MeinKempf
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 11,094
- 7,225
Wadau nimebaki kinywa wazi kwa kushikwa na bumbuwazi niliyopigwa baada ya mkuu Zitto Kabwe kudai kuwa kila wanaopanga kumteka au (kupita nae) kukumbana na kizingiti kizito mbele yake na hivyo kushindwa kutimiza hazma yao, anadai kila wakifika kwake wanaambulia bila bila , maana mara nyingi wakienda kumsaka , hujikuta wameambulia kukutana na Mti wa Mrumba au Bwawa la Karosho (sio korosho ) au mara nyingine jamaa hao huambulia kukutana na ziwa Tanganyika mbele yao ,na kama hawaamini maneno yake basi wathubutu kuingia anga zake waone mziki wake.
na hiyo inatokana na yeye kama mwana Kigoma wa mwisho wa reli kuwa amekamilika katika idara zote za ufundi (wa anga, majini na nchi kavu) , hali hiyo imepelekea hao jamaa ambao ni wabaya wake kuwa wakipata tabu sana kumkamata kila wakipanga mission yao.
Sasa je, anataka kutuaminisha kuwa alitumia mbinu hizo pia kipindi kile alichodai kulala bungeni wakati alipolalama kuwa (kuna watu) walimsaka ili tu waondoke nae kaajili ya mahojiano..??
Je , kwa mwanasiasa kijana , msomi na nguli kama Zitto anatoa picha gani kwa wale walio nyuma yake au wanaomwamini...?? Maana anaonekana anaamini katika njia mbadala katika kupata uhakika wa ulinzi wake.
Hapo ndipo ninapoona kumbe ile kauli yake ya kusema atayediriki ku deal na yeye basi atapukutka kama ukoo wa panya.
Kwa habari zaid tafuta chanzo cha gazeti la Mwananchi la tarehe 15 April 2017 ,kwani wao wamefafanua kwa kina habari hii.
Ukitaka unaweza fatilia habari hii: Wabunge waliotajwa kutekwa waanza kuchukua tahadhari
Zitto Kabwe aulizwa swali gumu Twitter, alivyojibu imeshangaza wengi
Wabunge waliotajwa kutekwa waanza kuchukua tahadhari