Zifahamu dalili zinazoashiria mwanamke ni mjamzito

niwaellyester1

Senior Member
Sep 7, 2010
123
19

Eti mimba inaanza kuonekana muda gani baada ya kuingia? yaani kama ikiingia leo, baada ya muda gani ndiyo itaonyesha kuwa ni positive?


MASWALI YA WADAU WENGINE KUHUSU DALILI ZA MIMBA
Helow,

Ni nini kinasababisha matiti kuwasha na chuchu kuuma, je ni dalili za ugonjwa na kuna tiba ya tatizo hili?

Msaada tafadhali
Habari za jioni wana JF,

Naomba kujua ni muda gani mwanamke huweza kuhisi ana mimba tangu siku alipojamiiana na mwanaume akiwa katika siku zake za hatari.

Je, ni siku mbili baadae au wiki kadhaa?

Naomba msaada wenu.
Habari zenu,

Nimefanya mapenzi katika siku za hatari ila jamaa alimwaga nje. Sasa ni wiki imepita naskia tumbo linauma na chuchu zinauma ingawa matiti hayajavimba.

Je, inaweza ikawa ni mimba?
Naomba msaada. Nimeona dalili hizi na ningependa kujua endapo ni dalili za ujauzito.

1. Kula kupita kiasi
2. Kuchagua chakula
3. kutopenda harufu ya mafuta
4. Kichefuchefu asubuhi
5. Kuhisi joto

Kama si dalili za ujauzito ni dalili za nini?
Habari ndugu zangu.

Ninaomba kujuzwa. Nina ujauzito wa mwezi mmoja kuna wakati kitovu kinauma na jana wakati naoga ktk harakati zavkujiswafi nimeona dalili za damu kidogo na sometimes nafeel km nataka kuingia Mp. Je, hii ni sawa?

Thanx in advance.


MICHANGO YA WADAU
Baadhi ya dalili za nje zinazoonyesha uwezekano wa kuwa na mimba
  • Maziwa kujaa na kuwa magumu kidogo.
  • Kunenepa ghafla kutokana na kuongezeka vikoleza mimba mwilini.
  • Mabadiliko kitabia ya ghafla yasiyozoeleka.


ZAIDI, SOMA:

Dalili za kwanza za mimba
Je, nina mimba?

Kuna baina ya wanawake wenye huonyesha dalili za mimba punde tu katika wiki kadhaa baada ya kushika mimba. kuna maswala mengi Kuhusu upataji mimba na ni siku gani mwanamke anaweza kupata mimba. Hebu tujadiliane kwa ufupi. Hedhi yaani mensturation period, ni wakati mwanamke anaweza kujua ya kuwa hana mimba.

Damu inayotoka wakati huu huwa nyekundu. Damu hii hutoka kila mwezi kwa wanawake walio na mzunguko wa kawaida. Pia damu hii huchukua siku tatu hadi tano kwa wale wenye mzunguko wa kawaida. Unapokosa hedhi, haswaa wakati umeshirikiana ngono, Kuna chanzo kubwa ya kuwa umeshika mimba.

“Kukosa Hedhi ni chanzo cha maisha”
Ni vyema kujua jinsi ya kujichunga ili wewe na mwanawe muwe salama. Hata kabla ukose hedhi (mensturation/period) Unaweza kudhani au kutumai una mimba. Tumaini Ni kwa wale waliooleka au wanaopenda kupata watoto. Wakati mwingine, Mimba huja na hofu, haswaa ukiwa umefanya ngono kando ya ndoa. Lakini usitie shaka, mtoto ni baraka na ni lazima na wajibu wa kila mzazi kujua wanapotarajia mwana.

Dalili za mimba kwa wanawake wengi huonyesha katika wiki za kwanza wanapopata mimba. Hizi dalili ni tofauti kwa kila mwanamke. Kuna wale ambao huwa na machungu na magonjwa zaidi ya wengine na kuna wale wanaopitia hali hii kwa njia rahisi mno.

SWALA NYETI!
Swali ambalo kila mwanamke anaweza kuwa nalo ni, Je ninaweza kushika mimba wakati nina hedhi?
Jibu la hakika ni Ndiyo! Ingawaje wanawake wengi hawawezi kushika mimba wakati wana hedhi, Kuna baina ya wengine wanaoweza kushika mimba wakati wanashirikiana ngono wkati wana hedhi. Hii si kawaida kwa wengi lakini kulingana na dakitari Jeannnette Lager, M.D, MPH aliyesomea maumbile ya wanawake, anatuelea jinsi mwanamke anaweza kushika mimba wakati ana hedhi sana sana kwa wale walio na mzunguko fupi zaidi yaishirini na nane au zaidi.
Haya basi hebu tufafanue zaidi juu ya ugunduzi ya kuwa umeshika mimba.

Dalili zifuatazo ya mimba ni maagizo tu ya kuelewa jinsi unavyoweza kukumbatia hali yako ukiwa na mimba.
  • Kukosa Hedhi (Missed Period)
  • Utoaji damu mwepesi (light spotting/implantation bleeding)
  • Kufura kwa Matiti (swollen Breasts)
  • Mhemko wa hisia (Mood swings)
  • Kutoa hewa ( lots of gas)
  • Kutapika au kuhisi kutapika (Nausea and vomiting)
  • Kufura tumbo (bloating)
  • Kukojoa kila wakati (frequent urination)
  • Constipation (Kuvimbika)
  • Mgongo kuuma Upande wa chini (lower back pain)
  • Kuumwa kwa kichwa (headache)
  • Kuzidi joto (increase of basal temperature)
  • Uchovu (fatigue)
  • Kutamani aina ya vyakula (food cravings)
  • Kulia (crying)
  • Kulala muda kwa muda (sleepiness)
Urahisi na kufura Matiti
Matiti yako yanaweza kuonyesha dalili za kwanza ya mimba. Wiki mbili baada ya kupata mimba, mabadiliko ya homoni yanaweza kufanya matiti yako kuwa makubwa kuliko kawaida, unaweza kuhisi kujikunakuna na uchungu kiasi, pia unaweza kuhisi kama matiti yako yamejaa au nzito.

Uchovu
Uchovu umekuwa hali na dalili ya kwanza mno kwa wanawake wajawazito. Homoni inayoitwa Progesterone huongezeka kwa wingi na inaweza kukufanya kuhisi usingizi kila wakati. Pia upunguzaji wa sukari katika damu, upunguzaji wa shinikizo la damu (blood pressure) na uzidishaji wa damu unaweza kukufanya uwe mchovu wakati wa mimba.

Utoaji damu mwepesi na machungu kwa tumbo ya uzazi
Kuna wakati, damu mwepesi (spotting) huwa dalili ya mimba mapema. Damu hii huwa nyepesi mno na haiwezi kulinganishwa na ule wa hedhi. Rangi ya damu hii ni waridi au kahawia kulingana na hali ya mwanamke. Wakati mbegu ya mwanamume na ule wa mwanamke yamekutana kumtengeneza mtoto, mwanamke anaweza kutoa damu nyepesi kuonyesha ya kwamba mwana amelazwa vyema katika tumbo la uzazi wa mwanamke.

Damu hii huchukua siku chache sana kutoka kulinganishwa na ule wa hedhi. Kuna wanawake wengine wenye hukosa kuonyesha damu hii mwepesi wanapopata mimba. sio lazima wanawake kutokwa damu wanaposhika mimba. ni muhimu kuelewa ya kuwa mwili ya kila mwanamke ni tofauti. Pia, machungu katika tumbo la uzazi wakati mimba hutengenezeka, unaweza kufanana na ule wa hedhi.

Damu [ni damu] si kitarasa”
Kuhisi kutapika au Kutapika
Ugonjwa wa asubuhi (morning sickness) unaweza kufanyika wakati wowote wa siku. Kuna wanawake waliosemekana kubebaa mimba ambao huwa na ugonjwa huu hivi punde wanapoamka, kuna wengine wanaopata ugonjwa huu wakati wa mchana na wengine wakati wa usiku. Kila mwanamke ana utofauti kulingana na maumbile ya mwili wake.
Wanawake wengi kwa jumla hupata (morning sickness) wiki mbili wanaposhika mimba. Kutapika huwa matokeo ya homoni inayoitwa estrogen inapoongezeka mwilini. Kuna wanawake wengi ambao hunusa harufu za aina mbali mbali, kama vile marashi, vyakula mbali mbali kama mayai, kwa haraka na pia harufu zingine huwafanya kuhisi kutapika au huenda kutapika.

Ukiwa unahisi kutapika, unaweza kula au kunusa ndimu au kukula matunda kama ndimu, Mizizi kama tangawizi na pia kuhakikisha una kunywa maji mengi kwa wakati huu. Kuna wanawake wengine husema wanaweza kuhisi ladha ya chuma ulimini mwao. Haya yote ni kwa sababu homoni estrogen imeongezeka mwilini juu ya kushika mimba.

Kutamani Vyakula vya aina aina au Kukataa hivi vyakula
Ukiwa umeshika mimba, unaweza kujipata una hisia ya vyakula fulani, ilhali kuna vyakula mbali mbali ulivyopenda sasa hutaki kuviona au kuvinusa.

Kuna wanawake wengi waliopenda mayai na sasa hata harufu ya mayai huwafanya kutapika. Na kuna wale wanaoanza kupenda matunda au vyakula vya aina mbali mbali wanapokuwa wajawazito.

Haya yote ni kwa sababu ya mabadiliko ya homoni mwilini, haswa kwa muhula wa kwanza (Mwezi moja hadi tatu) ya mimba. Pia unaweza kuhisi njaa wakati wowote wa siku. wanawake wengi ulimwenguni huanza kukula zaidi ya kawaida na hii ni ishara kubwa ya kwamba mwanamke amepata uja uzito.

Kuumwa kwa kichwa
Wakati unapopata mimba, uongezaji wa damu ni haswaa. Ndipo Kichwa kuuma muda kwa muda. Ni muhimu kupumua hewa safi na kupunguza kazi ya kimwili ili uweze kupumzika kila wakati.

Kuvimbiwa (constipation)
Hali ya kutoenda haja kubwa ni kawaida kwa mwanamke yeyote aliye na mimba. Dalili hii ni ile kati ya kwanza wakati mwanamke amepata ujauzito. Homoni Progesterone hufanya chakula kuenea polepole kwenya matumbo na hii husababisha ugumu wa kuenda haja kubwa.

Mhemko wa hisia
Katika Muhula wa kwanza wa mimba, utaweza kupata mhemko wa hisia. Unaweza kuhisi furaha halafu baada ya muda chache wahisi huzuni. Kuna wakati mwingine unaweza kujipata unalia kwa mambo madogo sana. Haya yote ni kwa sababu mwili wako unapitia mabadiliko kuweza kumtengeneza mtoto.

Kuhisi Kizunguzungu
Wakati damu linaongezeka na shinikizo la damu kupunguza, unaweza kusikia kichwa chepesi au kizunguzungu wakati wa kwanza kama dalili ya mimba. Wakati mwingine, ukosefu wa sukari kwa damu unaweza kufanya mwanamke mja mzito kuzirai.

Ni muhimu wakati unaposikia uwepesi wa mwili, kuketi chini au kujilaza na kuuweka miguu juu ya mto ili damu literemke kichwani. pia kuhakikisha unakula kila wakati unahisi njaa husaidia kupunguza hali hii.

Kuzidi kwa Kuhisi Joto
Unapoamka, joto la mwili wako huwa la kawaida kila siku. Unapopata mimba joto hili hugeuka na kuwa nyingi kushinda kawaida. Baada ya kuwa na hedhi, kuna wakati mwanamke huwa tayari kupata mimba wakati huu, joto la mwili huongezeka halafu hurudi kuwa la kawaida baada ya wiki mbili.
Ukigundua kuwa joto hili halijapungua baada ya wiki mbili, basi una chanzo kubwa cha kuwa na mimba haswa kama umeshirikaina ngono bila kinga.

Kukosa Hedhi
Baadhi ya dalili nyingi mwilini mwa mwanamke aliye na mimba, Kukosa hedhi ni ule wa kwanza mno haswaa kama (Period) yako ni ya kila mwezi. Utaweza kugundua umekosa mwezi wakati unapojua vyema umefanya ngono bila kujikinga.

Kujawa na hewa
Ni kawaida kwa mwanamke aliye na mimba kuhisi kana kwamba amejaa hewa tumboni na pia kutoa hewa hapa na pale. Hii ni kwa sababu tumbo la uzazi linapanuka kuhakikisha mtoto yuko na mahali pa kukua na kuzunguka.

Kuongezeka kwa hamu ya chakula
Wanawake wengi wanapopata mimba, ingawaje wengi wao huwa wagonjwa na wanahisi wasile vyakula kila wakati, Mwanamke akifikisha muhula wa pili, Hamu ya kula huongezeka.
Sababu ya hamu kuongezeka ni, mtoto aliye tumboni anahitaji chakula pia. Unaweza kuona mama aliyekula chakula sahani moja, anaanza kukula sahani moja na nusu na baada ya muda si mrefu anahisi njaa tena.
Homoni zilizo mwilini hubadilika na kumfanya mwanamke aliye na mimba kuwa na hamu ya kula kila wakati ili mtoto aweze kupata nguvu na kukua vema.

Kulala Muda kwa muda
Wakati mwanamke amekuwa mja mzito, Homoni (progesterone) huongezeka zaidi mwilini. Tulivyonena hapo mbeleni, Homoni hii hufanya kazi mwilini kuzembea.
Hii ndio sababu ya wanawake wengi walio na mimba kuhisi usingizi kila wakati. Tukumbuke kuwa, Mwana anayetengenezwa chupani mwa mamake, anahitaji nguvu zote ili kujistahimili.
Akina mama wanaochukua muda wa kupumzika huwasaidia wanawe kukua kwa njia bora. Pia, afya ya mama huongezeka anapochukua muda wa kulala wakati ana mimba.

Kuhisi una mimba kama matokeo ya ngono
Kuna wanawake wengi wanaojua tu wameshika mimba baada ya ngono. Hisia hizi huwa pembe ya kila mwanamke anayejua mwili wake vizuri.

Unapotazama enzi za kale, mamake msichana aliye na mimba angejua kwa haraka kuwa mwanake ana mimba bila kutizama dalili zote. Hisia kama hizi huwa ya ukweli na zilitumiwa na mababu zetu kujulisha wanawake wanaotarajia wana. Mila hii ilipitishwa kwa kizazi kimoja hadi kingine.

“Kulea mimba si kazi, kazi kulea mwana”
Kuchukua kipimo cha mimba (pregnancy test)
Njia iliyo sahihi kabisa na wa kisayansi na imeaminika kuwa ya haki ni kwa kupima mimba kutumia (pregnancy test).
Kipimo hiki huwa kimetengenezwa kitechnologia. Mwanamke aliyedhani kuwa ana mimba huikojolea kisha kutizama matokeo ya alama ngapi kipo kwenye kipimo hiki cha mimba. Kukiwa na alama mbili hapo basi mwanamke anatarajia mwana.

“Kuzaliwa kumoja, maisha mengi”
Kuna aina mbali mbali toka hapo jadi ya kueleza kama mwanamke ni mja mzito kama vile:-
  • Wanawake wa Misri walikuwa wanapima mimba kwa kukojolea mbegu za ngano siku kadhaa. Mbegu hizo zikianza kuonyesha hali ya kumea, mwanamke alisemekana kuwa na mimba
  • Njia nyingine ilikuwa ya kitunguu. Mwanamke aliweka kipande cha kitunguu kwa uke wake wakati wa usiku alipoenda kulala. Asubuhi ya kuamka, harufu ya kitunguu isipotokea mdomoni alisemekana kuwa na mimba.
  • Kwa wengine, Mwanamke alikuwa akojoe ndani ya beseni kisha kuweka kofuli au kifunguu ndani ya mkojo uliyo ndani ya beseni kwa muda wa masaa matatu au manne.Iliaminiwa kuwa ukisha mwaga hayo makojo na alama ya kofuli au kifunguu kibaki kwa beseni basi una mimba.
  • Mwanamke aliye na mimba ana mkojo wa rangi tofauti. Haswaa ya kijani. Rangi hii huendelea hadi mwisho wa mimba.
Unawezaje kujua haswaa una mimba?
Baada ya kufanya ngono bila kinga, na wakati mwanamke amefikisha umri wa kupata mtoto, (wakati msichana huanza mzunguko wa hedhi), ukiwa na dalili zote zilizotajwa hapo awali, jaribu kuenda na kuhakikisha na Daktari ili isiwe ni alama ya chanzo cha ugonjwa fulani na wala si mimba.
Ni muhimu kuhakikisha una mimba wakati unapofikiria u mjamzito. Pia ukisha pata uhakikisho, unaweza kuchukua vipimo bora vya kujitunza wewe na mwanawe.
Mwanamke yeyote aliyegundua yuko na mimba anahitajika kutibiwa vyema na wale walio karibu naye. Kila mwanamke anastahili kuonyeshwa heshima haswaa wale wanaobeba maisha ndani yao.
Imeaminika mwanamke aliye na furaha kila wakati anapokuwa na mimba huweza kuzaa vizuri na watoto wao pia huwa na furaha.

Upenyo wa Haraka
  • Uja uzito ni baraka na ni lazima kila mtu ajue kwamba maisha hupewa na Mola ili kuendeleza vizazi.
  • Aibu na laana kwa wanawake unastahili kukomeshwa haswa wakati ni wajawazito. Upendo na hali ya amani ni chanzo kubwa cha hawa wanaweke kujiwezesha kupitia muda huu kwa urahisi.
  • Kukula vyakula vizuri kama mboga iliyo na Iron (Chuma) na kalsiamu huwasaidia wanawake kuongeza damu. Pia kukunywa maji mengi wakati huu ni muhimu sana kwa kusaidia viungo vya mwili kujimudu.
  • Kufanya mazoezi kama kutembea kila siku ni muhimu kwa sababu wakati wa kujifungua unapokaribia huwa rahisi na machungu ya kuzaa mwana hupungua.
Kila la heri na ufanikio unapoanza safari hii ya uzazi. Pongezi mama


Chanzo: The African Parent
 
Baada ya week 2 ndio inaweza kuonekana hapo ni kwa uwakika zaidi, ila kwenye maduka kuna vipimo vya kujipa ile asubuhi tu ukiamka na ule mkojo wa kwanza kinaweza kuonyesha.
 
Baada ya week 2 ndio inaweza kuonekana hapo ni kwa uwakika zaidi...ila kwenye maduka kuna vipimo vya kujipa ile asubuhi tu ukiamka na ule mkojo wa kwanza kinaweza kuonyesha.
Nimejipima jana na hiyo UPT ila imeonyesha negative, hapa ni baada ya cku kama 5 hivi zimepita, so niendelee kusubiri?
 
nimejipima jana na hiyo UPT ila imeonyesha negative, hapa ni baada ya cku kama 5 hivi zimepita, so niendelee kusubiri

Basi hauna mimba maana hiyo UPT huwa inaonyesha kama unayo au labda wait mpaka baada ya week 2......
 
Mimba inakuwadetected na upt baada ya wk2, na inaanza kuonekana baada ya wk20 yaan baada ya miezi mitano. Lakin ultrasound inaweza ona hata chini ya hapo.
 
Ukipima na kifaa - pregnancy test, hata mimba iliyoingia jana inaonekana. So jaribu hiyo itakupa ukweli zaidi.
 
Kwa kwetu Tanzania, hatuko that much sophisticated interms of diagnostic facilities, vipimo tunavyotumia ni crude na vinachukua muda mrefu kupata matokeo. Kwetu kipimo tunachotumia cha UPT (urine for pregnancy test) kitakuwa positive siku ya 8 ( kama wiki moja hivi) mpaka ya 11 (roughly 2 weeks) baada ya missed period. Tunatumia pia USS (Ulatrasound), ambayo nayo itaona mimba (intradecidual gestation sac - kifuko cha mimba) wiki ya 4 mpaka ya tano ya ujauzito.

Kama uko Ulaya mimba yaweza kuwa diagnosed 5 days before the first missed period, yaani siku ya 9 since conception [tangu mimba kutunga na sio tangu kukosa siku zako-tofauti na UPT ambayo inakuwa positive siku 8 (roughly one week) baada ya kumiss period na sio baada ya conception, kwa sababu conception hutokea siku 14 kabla ya next menstruation] kabla hata hujakosa siku za mzunguko unaofuata, wanatumia vipimo kama ELISA na vingine.

Jaribu kurudia UPT on the 7th or 8th day since your first day of the last missed menses, na pia kama ni negative rudia siku ya 11, kama itakuwa negativu tena, TRY AGAIN next time you might succeed.
 
Mimba inakuwadetected na upt baada ya wk2, na inaanza kuonekana baada ya wk20 yaan baada ya miezi mitano. Lakin ultrasound inaweza ona hata chini ya hapo.
Nimekuelewa docta, ila kwa sasa nishaanza kuingia period inamaana mimba haikuingia, vp, naweza kukuPM kwa maswali zaidi?
 
Me niko hapa hapa TZ , nimeanza period leo so inamaana mimba imeingia, dhumuni langu ilikuwa nipate mimba ila ndio hvyo tena, vp can i PM u 4 more questions?
 
me niko hapa hapa TZ , nimeanza period leo so inamaana mimba imeingia, dhumuni langu ilikuwa nipate mimba ila ndio hvyo tena, vp can i PM u 4 more questions?

Pole but dont worry, ur welcome niwaellyester1, u can PM me if I can help
 
Kujua wakati una mimba


Wanawake wengi hujua wameshika mimba aghalabu wiki 3 baada kushika mimba. Mwili wenyewe utakuonyesha/utakutabiria kama:
  • Hedhi yako itakoma/itakuwa nyepesi
  • Utasikia uchefuchefu/utatapika (ugonjwa wa asubuhi morning sickness na inaweza kutokea wakati wowote wa siku pia).
  • Matiti yako yataanza kuwasha, kufura au yataanza kuwa makubwa.
  • Chuchu (ncha ya titi) na sehemu zilizokaribiana zitaanza kuwa nyeusi na zizizoweza kuvumilia.
  • Itakubidi kwenda haja ndogo mara kwa mara.
  • Utasikia uchovu
  • Kusokotwa na tumbo
Kama umeona baadhi ya dalili hizo, unaweza kuwa na mimba. Pata jaribio/uchunguzi kipimo cha mimba ili kupata yakini! Unaweza pimwa bure katika kliniki iliyokaribu nawe au ununue kifaa vya kujipmia nyumbani kutoka duka la dawa. Daktari wako anaweza kukupima pia au atakuelekeza kwa mtaalamu kama hauna.

Vipimo vya mimba

Vipimo hivi huchunguza kuwepo kwa Human Cherionic Cronadotropin (HCG) kwa mkoja au damu. HCG wakati mwingine hitwa Pregnancy Hormone na huwa kwa mwanamke tu wakati ana mimba. Kuna aina mbili ya vipimo: kipimo cha mkojo na kipimo cha damu.

Kipimo cha Mimba cha Mkojo
Wanawake wengi hutumia kipimo hiki ambacho pia huitwa cha nyumbani (HPT-home pregnancy test) kwa sababu ni rahisi kutumia na bahasa (rahisi kibei) kuna aina nyingi za vipimo hivi. Kwa kimoja, utakwanya mkojo wajo kwa kikombe na kukitumbukiza kijiti huko na kwakingine utaweka kijiti hicho kwenye viungo vya mkojo. Njia iliyobora ni itakayokuonyesha kiwango cha HCG, hivyo tafuta moja katika kiwango cha hCG kutoka 15 hadi 30. Utasaidiwa na mhudumu wako dukani la dawa au kliniki.

Vifaa hivi hufaa kwa asilimia 97-99 kuyakirisha uwepo wa mimba vinapotumiwa ipasavyo. Hivyo kufuata maagizo ni muhimu. Pia angatia wakati wa kuharibika wa kifaa kwani kifaa kilichoharibika hakitakupatia matokeo unayotarajia.

Kama utapata matokeo yasiyofaa/yasiyo hakika
Kama utajipima/utapimwa bado kidogo*, unaweza kuona kwamba hauna mimba ili hali unayo. Aina nyingi ya vipimo vya nyumbani hukushauri ujipime baada ya siku kadha bila kujali matokeo uliyopata awali. Kama unaendelea kupata matokeo yasiyofaa nab ado unashuku una mimba, ongea na daktari/mkaguzi afya waka.

Kama utapata matokeo yafaayo/ya hakika
Kama utapata matokeo ya hakika, fanya miadi na mkaguzi afya wako punde tu. Mkaguzi wa afya yako atayakinisha kama una mimba kupitia kipimo cha damu na ukaguzi mwingine (pelvic exam) na atakwambia chaguzi uliza nazo.

Kipimo cha Damu
Kama wataka kipimo cha damu badala ya kite cha nuymbani, fanya miadi na mkaguzi afya wako/dakatari wako.
 
Mke wangu ananiambia anahisi anaweza kuwa mjamzito na tokea tukutane nae hazijapita hata siku tano je dalili zinaweza kujitokeza.mana ananiambia mala kichefuchefu mala mate yanajaa mdoni hata hamu ya kula hana.

Je, inawezekana? Naomba msada wenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…