Zito na Lusinde TBC wazungumzia bajeti

swrc

JF-Expert Member
Jun 17, 2012
442
38
Mkuu,
Waziri kivuli wa fedha na ambaye ni naibu kiongozi wa upinzani bungeni na mbunge wa Kigoma kaskazini Mh.Kabwe Zuberi Zito pamoja na mtoa matusi mkuu wa ccm na mbunge wa Mtera Mh. Livingstone Lusinde wamekuwa wakiielezea bajeti ya serekali kabla ya kipindi cha bunge kuanza. Kwa pamoja wamekiri bajeti hiyo kuwa na mapungufu kwa kupendelea zaidi upande wa mijini dhidi ya vijijini ambapo ndipo walipo watanzania wengi maskini. Zito amekwenda mbele zaidi kwa kusema bajeti hiyo inauma na kupulizia. Zito kwa kujiamini zaidi ameeilezea bajeti ya upinzani kwamba ni kwa nini wameelekeza nguvu zaidi vijijini kwa kutoa mifano mabalimbali, tafiti zilizofanywa kitaifa na kimataifa, solutions na hitimisho kwa ujumla wake. Kwa ujumla bajeti ya upinzani inaonyesha ni jinsi gani inavyowajali asilimia 85 ya watanzania. Hakika Zito alifunika hasa kwa kuijenga hoja yake, kuitetea na kuihitimisha zaidi ya Lusinde. HAKIKA ZITO AMEONYESHA ANAWEZA.

Nawakilisha.:llama:
 
Back
Top Bottom