Zitto Zuberi Kabwe, mambo yanabadilika, muda unakwenda kasi sana!

Mar 17, 2016
193
188
Zitto Zuberi Kabwe, home boy wangu, huku kuna kamsemo kanasema "Ahuli halabhandi" (yaani ulipo walikuwepo wengine), ndio! Alikuwepo Mwalimu, akaja Ben, Mzee Ruksa, Jakaya na sasa Pombe Joseph, naye ataondoka atakuja mwingine, walikuwepo Aman Waridi Kaburu, na Augustine Lyatonga Mrema, nao wamepita, ni utaratibu wa kawsida wa maisha!. Lkn wote hawa watakumbukwa kwa waliyoyafanya yawe mema au mabaya.

Zitto Zuberi Kabwe ni moja ya vijana kwenye akili kubwa sana, wenye mvuto wa hali ya juu, bingwa wa kujenga hoja, mtu ambaye anaweza kuigeuza hoja ya kawaida kuwa nzito na Mwenye ushawishi kwa kada zote za watu, mtu ambaye akisimama na kujenga hoja utatamani aendelee, mbunge ambaye inawezekana anaongoza kwa kutoa hoja na michango mjarabu kwa mda wa miaka kumi na ushee sasa. Kijana ambaye nathubutu kusema ameleta Mapinduzi ktk bunge ikiwemo kuwavutia vijana wengi kufanya siasa ma pengine kuwashawishi wazee kuanza kuwaamini vijana ktk nafasi Fulani Fulani.kiufupi ukiulizwa umwelezee unaweza kesha na usimalize.

Lkn pamoja na hayo yote Zitto Kabwe kwa mda wa miaka kumi, amekuwa akiwaacha watu na maswali yasiyo na majibu, Zitto ameiangusha serikali ya awamu ya 4 Mara kibao na yeye hujigamba hvo hadharani, lkn kamwe hatukuwahi kuona akikiona cha motto kama makamanda wengine, amewaangusha mawaziri kibao na viongoz waandamizi kibao na kutamka hadharani kuwa hajawahi kushindwa vita, viongozi kadhaa waliowahi kukutana na timbwili lake waliishia kulalama tu kama watoto wadogo.
Ni zitto huyu ambaye mwaka 2010 aliibuka mbunge pekee kupitia CHADEMA mkoani kigoma huku NCCR iliyokuwa haijawekeza chochote Kigoma ikitoka na wabunge 4, Zitto huyu alishawahi kuungana na Mzee Machache kumchakaza Prof. Mhongo, mtu aliyeonekana kufanya kazi iliyotukuka pale Nishati, Zitto hachukui posho kitambo, aliwaacha Lema na Mama Makinda na maswali kibao kwani kwao posho ndo maisha ya wabunge.

Zitto huyu huyu, ktk tamhtiriya ya Escrow, alituletea majina, account na kiasi cha pesa kilichochukuliwa kupitia mkombozi Bank, lkn hadi kesho majina, account na pesa zilizochukuliwa pale Stanbick pamoja na kuwajua na nyenzo zilizotumia Kubenea hajawahi kutueleza, watu tukabaki na maswali aliwezaje Mkombozi akashindwa Stanbick, Zitto huyu pekee yake kati ya mashujaa watatu wa Escrow Saga aliyerudi bungeni, jamani Zitto!! Huyu jamaa alipambana na CDM last year akiwa jeshi la mtu mmoja, watu wakamtabilia kifo cha kisiasa lkn wapi!

Sasa mambo yanabadilika, mda unakwenda kasi, kwa mbali naye anaanza kuisoma namba, sasa ameanza kujihami, ni kama kuna kitu kimemkurupusha toka kichaka alipozoea kustarehe, kwa Mara ya kwanza Zitto kkt mapambano ameomba msaada toka kwa walee, lkn pia ni kama anawaonya wale wamzuie huyu anayemkurupusha toka kwenye kichaka chake, maana akimalizana naye nao hawatapona.

Sisi wasoma namba tuliokubuhu tunamkaribisha ubaoni, kitu kizuri ni kuwa usomaji namba wa Zitto ni wa aina yake, maana unaendana na kujibiwa kwa maswali yetu ya mda mrefu! Karibu tuisome namba kwa pamoja!
 
Zito amekuwa mkweli wa mambo na matendo yake na siku zote amesimamia Yale ambayo anaamini kuwa ni sahihi Bila kujali anaemkosoa au kumuunga mkono ana wadhfa gani. Binafsi namkubali sana, naamini atakuja kuwa kiongozi mkubwa katika hii nchi.
 
Hivi kwnn nyie wapinzani wengine mnamuonea wivu zitto. Ndio maisha yake aliochagua muacheni na harakati zake mnatumia nguvu kubwa badala kupambana na utawala wa kiimla hamjielewi mnamng'ang'ania zitto shame on you
 
Ngoja tumuangalie miaka hii mitano! Bila shaka hadi 2020 tutakuwa na majibu yote ya maswali yetu tata!
 
Hata ukipewa miaka Mia yy zitto ana mchango mkubwa ktk mageuzi ya nchi na mpk sasa one man army bado anaburuta mtazoza eeeeh lkn that's reality hayumbishwi anasmamia mtazamo na msimamo wake

Ngoja tumuangalie miaka hii mitano! Bila shaka hadi 2020 tutakuwa na majibu yote ya maswali yetu tata!
 
Watu aina ya zitto walizoea vyepesi hasa kubebwa na mafisadi na kukwapua pesa kutoka kwenye mashirika ya umma kwa kuwatisha watendaji kwa kutumia nafasi yake ya kuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge.
 
Zitto yuko sahihi sana kuhusu MAGUFULI, asibezwe hata kidogo, makosa yake ya nyuma yasihusishwe na huu ukweli anaousema kuhusu awamu ya tano.
 
Zitto Zuberi Kabwe, home boy wangu, huku kuna kamsemo kanasema "Ahuli halabhandi" (yaani ulipo walikuwepo wengine), ndio! Alikuwepo Mwalimu, akaja Ben, Mzee Ruksa, Jakaya na sasa Pombe Joseph, naye ataondoka atakuja mwingine, walikuwepo Aman Waridi Kaburu, na Augustine Lyatonga Mrema, nao wamepita, ni utaratibu wa kawsida wa maisha!. Lkn wote hawa watakumbukwa kwa waliyoyafanya yawe mema au mabaya.

Zitto Zuberi Kabwe ni moja ya vijana kwenye akili kubwa sana, wenye mvuto wa hali ya juu, bingwa wa kujenga hoja, mtu ambaye anaweza kuigeuza hoja ya kawaida kuwa nzito na Mwenye ushawishi kwa kada zote za watu, mtu ambaye akisimama na kujenga hoja utatamani aendelee, mbunge ambaye inawezekana anaongoza kwa kutoa hoja na michango mjarabu kwa mda wa miaka kumi na ushee sasa. Kijana ambaye nathubutu kusema ameleta Mapinduzi ktk bunge ikiwemo kuwavutia vijana wengi kufanya siasa ma pengine kuwashawishi wazee kuanza kuwaamini vijana ktk nafasi Fulani Fulani.kiufupi ukiulizwa umwelezee unaweza kesha na usimalize.

Lkn pamoja na hayo yote Zitto Kabwe kwa mda wa miaka kumi, amekuwa akiwaacha watu na maswali yasiyo na majibu, Zitto ameiangusha serikali ya awamu ya 4 Mara kibao na yeye hujigamba hvo hadharani, lkn kamwe hatukuwahi kuona akikiona cha motto kama makamanda wengine, amewaangusha mawaziri kibao na viongoz waandamizi kibao na kutamka hadharani kuwa hajawahi kushindwa vita, viongozi kadhaa waliowahi kukutana na timbwili lake waliishia kulalama tu kama watoto wadogo.
Ni zitto huyu ambaye mwaka 2010 aliibuka mbunge pekee kupitia CHADEMA mkoani kigoma huku NCCR iliyokuwa haijawekeza chochote Kigoma ikitoka na wabunge 4, Zitto huyu alishawahi kuungana na Mzee Machache kumchakaza Prof. Mhongo, mtu aliyeonekana kufanya kazi iliyotukuka pale Nishati, Zitto hachukui posho kitambo, aliwaacha Lema na Mama Makinda na maswali kibao kwani kwao posho ndo maisha ya wabunge.

Zitto huyu huyu, ktk tamhtiriya ya Escrow, alituletea majina, account na kiasi cha pesa kilichochukuliwa kupitia mkombozi Bank, lkn hadi kesho majina, account na pesa zilizochukuliwa pale Stanbick pamoja na kuwajua na nyenzo zilizotumia Kubenea hajawahi kutueleza, watu tukabaki na maswali aliwezaje Mkombozi akashindwa Stanbick, Zitto huyu pekee yake kati ya mashujaa watatu wa Escrow Saga aliyerudi bungeni, jamani Zitto!! Huyu jamaa alipambana na CDM last year akiwa jeshi la mtu mmoja, watu wakamtabilia kifo cha kisiasa lkn wapi!

Sasa mambo yanabadilika, mda unakwenda kasi, kwa mbali naye anaanza kuisoma namba, sasa ameanza kujihami, ni kama kuna kitu kimemkurupusha toka kichaka alipozoea kustarehe, kwa Mara ya kwanza Zitto kkt mapambano ameomba msaada toka kwa walee, lkn pia ni kama anawaonya wale wamzuie huyu anayemkurupusha toka kwenye kichaka chake, maana akimalizana naye nao hawatapona.

Sisi wasoma namba tuliokubuhu tunamkaribisha ubaoni, kitu kizuri ni kuwa usomaji namba wa Zitto ni wa aina yake, maana unaendana na kujibiwa kwa maswali yetu ya mda mrefu! Karibu tuisome namba kwa pamoja!

Narudia kumnukuu Waziri Mwakyembe (PhD) ni nchi masikini tu na zinazoendelea ndiyo watu ambao hata Shule hawana wanaweza kufanya na kufika hapa walipofika akina Sugu, Zito Mbowe &Co.

Zito kabwe aliweza tu kushamiri na kuonekana kwamba kuna anachokijua kwa sababu ya usanii, uongo na majungu aliozoea kuishi nao na tawala na mazingira ya wkt huwo pia ziliruhusu watu wa kaliba ya Zito yaani wanafiki, waongo na wapika majungu kumea na kushamiri, lkn kwa utawala huu wa PhD holders wa ukweli Zito atapotea kwenye ulingo wa Siasa za Tanzania kwa maana aina ya Siasa zake za Mujungu, Uongo na Unafiki hazina nafasi tena, kumbuka alivyodanganya Bunge juzi kwamba kulikuwa na mafuta ya wiki mbili baada ya hapo hakuna ndege itatua TZ mpka leo hii ni miezi karibia miwili Ma Airbus yanatua kama kawaida!
Rejea alivyodangnya kuhusu ktk kila shilingi 1000 unakatwa 280 bila hata ya kuujua undani wake, hivi ndivyo Zito kabwe alivyozoea kuishia, Majungu, uongo na Unafiki na unafiki huwo wa akina Zito ndiyo uliomuondoa Waziri Muhongo madarakani, Waziri Ndalichako alishutumiwa kuwaadhibu Waislamu na kuwafelisha, hii ndio aina ya watu tuliokuwa nao, yaani Waziri Ndalichako awafelishe Waislamu ili afaidike nini?!

Hivyo watu wa kaliba ya Zito Kabwe wanaishia na hawana nafasi tena, TanZania imezaliwa upya na hii inakuja kama shock kwa watu waliozoea Usanii na majungu kama Zito, Lowasa, Mbowe &Co.

Sasa Zito atafunguliwa mashitaka na Serikali si ajabu hii ni mara ya kwanza kwake kushitakiwa hiyo Wazungu wanaita a wake up call kwamba huu ni wakati mwingine na mambo ya usanii na majungu yameisha sasa, Zito Kabwe, Lisu &Co. wamefungiwa na Bunge si ajabu kwa kipindi kirefu kuliko ilivyowahi kutokea na nina uhakika hawakulitegemea hili yote hii ni kuwaaambia kwamba huu ni wkt mwingine na ma PhD holders hawataki mchezo na majungu bali wanataka kazi na kuing'oa hii nchi ktk hapa ili tuende mbele... hivyo kazi kwako Zito Kabwe &Co. aidha muende na flow au against it uamuzi ni wenu ...
 
Zitto ni wabunge wa mia wa ccm sasa Kama mtu sehemu mtu amepiga pushapu wanataka kuweka Sanamu kama kama Mbunge anasema Tulia ni sawa na Yesu kama Mbunge anataka Nasibu ajengewe sanamu
 
Wakati umebadilika kwa Zito na Gwajima. Wakati mmoja wao akikishinikiza Chama Tawala kimbane anayetishia maslahi yake binafsi ya 'wananchi' huku mwingine anaishinikiza Ikulu imbane aliyevuruga mikakati yake na ya 'wananchi'. Ni movie inayotaka umakini sana kuisoma. Kila la heri
 
Narudia kumnukuu Waziri Mwakyembe (PhD) ni nchi masikini tu na zinazoendelea ndiyo watu ambao hata Shule hawana wanaweza kufanya na kufika hapa walipofika akina Sugu, Zito Mbowe &Co.

Zito kabwe aliweza tu kushamiri na kuonekana kwamba kuna anachokijua kwa sababu ya usanii, uongo na majungu aliozoea kuishi nao na tawala na mazingira yawkt huwo pia ziliruhusu watu wa kaliba ya Zito yaani unafiki, uongo na majungu lkn kwa utawala huu wa PhD holders wa ukweli Zito atapotea kwenye ulingo wa Siasa za Tanzania kwa maana aina ya Siasa zake za Mujungu, Uongo na Unafiki hazina nafasi tena, kumbuka alivyodanganya Bunge juzi kwamba kulikuwa na mafuta ya wiki mbili baada ya hapo hakuna ndege itatua TZ mpka leo hii ni miezi karibia miwili Ma Airbus yanatua kama kawaida!

Hivyo watu wa kaliba ya Zito Kabwe wanaishia na hawana nafasi tena, TanZania imezaliwa upya na hii inakuja kama shock kwa watu waliozoea Usanii na majungu kama Zito, Lowasa, Mbowe &Co.

Sasa Zito atafunguliwa mashitaka na Serikali si ajabu hii ni mara ya kwanza kwake kushitakiwa hiyo Wazungu wanaita a wake up call kwamba huu ni wakati mwingine na mambo ya usanii na majungu yameisha sasa, Zito Kabwe, Lisu &Co. wamefungiwa na Bunge si ajabu kwa kipindi kirefu kuliko ilivyowahi kutokea na nina uhakika hawakulitegemea hili yote hii ni kuwaaambia kwamba huu ni wkt mwingine na ma PhD holders hawataki mchezo na majungu bali wanataka kazi na kuing'oa hii nchi ktk hapa ili tuende mbele... hivyo kazi kwako Zito Kabwe &Co. aidha muende na flow au against it uamuzi ni wenu ...
Mkuu nakuelewa sana, kwa sasa Zitto hana ubavu wa kuichezesha kidumbwe dumbwe serikali kwakuwa watu strong sana, unaanzia wapi kumtikisa Dr.Mpango, Ndalichako, prof. Mhongo, prof.Mbalawa, to be honest yangu aondoke Mr.Clean kwa mara ya kwanza nakuona serikali yenye strong men and women!
 
Back
Top Bottom