Zitto Kabwe kama Julius Malema! Fighting for survival

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,427
Reaction score
10,749
Habari,
ANC ni chama kikongwe na kinachoaminika kuwa na hadhi ya juu kiana harakati pengine kuliko vyama vingi sana Africa. Chama hiki kinapendwa nje na ndani ya South Africa kwa sababu ya sera zake na mfumo imara ulioachwa na Nelson Mandera. Ni chama kilichowatetea wanyonge na kufanikiwa pakubwa sababu ya umahili wa watangulizi na watu makini waliopata kuwepo na waliopo. Kwa wakati huu huwezi kukitaja chama hiki bila kumtaja Julius Malema, mwanasiasa kijana na machachari aliyekuwa na uthubutu wa kuwakoromea hata wakubwa wake pindi walipoenda ndivyo sivyo, kwa bahati mbaya mkubwa hakosei na alitimuliwa chamani kwa taratibu kama zilizochukuliwa kwa Zito kabwe. Alianza kuvuliwa uongozi wote, then alitimuliwa moja kwa moja.
Zitto Kabwe kwa wengi alionekana ni dira hasa ya vijana. Amefanya mengi makubwa na amefanikiwa kuwa na ushawishi mkubwa wa vijana wengi kuingia CHADEMA. Nawakumbuka vijana kama Mbunge Moses Machali na Mkosamali, ni baadhi tu ya vijana waliopikwa kwa siasa kali za ZZK. Amejitahidi kuwa mwana harakati wa kupambana na ufisadi papa (na wananchi wengi wamejua wizi wa nchi hii kupitia ZZK) na mbunge mwenye uthubutu lakini leo hii ameishia kuvuliwa madaraka!Sehemu nyingi ukimtaja mbunge huyu alijipatia sifa hata kwa watoto wadogo.

Ni hakika kwamba alikuwa amebeba kura nyingi za CDM na kuna hatari akaondoka nazo kwa wananchi wengi kutoipigia kura CDM (hasa wale wanaochagua chama). Wanaoshabikia kutimuliwa kwake si wengi kama wanaoona kaonewa kama ilivyotokea kwa Malema. Malema bado yupo na hachoki kuitetea nia yake ya ndani.

USHAURI WANGU
Mh Zitto, siasa unayofanya, mwenye kuujua ukweli halisi ni wewe na Mungu wako. Tuhuma zote unazopata sasa unajua zipi ni sahihi na zipi zinatolewa kwa uongo. Nchi hii inahitaji ukombozi halisi zaidi na si chama. Pale ulipokosea pasahihishe na pale unapopatia usikate tamaa. Uliaminika na bado kuna kundi kubwa linauamini utendaji wako. Simama tena na songa mbele kuikomboa Tanzania.
Kumbuka: Mwisho wa siku utaulizwa umeifanyia nini Tanzania na si CHADEMA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Nyoka akitoa gamba hawi mjusi, zito ndivyo alivyo
 
Tofautisha wanyama kama reptiles, amphibia, au animalia na ha species ya homo sapiens. Hapa utalikuta kundi la binadamu ambao wamepewa uwezo wa kurekebisha pale wanapokosea. Kama ZZK kakosea kweli na concious yake bado i hai anaweza kubadili na kurekebisha alipokosea na kuendelea na ukombozi.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mtakuja na kila theory, ila kimtaanoi tunasema 'adui mwombee njaa'.
 
Sawa binadamu ukosea na urekebisha makosa yake ili arudi katika mstari ulionyooka, lkn kwa situation ya siasa za bongo kumwamini Zito tena yahitaji muda sana alionywa ika akujali!
 
huwezi mfananisha malema na mnafki zitto ,malema alikuwa wazi hakuficha chochote ni sawa na nape kipindi kile
 
Unajua mnashindwa kuelewa vizuri siasa za nchi yenu(Tanzania) zikoje!,kwa Tanzania ufuasi wa wananchi kwa asilimia kubwa hua haujali mtu mmoja mmoja bali umaarufu wa Chama,tofauti kidogo na wenzetu wa Kenya wananchi huangalia umaarufu wa mtu au kabira,leo hii usijefikiria wabunge tulionao CDM bungeni walipata ubunge kwa nguvu ya hoja walizonazo,ila ni kwa sababu ya umaarufu wa CHADEMA.nakumbuka mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu,ktk kata moja ya wilaya ya mbozi ninakotokea kuna diwani wa CHADEMA alishinda kiti cha udiwani but 90% ya wanainchi walikua hawamfahamu hata yeye hakuamini kama ameshinda,kwa iyo usijidanganye eti mtu kama Zitto anaweza akaondoka na kura za watu CHADEMA,kwa Tanzania siasa zetu ni ufuasi wa umaarufu wa Chama na si umaarufu wa mtu...
 
Habari,
ANC ni chama kikongwe na kinachoaminika kuwa na hadhi ya juu kiana harakati pengine kuliko vyama vingi sana Africa. Chama hiki kinapendwa nje na ndani ya South Africa kwa sababu ya sera zake na mfumo imara ulioachwa na Nelson Mandera. Ni chama kilichowatetea wanyonge na kufanikiwa pakubwa sababu ya umahili wa watangulizi na watu makini waliopata kuwepo na waliopo. Kwa wakati huu huwezi kukitaja chama hiki bila kumtaja Julius Malema, mwanasiasa kijana na machachari aliyekuwa na uthubutu wa kuwakoromea hata wakubwa wake pindi walipoenda ndivyo sivyo, kwa bahati mbaya mkubwa hakosei na alitimuliwa chamani kwa taratibu kama zilizochukuliwa kwa Zito kabwe. Alianza kuvuliwa uongozi wote, then alitimuliwa moja kwa moja.
Zitto Kabwe kwa wengi alionekana ni dira hasa ya vijana. Amefanya mengi makubwa na amefanikiwa kuwa na ushawishi mkubwa wa vijana wengi kuingia CHADEMA. Nawakumbuka vijana kama Mbunge Moses Machali na Mkosamali, ni baadhi tu ya vijana waliopikwa kwa siasa kali za ZZK. Amejitahidi kuwa mwana harakati wa kupambana na ufisadi papa (na wananchi wengi wamejua wizi wa nchi hii kupitia ZZK) na mbunge mwenye uthubutu lakini leo hii ameishia kuvuliwa madaraka!Sehemu nyingi ukimtaja mbunge huyu alijipatia sifa hata kwa watoto wadogo.

Ni hakika kwamba alikuwa amebeba kura nyingi za CDM na kuna hatari akaondoka nazo kwa wananchi wengi kutoipigia kura CDM (hasa wale wanaochagua chama). Wanaoshabikia kutimuliwa kwake si wengi kama wanaoona kaonewa kama ilivyotokea kwa Malema. Malema bado yupo na hachoki kuitetea nia yake ya ndani.

USHAURI WANGU
Mh Zitto, siasa unayofanya, mwenye kuujua ukweli halisi ni wewe na Mungu wako. Tuhuma zote unazopata sasa unajua zipi ni sahihi na zipi zinatolewa kwa uongo. Nchi hii inahitaji ukombozi halisi zaidi na si chama. Pale ulipokosea pasahihishe na pale unapopatia usikate tamaa. Uliaminika na bado kuna kundi kubwa linauamini utendaji wako. Simama tena na songa mbele kuikomboa Tanzania.
Kumbuka: Mwisho wa siku utaulizwa umeifanyia nini Tanzania na si CHADEMA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Huyo ZZK wako ni mzee wa mifwedha na hatengenezeki tena ni nafuu ya ccm na matatizo yao yote kuliko huyo mtu wako mwenye akili chafu za kupiga kelele nyingi ili aitwe pembeni akatiwe kidogodogo hana tofauti na gaidi
 
:A S-confused1::A S-confused1:mazingira ya malema ni tofauti. hata hivyo je malema yuko wapi sasa na slogan zake za "kill the boer?":A S-confused1::A S-confused1:
 
Mtakuja na kila theory, ila kimtaanoi tunasema 'adui mwombee njaa'.

Bahati mbaya mimi ninaamini ktk Math 5:43-48, waombee adui zako mema na si mabaya! Siasa isikutoe utu!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hii kitu ya Zitto imefanya watu waonyeshe rangi zao halisi.
Safari hii tutaona undani wa kila mtu
Nimeusoma ule Mzalendo wa akina Zitto mara 3 nikatokea kuupenda na kuunga mkono kwa 90%
Hiyo 10% ni tatizo la matumizi ya lugha.
Sioni Uhaini katika mawazo yao.
Sioni mtu au watu na hata CCM wakiwatumia.
Mawazo yao ni ya kujenga zaidi.
Tactic waliyo tumia ni ya UPOLE wa HUA na Ujanja wa Nyoka.
Waraka unamgusa Mbowe zaidi kuliko mtu mwingine yeyote.
Kuna UFISADI mkubwa tu ndani ya CHADEMA na hili si jambo la kufumbiwa macho hata kidogo.
CHADEMA si kampuni ya mtu binafsi au Pet cash ya familia.
Moto umewashwa si wa mshumaa ni moto wa gesi huu.
 
Huyu jamaa hata kama anaushawishi mkubwa kwa watu. Tulipo sasa yatosha unafiki mbaya bora wamfukuze kabisa. Wasisikilize hata rufaa yake. Wanatuchezea akili zetu kama midori vile MFUKUZENI TU HAWAFAI TENA HUYO
 
Watu kwa kupenda sifa bhana...sasa ZZK ka-fight wapi sasa? analeta mapozi na fedheha kwa wananchi unadhani atabaki salama? ZZK wa zamani sawa .....wa sasa?? anatuuzia mbuzi kwenye gunia
 
Utu ni nini? Unapimwa kwa kifaa gani? Cut off ni ngapi?

Back
Top Bottom