Zitto Kabwe: Serikali haitaweza kukusanya zaidi ya 60% ya makadirio yake

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Mwenyekiti wa chama cha ACT wazalendo na mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema kuwa serikali haitaweza kufikisha mapato iliyojipangia, amesema ikijitahidi sana itafikia 60% tu, kwa kuwa vyanzo vyake havina uhakika.

Ametolea mfano kuwa kwenye chanzo kikubwa cha mapato amabyo ni forodha (customs) kimeshuka kwa asilimia 49.

 
Mwenyekiti wa chama cha ACT wazalendo na mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema kuwa serikali haitaweza kufikisha mapato iliyojipangia, amesema ikijitahidi sana itafikia 60% tu, kwa kuwa vyanzo vyake havina uhakika
Ametolea mfano kuwa kwenye chanzo kikubwa cha mapato amabyo ni forodha (customs) kimeshuka kwa asilimia 49

Anapiga ramli kama mganga wa kienyeji eti haitaweza!!!!! Yeye mwenyezi Mungu anajua ya mbele?????
Kakosa ya kuongea kaingia kwenye kupiga ramli
 
Anapiga ramli kama mganga wa kienyeji eti haitaweza!!!!! Yeye mwenyezi Mungu anajua ya mbele?????
Kakosa ya kuongea kaingia kwenye kupiga ramli
Yeye anapinga serikali kupiga ramli kuwa itakusanya 100% wakati kila mtu anaona kwa uwazi mapato ya forodha yanashuka.
Badala kujifunza mapungufu mnayoonyeshwa mnataka kumshambulia anayeokoa jahazi
 
Mropokaji. Yaani hii vita na Dr. Magufuli lazima imgaragaze huyu dogo. Kama alitoswa na kufukuzwa CHADEMA basi hata wanakigoma watamtosa na kumfukuza 2020!
 
Wenye akili watalichukua hili na kulifanyia kazi kwa manufaa ya nchi bali wale wenzetu wataanza kumkashifu kwa sababu akili ndogo ina tabia ya kukataa maono
 
Yeye anapinga serikali kupiga ramli kuwa itakusanya 100% wakati kila mtu anaona kwa uwazi mapato ya forodha yanashuka.
Badala kujifunza mapungufu mnayoonyeshwa mnataka kumshambulia anayeokoa jahazi
Sasa nyie vilaza mnataka nini sasa? Je mnataka serikali isikadirie mapato?? Mbona yeye kafanya makadirio ya mshahara wa ubunge ndiyo maana akaenda kugombea??
 
Naona dogo ana akili za kimasikini sikini. Kila siku tunaambiwa tujitabirie yaliyo mema yeye anataka serikali ijitabirie mabaya?? Yaani iseme kuwa safari hii mambo ni magumu?? Hivi hata Mungu kweli atakusaidia kama wewe kila ukiamka unajiona masikini umechapika, mgonjwa n.k.??? Mwambieni huyu kiumbe atumie akili japo kidogo, haya ni maji marefu, uchawi hauna nafasi ktk serikali ya safari hii, serikali safari hii haipigi ramri, ni HAPA KAZI TU!!!!!
 
Back
Top Bottom