Zitto njoo Morogoro Mjini

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
1,675
Reaction score
555
Namuomba mheshimiwa Zitto Zubery Kabwe kama hana uhakika wa kurudi bungeni kupitia Kigoma basi aje agombee Ubunge Morogoro Mjini kwani matumaini ya kupata Ubunge hapa 2015 ni makubwa sana ukilinganisha na Mikoa mingine Nchini.
 
Mkuu acha hizo, CHADEMA moro tumejenga wenyewe so ni lazima mgombea atoke hapa hapa mwenye mawazo mapya na fikra mpya, Zitto tayar kashafanya kazi yake muache akajenge taifa kupitia ulecture wa Lake Tanganyika University itakayoanzishwa hapo Kigoma, Hapa moro wapo makamanda wengi tu mfano Mwaipaja, Daza etc watatosha..
 
CHADEMA kuna Zitto Kabwe wengi, Dk Slaa wengi nk, acheni fikra potofu eti bila hao CHADEMA Hakuna, mnajidanganya, vijana wanazaliwa wengi
 
Duhh, mmeshaanza kampeni. Daza kafukuzwa, mwaipaja hajatangaza nia. Mambo bado sana
Ila Daza kaumia jamani, nasikia yuko Moi. Mwenye habari zaidi atujuze.
 
Duhh, mmeshaanza kampeni. Daza kafukuzwa, mwaipaja hajatangaza nia. Mambo bado sana
Ila Daza kaumia jamani, nasikia yuko Moi. Mwenye habari zaidi atujuze.

Hapana Mkuu sio campeni, Kweli Daza kafukuzwa lakini nashindwa kuamini kabisa huyu kamanda mpambanaji ilikuwaje mpaka akafukuzwa?!
 
Hapana Mkuu sio campeni, Kweli Daza kafukuzwa lakini nashindwa kuamini kabisa huyu kamanda mpambanaji ilikuwaje mpaka akafukuzwa?!
Aliwasainisha watu documment bila kuwwambia kwa nini wanasaini. Ila nahisi akitulia anaweza kusamehewa. Tatizo ni mcharuko, haeshimu hata vijana wenzake wenye hekima.
 
Aliwasainisha watu documment bila kuwwambia kwa nini wanasaini. Ila nahisi akitulia anaweza kusamehewa. Tatizo ni mcharuko, haeshimu hata vijana wenzake wenye hekima.

dah... Kweli alifanya makosa kama hivyo, inabidi atulie huenda akasamehewa arudi tena kambini kuendeleza mapambano.
 
Hapo ni Zito tu anafaa jamaa tunamkubali sana natamani awe mwenyekiti wa chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…