Zifahamu faida za Kamasi

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,604
Jamani wako watu wanaodhani makamasi ni kitu kibaya na kichafu kiasi cha kujisikia kinyaa.

Kamasi (mucus) linapatikana puani kwenye mfumo wa hewa. Hata kohozi ni kamasi pia la kooni.

Pua na koo (trachea) ni sehemu ya bomba linalopitisha hewa kwenda na kutoka ndani ya mwili kupitia kwenye mapafu. Ndani ya mapafu hakutakiwi kitu chochote kigeni zaidi ya hewa na unyevunyevu tu basi. Ili kuzuia vitu vigeni kama vumbi, moshi, chakula, maji na vitu vingine mfumo wa hewa unalindwa kwa kutumia vitu vifuatavyo:

1. Nywele puani (cilia) - nywele puani zinakamata na zinazuia vitu kama vumbi laini visiende kwenye mapafu. Nywele hizi kama papasi, huwa zinalisukuma vumbi nje pua. Usiwe na tabia ya kung'oa nywele za puani kila wakati.;

2. Epithelial/Mucus cells: Hizi ni cell zenye uwezo wa kutoa maji mazito sana (kamasi/kohozi). Zinazalisha makamasi na makohozi ili kukamata vitu kama mavumbi na wadudu visipite kwenda mapafuni. Ukiwa kwenye mavumbi mengi au wadudu kwenye njia ya hewa kamasi na kohozi nyingi na nzito litazalishwa puani na kooni ili kusaidia kuvinasa vitu hivyo visifike mapafuni. Unapo penga kamasi maana yake unasaidia kulitoa vumbi na vidudu vilivyonaswa kwenye kamasi. Unapotoa kohozi maana yake unatoa nje vitu vilivyonaswa visipite kwenda mapafuni. Kukohoa na kutoa makohozi (kubanja) ni jambo jema usilichukie.

3. Kikohozi: Kikohozi ni njia ya kuondosha madudu, mavumbi au vipele kwenye njia ya hewa. Hivyo kukohoa ni dalili kuwa kwenye mfumo wa hewa kuna kitu kisichotakiwa kubaki au kwenda kwenye njia ya hewa na mapafuni. Kikohozi in ishara kuwa kuna kitu (kipele, uchafu au kitu) kisichotakiwa kwenye pomba la hewa. Kikohozi cha zaidi ya siku tatu mfululizo kinamaanisha kuwa kwenye mfumo wa hewa kuna kitu kisichoondosheka kwa kuhoa kama vile vipele, vidonda (sores) au uvimbe kinachohitaji uchunguzi na matibabu ya haraka kabla vitu hivyo kushuka hadi kwenye mapafu (Lower respiratory system infections) na kusababisha vitu kama pneumonia na shida nyingine za mapafuni.

4. Kupiga chafya: Hii ni njia ya haraka sana na ya hali ya juu ya kuondosha vumbi, tumbaku, wadudu kwenye njia ya hewa kwa kutumia msukumo (pressure) mkubwa wa hewa inayosafiri kwa kasi kubwaya ajabu ili kupuliza nje kile kisichotakiwa kwenda kwenye mapafu.

5. Kupaliwa (chock): Hii ni njia ya haraka ya kufa na kupona ya kuzuia vitu kama maji, na chakula visiende kwenye mapafu. Mwili utapambana kwa nguvu zake zote hapa ili kuzuia maji au chakula visifike kwenye mapafu, hata ikibidi mtu kufa. Tusiwe na tabia ya kula/kunywa huku unaongea, watoto kulala na chakula mdomoni

Hivyo ndugu zangu kutokwa na kamasi au kohozi jingi ni dalili kuwa mfumo wako wa hewa umevamiwa na kitu kisichotakiwa kiende kwenye mapafu. Pia ni dalili kuwa mfumo wako wa hewa unafanyakazi vizuri sana. Kama afya yako ni mbaya sana mwili wako utashindwa kutoa makamasi au kohozi la kutosha kuzuia vitu visivyotakiwa (foreign bodies) viende kwenye mapafu. HIvyo ukiona unazalisha makamasi au makohozi mengi ujue afya yako bado ni nzuri. Yaana mwili una uwezo wa ku-detect anomalies.

6. Chembehai nyeupe (white blood cells): Uvamizi wa mfumo wako wa hewa ukiwa mkubwa hadi ukafika kwemye mapafu, mapafu yatatoa chembehai za kinga ya mwili za aina mbalimbali ili kupambana na uvamizi huo uliofika hadi kwenye mapafu.

Usichukie kamasi na makohozi bali chukua hatua haraka kuepuka vitu vinavoweza kufika kwenye mapafu yako kama vile mavumbi, mchanga, bacteria, viruses, fungus, n.k.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom