Zitto Kabwe: Nitajiuzulu Ubunge kama Serikali itanionyesha tani milioni 1.5 za Mahindi

Tayari serikali imesema ina akiba ya tani mil 3 na kwa sasa itagawa tani 1.5 milion. Ukipiga hesabu ni sawa na kusema milioni 3 x 10 ni sawa na milioni 30. (kila tani moja ni gunia 10
Je ni kweli kuwa serikali ina magunia milioni 30?
Je imezihifadhi wapi?
Je ile taarifa ya kuwa mwaka huu wamenunua tani 90 elfu na mwaka jjuzi tani 400 elfu sasa hizi tani mil 3 yaani gunia milioni 30 zilinunuliwa lini?
Na je uwezo wa NRFA ni kuhufadhi tani ngapi?
Naomba tafakuri
 
Sioni unachoongea hapa! Kuwa na Mkopo wa Bank kunahusika vipi? Akiwa na nyumba kwani Amejijenge kwa fenda za Serikali kama Trafic lights za Chato na Uwanja wa Ndege, Utadhani Nkandla ya Jacob Zuma. By the way kwani hizo nyumba Zitto alinunua kwa laki 3 kama zile Za Oysterbay, Msasani etc walizouziana CCM chini ya usimamizi wa Magufuli?
Au Zito hakupewa kama yule waziri wa zamani alipomgawia yule dada aliyekuwa mrupo wake!!
 
Tani milioni 1.5 za chakula? capacity ya maghala ya serikali ni chini ya tani 300,000, hizo tani milioni 1.2 zimehifadhiwa wapi?
 
Hivi unajuwa kwa siku moja Watanzania tunatumia tani ngapi za chakula?

Kwa uchache tunatumai zaidi ya tani millioni moja kwa siku.

Hakuna ghala kubwa linalohifadhi chakula zaidi ya magari yanayosambaza hicho chakula kila siku 24/7.

Ni punguani tu ataedhani kuna tani millioni moja na nusu zimekaa tu kwenye ghala zinaingia kusambazwa.

Ni on going process, inayoingiza na kutoka na kusambaza.

Unaposikia statistics zikitangaza kuwa Tanzania tunatumia tani million mia mbili za chakula kwa miezi Sita unafikiri zote zinakuwa ghalani!? Au huyo punguani anaebwabwaja hovyo alidhani ni hivyo?

Na minyumbu humu inafata tu bila kutumia akili zao hata kiduchu.
Wewe ni mpumbavu nchi inavuna tani 16.3Million kwa mwaka na chakula kinachotumika kwa madai ya wizara ya kilimo ni tani 13Millio ,tayari serikali iliruhusu wafanya biashara wauze tani 1.5Million.Maghala ya serikali yana uwezo wa kuhifadhi tani 246,000 halafu unatuletea ujinga wako humu kwenye mambo ya msingi.Jumla ya chakula chote kilichopo serikalini na maghala ya watu binafsi,mpaka kinachouzwa sasa sokoni ndio hizo tani 1.5Million.
 
Zitto anasumbuliwa na upweke ( loneliness ) inayompelekea kupata Frustration na Frustration is an emotion that occurs in situations where a person is blocked from reaching a desired outcome.

Kuna upweke wa aina nying
1 Interpersonal Loneliness.
2 Intellectual loneliness.
3 Cultural loneliness.
4 Cosmic or Existential loneliness.
5 Social loneliness.
Sasa nyinyi mchagulie aina ya upweke ambao unahisi anaweza kuwa nao

Chagua wa kwako kwanza.......
 
Maskin Juma Poor Manager. ..atafika 2018 kweli?kwa mwendo huu

NDUGU HII TAFSIRI UMEITOA WAPI!!!!!!!!!!

MAANA UNANIVUNJA MBAVU KWA KICHEKO INGAWA MWILI WENYEWE UMECHOKA NA MAISHA KAMA HIVI:-

Skeleton.jpg
 
Hakuna yeyote ataumbuka, ataubuka yeye aliyetemwa na Chadema.
Wewe una shida gani mbona haupo consistent?? Hapa hoja iliyombele yetu ni njaa. Mbona unaongea mengi kama concerned person? Wewe ni Faru nn? Ni wapi huielewi hoja ya Zitto? Mbona watu wanaiattack hoja vzr tu humu? Kwann unamuattack Zitto as Zitto na si hoja aliyoitia?? Rudi kwenye mada hatutaki kusikia vihoja hapa. Mara mafisadi wanashughulikiwa, Mara kafukuzwa chadema. Kuitetea Ccm lazma ujipange kijana mana hainaga mashiko.
 
WanaJF, mnaonaje tukisubiri hizo tani tuone kama zitasambazwa? UKIONA PANYA ANAMDHIHAKI PAKA UJUE KUNA SHIMO KARIBU.

NDUGU HII NI SIASA TU KWANI UMESAHAU KUWA SIASA NI MCHEZO MCHAFU?????

WATATOA TANI 88,000. KISHA WATASEMA TUMETOA TANI 1.5 MIL. JE NI NANI ATAHESABU KUHAKIKISHA KAMA NI 1.5MIL???

CCM maji taka.jpg
SIASA ZA MAJI TAKA HIZI.
NI HATARI SANA KUWEKA SIASA KATIKA UHAI WA BINADAMU. SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA WALIENDA MAREKANI KUTULETEA MAHINDI YA NJANO KWA SABABU WALIKUBALI KUWA KUNA UPUNGUFU WA CHAKULA. MBONA TULIKULA TUKAISHI HADI HALI YA CHAKULA ILIPOKUWA NZURI MSIMU ULIOFUATA????

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!​
 
naona wanasasia sasa wanaanza kujipanga vzr kisiasa, maana muda unayoyoma kwa kasi
 
Kauli ya Zitto:

Serikali ya CCM ikinionyesha tani 1.5m za chakula ambazo inataka kusambaza najiuzulu Ubunge mara moja.

Narudia, mpaka Oktoba 2016 kulikuwa na nafaka tani 90,400 tu Hivi kwenye maghala yote ya NFRA.

Tunashukuru kuwa Hivi sasa ajenda ya tishio la njaa inapata majawabu na matamko. Ndio wajibu wa vyama vya siasa. Kuibua masuala muhimu kwa nchi yetu.

Nimesikia Mwenezi wa CCM ameongea na waandishi Leo. Natarajia ndugu Ado Shaibu atamkaribisha mwenzake ulingoni
Namuunga mkono zitto kabwe.

Maghala ya chakula yote yana uwezo wa kuhifadhi tani chini ya laki tatu at full capacity

Waziri Mkuu alikuwa anatoa makadirio ya mavuno ya mwaka 2016 kwamba ni tani milioni tatu,na kwamba waliuza nje ya nchi tani milioni moja na nusu

Sasa je, kama maghala yana uwezo wa kuhifadhi tani chini ya laki tatu,hizo tani milioni moja na nusu zimehifadhiwa wapi?

Je, kama tathmini ilionyesha nchi ilivuna tani milioni tatu,hii si inamaanisha na zile nilizohifadhi nyumbani kwangu,ulizohifadhi nyumbani kwako,ulizovuna NA kula zikaisha,je waziri Mkuu atakuja majumbani kukusanya vyakula tulivyovuna ili asambaze?ana uhakika gani kwamba hayo mavuno bado yapo? Tanzania hii mkulima mdogo wa jembe la mkono ana uwezo wa kulima chakula cha kukaa zaidi ya msimu mmoja?
 
Hata Mimi namuunga mkono Zitto mia kwa mia kwa vile hii serikali haijanunua nafaka awamu hii ya tano. Na pia iliondoa ruzuku ya mbolea toka bilioni 76 hadi bilioni 10. Serikali inayotaka kujitosheleza kwa chakula haiondoi ruzuku ya mbolea kwa kubana matumizi.

Kama Zitto akionyeshwa maghala yenye hicho chakula mimi nitamuunga mkono kwa KUNYA hapa hapa JF
IMG-20170118-WA0005.jpg
angalia uwezo wa maghala kuhifadhi chakula,kwa maghala yote nchini,uwezo wake hauzidi tani laki tatu
 
Serikali juzi kupitia kwa Waziri wa Kilimo imesema ina tani milion 3 na kwa sasa inasambaza tani 1.5 milioni.
Sasa hesabu iko hivi.
tani 1 ni sawa na gunia 10 hivyo tani milioni 3 x 10 ni sawa na milioni 30.
Je ni kweli serikali imehifadhi gunia miioni 30 za mahindi?
Hizo gunia 30 miioni zilihifadhiwa wapi wakati walinunua tani 90, 000?
Je serikali itasambaza gunia milioni 15 kwa awamu hii.
Je ni kweli kuwa hakuna njaa? na kama hakuna njaa hizo gunia 15 milioni zinaenda kwa nani?
Tafakuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom