Zitto: Transparency on data regarding current infections, new infections, critical patients and deaths is very important in dealing with the Corona

Zitto una hoja nzuri ila unapenda kuigaiga sana...Halafu nikukumbushe sababu ya hali kuwa hivyo Ujerumani ni kuwa hawahesabu vifo vya coronavirus kama mgonjwa alikuwa na magonjwa mengine. Ni hayo tu.
 
Ya namna ya kutatua ugonjwa huu wa mazingira tuliyonayo. Ili kwamba tusifuate fikra za kikoloni.

1. Kuzuia wagonjwa kwa kuwaweka karantini hii yaitwa contain
Hivyo wagonjwa wapo wanaangaliwa maendeleo ya ugonjwa na ikiwa watapambana ndani ya siku 14 wataendelea kufanyiwa vipimo kabla ya kuwa clear.

Hii ya "containing" haiwezi kufanyika kwa mazingira ya nchi yetu na ndo maana wanachi wanashauriwa kunawa mikono na kutumia vitakasa mikono kila mara.

Pia huwezi kuzuia shughuli zingine za kiuchumi zisimame na ndo maana hata kule kwenye minada watu wanapiga kazi na wanahimizana kunawa mikono.

Haya mafua ya Corona si mabaya sana kulinganisha na mafua ya SARS.

Ni kutokana na hivyo basi nchi nyingi ambazo zilikumbwa na ugonjwa wa SARS zimetumia mbinu zilezile za kukabiliana an ugonjwa huu wa mafua wa Corona.

Nchi hizo ni Taiwan, Singapore, Korea Kusini, Hong Kong na Japan.

Hivyo Tanzania haiwezi kuzisikiiza nchi kama Uingereza au marekani mbazo zenyewe zinakabiliana na tatizo la Corona pamoja tatizo la raia wake kukataa kutii amari ya kuttembea mitaani mpaka wanapotishiwa kwa sheria ambazo wanaziita "Draconian rules"

Isipokuwa itafuata Model yake ya mfumo wake wa Afya na utoaji na upashaji taarifa ambapo mpaka sasa tunamsikiliza waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Hivyo wizara ya afya itatoa ushauri kwa wananchi na itatoa taarifa mpya kila zinapopatikana.
 
Zitto Ni wewe uliyeandika kuhusu Prof Dr. Janabi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina Shaka kabisa kuwa kwa kuwa barua hi imeandikwa kwa kiingereza imekuwa copied kwa mabeberu
 
Tayari Corona imekuwa agenda ya kupigia siasa!

Mara stimulus package kwenye sector ya utalii ndo kipaumbele mara transparency international!
 
Zitto Mheshimiwa hii barua kweli ulikusudia kumwandikia Mh Raisi wetu au umewaandikia Walimwengu? Kwanini usitumie tuu lugha yetu ya nyumbani?
 
Tayari Corona imekuwa agenda ya kupigia siasa!

Mara stimulus package kwenye sector ya utalii ndo kipaumbele mara transparency international!


Yaani wanazungumzia "Stimulus Package" ambazo ni nchi zilizoendelea tu ndizo zaweza kutenga fedha kama hizo kukingana na uchumi wao.

Ndo maana katika wanasiasa wajinga kabisa kuwahi kutokea nchini Tanzania Zitto Kabwe ni mmoja wao.
 
Zitto una hoja nzuri ila unapenda kuigaiga sana...Halafu nikukumbushe sababu ya hali kuwa hivyo Ujerumani ni kuwa hawahesabu vifo vya coronavirus kama mgonjwa alikuwa na magonjwa mengine. Ni hayo tu.
Japo nakubaliana na sehemu kubwa ya ushauri wa Zitto kwenye barua yake. Hila wana tabia za kusoma vichwa vya habari na kuchukua hizo sehemu kama mifano ya mafanikio bila ya kuangalia factor zingine mbali mbali kwanini sehemu fulani rate ya vifo ndogo.

Muhimu kuelewa rate of spread zinatofautiana ambapo Germany bado ipo nyuma hila na yenyewe inatabiriwa itawafikia tu wenzake kutokana na taratibu za Corona yeye anakwenda na mdumange wake iwapo awatachukua kama za wenzao kwenye kucheza nae.

Pili kuna swala la data sahihi za vifo. Leo ufaransa wamekuwa accussed kwa kuto jumuisha vifo vinavyotokea kwenye care homes za wazee wakati unaambiwa humo kuna nyumba luluki sasa zipo empty corona kaondoka na wazee, wamekiri na kujidai wana tengeneza system itakayo wajumuisha ina maana idadi yao ya vifo is distorted sio ya ukweli.

Huko kwenye nchi kama China na Asia ndio kabisa data zao sio za kuziamini kwa sana.

Put it this way the NHS ya UK has been voted the best health care system in the world in terms of planning, wider coverage and quality of service delivery for like ten years straight. Na kwa sasa wana wasiwasi juu ya uwezo wao kwenye kuhudumia wagonjwa wa Corona wakati bado awajazidiwa kama ilivyo Italy au Spain kwenye utoaji huduma. Makelele yote na hizi hatua serikari yao inazochukua ni kutambua wao sio special na Corona anaenda kwa mdundo wake ambao lazima ueshimike wanayokutana nayo wenzao na kwao pia itafika.

Sasa badala ya kujiaminisha sijui nani kafanikiwa kwa kupima sana etc sidhani kama inasaidia; hila busara ni kumueshimu Corona kwa namna anvyosambaa na kujaribu ku manipulate hayo mazingira kupunguza spread vinginevyo ni hatari tu kwa nchi maskini kama Tanzania.
 
For my self I agree with you Honourable Zitto Kabwe , God bless you.

A big salute to Hon. Zitto Zuberi Kabwe. The problem is, we have a President who never listens any advice from.anybody especially from opposition leaders..!
This is a calamity to our country.
God bless Tanzania.
 

Very True
 
Ana hoja za msingi, Ila kuna watu utakuta hata hawajasoma, kisa wameona tu jina ni kutoka kwa Zitto basi wameshaanza attack his personality in politics and not his attitude on the pandemic outbreak.

Ndugu yangu Mimi naona issue hapa seeI kwamba imetoka kwa Zitto!!Issue hapa kwa Mataga wengi Ni lugha!
Nashauri Mhe. Zitto aandike na ya Kiswahili ili tuongee lugha moja..!
Hata huyo mlengwa Sina hakika Kama atamwelewa Zitto...!!!
Tayari K/kuna Lumumbas wanadai na kumwona Mhe. Zitto ana fikra za Kikoloni kwa vile tu katumia Kiingereza kufikisha ujumbe wake...!!

Not Yet UHURU- By Ngugi wa Thiongo!
 

Uko sahihi kabisa ila kwenye suala la kuamini zipi ni taarifa sahihi bado hizi nchi nilizozitaja hapo juu, yaani Taiwan, Singapore, Korea Kusini na zingine nazo mifumo yao ya Afya imejaribu sana kupunguza kasi ya maambukizi kwa kutumia hiyo mkakati wa Contain,.

Kisha wakahakikisha wanafanya testing nyingi kwa raia na kuhakikisha raia wengi wanapimwa na kufikia mwezi janaury kesi nyingi zilikwishapungua kwa kiasi kikubwa.

Kwa mfano kisiwani Hong Kong mgonjwa akigundulika anawekwa katantini na anafungwa electronic tag mguuni ambayo ipo GPS connected.

Akitoka tu nje askari anakuja mlangoni na kuuliza waenda wapi?

Hivyo kwa kiasi kikubwa Hong Kong waliweza kulishughulikia hili tatizo kwa aina yake ya usimamizi na mfumo wake wa afya.

Hivyo tunatofautiana kwenye mifumo ya afya, teknolojia na maabara pamoja na vifaa vya kupimia.

Nchi kama UK upimaji umezorota kutokana na sababu zingine za logistics ambapo baadhi ya vipimo ni vya kuagiza kutoka China ambayo nayo imefanya lockdown hata kwenye viwanda na mabohari.

Hivyo masuala kama haya yanahitaji uelewa kidogo kabla ya kuyarukia na kutaka kuyatumia kisiasa.
 
Factors kama culture, society attitude, level of education, compliance ya wananchi, trust ya taasisi zao etc nazo zinachangia kwenye kuamua.

Nchi kama S.K na Japan ni very educated societies kushinda nchi nyingi za EU in terms population ratios na ni watiifu zaidi kiutamaduni kushinda EU kwa ivyo some leniency in lockdown measures put in places are likely because of suitability to their culture.

Uwezi kurudia kitu hiko hiko kwa nchi zetu ambazo mkuu wa nchi akipata nafasi ya ulinzi mdogo ndio anaona kama kapewa fursa ya kujumuika na wananchi wake tena kwa kujiachia anafanya na kuita kabisa na wapita njia we mzee njoo unywe kahawa.

Hao wananchi ndio kabisa kama unapitia comments za kwenye social media kuna mmoja nimesoma akijibu ushauri wa social distancing anadai yeye na wenzake walienda kula bata kama kawa wknd iliyopita tena anadai wali enjoy humo ndani shurti kukombatiana na mabinti halafu anamwambia huyo anaewapa ushauri asiogope sana kila mtu alitakiwa kunawa mikono na sabuni kabla ya kuingia club.

Pamoja na jitihada zote za elimu ya awali hawa kweli wakuwaachia kama South Korea kuranda ovyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…