Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,790
Inahuzunisha, wakati juzi tu tulisheherekea miaka 52 ya muungano wetu, mshirika mmoja wa muungano anawauzia wananchi wake bidhaa adimu na adhimu ya sukari kwa bei nafuu kwa vitendo na mwengine anauza bei rahisi kinadharia.
Serikali zote mbili zinaongozwa na CCM na zina sera sawa kuhusu kulinda viwanda vya ndani. Zanzibar wana kiwanda kimoja cha Sukari wakati mshirika wake ana viwanda kadhaa vya sukari.
Kwa kujali wananchi wake SMZ wameona kwanza walinde hali, maslkahi na mahitaji ya wananchi walio wengi kwanza na hivyo kuhakikisha kila mahitaji muhimu yanapatikana kwa bei nafuu inayomudiwa na wananchi wake.
Jana nilikuta zogo karibu na maduka ya rejareja hapa Zanzibar watu wakilumbana. Eti, wanabishiana aina gani ya sukari kati ya "Brown Sugar na White Sugar" yenye ladha tamu zaidi
Kumbe kweli kipato kina jeuri! Ushauri, tufanye serikali moja na Makao Makuu ya Serikal ya muungano yawe Zanzibar na yale SMZ yahamishiwe Pemba. Uhaba wa bidha adimu na muhimu wa kila mara utakua historia!