Zitto Kabwe kwenda Uswisi kukutana na watafiti wake Kuhusu Mabilioni ya USWISI

Bado una imani na TAKUKURU? Pimia mwenye kauli ya Dr. Hoseah kwa ubalozi wa Marekani,
"Unapodhuria mikutano ya vigogo wanataka utambue kwamba wao ndo wamekupa hicho kitengo. Na kama wakiona unatofautiana na matakwa yao, basi upo hatarini"
PCB ya enzi za Mwalimu ilikuwa nzuri sana. Mtu kama Chenge na "vijisenti" vyake angesimama yeye mahakamani kueleza namna alivyovipata hivyo vijisenti. Sasa hivi ni dola ndiyo inayotakiwa kutafuta ushahidi wa kwelikweli. Si uliona Costa Mahalu alivyopeta hivi karibuni kwenye ile kesi ya ununuzi wa jumba la ubalozi kule Italy?
 

1.Ushahidi namba moja ni kwamba hizo pesa hazikuingizwa na account bearer. Na tangu zilipoingizwa kwenye account mwenye account hajaigusa account yake.

2. Kampuni zilizodeposit hizo pesa ni za migodi. Ukijua ni kipindi kipi ziliingizwa utawasilisha list ya POLITICALLY EXPOSED PERSONS. Mpaka hapo tuna pakuanzia

Ila huyu huyu ZZK alisoma ushahidi bungeni wa mazingira ambayo mafisadi walizipata hizo kickbacks. Au ile ripoti ilikuwa ya nini?
 
Hongera zitto kwa kuangalia maslahi ya taifa..!tz kwanza ccm cdm baaadae!
 
Kinachotakiwa kwa sasa ni kuwa na sheria kali kabisa ya RUSHWA na UFISADI nchi hii ili tusiendelee kuibiwa. Wailokwishaiba kwa sasa hatuna la kuwafanya. Tuwaombe waendelee na moyo wao wa kuchangia makanisa, misikiti, harusi, misiba, ujenzi wa shule za kata,....., angalau kuturudishia kidogo kati ya nyingi walizoiba!
 

Kiongozi mzuri ni yule ambaye kabla ya kuongea jambo analitafakari kwanza na akija kutoa kauli anaisimamia kauli yake! lakini Kiongozi anayebadilikabadilika kama kinyonga hafai!Mheshimiwa Zitto Kabwe alipoibua kashfa hii mara ya kwanza alitishia kuwa serikali isipowataja walioficha mabilioni Uswis yeye angewataja kwenye Bunge la October! Serikali haikuwataja badala yake Zittto kapeleka hoja binafisi bila kutaja wahusika,.. Zitto amedhihirisha kwanza aliposema angewataja kwenye bunge la October hakutafakari vya kutosha kabla ya kutoa kauli hiyo, kushindwa kuwataja ameonesha kuwa hasimamii kauli zake na kuanza kusema ni muhimu uchunguzi kufanyika kuliko kutaja majina ameonesha ni kiongozi kigeugeu, Hitimisho lake ninkiongozi asiyefaa!!
 
kuwepo kwa sheria kali ni swala moja lakini utekelezaji wa sheria hiyo ni swala lingine, kuna sheria nzuri na kali kabisa amabazo zinatoa fursa kwa wahujumu uchumi na mafisadi kufilisiwa lakini mahakama zetu zipo politicized! mfano mzuri hebu fikiria kesi za akina Yona na Mramba imechukua miaka mingapi? kama tupo serious hata mwezi mmoja unataosha kuwahukumu maana hadi kuwakamata na kuwafikisha mahakamani maana yake una ushahidi wa kuwatia hatiani sasa je kinachovuta kesi hiyo zaidi ya miaka mitano ni nini kama sio siasa! kikubwa ni kuiondoa serikali hii madarakani na kuweka serikali inayoheshimu sheria na mahakama,
 

sijawahi ona ndumilakuwili kama huyu kijana....yeye si alisema kua kama serikali haitawataja wenye accounts huko swiss basi atawataja yeye kwa sababu majina anayo? iweje sasa hivi anasema kutaja majina sio suluhisho? leo aseme hivi kesho abadilike aseme vingine huyu ndio mnataka awe Rais wa nchi yenu.... i beg to differ
 
Tuweke tu sheria kali na taasisi za kidola zenye nguvu. Watapatikana watu watakaozilinda na kuzitumia. Tunamwona mtu kama Maghufuli anavyozitumia sheria zilizopo kulinda na kuhifadhi barabara zetu. Shida iliyopo ni sheria hafifu na dhaifu mno zinazowapa mianya mahakimu na majaji kuamua wanavyotaka. TAKUKURU limebaki ni dude tu la kusukumia maisha.
 
Lishweni unafiki wa Zitto na Mwananchi.

Mwenzenu yupo kisiasa nyie mpo kizalendo! Haahaa njia mbili tofauti kabisa!

Mkija kufunguka mtajuta kumchekea!
 
mwacheni Zitto aendelee na harakati zake kama mwongo au mkweli itafahamika tu.!!
 
Hoja nzito safari hii ya zito iratibiwe vizuri na ulinzi wa kutosha uwepo ,mambo hayo yanagusa mambo ya watu yaliyokuwa ni siri .
 
mwacheni Zitto aendelee na harakati zake kama mwongo au mkweli itafahamika tu.!!

Mkuu umenena vyema, sielewi watu wanapata presha ya nini. Uzuri wa uwongo siku zote una mwisho wake!
 
kwa mtazamo wangu ni wewe ndiye unayetaka kuivuruga CHADEMA,kupeleka hoja bungeni ni ya mbunge binafsi bali chama kinaweza kumuunga mkono,na ndivyo CHADEMA walivyofanya,na kutaka kuharibu maana nzima ya Zitto katika kuleta uzalendo wake na kutaka kuwawajibisha mafisadi walioficha hela nje.
hata kama kuna wananchi wengi mimi nikiwemohatujapendezwa na msimamo wake wa kutangaza nia yake ya kugombea urais,lakini amejaribu kufafanua.
sioni mamtiki kudai hoja hii iliyopelekwa na kuwa adopted na bunge eti ni nia yake ya kutaka kwenda ikulu very poor reasonong.
Usiogope kutumia ubongo kufikiri usipende majibu rahisi kiasi hicho kwa mtu ambaye nigeat thinker,kwa sababu kunathread hapa ilizungumzia urafiki wa Zitto na Kikwete,na baadhi ya watu wanadai Zitto anataka kuivuruga CHADEMA,na LOWASSA HAELEWANI NA kIKWETE,TBC ni ccm basi Zitto ana njama na Kikwete.
Soma thread na nini Zitto amesema halafu njoo na mambo relevant tupate elimika si chuki na majungu
 
Alisema Desemba 10, mwaka huu anatarajia kwenda Uswisi kukutana na watafiti wake, huku mmoja akiwa anatokea Uingereza na kwamba, atawapatia taarifa ya mahali taifa lilipofikia kuhusiana na fedha hizo.

Kuchamba kwingi.....
 

Wala usitie shaka in no time every evil shall be exposed hakuna cha CIA wala nini, they are lesser powers my friend watch and see how head of power and principalities works.....Saa nyingine nawaonea huruma binadamu kwakukosa confidence kwa sababu ya ignorance...Naomba niwaambie wakati wa vita vya mjerumani majeshi yao yalikuwa yanapita na kufagia kama kimbuga katika nchi mbalimbali za ulaya lakini wenye kumbukumbu watuambie what happened walipoikaribia Uingereza? Je leo waingereza watajidai wao walikuwa na nguvu kuliko majeshi ya mjerumani? You cannot just decide to rule this world as if everybody is dead....I for one have refused and ready to fight for the integrity of my country I fear none and am assured of victory!

Nimeahidi nanarudia tena hakuna mmoja katika ukoo wa mafisadi na associates ataikaribia Ikulu ya Tanzania come 2015.....Wacha wahangaike lakini when it comes to crossing the line tutaona nani mkweli!
 

kilugha ya kimapinduzi tunawaita hawa waafrica wenye pesa nje ni petty bourgeois na wale wa kimagharibi wakisadiwa na vyombo vyao vya kijasusi kama CIA, mashirika ya kimataifa kama WB, IMF na WTO, makapuni makubwa kam Halliburton, na serikali zao kupitia balozi zao hawa ni bourgeois wenyewe mapapa. sasa ili wafyinze lazima watengeneze kamfumo tegemezi na kuunda katabaka ka vibaraka watakaosaliti jamii zao na kujiunga nao japo kando kando at the periphery and not at the core.

mfumo unaendeshwa kwa njia ya uwekezaji uchwara, misaada uchwara, kusapoti demokrasia kwa shungo upande n.k ili rasilimali za kitaifa ziendelee kutumika na kuendesha chumi kubwa za kibepari zilizo kwenye centre/core ya mfumo huu.
 
Reactions: Ame
zitto akipiga sana kelel atajikuta ameeingizwa kwenye hili kundi taratibu na ka akaunti kamoja pale Zurich kenye $5 mil hivi huku wakisema watampa urais baada ya muda fulani. kelele zitaisha na atapumzika na hii biashara akiendelea kua mbishi kitampata kilichowapata wote waliojaribu kushindana na mfumo na hamna anayewaongelea leo hii.

the choice is yours, and the choice is always easy
 
Chezea uchumi uchumi wako vyovyote utakavyo lakini usichezee uchumi wa wenzako,kwani hayo mapesa yanayosemekana kufichwa huko ndio uchumi/mitaji ya watu wa mataifa hayo.anyway tunamtakia kila la heri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…