Fuatilia hotuba yake alipokuwa UN, alilalamikia vikwazo na akomba vifutwe sababu nchi yake inateseka. Hajasema lolote kuhusu kujitoa. Tafuta kwenye jarida la UN utaona alichokisema na hiki cha sasa.mugabe ni mkweli ....ila tatizo la viongozi wengi wa afrika ni vibaraka na wasaliti......big up mugabe
Wewe unachangia senti 10 wenzako wanatoa billion then unataka wote muwe na haki sawa katika maamuzi,mkata check kubwa ndio anaamua kama hutaki hamaWords makes a lot of sense to be honestly
U.N. its really unfair kabisa
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema Bara la Afrika lipo tayari kujitoa katika Umoja wa Mataifa (UN) iwapo madai yake ya kutaka mabadiliko katika umoja huo hayatatekelezwa.
Mugabe ametoa kauli hiyo mara tu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Harare na kupokelewa na mamia ya wanachama wa chama tawala ZANU-PF na kulakiwa akitokea New York, Marekani.
Amesema kuwa Umoja wa Afrika (AU) unajiandaa kuunda kundi la kusimamia kujitoa likijumuisha mataifa mengine kama Urusi, Uchina na India iwapo Baraza la Usalama la UN halitajumuisha wanachama kutoka katika Bara la Afrika hapo mwakani.
Akihutubia Baraza Kuu la UN, Jijini NewYork, Mugabe alizishutumu nchi za magharibi kwa kuchangia kudorora kwa uchumi na kupelekea hali kuwa mbaya sana katika nchi yake.
==============================
PRESIDENT Robert Mugabe claimed Saturday said African countries and nations from other regions such as Asia are prepared to pull out of the 70-year-old United Nations and form a rival organisation.
The Zimbabwean leader said that the idea follows numerous bids by the Africa Union to join the United Nations Security Council which have been blocked being blocked some council states.
He was addressing thousands of Zanu PF supporters gathered at Harare International Airport to welcome him back home from the United Nations General Assembly which was held in New York last week
Currently the five UN security council members are China, Russia, Britain, France, and United States.
“This year we went to UN as an African committee after we agreed to join hands and speak with one voice on the issue of vetoing power,” said the 92-year-old leader.
“It’s unfortunate that we had not finished and agreed on our position as the African Union, but I hope all will be fine next year.”
“But next year in September if they keep on refusing to accept and give the Africa Union the vetoing powers we will pull out.”
He went on to say that not all countries were against the AU’s membership of the security council, revealing that Russia and China backed Africa’s position.
Source: New Zimbabwe
mugabe ni mkweli ....ila tatizo la viongozi wengi wa afrika ni vibaraka na wasaliti......big up mugabe
Haya maelezo umeyatoa wapi? Ni kweli Mandela alitumia pasipoti ya Tanzania kusafiria nje ya taifa lake.
Na ni kweli fedha za Gaddafi zilitumika katika kutafuta ukombozi wa Afrika ya Kusini.
Ni kweli pia fedha za Gaddafi zilikuwa kwenye mpango wa kuboresha benki ya Afrika lakini mpango wake haukufanikiwa! Hii ni kutokana na kupata upinzani mkali kutoka kwa benki za IMF na WB, ambazo kwa kiasi kikubwa zinamilikiwa na mataifa ya magharibi kunyonya mataifa masikini!
Lakini si kweli kuwa Umoja wa Afrika na viongozi wa Afrika walikuwa hawana msaada kwa Gaddafi! Viongozi wa Afrika kupitia umoja wao, AU walikuwa tayari wameshatoa mapendekezo ya nini kifanyike ili kuinusuru Libya kuingia kwenye machafuko.
Na hayo mapendekezo tayari yalishakubaliwa baina ya pande zote mbili. Lakini nia na madhamuni ya nchi za magharibi ilikuwa ni kuundoa utawala wa Libya na uhai wa Gaddafi.
Jaribu kuangalia haya mahojiano ya aliyekuwa mwenyekiti wa AU kipindi hicho, Jacob Zuma. Amefafanua vizuri sana kuhusu; hatma ya Afrika baada ya mpango wa Gaddafi kutofanikiwa, machafuko ya Libya na kile kinachoendelea Syria hivi sasa. Pia amegusia mabadiliko ya kimuundo wa benki za IMF na WB, na uhusiano uliopo kati ya China na Afrika..
Baadae alikuja kuzungumza Robert Mugabe kwenye mkutano wa UN..
Lakini hivi karibuni mataifa ya magharibi haya haya yaliyoshiriki kumtoa Gaddafi yamekiri kuwa yalifanya makosa.! Sasa tutaendelea kuwa wanyonge hivi hadi lini?
Ujue hivi vyombo vya habari vya magharibi vinapotosha sana walimwengu. Kuna tofauti kubwa sana kati ya "kuomba" na "kudai".
Jaribu kuangalia tena hotuba yake ya kwanza kuhusu Zimbabwe kuondolewa vikwazo.
Huyu rais Mugabe haombi kama tunavyoaminishwa na vyombo vya habari vya magharibi bali anadai kile anachokiamini kuwa ni haki kwa taifa lake la Zimbabwe.