Zijue Sehemu 6 Muhimu za Mabasi yaendayo Kasi

As Salafiyyu91

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
2,537
2,530
6e1a7eb4e008f8ad120b330ff91ca68e.jpg


Ndugu Wanajamvi ule
MRADI wa mabasi yatakayo kwenda mwendo wa haraka katika barabara teule mpya jijini Dar es Salaam unaweza kuwa na ufunguo wenye sulushisho dhidi ya foleni na misongamano ya magari jijini humu.

Matarajio ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ni kwamba kuzinduliwa kwa mradi huu kutakuwa ndio mwisho wa tatizo sugu la foleni katika barabara zake nyembamba ambazo nyingi mtindo wake ulijengwa na Wakoloni zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Pamoja na kuwahi kuwepo aina hii ya mabasi katika miaka ya 1980, sasa mabasi haya yamerudi tena katika ubora wa kipekee na tofauti hasa katika suala zima la uundwaji wake wa kuvutia zaidi na ulio na mapambo mengi kama vile televisheni, kiyoyozi, kamera za usalama(CCTV Camera) ambazo zitasaidia kuonyesha usalama ndani ya basi, endapo utatokea uhalifu wowote muhusika ataonekana mara moja. Pamoja na kuwepo vyote hivyo pia kuna na viti kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ambao ni walemavu wa viungo pamoja na mama wajawazito.

TUANGALIE BAADHI YA SEHEMU KATIKA BASI HILI;


A. STELINGI - STEERING WHEEL

Mfumo wa stelingi ni ZF ya Ujerumani, wenye ubora wa kimataifa na unaozingatia usalama wa basi liendeshwapo barabarani muda wote. Pia kiti cha dereva kina uwezo wa kumpunguzia uchovu wa kukaa kwa muda mrefu ili kumsaidia kuwa makini aendeshapo basi husika ili kuepukana na ajali.

B. TAIRI - TYRE

Matairi bora yaliyothibitishwa na viwango vya kimataifa (ISO) ili kuweza kukabiliana na mabadiriko ya tabia nchi.

C. KIZIMIA MOTO - FIRE EXTINGUISHER

Mitungi maalum ya kuzimishia moto utokanao na vimiminika (mafuta), gasi, hitilafu za umeme n.k

D. INJINI - ENGINE

Aina ya injini ni CUMMINS iliyotengenezwa nchini Marekani (USA) ndio inayotumika katika mabasi yaendayo kwa haraka, injini hii kwa kiasi kikubwa imepunguza uchafuzi wa mazingira, imedhibiti uchafuzi wa mazingira (air pollution), makelele (noise pollution)

E. KAMERA ZA USALAMA - CCTV CAMERAS

Skrini ndogo yenye ukubwa wa inchi saba inayo dhibiti kamera 16 zilizomo ndani ya basi zinazo onesha yote yanayojiri ndani ya basi na kwa kupitia teknolojia iliyowekwa ndani ya kila basi yenye uwezo wa kutuma picha za matukio yote yanayojiri ndani ya basi liwapo barabarani kwenda kituo kikuu cha udhibiti na uchunguzi na matukio ya kihalifu na uharibifu wa samani.

F. VITI - SEATS

Ndani ya basi haki za walemavu, wazee, wajawazito zimezingatiwa kwa kutengewa viti maalum kulingana na mahitaji husika ikiwemo vikuju vya kushika kwenye bomba kwa abiria wanao simama.
 
Kwenye camera hapo ndipo tunapohitaji zaidi ili tuwanyooshe waharibu wa seat na wale wanaochorachora,pamoja na wezi wa mifukoni
 
Kwenye camera hapo ndipo tunapohitaji zaidi ili tuwanyooshe waharibu wa seat na wale wanaochorachora,pamoja na wezi wa mifukoni
Tena vijana inabidi watahadhari sana na wizi wa simu na Mali za Abiria wizi wao utawatokea puani
 
naona tungebadili jina tutoe mwendo kasi tuyaite mabasi yasiyo na foleni kwani kituo hadi kituo dereva hata hamalizi gia anakuwa asha simama
 
Kwenye camera...sawa je kuna kitengo maalumu kitakachoshughulikia waharibifu wa vifaa vilivyomo humo ila siku na kimejipangaje kuhakikisha viti na vitu vingine tunavikuta kama vilivyo mwaka mzima...na je wapo tayari kutumbuliwa endapo tukiona michoro na mikwaruzo humo kwenye mabasi?

Swala la ma tyre kuwa madhubuti litakuwa endelevu....au ni hayo yaliyokuja na mabasi baada ya hapo tutaanza story za mchakato na upembusi yakinifu...au tutasubiri yaishe ndipo tuagize....itapendeza sana kukiwa na consistence
 
Back
Top Bottom