4.8 magnitude earthquake hits Arusha

Thanx. Hii itasadia kuwaelimisha wa TZ kuwa wapo watu wanafanya kazi dunia na wanauwezo wa kutambua yanayotokea ndani ya taifa lako. Tunahitaji kuwekeza sana kwenye elimu hasa ya sayansi kama tunataka kufika walipo wenzetu hata kama ni baada ya miaka 1000.
(hapo kwenye red) ...sisi bado unakuta vibao vya "usikae hapa", "usipige picha hapa" kama ni jeshini au kwingine!!!

Inabidi kuchukua tahadhari maana uzoefu unaonyesha kuwa yakitokea sehemu inaweza kuwa zaidi ya mara moja kwa mida inayokaribiana.

Poleni sana
 
Poleni sana ndugu zetu kwa 3 au 4 ni kubwa kimtindo kwa bongo hasa ukitegemea majengo yetu hayajajengwa kukabiliana na tetemeko la ardhi
Kuna wakati nilikuwa sehemu fulani ya dunia tukapatwa na tetemeko la ardhi 7.4 sina hamu nikisikia hili neno.
 
Small earthquake rattles rural Tanzania
The Associated Press
More News

The U.S. Geological Survey says a 4.8-magnitude earthquake shook rural Tanzania southwest of Mount Kilimanjaro.

Friday's earthquake could be felt as far away as Nairobi, Kenya, by people on high floors of downtown buildings. Nairobi is 220 miles (350 kilometers) northeast of the epicenter.

The U.S. Geological Survey says the epicenter was 90 miles (145 kilometers) southwest of Arusha, Tanzania.

Africa does not have any known major earthquake zones. The area southwest of Mount Kilimanjaro is one of the few regions on the continent with regular seismic activity.

Small earthquake rattles rural Tanzania - KansasCity.com

145 Km away from Arusha North East ...Hayo ni maeneo ya Babati kuelekea katesh and Singida

....Tupeni taarifa!!
 
Mm sikuweza kusikia chochote maana nilikuwa Underground mita 800 kutoka surface, ila tulipewa taarifa baada ya dk 15 tetemeko kupita.
 
Nipo Babati, kwa kweli naona kama sehemu nyingne ilikuwa afadhali, maana watu walitimka kutoka ndani ya nyumba walizokuwamo kukimbia kimbia kwa kiwewe, binafsi nilipata mshtuko sana. Habari zaid huku ni kuwa kuna nyumba zimepata nyufa kubwa na kuna mwanafunzi wa shule ya msingi Masaka amejeruhiwa na bati lililodondoka kutoka kwenye paa la shule hyo!!
 
Nyakati za mwisho anayejua ni Mungu tu!

Wewe vipi tena, Mungu si alikwambia dalili za mwisho? Mimi pia ni mbishi lakini nimetafakari mfululizo wa matetemeko makubwa miaka 5 iliyopita nimeanza kuiona picha.
 
poleni Arusha,
Mungu epushia mbali.... maana likitokea kweli sasa serikali ndio itakuwa imepata sababu ya kukwepa majukumu kisa? Tetemeko! Kama yale ya mtikisiko wa uchumi, Jk aliimba hadi tukajuta.

Nakubalina na wewe mkuu. Kwa hili ni kumuomba Mungu atuepushe na hili balaa kabisa, kwani serikali ambayo inashindwa kutatua suala la ajli za barabarani kweli itaweza kusaidia watu kwenye matukio kama haya kweli? I don't think so. Yaani kama nawaona wakina mama Yeeyo ndani ya zila Manyatta zao aisee!
 
Nikiwa mezani nimekuta laptop inacheza...Nikasimamakuangalia ninini kinafanya meza icheze, lakini sikuona kitu!
Mara nikasikia watu wanashuka ghorofani kwa kasi, nikaconfirm kuwa ni tetemeko!Lakini halikuwa kubwa sana!

Poleni jamani, tumshukuru Mungu halikuleta madhara
 
Back
Top Bottom