ZIARA YA WAZIRI MKUU YAWATIA KIWEWE MA RC NA MA DC KAGERA

Don san tan

JF-Expert Member
May 23, 2015
563
433
Bukoba. Kasi ya kutumbua majipu
imeonekana kuwatia kiwewe wakuu wa
Wilaya za Mkoa wa Kagera kwa
kufanya kazi na mikutano ili
kuhakikisha hakuna makosa
yatakayoonekana wakati wa ziara ya
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ya
kukagua miradi ya maendeleo
inayoanza kesho kutwa.
Kwa wiki moja sasa, wakuu hao
wanafanya mikutano ya kila siku na
kukagua miradi hiyo ili kuhakikisha
hakuna makosa yanayoweza
kusababisha kutumbuliwa majipu.
Mkuu wa Wilaya ya Missenye, Festo
Kiswaga alisema mwishoni mwa wiki
iliyopita kuwa wamechukua tahadhari
kwa kuhakikisha kila eneo liko salama.
“Tunafanya maandalizi kila sehemu na
idara maana ni vigumu kutabiri Waziri
Mkuu atatembelea wapi,” alisema
Kiswaga.
Alisema ratiba ya maeneo
atakayotembelea Waziri Mkuu
imebadilika mara tatu tangu
walipotaarifiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Jackson
Msome alisema wanalazimika
kuzingatia kanuni ya mchezo wa soka
kwa kuelekeza maandalizi kila idara
kuanzia sehemu ya ulinzi, kiungo na
ushambuliaji.
“Ni lazima kujiandaa kila idara
kufanikisha ziara ya Waziri Mkuu kwa
sababu hatuwezi kujiamini na ratiba
bila kuchukua tahadhari ya ziara za
kushtukiza eneo lolote,” alisema
Msome.
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Darry
Rwegasira alisema licha ya ratiba
kuonyesha kuwa Waziri Mkuu
atatembelea na kuzindua jengo la
upasuaji katika kituo cha Afya cha
Nyakanazi, wamefanya maandalizi
katika eneo lote ili kuepuka
kushtukizwa iwapo ratiba itabadilika
ghafla.
Mfanyabiashara mjini Bukoba, Dennis
Gregory alisema wanakusudia
kuwasilisha kwa Waziri Mkuu
changamoto ya bei ndogo ya kahawa
inayouzwa nchini ikilinganishwa na
Uganda.
 
Naomba akifika missenye, aanze na wale wale wote waliohusika kujenga Barbara za mitaa ya mji wa bunazi yalipo makao makuu ya wilaya, ziko chini ya viwango sana, jengo lagorofa mbili la halmashauri ni wizi mtupu, pale mzani mtukula wizi mtupu, bidhaa za magendo zinapitishwa minziro bypass kwenda Uganda no kodi wala kukaguliwa, TRA KYAKA, MORE THAN THIEVES, Polisi pale mtukula ni kituko, sina majina yao aende ajionee, maofisa maliasili, wanakamata mbao, nafikiri wameshakamata kama mbao milioni, wamuonyeshe walau mia mbili tu, najua hata hizo hawana, mtendaji wa kata Minziro, huyo yeye tangu amepelekwa pale, ni kuzurula tu hakuna maendeleo yoyote, toeni leta mwingine, mradi wa maji huo ni kichekesho, mtoKAGERA, unapita, katikati ya mji, lakini watu hawana maji, huyo mbunge KAMALA, mfukuzeni hata kwenye msafara askaribie, hana loolote, bogus, wafugaji haramu ni income source ya watu hapo, KMK, AKIKOSA JIPU HAPO HATA MOJA, NITAJUA KAHONGWA
 
Back
Top Bottom