Ni muhimu sana kwa wanasiasa wetu kuepuka kuupotosha umma kwa kutafuta taarifa sahihi kabla ya kutoa matamko. Baada ya kusoma waraka kwa Mhe Zitto nami nimefanya utafiti mdogo na kubaini mengi aliyosema Zitto hayako sahihi.
Serikali ilitangaza kuanza ujenzi wa Reli ya Kati na imetimiza ahadi hiyo kwa kuanza mchakato wa kupata mkandarasi kwa njia ya Zabuni. Zitto anafahamu fika, Bunge lilipitisha bajeti ya kuanza ujenzi wa Reli hiyo na kutenga kiasi cha Trilioni Moja za kuanzia. Zitto anafahamu pia kwamba ili kutumia fedha za Serikali zilizotengwa kwenye bajeti ni lazima mkandarasi apatikane kwa uwazi kwa njia ya zabuni.....
Serikali imetangaza zabuni na hivi sasa tathmini ya zabuni hiyo inafanyika baada ya wakandarasi kujitokeza kuomba tender hiyo. Zoezi la tathmini sio kazi nyepesi kama ya kukaanga njugu....ni lazima kufanya due dilligence ya makampuni yaliyoomba kazi hiyo ikiwa ni pamoja na kutembelea kazi ambazo yamekwishafanya ili kuepuka kuingizwa mkenge....
Zoezi la zabuni linafanywa kwa uwazi, kampuni itakayoshinda itatangazwa hadharani....hadi sasa tangazo halijatolewa lakini Zitto amerukia kudai kwamba kampuni ya Uturuki imeshinda wakati hapo hapo juu yake anasema "Leo ni mwezi Januari hata zabuni ya kampuni iliyoshinda kutekeleza mradi huo Serikali haijatangaza" kuna contradiction kwenye maneno yake.
Kitu kingine ambacho sijamuelewa....hivi ziara ya Rais wa Uturuki inahatarisha vipi mahusiano yetu na China? Tanzania ni nchi isiyofungamana na upande wowote...na kwa uelewa wangu mdogo, China na Uturuki hazina ugomvi wowote ule.....sasa Zitto anavyosema Serikali ijitizame upya mahusiano yake na China msingi wake ni nini?
Ingekuwa anayekuja ni Waziri Mkuu wa Japan walau kwa mbali onyo lake lingekuwa na mantiki.....lakini Uturuki? Isitoshe hii sio mara ya kwanza kwa Rais wa Uturuki kufanya ziara nchini na baada yake marais wa China wawili wameshakuja nchini...
Zitto ametengeneza hisia kwamba mahusiano ya Tanzania na China hayako vizuri....hivi kipimo chake ni nini? Hivi mahusiano yangekuwa mabaya kama anavyotaka kutuaminisha....Tanzania leo hii ingechaguliwa na China kuwa miongoni mwa nchi (4) za kipaumbele za kupokea Viwanda kutoka China?
Je kama mahusiano yangekuwa mabaya Waziri wa Mambo ya Nje wa China angekuja Tanzania wiki moja tu iliyopita na alipoongea na waandishi wa habari kasema mwenyewe Tanzania ni mshirika wa kutumainiwa wa China barani Afrika? Hivi Zitto hakusikia Waziri yule alipotangaza uamuzi wa China kusaidia ujenzi wa makao makuu Dodoma?
hakusikia uamuzi wa China wa kuleta viwanda kwa wingi? Ni kweli kwamba Tanzania imekuwa na China muda wote na imeendelea kuwa na China muda wote na itaendelea kuwa na China muda wote. Isitoshe ni muhimu Zito akaelewa kwamba mahusiano kati ya China na Tanzania yamejengwa katika misingi ya kuheshimu Uhuru wa taifa na kutoingiliana katika masuala ya ndani (Sovereignty and non inteference on internal affairs),
kutetea haki za wanyonge, kushirikiana katika kuleta maendeleo. Vilevile siku zote China inahieshimu Tanzania kwa kuendelea kusimama nayo kwenye mambo yake ya msingi kama kuitambua China kama taifa moja lenye mifumo miwili na kwamba Taiwan,Tibet na Macao ni sehemu ya Jamhuri ya Watu wa China.
Hayo ni mambo ya msingi ambayo yanaifanya China iendelee kuiheshimu Tanzania....mbali na mambo mengine ya kihistoria kama vile juhudi za Tanzania kuisaidia Jamuhuri ya Watu wa China kutambulika katika Umoja wa Mataifa na kuingia kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hata siku moja uhusiano wa kidiplomasia na China hauwezi kutetereka kwasababu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi iwe ni wa barabara, Reli au Bandari....
Kama ingekuwa hivyo, basi leo hii uhusiano na China ungekuwa ushakufa kwasababu mwaka 2009 China ilishaidinisha Mkopo wa Dola za Kimarekani Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Gati 13 na 14 za bandari ya Dar es Salaam, lakini baadaye Serikali iliachana na mradi ule kwasababu ulikuwa na harufu ya rushwa iliyomfanya Waziri wa Uchukuzi wa wakati huo Omar Nundu aondolewe......
Jambo lile lilikuwa la kibiashara, halikuwa na athari yoyote kwa mahusiano ya Tanzania na China sana sana baada ya tukio lile, miaka miwili baadaye China iliipatia Tanzania Dola Bilioni 1.2 kujenga bomba la gesi.
Zitto anasema Rais hajali misingi imara ya sera ya mambo ya Nje...hivi Zitto anaijua misingi hiyo? Nijuavyo mimi misingi ya Sera ya Mambo ya Nje ni pamoja na Kuishi kwa amani na mataifa mengine (peaceful co-existance), kulinda usalama wa taifa, kujenga na kuendeleza Ujirani Mwema, kutofungamana na siasa za upande wowote, kupigania maslahi ya taifa n.k
Haya yote Serikali imeendelea kusimamia kwenye misingi hiyo na kuienzi....Rais toka amechaguliwa amekwishatembelea nchi za jirani na anaendelea kufanya hivyo..... Rais ameendelea kukutana na wageni kutoka nchi mbalimbali,za magharibi na mashariki bila kubagua nchi yoyote, Tanzania imeendelea kushiriki kwenye ulinzi wa amani DRC, imeendelea kutafuta amani Burundi.... haya yote ni ushahidi wa kusimama katika Misingi ya Mambo ya Nje.
Zitto amedai Rais na Serikali ndani ya mwaka mmoja amevunja misingi ya sera ya mambo ya Nje kuhusu Sahara Magharibi... akilenga kuonyesha ni kosa Tanzania kuwa na mahusiano na Morocco...asichoeleza ni kwamba siku zote....hata kabla ya ziara ya mfalme, Tanzania imekuwa na mahusiano ya kidiplomasia na Morocco.....
ubalozi wa Tanzania Paris unawakilisha Tanzania Morocco na ubalozi wa Morocco Nairobi unawakilisha nchi hiyo Tanzania...Kingine ambacho wengi hawakijui ni kwamba Algeria na Afrika ya Kusini mataifa ambayo yamesimama bega kwa bega na Tanzania kuitetea Sahara ya Magharibi wamekuwa na mahusiano ya kidiplomasia na Morocco..
tena wao wana Balozi zao kabisa kule Morocco..... kuwa na mahusiano ya kidiplomasia hakuzuii mataifa kutofautiana kimisingi au kimtazamo....na kutofautiana kimtazamo hakuzuii kuwa na mahusiano ya kidiplomasia....Leo hii Iran ina tofauti za kimtazamo na Marekani,lakini wanao Ubalozi kwenye nchi hiyo....
Kuhusu mahusiano na Israel,pamoja na kwamba tumekuwa na mahusiano ya kidiplomasia na taifa hilo hata kabla serikali ya awamu ya tano haijaingia madarakani, msimamo wa Tanzania kuhusu Palestina haujawahi kubadilika. Sijui Zitto taarifa zake anazipata wapi?
Kumbukumbu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba katika Kikao cha 71 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilichomalizika mwezi Desemba mwaka jana, Tanzania imepiga kura kuunga mkono maazimio yote kuhusu haki za Wapalestina ndani ya Kamati ya Tatu ya Umoja wa Mataifa......Maazimio hayo ni pamoja na:
Azimio Na A /RES/71/247 kupigania haki ya wapalestina kujitawala wenyewe kwenye ardhi yake ikiwemo Jerusalemu Mashariki
Azimio Na: A/RES/71/98 - kupinga Shughuli za Israel zinazodhuru haki za wapalestina kwenye maeneo yaliyokaliwa na Waisrael
Azimio na: A/RES/71/97- Kupinga Israel kuweka makazi ndani ya maeneo ya Wapalestina
Azimio na: A/RES/71/95 - Kuunda Kamati ya Kuchunguza vitendo vya Waisraeli vinavyoathiri haki za binadamu ndani ya maeneo ya Wapalestina
Azimio na: A/RES/71/94- Kulinda Mali za Wakimbizi wa Palestina na mapato yao
Sasa sijui Zitto anapodai Rais amekiuka misingi ya sera ya mambo ya Nje kuhusu Wapalestina- hoja yake inatokea wapi?