simon james
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 283
- 140
Inasikitisha sana
"Ndugu zangu,
Najaribu kutuliza mawazo ili angalau niweze kuwapa kidogo tulipofikia na tunakoelekea juu ya suala hili. Kwa kweli haivumiliki ukimwona ulimboka kwa jinsi alivyotendewa na hali aliyonayo; kwa wale wanaojua hali za kitabibu, "this is a very unstable condition that demands permanent watch 24/7".
Kwa taarifa tulizokusanya, ulimboka na mwenzake waliitwa na Afisa mmoja (Jina linahifadhiwa) ili kuzungumza mambo (fulani) na wakiwa wanaendelea na mazungumzo bila kuwa na mwelekeo wa muafaka, jamaa akawasiliana na watu (fulani) kwa simu. Ghafla wakajitokeza "ASKARI" wakawataka yule (Afisa) na Dr (aliyeongozana na Ulimboka) waendelee na shughuli zao na kuwambia "Tunamtaka huyu". Wakatumia nguvu, wakamburuta na kumtia kwenye gari jeusi na kuondoka naye wakidai wanampeleka Polisi.
Huku wakiwa wanamtesa, walimlazimisha mambo kadhaa (kwa sasa tusiyataje) wakaenda naye asikokujua, wakampiga sana kwa ngumi, mateke na magongo na wakati mwengine wakitumia Bunduki zao. Wakiwa wanampiga pia walikuwa wakisema kuwa amewatesa/wasumbua sana na kuwa anajifanya mjanja mbele ya (Srk) na hivyo wanamalizana naye; akapoteza fahamu...
Wakamtupa eneo la mapori huko Tegeta hadi alipookotwa na wananchi asubuhi na kukabidhiwa mikononi mwa Wanaharakati waliompeleka Hospitali Muhimbili.
Wakati akipokelewa MOI tayari baadhi ya wanaharakati walishafika eneo lile, kumbe kati ya walimpokea alikuwamo kijana anayesadikiwa kuwa ni "Askari". Huyu aligundulika baada ya mda mfupi akiwa amejificha chooni akiwasiliana kwa simu na watu aliokuwa akiwaambia " Hajafa. Bado anahema.... na maneno mengine yaliyoashiria kuwa waliofanya 'kazi' ile hawakukamilisha 'maagizo'. Vijana wakamfundisha adabu kwa hasira na kumkuta akiwa na Redio Call, ambayo baada ya muda mfupi Polisi FFU walifika na gari na vifaa vya vurugu wakiisaka ile Radio.
Nashindwa kuendelea....."
NB: Haya ni maelezo ya mwanaharakati Albanie Marcossy aliyehusika kumsaka kama nilivyoyanukuu Mabadiliko Group.