Zuzu bhana!!!

Django

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
354
Reaction score
147
Mwalimu: alimuuliza zuzu kwanini unachelewa shule?
Zuzu: alijibu natoka mbali na shule
Mwalimu: unatoka mbali mbinguni?
Zuzu: mbinguni kwa mbele kidogo....
 
Baadae kwenye kipindi cha sayansi mwalimu akawaambia wanafunzi wachore picha ya barafu. Zuzu kwa hakuwa anaweza kuchora picha ya barafu, akapiga hesabu akaamua kulikojolea daftari. Mwalimu alipopita kukagua akakuta daftari ya zuzu imelowa. Mwalimu: we zuzu mbona daftari lako limelowa.? Zuzu: itakuwa barafu niliyochora imeyayuka!
 

tehe tehe tehe tehe tehe
 
Hahahaha ana akili sana

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 

he he he he teeee, dhudhu bana...!
 
Uzuri wa zuzu anafikiria sana na majibu yake huwa ni ya papo kwa papo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 


na hata alipoambiwa achore train hakuchora mwalimu alipopita akamwambia nilichora ila umechelewa limeshaondoka, kweli ni zuzu
 
Zuzu kaibiwa yebo msikitini akawa analia ile mbaya Shekhe akamwambia "usilie mwachie mungu" Zuzu akajibu "Mungu hazimtoshi zile yebo ni ndogo"
 
mwal akawaambia wanafunzi wachore ng'ombe anakula majani, zuzu alikuwa hawez kuchora. mwl baada ya kukagua wote akafika kwa zuzu
Mwl: Yuko wapi ng'ombe uliyemchora?
Zuzu: Amekwenda kula majani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…