Search results

  1. Mindi

    Zitto Kabwe Jitafakari

    Nilimsikiliza Zitto Kabwe, mmoja wa vigogo katika viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani hapa Tanzania, akitoa hotuba yake katika mkutano wa Baraza la Vyama vya siasa. Nilimsikia akimuomba Rais Samia, kwa unyenyekevu mkubwa, "asaidie" ili Mbowe awe huru. Nilisikiliza pia majibu ya rais...
  2. Mindi

    Athari za Majaji walioteuliwa na Hayati Magufuli

    Tumewahi kusikia malalamiko kuhusu kada ya majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Malalamiko hayo, kwamba kuna majaji hawana viwango vya kiweledi vinavyotakiwa, yalitolewa bungeni, na mh. Tundu Lissu enzi hizo. Nakumbuka Spika wa wakati huo, Anne Makinda, alikasirishwa sana na kauli hiyo ya Mh...
  3. Mindi

    Mamlaka iliyomteua Sabaya na kutomtumbua, inahusika pia na hukumu hii

    Sabaya amehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa ujambazi wa kutumia silaha. Katika kujitetea, mara nyingi amesema kwamba alikuwa anatekeleza maagizo ya mamlaka iliyomteua. Kwa maoni yangu, hata bila utetezi wake huo, kitendo cha mamlaka ya uteuzi kunyamazia vitendo vyake vya ujambazi, ni kuhusika...
  4. Mindi

    Tuhuma za Polisi kubambikiza kesi, kunyanyasa, kutesa na kuua watu, zinahitaji hatua madhubuti

    Kumekuwa na tuhuma nyingi zikielekezwa Jeshi la Polisi kuhusu kubambikiza kesi, kunyanyasa raia ambao ndio wanapaswa kuwalinda, utesaji wa watuhumiwa hadi wengine kuuwawa, kama ilivyotokea kwa mdogo wa mh. Heche, aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya CHADEMA. Huyu alikamatwa na polisi, na akiwa...
  5. Mindi

    Ndugai Aanze na "Waheshimiwa" Wabunge kabla ya "Wasomi" Mawakili

    Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameeleza "kukerwa" kwake na kada nne kwamba wanajiona ni bora kuliko wengine. Kwa mfano Mawakili, ambao wana utaratibu wa kuitwa "Wakili Msomi" kabla ya kutaja jina. Hoja ya Ndugai ni kwamba iweje Mawakili waitane "Msomi" ambapo wasomi wako wengi tu, siyo Mawakili...
  6. Mindi

    Rais Samia kutoka nia ya kukutana na vyama vya upinzani hadi "Ngoja tuimarishe uchumi kwanza"

    Moja ya kauli za mwanzo kabisa za Rais Samia ambazo zilileta msisimko nchini ni kusudio lake la kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani. Msisimko ulitokana na ukweli kwamba Rais Magufuli hakuwa na mpango wa aina hiyo kabisa, badala yake mkakati wake ulikuwa kuviua kabisa vyama vya upinzani...
  7. Mindi

    Hivi tuseme ukweli, kati ya CCM na CHADEMA ni nani hasa chama imara cha siasa?

    CCM pamoja na historia ndefu ya kutokea TANU, Pamoja na kwamba ipo madarakani miongo kadhaa, haijui maisha nje ya utawala, bado ni chama dhaifu sana kiasi kwamba hakiwezi kusimama chenyewe bila kubebwa na baiskeli ya wagonjwa ya Polisi, msukumaji usalama wa taifa. Haiwezi kufanya chochote bila...
  8. Mindi

    Msimamo wa Tanzania kuhusu Korona uliotolewa katika kikao cha Umoja wa Afrika AU ni ubabaishaji

    Nimemsikiliza waziri Kabudi ambaye alimwakilisha Rais Magufuli kwenye kikao cha Umoja wa Afrika. Wakati Rais Ramaphosa wa Afrika ya Kusini akiwa ni mwenyekiti anayemaliza muda wake, akieleza jinsi korona ilivyovuruga mipango ya maendeleo katika bara la Afrika, Tanzania ilitoa msimamo wake na pia...
  9. Mindi

    Kutovunjwa hoteli ya Desderia na Mikakati ya Serikali ya Magufuli

    Tukio la hivi karibuni la Rais Magufuli kutoa agizo la kuzuia "uvunjwaji" wa hoteli kubwa ya nyota tatu, inayomilikiwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya, maarufu "Sugu", linaibua hoja mbalimbali. Tukirejea miaka 5 ya kwanza ya Magufuli, DC Sabaya wa Hai, anaonekana alipewa "kazi" maalum ya "kumkaba"...
  10. Mindi

    Hotuba ya Rais Magufuli mbele ya Mgeni wake Rais Museveni imejaa Hofu ya Kampeni

    Hapa niandikapo, Rais Magufuli amehitimisha hotuba yake. Sasa hivi anaongea Rais Museveni. Hotuba ya Rais Magufuli imejikita katika kuchambua faida ya bomba la mafuta toka Uganda. Lakini kilichojitokeza hasa ni ile "tone" ya Magufuli. Alikuwa anarudiarudia maneno, hana amani, tofauti na...
  11. Mindi

    Sekula mpya ya uchangiaji huduma za Bima ya Afya ni Mwiba kwa wafanyakazi

    Bila shaka kama mkakati wa kuongeza mapato ya serikali, bila kujali athari kwa wafanyakazi, hasa wastaafu, serikali ya Rais Magufuli imekuja na "uboreshaji" wauchangiaji huduma za Afya kwa njia ya Bima. Wafanyakazi wa serikali na mashirika yake, kwa mujibu wa sheria, hukatwa michango ya...
  12. Mindi

    Magufuli aliahidi kuboresha mafao ya Wafanyakazi. Badala yake kavuruga maslahi yao, na ametumia fedha za mafao yao kujipaisha zaidi

    Moja ya simulizi za kusikitisha katika utawala wa awamu ya Tano, ni kisa cha wafanyakazi wa Tanzania. Zipo kada nyingi zilizoumizwa sana na utawala huu, mojawapo nyingine ni wakulima. Hawa wote wametumika kama nyenzo tu ya kufanikisha miradi ya awamu hii, huku wao wenyewe na familia zao...
  13. Mindi

    Kuwakemea Viongozi wa Dini, Magufuli Ameweka Rekodi Mpya

    Nimemsikiliza Rais Magufuli, akihutubia taifa baada ya kumwapisha Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba. Kuna mengi aliyoongea JPM ambayo yanavutia mjadala. Mimi nijikite kujadili kwa kifupi alichosema Rais kuhusu Imani, Biblia na Viongozi wa Dini. Nianze kwa kumtahadharisha Rais...
  14. Mindi

    Sasa ni dhahiri Rais wetu Magufuli amekwama

    Katika hotuba aliyoitoa Rais wetu hivi karibuni kule Chato, kuna mambo kadhaa ambayo yanatuonesha kwamba hali ya nchi kwa sasa ni tete: 1) Kwamba Rais yuko Chato kwa muda mrefu sasa kwa kawaida Rais wetu Magufuli huenda Chato kwa mapumziko. hivi sasa ni muda umepita tunaona Rais yupo Chato...
  15. Mindi

    Pale Tanzania ilipoaibika

    Ilikuwa ni siku ya aibu kubwa sana ambayo ni wachache wenye macho waliona jinsi Tanzania tulivyoaibika. Tanzania, ambayo ni hivi karibuni tu tumetoka katika uchaguzi unaonuka uvundo mkali, ambapo jitihada za makusudi zilifanywa kupora uchaguzi mchana kweupe kwa mbinu mbalimbali chafu (kufunga...
  16. Mindi

    Haya sasa ni Maradhi ya Rais Magufuli

    Rais Magufuli amezuia wapinzani wasiseme wala kukohoa. kazuia bunge live. alimwagiza Ndugai awashughulikie wabunge wa upinzani ndani ya Bunge na yeye atawashughulikia nje ya Bunge. Alipoona haitoshi kuzuia mikutano ya nje, sasa anadhibiti hata mikutano ya ndani. Kwenye uchaguzi wa...
  17. Mindi

    Ukibogoyo wa Mzee Warioba

    Mzee Warioba ni moja ya wazee wanasikitisha sana. Huwa anachomoza mara moja moja na kutoa maneno machache. Ukifika wakati wa kusimama na kujenga hoja kali za kuipeleka nchi panapoeleweka, anasinyaa. Ripoti ya Warioba kuhusu Rushwa, ambayo ilikuwa ndiyo hasa muarobaini wa Rushwa, iliwekwa...
  18. Mindi

    Sasa ni wazi kwamba CCM ni Dhaifu

    Inaonekana mastratejisti wa CCM hawajaelewa uzito wa Waraka wa Makatibu wakuu wastaafu wa CCM, wazee Kinana na Makamba. Ukiusoma huo waraka katika hali ya kawaida tu, utaona kwamba waliouandika ni watu wenye weledi na wametafakari sana na kuchagua maneno na sentensi za kutumia. kuna strateji...
  19. Mindi

    Kwa hili la sherehe za Kitaifa rais Magufuli kafanya mazishi tu walioua wengine

    Ukiangalia mataifa mengine, hasa yaliyoendelea, moja ya sifa inayotofautisha na mataifa yetu haya ni KUJUA NA KUTHAMINI HISTORIA YA TAIFA LAO. Mimi nikiangalia naona kwamba sisi hatuijui vema historia ya nchi yetu, na ya Taifa letu. Kuna mambo mengi ambayo hayajafanyiwa utafiti...
  20. Mindi

    Tanzania inawahitaji akina Mussa Assad Wengi zaidi ili tuendelee

    Katika vipindi vya TV na Redio kwa muda sasa tumekuwa tukilishwa hotuba za JPM, makaribisho, sifa na maelezo ya kazi kubwa anayofanya rais wetu katika maeneo mbalimbali kuanzia Mtwara, Ruvuma na Njombe. Lakini ukichambua kwa makini utaona kwamba pamoja na jitihada kubwa anazofanya Rais...
Back
Top Bottom