MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Baadaya Zitto kudai kwenye mkutano wa hadhara kuwa Chama cha ACT-Wazalendo kitawasilisha bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Rais Magufuli kufuatia sakata la njaa ambapo baadhi ya wananchi wanakufa kwa kukosa chakula. Baadhi ya watu wamepongeza na wengine kwenda mbali zaidi na kudai apeleke hoja yake katika bunge linaloanza tarehe 31 Januri 2017.
Ninaamini Zitto hakutoa hoja hii kwa kutokujua bali alifanya hivyo kwa sababu anaendesha siasa zinazoitwa Politics of stupid.
Politics of stupid involves sensational politics which are intended to be shocking and exciting rather than serious.
Siasa anazofanya Zitto ni aina ya siasa ambazo zinashtua na kutia moyo kundi la watu ambao hawana uelewa wa sheria, hali halisi ya kisiasa na kiuchumi nchini.
Zitto ananikumbusha sensational politics za Obama wakati hajaingia madarakani hasa kuhusu gereza la Guantanamo Bay, Cuba.
Wakati wa kampeni alisikika mara nyingi akisema“I will shut down the prison at Guantanamo. It is expensive, it is unnecessary, and it only serves as a recruitment brochure for our enemies,”
Waliofahamu ukweli wa siasa za Marekani na mazingira yake walimshangaa huku wengine wakimcheka lakini baadhi ya watu waliamini kama wale wanaoamini maneno ya Zitto kuhusu kupeleka hoja bungeni ya ku-impeach Rais Magufuli.
Mwezi January 2009, siku ya pili baada ya Rais Obama kuapishwa alitoa an executive order iliyoelekeza kufungwa kwa gereza ndani ya mwaka mmoja.
Wafungwa baada ya kusikia habari hiyo, walianza kupiga kelele kwa walinzi wakisema,“Have you heard? We’re getting out of here!”. Obama anaondoka na gereza halijafungwa. This is Politics of stupid.
Katika kitabu cha Mwl.Nyerere kinachoitwa ''Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania'' ambacho kilitoka mwaka 1993, Mwl. Nyerere alinukuliwa akisema, ‘’Narudia: kumbadili Waziri, hata Waziri Mkuu, si jambo la ajabu. Anaweza kujiuzulu, anaweza kufukuzwa na nchi isitikisike. Lakini huwezi kumtikisa Rais wa nchi bila kuitikisa nchi yenyewe. Ni vizuri jambo hili likatamkwa wazi wazi na likaeleweka sawa sawa. Maana watu wengine wananong'onanong' ona kuwajibika kwa Rais kana kwamba ni jambo la mchezo mchezo tu. Kulazimika kumchukulia hatua Rais wa nchi ni mkasa na balaa kwa nchi yoyote ile’’.
Hoja ya Mwl. Nyerere ilisadifu ukweli ambao hata baadhi ya wanasiasa wa kambi ya upinzani wanafahamu ukweli huo katika mazingira ya sheria na siasa zetu.
Wakati akichangia kwenye Mjadala ya Kashfa ya Tegeta escrow account, Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba, Tundu Lissu alinukuliwa akisema, ‘’Tunafahamu utaratibu wa kumu-impeach Rais ni mgumu, tuanze na Waziri Mkuu ambaye tunamuweza humu ndani wakati tunafikiria namna ya kumu-Impeach huyu aliye authorize malipo ya mabilioni haya, tuanze na hawa tunaowaweza, Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Profesa Muhongo, Profesa Tibaijuka na majizi yote yaliyotajwa humu tuanze nayo’’.
Kuna baadhi ya watanzania wajinga wanaamini Zitto atawasaidia kumuondoa Rais Magufuli kwenye kiti cha Urais badala ya kutumia sanduku la kura kwenye Uchaguzi Mkuu 2020. Hawa ni aina ya Watanzania ambao wanaweza kuamini kama Zitto akijitokeza na kuwaambia anaweza kutembea kwa miguu kutoka Tanzania mpaka Marekani.
Siasa za kweli hubeba uhalisia na sio delution and theory.
Politics of stupid hukonga nyonyo za blind followers lakini hazina manufaa yoyote katika ukuaji wa chama.
Chama cha ACT-Wazalendo hakiwezi kukua na kuimarika kwa kutegemea politics of stupid.
Zitto unatakiwa uijenge ACT-Wazalendo katika msingi wa siasa zilizobeba uhalisia katika mazingira ya kisiasa nchini. Achana na sensational politics.