ZANZIBAR: Viongozi wa CUF washutumiwa kuchochea vurugu Pemba

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,880
6,367
Jeshi la Polisi Zanzibar, limesema kuwa vitendo vya kihalifu vya uvunjifu wa amani vinavyotokea kisiwani Pemba vinachochewa na viongozi wakuu wa chama cha Wananchi CUF.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa, naibu mkurugenzi wa upelelezi na Makosa ya jinai wa Jeshi hilo, Salum Msangi alisema kuwa viongozi wakuu wa CUF wamekuwa wakiwatuma wafuasi wao kufanya vitendo vya hujuma kisiwani Pemba kwa madai kuwa serikali iliyopo madarakani sio halali.

Alisema kuwa jeshi la polisi linataarifa za uhakikia kuhusu viongozi wa CUF wakiwapongeza wafuasi wao na kuwapa zawadi ya fedha kwa kuweza kufanya vitendo vya hujuma kisiwani humo ikiwemo uchomaji moto wa majengo mbalimbali na kuhujumu mikarafuu na mazao mbalimbali.

“Tunao ushahidi viongozi wa CUF wamewakusanya wafuasi wao na wanawapa pongezi wale ambao wameza kufanikiwa kufanya vitendo vya hujuma dhidi ya wananchi”alisema.

Alisema kuwa jeshi hilo halitamvumilia mtu yoyote atakaehusika kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na wala halitakua na muhali katika kuchukua hatua za kisheria bila ya kujali cheo cha mtu.

Aidha alisema kuwa jeshi hilo linawashikilia watu zaidi ya 20 kisiwani Pemba ambapo wanahusishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Akizungumzia kuhusu ripoti ya Chama cha wananchi CUF waliyoitoa juzi ya kulipeleka Jeshi hilo mahakama ya kihalifu ya kimataifa (ICC),alisema jeshi hilo haliogopi kupelekwa huko na kusema kuwa taarifa zilizomo katika ripoti hiyo zinazohusu jeshi la polisi ni za uongo.

“Kama ICC tutaanza kuwapeleka wao viongozi wakuu wa CUF ambao wao ndio wachochezi wakubwa wa uvunjifu wa amani ya nchi na taarifa zao zote tunazo”alisema Msangi.

Hata hivyo alisema jeshi la polisi linaendelea kuwaita watu mbalimbali na kuwahoji akiwemo Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho.

Jeshi hilo liliwapa tahadhari viongozi na wafuasi wa vyama vya siasa kuacha tabia ya kuwashawishi wafuasi wao kufanya vitendo vya hujuma wakati wao wametulia majumbani mwao.
 
CUF IMEPOKONYWA USHINDI
 
Swala la Zanzibar lisipoangaliwa kwa umakini litaleta madhara
Wahenga walisema bandubandu humaliza gogo
 
ICC halipelekwi jeshi, anapelekwa mtu. Kwa hiyo watapelekwa viongozi wanaohusika kutoka polisi. Huyo msangi asitumie neno "kulishitaki jeshi" ili kupata huruma ya wananchi. Washitakiwe tu.!
 
Wewe Msangi hebu nikuulize hivyo vichwa vyenu wewe, wanao, na mkeo vina thamani ya shilingi ngapi kwani kuna watu wanvihitaji kuvinunua sema ulipwe viondoshwe maana unajitia ushimbutu sana wewe .

Tumo humu humu ndani ya jeshi la Polisi basi fanya ujinga wako uone, shenzi
 
Wewe Msangi hebu nikuulize hivyo vichwa vyenu wewe, wanao, na mkeo vina thamani ya shilingi ngapi kwani kuna watu wanvihitaji kuvinunua sema ulipwe viondoshwe maana unajitia ushimbutu sana wewe . Tumo humu humu ndani ya jeshi la Polisi basi fanya ujinga wako uone, shenzi
Mmmmh!!
 
Watajiju hukohuko watakao athirika hasara yao watafaidi bahati yao.
 
Wewe Msangi hebu nikuulize hivyo vichwa vyenu wewe, wanao, na mkeo vina thamani ya shilingi ngapi kwani kuna watu wanvihitaji kuvinunua sema ulipwe viondoshwe maana unajitia ushimbutu sana wewe . Tumo humu humu ndani ya jeshi la Polisi basi fanya ujinga wako uone, shenzi
Unaongea nin wew!!
 
Zanzibar angepewa Baloz Ally Karume huyu ndio angewanyoosha hao waliokuwa wanapongezwa, tatizo la uyu wa sasa ni mpole sana na ndio maana maalim anamchezea.sharubu sana.
 
Hivi wale waliopita na MABANGO YA UBAGUZI WA RANGI walifungwa gereza lipi??AU kesi yao bado iko Mahakamani???
 
Mi cjui binadamu tukoje,hivi huyo shein haoni aibu?Kila unakopita unajua wananchi hawakukuchagua halafu unapeta tu?Binadamu tumeumbwa tofauti,mimi nisingeweza!
 
Wewe Msangi hebu nikuulize hivyo vichwa vyenu wewe, wanao, na mkeo vina thamani ya shilingi ngapi kwani kuna watu wanvihitaji kuvinunua sema ulipwe viondoshwe maana unajitia ushimbutu sana wewe . Tumo humu humu ndani ya jeshi la Polisi basi fanya ujinga wako uone, shenzi
Unafaa kukamatwa na kufikishwa mahakamani mara moja
 
Aidha alisema kuwa jeshi hilo linawashikilia watu zaidi ya 20 kisiwani Pemba ambapo wanahusishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Kauli kama hizi kutoka jeshi la Polisi Zanzibar imekuwa kama nyimbo ya Bi Kidude inayojirejea hapo kwa papo.

Tulielezwa kuwa wale waliohusika na kuuchafua uchaguzi wa Oktoba 25 watafikishwa mahakamani lakini mpaka leo kimya? au walikuwa wanamaanisha ICC?
 
Back
Top Bottom