Zitto Kabwe: Baada ya kusoma gazeti la Jamhuri, nina maswali haya kwa serikali

NgugiAchebe

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,025
688
Juu ya Sakata la Ndege, Serikali Ina Maswali Mengi ya Kujibu

Nimesoma ripoti maalum ya Gazeti wiki la Jamhuri la Leo Jumanne, Mei 9, 2017 yenye kichwa cha habari 'Zitto Anyukwa' inayohusu uchunguzi wa gazeti hilo juu ya ununuzi wa ndege ya Dreamliner kutoka shirika la ndege la Beoing, ununuzi ambao binafsi kwa nafasi yangu ya ubunge unaonipa mamlaka ya kuisimamia serikali, nimeutulia mashaka na kuomba maelezo zaidi ya serikali bungeni juu ya ununuzi huo.

Nawapongeza sana Waandishi na Wahariri wa Gazeti hili Kwa kufanya uchunguzi kuhusu suala la manunuzi ya ndege Hii ya Boeing 787-8 Dreamliner. Magazeti ya habari za uchunguzi ni taasisi imara na muhimu mno katika kujenga utamaduni wa uwazi, uwajibikaji na uadilifu nchini, utamaduni ambao Chama chetu cha ACT Wazalendo kinapigania kuusimika nchini. Gazeti la Jamhuri limethubutu kufanya vile wengine wameshindwa kufanya.

Gazeti la Jamhuri limeibua masuala mawili muhimu sana katika ripoti yao hii maalum, mosi limeeleza kuwa ndege inayonunuliwa ni mpya kabisa, ambayo bei yake kwa mujibu wa taarifa rasmi za Shirika la ndege la Beoing ni Dola za Kimarekani milioni 224.6 (zaidi ya shilingi bilioni 450), pili jamhuri wameeleza kuwa pamoja na kununua ndege mpya kabisa (ambayo bei yake ni zaidi ya shilingi bilioni 450) bado tumeuziwa ndege hiyo 'mpya kabisa' kwa bei ya dola milioni 150 (zaidi ya shilingi bilioni 330).

Baada ya kusoma ripoti husika, nimepata maswali muhimu yafuatayo yanayopaswa kujibiwa na Serikali (na naamini Jamhuri watatusaidia kuyauliza):

1. Jamhuri wanasema bei ya 'ndege mpya' ambayo si 'terrible teen' (zile zenye matatizo ambazo wenzetu duniani wameuziwa kwa bei ya chini), kwa mujibu wa mkataba waliouona Kampuni ya Boeing na Serikali ni dola za Kimarekani milioni 150 (zaidi ya shilingi bilioni 330) na si dola milioni 224.6 (zaidi ya bilioni 450) inayosemwa na Serikali. Bei sahihi ya 'ndege mpya' ni ipi kati ya hizo mbili?

2. Kwa mujibu ya Randama ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika mawasilisho ya Bajeti ya mwaka 2017/18, ambayo iliwasilishwa kama Taarifa ya Waziri wa Wizara husika, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Serikali ilieleza kuwa imeilipa Kampuni ya Beoing kiasi cha dola milioni 67 (zaidi ya shilingi bilioni 134) ambazo ni 30% ya bei ya dola milioni 224.6 ambayo ndiyo bei ya ndege mpya kwa mujibu wa Boeing wenyewe (na kwa mujibu wa Serikali yenyewe Bungeni). Je Serikali mpaka sasa imelipa 30% ya $224.6m ambayo ni $67 (kama ilivyosema yenyewe) au imelipa 30% ya $150m ambayo haiwezi kuwa hiyo $67m.

Binafsi nimeomba Mkataba husika kwa mujibu wa sheria na taratibu za kibunge. Tukipata tutawajulisha. Lengo letu la kuhoji ni kupata ukweli, kujiridhisha na kusimamia matumizi sahihi ya fedha na rasilimali za umma kwa mamlaka tuliyopewa nanyi wananchi.

Hatuna nia mbaya Kabisa na mchakato wa kuboresha Shirika letu la Ndege la Taifa. Uboreshaji huu ulikuwa ni msimamo wa Chama chetu kwenye ilani yetu ya uchaguzi. Tunao wajibu wa kuhakikisha unafanyika kwa usahihi.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge, Kigoma Mjini - ACT Wazalendo
Mei 9, 2017
Dodoma
 
Hawa jamaa wa Gazeti la Jamhuri shida sana!

Kuna mmoja aliwahi kuomba tangazo na pombe zile kali kabisa ikulu

Nadhani habari hii ya ndege ilikuwa ni PR kwa niaba ya serikali(tangazo)
 
Ata kama,ila wameketa ukakasi zaidi. Bei walioandika ni tofauti na bei ya serikali. Tumuamini yupi sasa? Hapa tumepigwa tena.
 
nikionaga jambo moja lina majibu mengi (zaidi ya moja) tofauti, najua tayari kuna ukweli unafichwa. Ununuzi wa hizi ndege (plus ujenzi wa reli ya SGR) kuna pesa imepigwa tena nafsi yangu inanishawishi ni Mkulu mwenyewe. Napoona mazungumzo na maafikiano ya manunuzi makubwa kama haya anayafanya mwenyewe binafsi napata ile picha ya alivyokuwa anazunguka na mafaili ya kuuza/kununua baadhi ya nyumba za serikali alizosimamia kuuzwa. Yaani miaka aliyokaa pale Wizara ya Ujenzi imempa uzoefu wa upigaji wa style hii yaani anadesa. Na kwa vile jamaa ni very very weak ku-withstand kukosolewa au kuhojiwa au kwa challenged lazima azime uhuru wa habari/uhuru wa kuhoji kwa masuala tata kama haya. Ni fikra zangu na sio lazima zifanane na zako.
 
Jamaa kafanya kosa hata kama ndge ni mpya hata kama imepatikana kwa bei chee, kwa nini hakufuata taratibu za manunuzi ya umma? ! na kwa nini serikali inatumia nguvu kubwa kukanusha yanayosemwa badala tu ya kuweka mikataba kwenye magazeti ya serikali ili kila mwenye kiu ya kujua ajue?! Zaidi ni porojo za kusifia?
 
Kuna ukakasi Mkubwa sana kwenye ununuzi WA ndege hizi sio boingi tu hata Yale mapanga boyi bado tumepigwa lakini wabunge wameshindwa kuhoji tu boing tepigwa hadharani kabisa inakuaje bong waseme tumenunua kwa being hiii Na serkali waseme tumenunua kwa bei ya nyingine
 
Safi sana, na sisi leo tunajadili ndege, miaka michache nyuma mjadala ulikuwa Escrow, Richmond, EPA, Lugumi na mambo mengine mengi ya kifisadi, haya ni mafanikio makubwa sana, mimi kama mtanzania mzalendo najivunia sana mafanikio haya, maana shirika hili lilishaanza kufa kwani ndege ya mwisho ilinunuliwa tangu enzi za Nyerere 1970s.

Katika kujadili hili ni lazima tuwe makini kwani wengi wetu hatua uelewa wa masuala ya ndege, mimi binafsi sipo upande wa yeyote kuhusu hili, simuungi mkono Zitto wala Serikali, binafsi ni mgumu sana kuwaanini wanasiasa, si Serikali wala Zitto wote ni siasa tupu.

Kwa hili la ndege nimefuatilia sana posts za Zitto, ambazo mimi naziona kwa kiasi kikubwa ni za kubeza na wala si za kushauri, ni vema basi kama ana uhakika ndege tunayouziwa ni kuukuu, au bei ni kubwa angeishauri Serikali nini cha kufanya, hatujachelewa kwani hata pesa bado haijalipwa yote na wala ndege bado haijafika.
 
Uuzwaji wa zile nyumba wakati Sumaye anasema JPM hakuuza bali ni yeye na Mkapa. Ulikuwa wapi?
 
ZZitto mbona sikuelewi?.Hoja zako zote zimepanguliwa na hili gazeti na sasa unafuatilia walichokosea wao?.Angalia Zitto usije ukatumiwa na washindani wa kibiashara wa ATCL.Angalia Yuki Kenya Airways,South Africa Airways,Precision Airways nk hawafurahii kufufuka kwa ATCL.
Kama ujaelewa sii urudie kusoma !!? Uoni tafauti ya bei ya serikali na bei ya gazeti la jamhuri
 
ZZitto mbona sikuelewi?.Hoja zako zote zimepanguliwa na hili gazeti na sasa unafuatilia walichokosea wao?.Angalia Zitto usije ukatumiwa na washindani wa kibiashara wa ATCL.Angalia Yuki Kenya Airways,South Africa Airways,Precision Airways nk hawafurahii kufufuka kwa ATCL.
Hiyo mbona ndio kazi yake mbunge wa mtera aliwahi kumhoji zito lakini sisi tulipuuza kwa kushabikia mhongo aondolewe uwaziri katika suala la escrow
 
Kuna ukakasi Mkubwa sana kwenye ununuzi WA ndege hizi sio boingi tu hata Yale mapanga boyi bado tumepigwa lakini wabunge wameshindwa kuhoji tu boing tepigwa hadharani kabisa inakuaje bong waseme tumenunua kwa being hiii Na serkali waseme tumenunua kwa bei ya nyingine
Acheni kucomment kabla ya kusoma hiyo habari katika gazeti la jamhuri.
simple tu.google. gazeti la jamhuri.
Hapo utakuta hata zito kahojiwa,mchakato wa kuinunua ndege.
kuhusu bei ,kuna bei ya boing oficial.lakini kumbuka hiyo sio bei fix,kunakuombana heri vilevile,ndio maana sie tumepewa discount,halafu sisi tulikuwa na pesa wakati wa kuongea,
hatukwenda kama masikini,tulikwenda kubagain kama matajiri wafanyabiashara wakubwa na kwamba tunawza nunua kwao tena baadae.hivyo lazima wakushushie bei kwa spund zetu kali.
kumbuka hao walikuwa wana ushindani mkali sana na Air bus.kutuuzia ndege.
sasa tulipo mchagua yeye lazima awe rafiki yetu mkubwa kibiashara.
Zitto anaweza kuwa anatumiwa na Air bus wapinzani wa boing,kwani walichukia sana baada ya sisi kuwapiga chini!!
Safi sana, na sisi leo tunajadili ndege, miaka michache nyuma mjadala ulikuwa Escrow, Richmond, EPA, Lugumi na mambo mengine mengi ya kifisadi, haya ni mafanikio makubwa sana, mimi kama mtanzania mzalendo najivunia sana mafanikio haya, maana shirika hili lilishaanza kufa kwani ndege ya mwisho ilinunuliwa tangu enzi za Nyerere 1970s.

Katika kujadili hili ni lazima tuwe makini kwani wengi wetu hatua uelewa wa masuala ya ndege, mimi binafsi sipo upande wa yeyote kuhusu hili, simuungi mkono Zitto wala Serikali, binafsi ni mgumu sana kuwaanini wanasiasa, si Serikali wala Zitto wote ni siasa tupu.

Kwa hili la ndege nimefuatilia sana posts za Zitto, ambazo mimi naziona kwa kiasi kikubwa ni za kubeza na wala si za kushauri, ni vema basi kama ana uhakika ndege tunayouziwa ni kuukuu, au bei ni kubwa angeishauri Serikali nini cha kufanya, hatujachelewa kwani hata pesa bado haijalipwa yote na wala ndege bado haijafika.
Jamaa kafanya kosa hata kama ndge ni mpya hata kama imepatikana kwa bei chee, kwa nini hakufuata taratibu za manunuzi ya umma? ! na kwa nini serikali inatumia nguvu kubwa kukanusha yanayosemwa badala tu ya kuweka mikataba kwenye magazeti ya serikali ili kila mwenye kiu ya kujua ajue?! Zaidi ni porojo za kusifia?
 
Wakati Zitto anatoa taarifa za awali alztoa wap mbona kaufyata? Tuna amn kua Zitto mtaft sn ila hl kachemka alitulsha matango pori yumkn acje kuwa anatumika kuichafua hii program ya ununuz wa ndege maana huko nyuma aliaminiwa sn hvyo wanaomtumia wanaamn kua Zitto aksema wananchi watakubali tuuuuuuuu kwa kua ni Zitto. Zitto una access kubwa come up with vivid information don't falsify we Tanzanians.
 
nikionaga jambo moja lina majibu mengi (zaidi ya moja) tofauti, najua tayari kuna ukweli unafichwa. Ununuzi wa hizi ndege (plus ujenzi wa reli ya SGR) kuna pesa imepigwa tena nafsi yangu inanishawishi ni Mkulu mwenyewe. Napoona mazungumzo na maafikiano ya manunuzi makubwa kama haya anayafanya mwenyewe binafsi napata ile picha ya alivyokuwa anazunguka na mafaili ya kuuza/kununua baadhi ya nyumba za serikali alizosimamia kuuzwa. Yaani miaka aliyokaa pale Wizara ya Ujenzi imempa uzoefu wa upigaji wa style hii yaani anadesa. Na kwa vile jamaa ni very very weak ku-withstand kukosolewa au kuhojiwa au kwa challenged lazima azime uhuru wa habari/uhuru wa kuhoji kwa masuala tata kama haya. Ni fikra zangu na sio lazima zifanane na zako.
duuuh !!
 
Back
Top Bottom