johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,127
- 164,543
Ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja iwe ni kwa kuongea au kwa maandishi.Juzi ametoa angalizo kuhusu baa la njaa/ukame,bajeti na ujenzi wa reli ya kati na jana mawaziri wamejibu halikadhalika mwenezi wa chama naye amezungumza leo.Tunahitaji viongozi wa aina hii wenye mbinu za kumtoa nyoka pangoni na kumfanya bubu aseme.Hata ile hoja yake ilikuwa ni mbinu tu ya kuitaka serikali iseme kwa takwimu na hatimaye imesema na imeeleweka.Ninamwona Zitto kama mwanasiasa anayeendana na kasi ya JPM na inawezekana mawazo chanya anayopeleka serikalini yakafanyiwa kazi na hii itazidi kumjenga.2025 huko upinzani viatu vya Lowasa havina mvaaji Je Zitto vitamtosha?