Zijue aina za biashara unazoweza kiuzifanya bila mtaji

Kiazi

Kuwa na adabu. Siyo kuja kuongea sijui umetoka kusoma kitabu cha nanauka then unayabeba huko. Eti Biashara unaweza kufanya bila mtaji. Labda kuokota kumbikumbi na konokono unawauza au mikusu huko iringa
Vip biashara ya udalali unatumia mtaji upi??? Achana na wale wenye ofisi nazungumzia wale walioweka bango kwenye nguzo za umeme.
 
Inategemea denifition yako ya mtaji,acha kucopy na kupaste,kiufupu hakuna biashara unwz fanya bila mtaji,period
 
kuwa na kalamu na daftari ni mtaji. maybe unatumia computer ni mtaji.
hata nauli ya kwenda eneo la kazi ni mtaji. mlo wa kila siku ni mtaji.

HAKUNA BIASHARA BILA MTAJI labda huelewi maana ya mtaji ni nini.
 
Angalau ukiwa na ujuzi na Computer yenye specifications za kusupport software za graphics. Ofisi itabaki networking yako tu.
Na computer lazima uwe nayo, alafu graphics designing ipo very wide mfano Kuna wale wanaotengeneza stickers Kuna kamtambo fulani wanatumia.
 
Zipo nyingi tu mkuu ila wajuaji wengi humu
Mkuu Baba kwa upande wangu nakushuru saaaana! na Mungu naye mjua akubariki mnoooo Baba!!...mengineyo yoote humu vumilia tu! ndo binadamu tulivyo!..hakuna namna! tunaishi nao!
 
Plan zipi hizo tukuoe mtaji uwe unatuletea ka percentage
Nipo serious.
maana fikiria habari hizo unamueleza mwanamke yeye atafikiria hilo.

Sisi huku mtaani tuna plan nyingi ila mwisho wa hitimisho ! Mtaji tutapa wapi
 
Wengi huamini kuwa lazima uwe na fedha ndio uanzishe biashara na ndio sababu yao kuu ya kukaa bila kujishughulisha, Ukweli ni kwamba mtaji ni moja ya kitu muhimu sana katika kuanzisha biashara, lakini kuna aina ya biashara ambazo zinahitaji gharama ndogo sana kuanzisha na kukupelekea kupata faida kubwa sana.

Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo sana kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa juhudi sana ukiwa upande wa huduma(services) na kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria kuanza kukodi ofisi yako, kuajiri watu wengine nk , ingawa ni rahisi kutoka ukiwa upande wa huduma lakini inahitaji ujuzi au weledi fulani hivi ili uweze fika kilele cha mafanikio hapa simaanishi lazima uwe umesoma chuo kikuu maana ujuzi au utaalamu wa jambo halihusiani na degree ya chuo kikuu.

Unaweza pata ujuzi kwa kuhudhuria semina mbalimbali, workshop mbalimbali, au kufundishwa na mtu mwenye ujuzi husika na baada ya kupata ujuzi kuanza fanyia kazi katika maisha yako ya kawaida kila siku na kuwa bora kwa upande huo.

Nimejaribu kuorodhesha aina i 13 za biashara unazoweza anzisha pasipo kuwa na mtaji kabisa au mtaji kidogo sana. Hizi ni aina ya biashara ambazo nimezifanya kwa muda sasa na kuona matunda yake na nyingine nimeshuhudia watu wakifanya na kufanikiwa.

Zifuatazo ni baadhi ya biashara unazoweza anzisha kwa mtaji mdogo sana au pasipo mtaji kabisa:

1.Huduma za kuandika miradi biashara (business plan), kama ilivyo kwa tafiti za uchanganuzi yakinifu (hali halisi ya biashara) wajasiriamali wengi huepuka kufanya kazi hii ngumu ya kuandika mradi biashara(business plan) yao. Ukweli ni kuwa wajasiriamali wengi hawajui hata kuandika business plan katika uwezo wa kuwashawishi wawekezaji kuja kuwekeza na huwa hawawekezi muda wa kutosha kujifunza kwa hilo. Kama unaweza timiza hitaji hili biashara ipo mikononi kwako.

2.Mshauri wa mambo ya biashara: Wewe ni mzoefu wa ujasiriamali au mmliki wa biashara? Unajua nini kinahitajika ili uanzishe biashara, kujenga biashara, kuingoza biashara na kukua? Sasa unaweza kuanza kazi ya ushauri wa biashara. Unaweza saidia kampuni au biashara mbalimbali kutoka chini ya uvungu na kwa kutoa ushauri na maelekezo muhimu. Unaweza kuwasaidia watu walioajiriwa kuanza kutoka kwenye ajira na kuingia katika ujasiriamali kwa malipo.

3.Huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu. Wewe ni mzuri katika kuandaa vitabu vya uhasibu vya kampuni au biashara mbalimbali?unaweza weka ulingano kwa vitabu vya uhasibu Sasa hamna kitu kinaweza kukuzuia wewe kuanza huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu anza sasa.

4.Kutoa huduma ya kuandaa nakuendesha matukio(event management), kampuni nyingi kila mara huwa na matukio mbalimbali mfano semina, siku ya familia, sherehe mbalimbali mara nyingi kampuni kama kampuni haiwezi kufanikisha kwa ufanisi uandaaji wa matukio haya, na hivi ndivyo ilivyo kutokana na wafanyakazi wao kuwa na majukumu husika tofauti na kuandaa matukio ya kampuni na kuyasimamia, hivyo ili kuwa na ufanisi hapa inabidi kampuni zikodi watu wanye ujuzi wa kuandaa shughuli husika kwa uhakika, wewe kama una ujuzi na uzoefu wa kuandaa shughuli kama hizo mwanzo mpaka mwisho uwanja ni wako. Mfano kuna matukio kama siku ya familia, semina kwa wafanyakazi, maonyesho ya biashara ndani na na nje ya nchi kwa kampuni husika.

5.Kuanzisha tovuti kwa ajili ya huduma mbalimbali, Unaweza anzisha tovuti na kutoa huduma ya taarifa watu wanatafuta ,baada ya kupata watu wengi wanaotembelea tovuti yako, unaweza sasa ongea na kampuni kadhaa kuja kutangaza na wewe na kutengeneza fedha za kutosha.

Kama hujui jinsi ya kutengeneza tovuti usijali kuna tovuti za bure kabisa ambazo zimetengenezwa tayari kinachohitajika ni wewe kujaza fomu zao na ndani ya dakika moja unakuwa na wewe natovuti yako, na kama unahitaji nunua domain inaweza ikawa moja kwa moja tovuti yako.

6. Mshauri wa masoko

Je wewe unaweza nionyesha mimi njia ya gharama ndogo ya kuongeza wateja wangu kuanzia aslimia 30% -70% au zaidi? kama ndio biashara ipo mikononi mwako. Unaweza jiweka wewe mwenyewe katika ushauri wa masoko kwa wamiliki wa biashara ndogo na kati hata kubwa jinsi ya kuwateka na kuwavuta wateja na kuongeza mauzo ya bidhaa kwa ada fulani ,kutokana na huduma husika.

7.Mtafsiri wa maandiko mbalimbali kwenda lugha ya wazawa; Kampuni nyingi za nje zinazokuja hapa nchini, huwa wanahitaji kutafsiri taarifa zao kwenda lugha ya wazawa, mfano mradi Fulani, tovuti zao, mfano kama ni kampuni ya vitabu mwandishi mmiliki angependa ili auze kwa wazawa inabidi atafsiri kwenda lugha ya wazawa, Pia mfano kuna hata miradi mbalimbali ambayo inatakiwa iangaliwe na wazawa nk.

8. kutafiti fursa mpya za biashara, nina marafiki zangu ambao walianza kutoa huduma ya kutafi fursa mpya na wanafanya vema kwenye hii biashara. Wanachofanya ni kutupia jicho kwa mambo yajayo, mwelekeo, mahitaji au fursa za biashara; na kuandaa mradi/mpango kuhusiana na hilo na kuuza hilo wazo kwa makampuni makubwa. Wakati mwingine wanakuja na mawazo ya bidhaa na mawazo ya biashara yenye soko moja kwa moja kubwa la kutosha; na kuuza hayo mawazo kwa makampuni kwa ajili ya kuayaendeleza. Kama kazi hii unaipenda unaweza anza kutoa huduma kutafiti fursa mpya za biashara.

9. Mshauri wa mitandao ya kijamii (social media consultancy), Kwa hii dunia mitandao ya kijamii imechukua asilimia kubwa sana. Je wewe unajua jinsi ya kutengeneza foleni kwa mitandao ya kijamii? Unajua jinsi ya kuboresha na kuelimisha umma juu ya chapa(brand) za makampuni ndani ya mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na linkedin? Basi unaweza kuwa mshauri wa mitandao ya kijamii na kutengeneza fedha zako.

10. Kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni, Je wewe ni mzuri katika kuandika katiba za kampuni?unajua jinsi ya kuchagua jina sahihi la kampuni?unajua stepu zinazohitajika ili ukamilishe uandikishe jina la biashara? Anza sasa fungua biashara yako ya kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni .

11. Kutoa huduma za kuandikisha hakimili za bidhaa au huduma yako

12. Huduma za ushauri kwa biashara ndogo

13. Kuandika kitabu kizuri na kukiuza kwa umma.
Ongezea na Real Estate Business
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom