4G router ya kampuni gani ya simu inafaa kwa Smart TV

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,867
8,278
Wakuu nisiwapotezee muda, kwanza kabisa nikiri kuwa sina utalaamu na mambo ya watoa huduma za mawasiliano hapa Tanzania hasa makampuni ya simu.

Tatizo langu ni kuwa nilinunua smart tv na kuja nayo huku wilayani nikitegemea nitaweza kutumia intanet ya TTCL kupitia simu za waya kama vile wanavyojitangaza kwenye vipeperushi.

Bahati mbaya sana TTCL ya hapa wilayani ni kama imekufa kwani hawatoi huduma ya simu za waya au mezani wanadai nyaya zote zimeibiwa na vibaka na nikaambiwa niandike jina ili huduma ya mkonga wa Taifa ikija basi niwe kati ya watu wa kwanza kuhudumiwa lakini hadi sasa hakuna lolote linalofanyika

Sasa imebidi labda niwe najaribu mara moja moja kutumia hizi 4G router zinazotangazwa na hawa watoa huduma za simu.

Sijui kwa uzoefu wenu hasa huku mawilayani ni 4G router ya kampuni gani inafaa?

Ni hilo tu manguli wa teknolojia.
 
Kama una smartphone jaribu voda kama unapata 4g

IMG-20230708-WA0000.jpg
 
Matumizi ya Smart tv kwa maana Ya Netflix na zifananiazo?

Ngumu kwa hizi GB za kupimiwa unless uwe unaibia ibia kwa kuangalia kidogo na kuzima na hii yenyewe inabidi uwe makini sana uhakikishe unaset hizo app Quality isizidi 720p.

Kuna njia kama mbili hapo

1. Ununue Router Universal ambayo utatumia mtandao wowote, usijifunge na mtandao mmoja Bongo, vifurushi vinabadilika kila siku, fanya mpango upate postpaid ya Tigo, Voda ama Airtel vifurushi vyake vina unafuu. Router ukicheki jiji ama kupatana unapata za kutosha. Vodacom wana unlimited ya 50,000 unatumia kwa speed kubwa kama GB 20 kisha speed ina drop, sijajua ikidrop speed kama inatosha kustream angalau 480p, kama inaweza hii inakufaa kwa smart tv, 480p si Quality kubwa lakini angalau muda wote utakua online.

2. Vodacom Supakasi, hii ni Unlimited kwa 4G ni 115,000 kwa mwezi kama utaweza ku Afford,

Ukitoa mitandao ya simu kuna satelite internet sema hizi zina ping kubwa sana zinafaa tu kuangalia vitu ambavyo sio live.
 
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi ngoja hii mada nicopy kama marejeo yangu, ubarikiwe sana mtaalamu
 
Back
Top Bottom