Hakuna cha ajabu kuhusu hao watoto. tatizo kama taifa tumepoteza muelekeo katika elimu. Inatia aibu na kusikitisha sana katika hili. Suala la ubora katika elimu inaonekana ni msamiati mgumu sana kwa serikali yetu. Ni muhimu kama taifa tukatambua kuwa njia iliyobora zaidi katika kugawana keki ya...
Ni kweli JokaKuu. Njia uliyopendekeza itaisaidia sana CHADEMA na wanahitaji kuwa na angalau vipindi maalum kila wiki angalau vipindi vitatu vya saa moja moja kwenye televisheni na redio.
Ni kweli pia suala la Afya nalo ni muhimu sana na niamini kuwa yote yanawezekana kuyatekeleza kwa pamoja. Tatizo viongozi wetu hawana dhamira na nia ya kuibadilisha na kuiendeleza nchi yetu. Jamani hali ya shule zetu inatisha kupita kiasi.
Ni muhimu sana kama taifa tukaelewa na kukubaliana kuwa njia bora zaidi ya kuifikia kila familia na kuisaidia kupambana na umaskini ni kwa kila familia kuipatia elimu bora hasa kupitia watoto wa familia husika.
Wiki ijayo Wabunge wetu wanaelekea Dodoma kwa ajili ya kikao chao cha kwanza baada ya uchaguzi mkuu.
Wakati wabunge wetu wakielekea Dodoma je wanayafahamu haya
1. Kiwango cha fedha anacholipwa Mbunge mmoja kwa mwaka ni zaidi ya fedha ambayo Serikali inatoa kama ruzuku katika kuendesha zaidi ya...
Ila tunakoelekea Serikali haina njia lazima ihakikishe vijana wetu wanasoma katika mazingira yanayokubalika, wanakuwa na walimu bora na wakutosha na pia wanafanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho kuanzia shule za msingi.
Inabidi wanasiasa wetu sasa wafikie hatua ya kuona aibu na wamuogope MUNGU. Ni muhimu sana hata kama kijana ataishia kidato cha nne awe amepata elimu iliyo bora.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.