2015; Mbunge ni lazima awe amesoma kidato cha sita

Pasco_jr_ngumi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,802
282
Ni mawazo yangu!!!

Wale wenye madegree bila kusoma kidato cha sita wasiruhusiwe kugombea Ubunge!!!""""
 
Au wadau mnasemaje??? Sipendi watu wa kuungaunga hadi kupata degreee; they are not compentence
 
Sikuelewi hata kidogo unapo propose elimu kwenye katika kuwatumikia wananchi kisiasa.Kwanza kabisa ninaomba ufahamu siasa siyo profession na kwa hivyo basi, mwanasiasa kazi yake siyo kama ya ualimu, udaktari, uhandisi au polisi n,k.Tatizo kubwa nchini, watu wengi wanafikili siasa ni proffesion kama zile nilizozitaja hapo juu. Ndiyo maana Tanzania tuna utitili wa vyama vya siasa na wanaotaka kuwa wana siasa na ukichunguza kwa undani, utagundua kuwa nia yao kuu si kuwatumikia wananchi bali kujinufaisha tu kimaslahi. Hii kasumba ndiyo inayozaa rushwa na siasa uchwara na ubinafsi.

Kwa kukusaidia, hata katiba ya nchi haijaweka kiwango cha elimu kwa mtanzania kuwa Raisi ikilitambua hilo.
Watanzania wengi tunakuwa na tabia na kasumba katika siasa ya kuangalia zaidi kigezo cha elimu badala ya nini amewafanyia na atawafanyia wananchi.
Sikubaliani hata kidogo na maoni yako kwa sababu yanalenga sana katika ubaguzi wa kundi fulani katika jamii ili lisijihusishe na ujenzi na maendeleo nchini.
 
Back
Top Bottom