuwa unakusudia nini. Kwa bahati mbaya sana amesema yeye ni Democrat, litakalotokea na litokee. Katika mazingira kama hayo, mimi nashindwa kubadilisha msimamo wangu. Kwa hiyo, nimalizie kwa kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwa kuunga mkono hoja yangu na wale ambao hawakuunga mkono, wote wamekuwa wakitimiza wajibu wao wa kidemokrasia. Ningependa na mimi vile vile nithibitishe kuwa ni Democrat. Kwa hiyo, nayameza maamuzi yangu haya kwa uchungu mkubwa, lakini sina njia nyingine ya kusaidia heshima ya Jimbo langu. Mheshimiwa Spika, asante sana! Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja! (Makofi)


(Hoja Ilitolewa Iamuliwe)



SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hoja iliyo mbele yetu iliyoletwa na Mheshimiwa Mudhihir, ni kwamba Mheshimiwa Kbwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini katika matamshi yake ya tarehe 16 mwezi wa 7, alimsingizia Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini kwamba amelidanganya Bunge na hivyo kumfanya yule Waziri aonekane ni mwongo. Nilimpa nafasi kuleta hoja hapa ya kuunda kamati teule. Ameileta, Bunge hili limeikataa baada ya kuridhika na maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini kwamba hakuna haja kwa sababu maelezo hayo yamejitosheleza na bado kuna nafasi ya kupata hata makala nyingine za maelezo zaidi. Kwa hiyo, sasa hoja iliyo mbele yetu kutokana na hilo ni hiyo ya Mheshimiwa Mudhihir kwamba sasa Mheshimiwa Kabwe Zitto kwa kosa hilo alilotenda, asimamishwe chini ya Kanuni ya 59(iii) kwa kipindi chote cha Bunge hili kilichosalia na Bunge la Tisa. Sasa nitawahoji…

(Hoja Ilitolewa Iamuliwe)

(Hoja Iliamuliwa na Kuafikiwa)
(Bunge Liliafiki Hoja ya Kumsimamisha Shughuli za Ubunge
Mheshimiwa Kabwe Z. Zitto Kwa Mkutano wa Nane na wa Tisa)


SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, natamka kwamba Mheshimiwa Kabwe Zitto, amesimamishwa shughuli za Ubunge kuanzia sasa hadi Mkutano wa Januari mwaka ujao. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, sina mengi zaidi ya kusema imekuwa ni siku ndefu. Nadhani wote tumejifunza kutokana na yote yaliyotokea. Kwa hiyo, sasa naliahirisha Bunge hadi kesho saa 3.00 asubuhi.

(Saa 02.05 Usiku Bunge Liliahirishwa Mpaka Siku ya
Jumatano Tarehe 15 Agosti, 2007 Saa Tatu Asubuhi)
 
Msanii ... una hakika na hicho kwenye bold hapo juu?

...haha what you need to know? hujui alikuwa ktk serikali ya mkaa hapa anayetuhumiwa kufisadisha taasisi ya urais kwa kujiingiza ktk ujasiriamali akiwa kiongozi mtukuka??

Mwafrika naona unataka kunikamatisha hahahahahaha
 
Thank you Asha ila its toooo long and ujuavyo kuna wengine humu tu wavivu wa kusoma hahahaha
But nakubaliana nawe kuhusu mchango wa stela manyanya bungeni wakati wa suluba ya zitto
ila my concern ni kwamba, wabunge wa ccm ndio waliopiga kura nyingi kumfyatua bungeni zitto, na humo bungeni akina kilango na wengine walikuwemo na waliweza kusimama na kutoa maelezo ambayo yangeweza kubadilisha mwelekeo. ila kwa aibu yao Rais ndiye aliyeunda tume na sasa wana haha kurudisha imani iliyoangukia ktk kilindi.

Nipo sahihi kutomuamini mama malecela kwani inatia shaka sana kuona wacheza ngoma za kiganga wakiimba kwaya kanisani.....
 
Thank you Asha ila its toooo long and ujuavyo kuna wengine humu tu wavivu wa kusoma hahahaha
But nakubaliana nawe kuhusu mchango wa stela manyanya bungeni wakati wa suluba ya zitto
ila my concern ni kwamba, wabunge wa ccm ndio waliopiga kura nyingi kumfyatua bungeni zitto, na humo bungeni akina kilango na wengine walikuwemo na waliweza kusimama na kutoa maelezo ambayo yangeweza kubadilisha mwelekeo. ila kwa aibu yao Rais ndiye aliyeunda tume na sasa wana haha kurudisha imani iliyoangukia ktk kilindi.

Nipo sahihi kutomuamini mama malecela kwani inatia shaka sana kuona wacheza ngoma za kiganga wakiimba kwaya kanisani.....

Msanii,

ni haki yako kutomwamini Mama Malecela kama vile wengine wameamua kutomwamini yeyote yule katika siasa za Tanzania. Katika hili la Mama Malecela, amethibitisha na anazidi kuthibitisha kuwa anaweza kusimama na kutetea kile anachoamini (hata ikiwa kama ni kumtosa Tingatinga - unakumbuka hii statement).

Katika hili, nampa support yangu.
 
Fine! analyse Anne n all ways possible..That is not what im in to.

Let me Give a strong warning to anybody with Neagative motive against her.

This is not the seasons for such things.

Anybody with such move? ..is destined to meet a seriouse Shame!

You want to fight Anne?

Just be clearn.

Love The peolple of this national.

Love This country.

Just work for its Goodness.

Nothing else?

This isnt The time...

Not say we didn worn you..when all the Hell get in you when you try harm Anne.

Dont and Never!

Hope am nt undestood!! You better get this clear.
__________________
 
...haha what you need to know? hujui alikuwa ktk serikali ya mkaa hapa anayetuhumiwa kufisadisha taasisi ya urais kwa kujiingiza ktk ujasiriamali akiwa kiongozi mtukuka??

Mwafrika naona unataka kunikamatisha hahahahahaha

No sitaki kukumata na ndio maana nimekupa swali ili uweke context kwenye maandishi yako. Ningetaka kukumata ningeanza kukushikia bango mkuu. Mama Malecela amekosha moyo wangu na I am very proud of her.
 
nisije nikawa mvivu wa kusoma nitaenda ktk hansard za bunge nikasome kule....
But i believe i was there and you know the vote casted and the majority (ccm) had their best to hammering Zitto out.

About Anne Kilango, she was also a minister ktk serikali fa fisadi then lini amekuwa mlokole mpaka amkane shetani na mambo yake yote??? Just think think and not stink..... shehe yahaya hutumia majini kuagua watu lakini anamcondem shetani.... inakuja hiyo??? isije ikawa changa la macho.

Lakini kwa ccm (wakali wa propaganda) yote yawezekana. mchanga unaweza kuwa sukari

Hapana Mkuu Msanii,Mama Kilango hajawahi kuwa Waziri katika serikali ya Awamu yeyote...Muda mrefu alikuwa mfanyakazi wa shirika la ndege Tanzania (ATC),Na kwa muda mfupi akafanyakazi kwenye shirika la ndege KLM (DSM) kabla ya kujikita kwenye Biashara zake binafsi,kutokea huko ndio akaenda kugombea Ubunge wa Same Mashariki.

Tumpe Ushirikiano huyu Mama anafanya kile wengi wameshindwa kukifanya huko Bungeni.
 
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, Sodoma na Gomola, alipokuwa amesikitishwa, amewatuma wale Malaika, lakini kuna waliokuwa wanahuzunika, wakaomba kama unaweza ukapataikana msamaha. Akasema hata wangekuwa watano, ningesamehe. Akashuka mpaka akatokea Bwana Rutu na Familia yake. Sasa na mimi najiuliza, katika yale yote ambayo kijana huyu Mbunge anayachangia, Je, hatuwezi kuona hata moja ambalo ni jema? Kwa hiyo, ninaomba kwamba badala ya kumsimamisha kwa sababu Chama cha Mapinduzi (sasa niko kwenye siasa) ndicho kilichosababisha kuwa na Vyama vya Upinzani, kilikubali chenyewe kwamba tuwe na hali ile ya kubadilishana mawazo, kwa hiyo kwa misingi hiyo kwa kutumia nafasi hiyo ya Chama, naomba siyo nia yangu kupingana na hali iliyopo, nina uchungu sana na mambo yaliyojitokeza, lakini naomba kama kuna uwezekano wa kupunguza adhabu hiyo, basi nitakuwa nimefarijika zaidi. Mheshimiwa Spika, asante!

SPIKA: Pendekeza adhabu mbadala, ndio Kanuni zinavyosema!

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, adhabu mbadala ninayoiona ni yeye kusema kwamba hatarudia tena kusema maneno kama hayo Bungeni.

SPIKA: Naona hiyo, haikuungwa mkono!
MHE. DR. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Spika, kwanza ningependa nichukue fursa hii kusema naunga mkono hoja mabyo imetolewa na ndugu yetu Mheshimiwa Mudhihir. Ninaunga mkono hoja hii na ninataka niseme hili kwa uchungu sana kwamba Bunge hili lazima liwe Bunge lenye heshima ambayo tumeachiwa tangu miaka mingi iliyopita. Mimi sijapata kukuta debate ikawa kama ya leo. Na lilipoanzia, kwanza yeye alianza kusema Waziri amelidanganya Bunge hili. Sasa wengine tunajaribu kusema labda tunasema Karamagi, hapana, siyo Karanmagi, ni Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Taznania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo hili alilolisema, kwanza limemdhailisha Waziri, limedhalilisha Serikali. Pili, linaleta hisia kwamba Mawaziri wa Chama cha Mapinduzi waongo. Na wana-CCM, tukumbuke, tunapoapa tunasema “nitasema kweli…”

WABUNGE FULANI: Daima.

MHE. DR. JOHN S. MALECELA: Hapa tumeona Mheshimiwa Karamagi akaisema kweli na wote hapa katueleza na tukaamini na tukakubali kwamba kweli hakudanganya Bunge hili. Kwa hiyo, mimi ningependa kwamba katika hili tusiwe na huruma kwa sababu wanasema “mdharau mwiba ataota nini…?”

WABUNGE FULANI: Tende.

MHE. DR. JOHN S. MALECELA: Sasa huu mwiba tuuondoe leo. Wengine watasema kwamba ooh labda hii itampa sifa kwa watu, hapana! Tusipomuadhibu, kwa watu itaonekana Serikali ya CCM, Mawaziri wa CCM wanasema uongo kwenye Bunge ambayo si kweli. Hii ni Serikali ambayo imechaguliwa na Mheshimiwa Rais Kikwete, Serikali tunayoiamini chini ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Edward Lowassa. Na kweli, tuseme kweli kwamba Serikali yetu kila mara inajitahidi. Mawaziri wanapojibu hapa, wanajitahidi kweli kweli, kutoa mambo ya kweli na wakiona haitoshi, huwa wanasema au tuwafuate tuwaongezee au wanasema watatuandikia barua baadaye. (Makofi)

Makeshimiwa Spika, kwa kweli baada ya kusema hayo, mimi ningewaomba Wabunge wote pamoja na hata Wapinzani kwamba….shauri yenu, mimi mradi naomba tu, cha hakika sibembelezi! Ila ninachosema yeyote atakayepita katika njia ambayo Kabwe amepita, lazima tumuadhibu na kwa hiyo nakubalina na hoja ya Mheshimiwa Mudhihir kwamba Kabwe aadhibiwe na ni leo. Mheshimiwa Spika, Asante! (Makofi)

nIMEWALETEA JINSI ALIVYOTETEA NA JINSI TINGATINGA LILIVYOPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KWENYE JENEZA LA HAKI NA UKWELI.
 
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, Sodoma na Gomola, alipokuwa amesikitishwa, amewatuma wale Malaika, lakini kuna waliokuwa wanahuzunika, wakaomba kama unaweza ukapataikana msamaha. Akasema hata wangekuwa watano, ningesamehe. Akashuka mpaka akatokea Bwana Rutu na Familia yake. Sasa na mimi najiuliza, katika yale yote ambayo kijana huyu Mbunge anayachangia, Je, hatuwezi kuona hata moja ambalo ni jema? Kwa hiyo, ninaomba kwamba badala ya kumsimamisha kwa sababu Chama cha Mapinduzi (sasa niko kwenye siasa) ndicho kilichosababisha kuwa na Vyama vya Upinzani, kilikubali chenyewe kwamba tuwe na hali ile ya kubadilishana mawazo, kwa hiyo kwa misingi hiyo kwa kutumia nafasi hiyo ya Chama, naomba siyo nia yangu kupingana na hali iliyopo, nina uchungu sana na mambo yaliyojitokeza, lakini naomba kama kuna uwezekano wa kupunguza adhabu hiyo, basi nitakuwa nimefarijika zaidi. Mheshimiwa Spika, asante!

SPIKA: Pendekeza adhabu mbadala, ndio Kanuni zinavyosema!

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, adhabu mbadala ninayoiona ni yeye kusema kwamba hatarudia tena kusema maneno kama hayo Bungeni.

SPIKA: Naona hiyo, haikuungwa mkono!
MHE. DR. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Spika, kwanza ningependa nichukue fursa hii kusema naunga mkono hoja mabyo imetolewa na ndugu yetu Mheshimiwa Mudhihir. Ninaunga mkono hoja hii na ninataka niseme hili kwa uchungu sana kwamba Bunge hili lazima liwe Bunge lenye heshima ambayo tumeachiwa tangu miaka mingi iliyopita. Mimi sijapata kukuta debate ikawa kama ya leo. Na lilipoanzia, kwanza yeye alianza kusema Waziri amelidanganya Bunge hili. Sasa wengine tunajaribu kusema labda tunasema Karamagi, hapana, siyo Karanmagi, ni Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Taznania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo hili alilolisema, kwanza limemdhailisha Waziri, limedhalilisha Serikali. Pili, linaleta hisia kwamba Mawaziri wa Chama cha Mapinduzi waongo. Na wana-CCM, tukumbuke, tunapoapa tunasema “nitasema kweli…”

WABUNGE FULANI: Daima.

MHE. DR. JOHN S. MALECELA: Hapa tumeona Mheshimiwa Karamagi akaisema kweli na wote hapa katueleza na tukaamini na tukakubali kwamba kweli hakudanganya Bunge hili. Kwa hiyo, mimi ningependa kwamba katika hili tusiwe na huruma kwa sababu wanasema “mdharau mwiba ataota nini…?”

WABUNGE FULANI: Tende.

MHE. DR. JOHN S. MALECELA: Sasa huu mwiba tuuondoe leo. Wengine watasema kwamba ooh labda hii itampa sifa kwa watu, hapana! Tusipomuadhibu, kwa watu itaonekana Serikali ya CCM, Mawaziri wa CCM wanasema uongo kwenye Bunge ambayo si kweli. Hii ni Serikali ambayo imechaguliwa na Mheshimiwa Rais Kikwete, Serikali tunayoiamini chini ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Edward Lowassa. Na kweli, tuseme kweli kwamba Serikali yetu kila mara inajitahidi. Mawaziri wanapojibu hapa, wanajitahidi kweli kweli, kutoa mambo ya kweli na wakiona haitoshi, huwa wanasema au tuwafuate tuwaongezee au wanasema watatuandikia barua baadaye. (Makofi)

Makeshimiwa Spika, kwa kweli baada ya kusema hayo, mimi ningewaomba Wabunge wote pamoja na hata Wapinzani kwamba….shauri yenu, mimi mradi naomba tu, cha hakika sibembelezi! Ila ninachosema yeyote atakayepita katika njia ambayo Kabwe amepita, lazima tumuadhibu na kwa hiyo nakubalina na hoja ya Mheshimiwa Mudhihir kwamba Kabwe aadhibiwe na ni leo. Mheshimiwa Spika, Asante! (Makofi)

nIMEWALETEA JINSI ALIVYOTETEA NA JINSI TINGATINGA LILIVYOPIGILIA MSUMARI WA MWISHO KWENYE JENEZA LA HAKI NA UKWELI.

Mheshimiwa MK,

Sidhani kama unataka kutumia maneno ya Tingatinga kumhukumu Mkewe?!?
 
Yaani mnanipa shida sana kuwaelewa ,hivi CCM mmoja akiruka na kusema hovyo kwa kuwa tu dalili na ishala zinaonyesha kama amekosa kula ,inakuwa tayari mumeshapata mshikaji ,hivi tutategemea kuanguka kwa CCM mpaka lini , kwa nini wasemaji wasiwe kutoka vyama vya upinzani ni kumtegemea huyu na yule magogo ya CCM yakiumana ,yaani watu wanaingia tamaa kifisi halafu jamaa hao wanajiuzulu na mambo kwisha.
Kunahitaji kubadili muelekeo wa uhakika kuliko huu wa tamaa ya kuanguka mkono unaopungwa.
 
Hapana Mkuu Msanii,Mama Kilango hajawahi kuwa Waziri katika serikali ya Awamu yeyote...Muda mrefu alikuwa mfanyakazi wa shirika la ndege Tanzania (ATC),Na kwa muda mfupi akafanyakazi kwenye shirika la ndege KLM (DSM) kabla ya kujikita kwenye Biashara zake binafsi,kutokea huko ndio akaenda kugombea Ubunge wa Same Mashariki.

Tumpe Ushirikiano huyu Mama anafanya kile wengi wameshindwa kukifanya huko Bungeni.

Asante Mwawado kwa ufafanuzi kwenye hili!
 
Yaani mnanipa shida sana kuwaelewa ,hivi CCM mmoja akiruka na kusema hovyo kwa kuwa tu dalili na ishala zinaonyesha kama amekosa kula ,inakuwa tayari mumeshapata mshikaji ,hivi tutategemea kuanguka kwa CCM mpaka lini , kwa nini wasemaji wasiwe kutoka vyama vya upinzani ni kumtegemea huyu na yule magogo ya CCM yakiumana ,yaani watu wanaingia tamaa kifisi halafu jamaa hao wanajiuzulu na mambo kwisha.
Kunahitaji kubadili muelekeo wa uhakika kuliko huu wa tamaa ya kuanguka mkono unaopungwa.

Mkuu mbona watu wa upinzani watasema mara ngapi?

Kuna tatizo gani kama mwana ccm anayepigana na ufisadi akiungwa mkono?
 
Back
Top Bottom